CHOZI LA HERI
QUESTIONS AND MARKING SCHEMES
- Eleza ufaafu wa anwani Chozi la Heri (ala20)
- Kwa kurejelea kila sura onyesha jinsi mwandishi alivyoisuka kazi yake kufanikisha mtiririko na muumano wa
- Athari ya vita katika nchi ya Wafidhina ni kioo cha bara la Jadili (ala 20)
- Jadili dhana ya chozi katika riwaya ya Chozi la Heri (ala20)
- Mwanamke katika jamii hii ametwezwa na kutwazwa jadili ( ala20)
- Akikosa la mama hata la mbwa huamwa kwa kurejelea methali hii eleza umuhimu wa mashirika ya misaada (ala20)
- Jamii ya Chozi la Heri ni taswira ya jinsi ukabila unavyoathiri bara la Afrika (ala20)
- Malezi ya watoto katika riwaya ya Chozi la Heri ndicho kitovu cha ufanisi na matatizo yote yanayowapiku watoto (ala20)
- Utumizi wa afyuni katika jamii umeleta mathara mengi . Thibitisha (ala 20)
- Jadili athari na dhiki zinazotokana na uongozi mbaya (ala 20) 11)Mla, naye huliwa zamu yake ikifika . kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri thibitisha
ukweli wa kauli hiyo (ala 20)
12)Riwaya ya Chozi la Heri imejaa aina mbalimbali za migogoro jadili. (ala 20) 13)Uozo wa maadili na kuvunjwa kwa haki ni jambo ambalo lilikuwa la kawaida katika
nchi ya Wahafidhina. Thibitisha (ala20)
14)Riwaya ya Chozi la Heri ni ya Utamaushi jadili kauli hii (ala20)
MASWALI YA MUKTADHA
TIA DONDOO KATIKA MUKTADHA WAKE
- “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa”
- “ Usiku umekuwa mpevu, twende tusije tukamtia mama kiwewe’’
- “ Huenda nikapata mbinu ya kujinasua baadaye’’
- “ Di, Mimi nitawakimu kwa viganja hivi vyangu. Hamtapungukiwa na lolote’’
- “Basi Doc, nakubaliana na rai yako”
- “ Huyu hapa ameletwa na wasamaria wema leo asubuhi’’
- “ Je ni yule aliyeletwa jana usiku wa kuamkia jana’’
- “ Hatuwezi kumkabidhi mzee wetu huyu kifaranga kitekite hivi, tutakuwa tunampagaza uzazi”
- “ Yako ya arubaini imefika”
- “ Wenye hadhi na mali wanahitaji wafanyikazi wa kuwaendelezea biashara zao’’
- “ Usiwe na mawazo finyu na hasi kuhusu kumpanga mtoto’’
- “ Karibuni naona mmetuletea kilaika’’
- “ Tulipata ombi lenu kuhusiana na suala la kumpanga mojawapo wa watoto wetu’’ 14)“ Ndugu zako wako hai na bila shaka mtakutana”
- Yote haya yamewezekana kutokana na mwongozo mlionipa Zaidi , utulivu nilioupata nilipoambulia familia hii ulinipa msukumo kila mara nilipokabiliwa na ndaro
- “ Njoo nikujuze kwa yule binamu vuuk ambaye hukwambia habari yake kila mara”
- “ Atanguliaje kisimani hunywa maji maenge”
- “ Mlaani shetani” 19)“ Huyu ana imani”
- “ Umu hawa ni marafiki wangu wa chanda na Ni watu wakarimu na wenye imani’’
- “ Nashukuru kwa kunielekeza kwa wazazi wetu hawa”
- Wote wawili walitazamana, kila mmoja akiapa moyoni kuwa amewahi kumwona kiumbe huyu mahali.
- Kweli mimi nilikuwa sikio la mbuzi ambalo nyanya alizoea kusema husikia chunguni
- “ Leo waonaje tukiwajaribu mababe wetu? Ni vizuri kuanza mapema kabla ya jua la utosini”
- “ Mama zenu walienda wapi?” 26)“ peace be with you’’
- “ Kweli milima ndiyo haikutani”
- “ Nahisi kama nasimulia kisa kirefu chenye mwisho mwema”
- “ Si kwamba sijawatafuta hamna kituo cha polisi ambacho sijabisha hodi”
- “ Haiwezekani! Hili haliwezekani! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”
MASWALI YA SIFA ZA WAHUSIKA NA UMUHIMU WAO
Jadili sifa za wahusika wafuato na umuhimu wao;
- Ridhaa
- Mwangeka
- Mwangemi
- Umulkheri
- Lunga
- Bwana Kaizari
- Mwekevu
- Mzee Mwimo msubili
- Tila
- Kairu
- Zohali
- Mwanaheri
- Chandachema
- Neema
- Sauna
- Pete
- Mwaliko
- Mwalimu Dhahabu
- Dickson
- Bwana Maya
- Naomi
- Mzee Kedi
- Hazina
MASWALI YA MBINU ZA LUGHA NA TAMATHALI ZA USEMI
Jadili mbinu zifuatazo zilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri
- Jazanda
- Taharuki
- Kisengerenyuma
- Barua
- Ndoto
- Kinaya
- Taswira
- Swali la balagha
- Sadfa
- majazi
MAJIBU YA MASWALI
- UFAAFU WA ANWANI Anwani ya Riwaya hii ni Chozi la
Anwani hii imeundwa kwa maneno mawili yaani CHOZI NA HERI.
Kwa mujibu wa matumizi ya neno Chozi katika riwaya hii, limetumika kuashiria tone la maji au uowevu unatoka machoni aghalabu mtu anapolia au kufurahi.
Neon HERI limetumika kuonyesha maana ya amani,Utulivu, mafanikio na usalama .
Kwa hivyo, chozi la heri ni kirai ambacho kimetumika kuonyesha chozi la mhusika ambaye amepata utulivu, amani na usalama nafsini mwake. Ni wazi kusema kuwa , mwandishi amefanikisha kwa hali ya utendeti kuonyesha ufaafu wa anwani rejelewa kwa kurejelea mifano hii:
- Kaizari anamsimulia mwamu wake Ridhaa yaliyotokea, kwamba siku ya nne baada ya mapinduzi walisikia hodi na mkewe akaeleke a kufungua Alisalimiwa kwa kofi na kuulizwa kiko wapi kile kidume chako kijoga? Nasikia ni mmoja wa wale waliotuuza kwa kupigia Mwekevu kura. Ati as for me and my family we will support our mother. Ninyi ndio vikaragosi wanaotumiwa na wasaliti. Kabla hajajaribu lolote alikuwa amekula mikato miwili ya sime, akasirai kwa uchungu. Baadaye genge hili liliwabaka Lime na Mwanaheri . alijaribu kuwapa wanawe huduma ya kwanza na
kisha baadaye wanakumbwa na matatizo ya vyakula na maji katika kambi ya wakimbizi walikokimbilia waathiriwa. Mto wa mamba haukuwa safi ila baadaye waliyanywa maji ambayo walidiriki kupata huku wakisema ni heri nusu shari.
- Bwana kaizari anasimulia namna vita vilivyowaathiri na walipokimbilia kambi za wakimbizi, anasema kuwa waliokuwa wamabahatika kubeba nafaka haba walizitoa zikatumiwa kwa Sasa matumbo yalianza kudai haki
- Ridhaa katika kumbukizi zake katika msitu wa heri, hakukuwa na wakazi wengi, kwa hivyo, alikosa ushirika wa ndugu zake. Aidha anapojiunga na shule siku za awali alitengwa na wenzake kwani hawakutaka ashiriki michezo yao. Kijana mmoja mchokozi alimwita ‘mfuata mvua’ aliyekuja kuwashinda katika mitihani yote na kwamba ni yet anayewaibia kalamu zao. Ridhaa hakungoja mwenzake amalize dukuduku lake alichukua mkoba wake na akafululiza nyumbani na kujitupa mchangani na kulia kwa kite na shake. Mamake alimliwaza na kumhakikishia kumwona mwalimu siku iliyofuata. Tangu siku hii, huu ukawa ndio mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa kwani baada ya mwalimu kuzungumza na wanafunzi umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano,Ridhaa alipata utulivu, amani na usalama shuleni na kungaa kwa elimu hadi kufikia Kilele cha cha elimu na kuhitimu kama daktari huku utendakazi wake ukimletea
- Kaizari anamshukuru Mungu uk16 kwa kuwa hai licha ya kwamba aliwatazama mabinti zake wakifanyiwa ukaini na vijana wenzao. Pia anapomtazama mkewe anashindwa kama inahalisi kumwita mkewe kwa sababu ya vile uso wake ulikuwa umevamiwa na Amevimbiana kama dongo la unga ngano. Anasema kuwa ametiwa hamira lakini yeye hana hamira ila ni matokeo ya ubahaimu wa binadamu. Licha ya hayo yote anashukuru kuwa wako hai.
- Ridhaa anajihisi kama yule Ayubu kwenye kitabu kitakatifu ambaye ibilisi aliifakamia familia na mali yake takribani kutwa moja. Hata hivyo, anajihisi nafuu na kiumbe kipya kwani wapwa wake Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu kutoka kwa vijana wenzao ambao walitumwa na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mkewe Kaizari yaani Subira alikuwa katibiwa Uk36
- Ridhaa na mwangeka wakiangaliana kila mmoja akitweta kwa mpigo wa kasi wa Walitaka kukimbiliana ila hakuna aliyetaka kuanza. Ridhaa hakuamini kuwa Mwangeka angerudi akiwa hai. Fahari ya uzazi na ulezi inayeyusha woga na shaka
huku Mwangeka akajirusha kifuani mwa babake huku wakiambiana kimoyo moyo ni hai sijafa uk46
- Uk 51 Mwangeka anashaangazwa na hali ya babake ya kutozika mabaki ya familia Baba mtu anamkazia tu macho , bila shaka ameelewa anachowazia mwanawe.Mwangeka ana huzunishwa sana na kitendo hicho cha unyama cha kuacha familia yake , mamake na wanuna wake kama majivu. Matone ya machozi yalitunga machoni, Mwangeka. Akayaacha yamdondoke na kumcharaza, yatakavyo. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa machozi haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani kidogo. Moyo wake ukajaa utulivu sasa kwa kujua kuwa wino wa Mungu haufutiki methali hii Mwangeka anaiona wazi ambayo mpinzani wake aliishi kuirudia mara aliposhindwa na Mwangeka.uk 52
- Katika Msitu wa Mamba kulikuwa na maelfu ya watu waliogura makwao. Kati ya familia kwao bila matumaini ya kurudi. Kwa Kangata na mkewe Ndarine, hapa palikuwa afadhali kwani hawakuwa na pa kwenda kwa kuwa hata kule walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao maskwota hivyo wakaamua kukumbuka asali na maziwa ya Kanaan hii mpya . Uk 57
- Msimamo wa Lunga wa watu kutopewa mahindi yaliyokuwa hatari hata kwa kipanya unasababisha kupigwa Anakuwa mkulima stadi, marafiki zake wanampa jina la msimbo mkulima namba wani. Uk 70
- Umu anapojitosa jiji analiona kama bahari isiyo na kikomo . Akiwa jiji baridi ya vuli inamtafuna huku pia akiwa na mkeketo wa njaa kwenye uchango huku akiwa na matumaini ya kukutana na kijana Hazina ailiyemsaidia akiwa anakataswa na mamaake. Wanapokutana Hazina alibahatika na sasa ni mfanyikazi katika hoteli moja pale mjini. Umu anapomweleza juu ya matatizo yake Hazina anamwonea huruma huku machozi yake yakimdodoka kwa mchanganyiko wa furaha na majonzi.uk87
- Kukutana kisadfa kwa Dick na Umu katika uwanja wa ndege kulileta utulivu, walikumbatiana kwa furaha. Machozi yaliwadondoka hawa mandugu wawili na wakawa wanalia kimyakimya.Walijua fika kuwa jaala ilikuwa imewakutanisha na kwamba hawatawahi kutengana Maisha sasa yalianza kuwa ya heri kwao.uk 128
- Baada ya miaka kumi ya kuuza mihadarati Dick alifaulu hatimaye kujinasua kutoka
kwa mwajiri wake. Alianza biashara yake mwenyewe ya kuuza vifaa vya umeme. Sasa akaanza kujitegemea kwa kuwa amejiajiri. Alikuwa ameufungua ukurasa mpya katika maisha yake. Maisha yake sasa ni ya heri.
- Zohali alikuwa mtoto wa nyumba kubwa wazazi wake walikuwa wa hadhi ya juu. Babake alikuwa mkurugenzi katika shir ika la utohaji huduma za simu huku mamake akiwa mwalimu mkuu wa shule ya kitaifa. Anakumbwa na changamoto za ujana na kushindwa kudhibiti matamanio yake huku akipata ujauzito. Wazazi wake wanamdhulumu na kuishia kutoroka nyumbani. Anaokolewa na Mtawa Pacha anapata utulivu uk100
- Chandachema anapata utulivu baada ya kuokolewa na shirika la kidini la hakikisho la haki na Alikuwa mtoto wa mwalimu wa Fumba na Rehema ambaye alizaliwa nje ya ndoa kati ya mauhusiano ya mapenzi ya mwalimu na mwanafunzi wake. Anakosa malezi mema na madhila ya unyanyasaji wa kijinsia uliosababishwa na bwana Tenge.uk 107
- Uk 127 Mwangeka wanapomuaga binti yao Umu alimwambia kuwa siku ile tuliyokuja kukuchukua kwa mwalimu Dhahabu ilikuwa siku ya heri
- Dick alimweleza Umu kuwa siku waliokutana katika uwanja wa ndege na wakasafiri pamoja, hiyo ndiyo ilikuwa siku ya heri zaidi kwake. Nasaha alizopewa na Umu zilimfunza thamani ya maisha. Kisadfa, huu ndio wakati Dick alikuwa ameamua kubadilisha maisha ya kuuza dawa za kulevya na kuamua kuuza vitu vya
- Baada ya Mwaliko kujitambulisha kwa Umu na Dick na kushukuru pia wao wanashukuru kupata walezi wazuri, umu na Dick hawakungojea Walikimbia wote wakamkumbatia ndugu yao,wakaanza kulia huku wakiliwazana. Sophie na Ridhaa pia walijiunga nao, wote wakalizana na baadaye wakashikana mikono. Ikawa ni hali ya utulivu. Uk 189
- Mwaliko alimwambia babake kuwa kuja katika hoteli ya Majaliwa kuliwaletea heri kwa kuwa familia yao sasa imepanuka. Sasa amekutana na watu aliokuwa tu anasikia Anasema kuwa imekuwa heri tena kuwa, uncle Mwangeka ndiye mzazi na mlezi wa ndugu zake. Uk 190
- Dick alitoa shukrani tele kwa Umu kwa kuwa ni yeye alimpa matumaini kuwa siku moja watampata ndugu yao Mwaliko hata anapomtazama Umu, macho
yake yakiwa yamefunikwa na vidimbwi vya machozi, anajua kuwa familia yao imerudiana japo katika mazingira tofauti.
- Mwangeka anapomtazama Apondi anamfurahia kwani yeye ndiye anayempa utulivu wa Hapo kabla babake aliishi kumwambia aweze kumtafuta mpenzi na kumuoa ila aliishia kusema kuwa alishindwa kumsahau Lily na Becky. Hata hivyo, Ridhaa alijua kuwa wakati ndio mwamuzi, ipo siku atakapotokeza hurulaini wake Mwangeka. Ataifungua kufuli kubwa iliyoufunga moyo wake na hiyo itakuwa siku ya kumwaga chozi la heri
2) MTIRIRKO WA VITUSHI
SURA YA KWANZA
Sura hii inaanza kwa kumrejelea mhusika, Ridhaa ambaye alikuwa amesimama kwa maumi-vu kwa yaliyompata. Amelitazama wingu la moshi ambalo lililojikokota kwa kedi na mbwembwe, aidha linamkumbusha ukiwa aliozaliwa nao na ambao anahofia kuwa angeishi na kuzikwa nao. Alipogeuka alitazamana ana kwa ana na tanuri la moto ambalo liliteketeza jumba lake la kifahari. Katika mkasa huu wafuatao waliangamia Terry mkewe Ridhaa, bintiye Tila, LilyMkewe Mwangeka na mjukuu wake Becky.
Ridhaa anatatizika sana na milio ya kereng’ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kinyama. Milio hii ilimtia kiwewe aidha alijaribu kumjuza mkewe ila alipuuza kwa kumwambia kuwa yeye ndiye ameishi kumwambia kuwa asishikamane na mambo ya ushirikina anamkumbusha Ridhaa kuwa aliwahi kumwambia kuwa ni vizuri kuiacha mielekeo ya kijadi ambayo huyafifilisha maendeleo. Anazidi kumuuliza hata iwapo jambo likawa atafanya nini? Ndipo Terry anamjuvya kuwa la muhimu ni kumlaani shetani kwani Iiandikwalo ndilo
Mazungumzo haya baina ya Terry na mmewe Ridhaa yalikuwa ya mwisho kabisa kutokea Terry akiwa hai. Ridhaa anatamani kuwa alikuwa na muda zaidi wa kumuuliza mkewe maswali ambayo sasa yameivamia akili yake. Machozi yalifurika machoni mwake kwa yale yaliyompata. Katika kumbukizi zake anakumbuka maneno ya marehemu mamake kuwa machozi ya mwanamme hayapaswi kuonekana mbele ya majabali ya maisha. Ila Ridhaa aliacha machozi yamcharaze yatakavyo hakujali la mama wala la baba; alijisikia kama mpigana masumbwi aliyebwagwa na kufululiziwa makonde bila mwombezi.
Anakumbuka mambo yalivyokuwa usiku huo, ambao uliyatia giza maisha yake. Anakumbuka mayowe ya mkewe akimsihi Mzee Kedi asiwauwe kwani wao ni majirani wake. Baada ya mayowe haya ndipo alisikia mlipuko mkubwa kisha akashikwa na uziwi wa muda uliofuatwa na sauti nyingine ya Mkewe “Yamekwisha”. Kumbukumbu hii ilimpa kuzimia na alipozinduka alijipata kalala kando ya gofu la jumba lake lililokuwa linafuka moshi.
Ridhaa anakumbuka jumba lake ambalo sasa ni majivu familia yake na mali yote hii kuteketea kwa siku moja . Anaporudi kulikokuwa sebule ndipo alikumbuka kuwa Mwangeka
-kifungua mimba wake alizaliwa kwenye chumba hiki miaka thelathinl iliyopita. Alishangaa ni vipi Mwangeka aliweza kunusirika mkasa huu na ndipo akawaza kuwa wadhifa aliopewa kwenda Mashariki ya Kati kudumisha amani ulitokea kuwa wongofu wake. Katika kumbukumbu zake anaukumbuka mjadala mkali baina yake na bintiye Tila kuhusu mafanikio ya baada ya uhuru. Tila anaonekana mwenye tajriba ya uanasheria kwani masuala aliyozua yalikuwa motomoto .Tila kupitia maswali ya Tila ni wazi kuwa baada ya kuondoka kwa mkoloni mweupe mkoloni mweusi aliweza kuchukua hatamu. Tila anaonyesha vilevile kuwa licha ya kuondoka kwa mzungu waafrika wanaendelea tu kuwa wategemezi si kwa lishe tu, bali pia kwa ajira. Na kazi zenyewe ni vibarua vya kijungu jiko. Tila alishangaa ni kwa nini wao hawajaanza kujisagia kahawa au chai yao. Haihalisi mbegu ziwe zetu, tulikuze zao lenyewe kisha kumpelekea mwingine kwenye viwanda vyake alisage kisha kuja kutuuzia hiyo kahawa au chai kwa bei ya kukatisha tamaa alisisitiza Tila.
Ridhaa anamkumbuka baba yake Msubili na mtazamo wake kuwa jamii yao iligeuka kuwa hazina ya wafanyakazi ambamo Wazungu wangeamua kuchukua vibarua kupalilia mazao yao. Aidha tunarifiwa kuwa hakuwa mkaazi asilia wa Msitu wa Heri.Alikuwa wa mfuata mvua kama walivyoitwa walowezi na wenyeji kindakindaki. Babake alikuwa na wake kumi na wawili. Wake hawa walijaliwa na wana wa kiume ishirini na ndipo ardhi ya mzee Mwimo Msubili ikawa haitoshi kuwalea madume hawa. Jambo hili limfanya mzee mwimo kuwahamishia wake wawili wa mwisho Msitu via Heri . Siku hizo ilikuwa rahisi mtu kuwa na shamba mahali kokote katika eneo lililomilikiwa na kabila lake kwani umiliki wa mashamba ulitegemea bidii ya mtu.
Mamake Ridhaa alikuwa mke wa mwisho wa Mzee Mwimo. Ridhaa alikuwa mwenye umri wa miaka kumi walipohamia Mlima wa Heri na alikuwa bado hajaanza shule. Walipowasili humu hamkuwa na wakaazi wengi na ilimchukua muda kuzoeana na watoto wa majirani ambao waliwaona Ridhaa na nduguze kama waliokuja kuuvuruga utulivu wao.
Ridhaa alikuwa kati ya waathiriwa wa hali hii kwani alitengwa na wenzake siku ya kwanza shuleni katika michezo mbalimbali. Alichokozwa na mwanafunzi mmoja aliyemwita ‘mfuata mvua’ na kumwambia hakutaka kucheza naye kwani alikuja kuwashinda katika mitihani yote. Ridhaa hakungoja mwezake amalize dukuduku lake alichukua mkoba wake na kufufuliza moja kwa moja hadi nyumbani na kujitupa mchangani huku akisema hangerudi hiyo shule tena. Mamake Ridhaa alizungumza na mwalimu naye mwalimu akazungumza na wanafunzi na kuwasisitizia umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano. Huu ukawa ndio mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa.
Baadaye Ridhaa alimuoa Terry. Alijaliwa na wana ambao waliangamia isipokuwa Mwangeka kifungua mimba. Ridhaa anashangaa ni kwa nini Mzee Kedi alimgeuka kwani ndiye aliyemsaidia kupata shamba hilo lake. Familia zote mbili zilikuwa na mlahaka mwema. Ridhaa ameyafanya mengi mazuri kikijini hadi kikaacha kuitwa Kalahari. Ikawaje aliowatendea hisani wamelipa kwa madhila? lweje watu waliokula na kunywa pamoja ndio waliomlipulia aila na kuyasambaratisha maisha yake? Haya maswali yasiyo na majibu yalimsumbua akilini mwake. Alipowaza alianza kuelewa sababu ya vikaratasi kuenezwa kila mahali vikiwatahadharisha kuwa mna gharika baada ya kutawazwa kwa Musumbi- kiongozi mpya. Anaelewa sababu ya jirani kuacha kumtembelea kwake kwa ghafla. Anaelewa sababu ya mke wa jirani kulalamika kuhusu kuuzwa kwa mashamba ya wenyeji kwa wageni. Alielewa kuwa alikuwa mgeni wala si mwenyeji hata baada ya kuishi pale miongo mitano.
Katika usingizi alikumbuka habari iliyosomwa katika runinga miaka miinne iliyopita. Habari ilyosababisha kubomolewa kwa majumba yake matatu yakibomolewa. Majumba haya sasa yamegeuka udongo. Pigo hili la pili aliliona kali zaidi. Alibaki akijiuliza maswali akishangaa ni upi utakuwa mstakabali wake, wa mwanawe Mwangeka na Subira, dada yake Ridhaa aliyeishi maili kumi kutoka pale.
Maswali ya ziada:
- ‘’ kwamba liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny?’’ i)Eleza muktadha wa dondoo
- onyesha ukweli wa kauli hiyo
- eleza wasifu wa nafsineni
- Umekuwa kama jani linalopukutika msimu wa machipuko!
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Eleza madhara ya ukosefu wa amani
- Hata hivyo wengi wa mabwenyenye hao walipuuza notisi hii
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Onyesha mbinu iliyotumika na uipigie mifano zaidi kutoka kwa riwaya
SURA YA PILI
Sura hii inaanza watu wakiwa katika kambi za ukimbizi katika mazingira haya mageni ila si mageni kwani ni mumo humo kwao kwani si ughaibuni wala nchi jirani. Watu wa kila tabaka walikuwa yaani waliokuwa nacho na wachochole wote wako pamoja katika kambi hii. Kuna kiasi fulani cha usawa. Aidha inaaminika kuwa wanadamu huwa na tofauti ya mandhari wanamofia. Kuna wanaofia zahanati za kijijini na wapo wanaolala maumivu yao yakiwa yamefishwa ganzi katika hospitali za kifahari huku wakiliwazwa na mashine. Kuna wengine ambao hufia kwenye vitanda vya mwakisu vitongojini baada ya kupiga maji haramu.
Katika kambi hii watu wanang’ang’ania chakula haswa uji. Hata aliyekuwa waziri wa Fedha miaka mitano iliyopita yumo katika kambi hii aking’ang’ania chakula na wenzake. Mvua kubwa inanyesha na matone mazito kuwaangukia wanawe wakembe wa Ndugu Kaizari- Lime na Mwanaheri. Hana hata tambara duni la kuwafunikia. Kaizari anabaki kumshukuru Mungu tu kuwa wako hai. Ubavuni amelala mke wake Subira ambaye haihalisi kumwita mkewe kwani uso wake ulikuwa umevamiwa na majeraha.
Ukosefu wa chakula unasababisha Ridhaa, Daktari, Mkurugenzi mzima wa Wakfu wa Matibabu nchini kula mizizi. Tunarifiwa Kaizari anaanza kusimulia yaliyojiri siku ile baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya kana kwamba Ridhaa alikuwa mgeni wa haya. Anasema kuwa baada ya kutawazwa kwa kiongozi mwanamke mambo yaliharibika. Watu wakashika silaha kupigania uhuru wao, uhuru ambao walidai hawakupewaWakaupigania. Mwanaharakati Tetei alitoa kauli kuwa, wanaume watatumikishwa kwa walivyofanywa enzi hizo katika visakale vya majirani wao walipokuwa wakiongozwa na mwanamke wa kiimla . walikerwa na haki za jinsia ya kike kama vile; Affirmative action na a third should be Women. Bi. Shali alionekana kuwakosoa wapinzani wa Mwekevu kwa kile aliona kuwa
Mwekevu alistahili ule ushindi kwani alijitosa katika siasa na kuomba kura kama wanaume
, akastahimili vitisho na matusi aidha anashangaa jinsi watu ni wasahaulifu wa mradi wa kuchimba visima ambao umewafaidi sana.
Kaizari aliendelea kumsimulia Ridhaa chanzo cha vita kuwa vilianza kati ya kundi la wafuasi wa Mwekevu na lililokuwa likiunga mkono mpinzani wake mwanamume Vita vikachacha kwani wapinzani walikidai kuwa haingewezeka mwanamke kushinda mpinzani wake mwanamume na badala yake waliiba kura na wafuasi wake kuwanunua wanawake ambao ndio wapiga kura wengi.Aidha wafuasi wa Mwekevu waliona huu ndio muda mwafaka wa Mwekevu kupewa nafasi ili alete mabadiliko. Athari ya vita hivi ilikuwa ni pamoja na ;
- watu kuuawa, kuacha makwao na kukimbilia maisha yao
- kupotesa mali kwani waliokimbia makwao kila walichokiacha kiliteketezwa
- kupora maduka ya Kihindi, kiarabu na hata Waafrika wenzao
- Misafara ya wakimbizi ikawa kwenye barabara na vichochoro vya Wahafidhina
- Mizoga ya watu na wanyama
- magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa moto
- uharibifu wa mali na
- Nyimbo za uchochezi mpinzani wa Mwekevu anambiwa tawala wahafidhina , mwanzi wetu tawala.
- Kuchomwa kwa magari kana kwamba ni mabiwi ya taka
- Vilio kwa waliokuwa wakiteketezwa
- Kubakwa kwa mabinti wa Kaizari yaani Lemi na Mwanaheri
- Askari wa fanya fujo uone kuwafyatulia risasi vijana walioamua kufa
- Magonjwa ya homa ya matumbo
- Njaa na ukosefu wa maji safi
- Kukimbilia chakula kwa watu wazima jinsi wafanyavyo watoto
Aidha Kaizari anaeleza jinsi ambavyo alivamiwa kwake kubishiwa hodi, mke wake Kaizari, Subira akaenda kufungua, huku akisalimiwa kwa kofi. kubwa kisha akaulizwa alikokuwa kidume chake kijoga. Alipigwa mikato miwili ya Sime hata kabla hajajibu lolote, akazirai kwa uchungu. Baadaye genge lile likawabaka mabinti wake Kaizari. Mahasimu hao wakaondoka baada ya kuutekeleza unyama huo bila kumgusa Kaizari, auguze majeraha ya moyo. Alijizatiti na kuwapa wanawe na mke wake huduma ya kwanza ni katika pilka pilka zile, sauti ya Jirani yao Tulia iliita ikiwasihi kutoka iwapo walitaka kuishi. Tulia alimsaidia Kaizari kufunganya na kumsindikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake. Akamjuvya kuwa uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja. Akamshauri aihamishe aila yake kwa muda kwa sababu ya usalama. Akamhakikishia kuwa huo sio mwisho wa kuonana. Huu utakuwa mwanzo wa uzao wa jamii mpya isiyojua mipaka ya kitabaka, jinsia na kikabila. Jirani alipompungia mkono,
Familia ya Kaizari iliweza kuabiria matwana iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi kana kwa inakimbizwa. Waliyashuhudia mengi katika safari hii ya shaka kama vile mabasi kuchomwa
. Baadaye, gari lilikwisha petroli ikawa sasa ni mtu na malaika wake. Walijitoma msituni, usiku wa kwanza wakila mate kutokana na ule ugeni wa kutojua hata kuliko na matunda mwitu. Aidha anasema kuwa walibahatika kwani ni katika msitu huo mto wa mamba ulipita ila Kulikuwa na changamoto ya maji safi ya kunywa kwani maji hayo hayakuwa safi ya kunywea.
Wakimbizi hao waliweza kujenga vibanda ambavyo viliezekwa kwa nyasi na kukandikwa kwa udongo. Wengi walipata homa ya matumbo na wengine kuyapoteza maisha yao. Wakimbizi walizidi kuongezeka nayo hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu. Idadi kubwa ya wakimbizi ilifanya kuwe na vyoo vya kupeperushwa- yaani sandarusi ambazo hutumiwa kama misalani. Siku za mwanzomwanzo Kaizari hakuweza kutumia misala hii, lakini alisalimu amri na kusema potelea mbali, lisilo budi hutendwa. Lakini kutokana na tishio Ia maenezi ya kipindupindu aliwasihi kuchimba misala kwa jina long drop. Tatizo la njaa pia lilishamiri kwani waliokuwa wamebahatika kubeba nafaka chache walizitoa zikatumiwa na wote, zikaisha.
Siku ya kumi na tano Selume mke wa mpinzani wa msumbi mwekevu alipitia kwenye kibanda cha Ndugu Kaizari. Selume alikuja kuwaeleza kuwa alikuwa amesikia fununu kuwa
upo mradi wa kuwakwamua Wakimbizi kutokana na hali hii. Shirika la Makazi Bora, lilikuwa limejitolea kuja kuwajengea wakimbizi nyumba bora. Misikiti na makanisa yalikuwa yamekusanya vyakula ili kuwalisha wahasiliwa. Watu walijawa na matumaini. Siku ya ishirini lori kubwa liliingia na watu wakakimbilia chakula kama watoto wafanyavyo. Watu waligawiwa chakula na akina mama – wa Mother’s union, woman’s Guild na waliokuwa wamepakiwa nyuma ya lori hilo. Msukumano ulianza hadi mlinda usalama mmoja alipojitokeza na kuwasihi kuweka usalama. Watu wengine kama Mzee Kaumu walishangaa walipokuwa hawa wangwana wakati madhila haya yalipowapata. Kwa kuwa tabia ni ngozi, Bwana Waziri Mstaafu aliyekuwa na uzoefu wa kuwaelekeza watu huko wizarani, alisaidia kukigawa chakula. Pia Kaizari na Selume waliitwa kusaidia. Hata hivyo, bwana Kute alifanya ujanja ili kupata mafungu zaidi. Mwandishi anaonyesha hali ya ufisadi ya juu kwa kusema kuwa hata chakula cha msaada , kilicholetwa kwenye madhabahu ya kidini , kinaweza kufisidiwa.
Maswali ya ziada:
- “ Sasa ana haki gani ya kutuomba kudumisha utulivu baada ya kuivuruga yeye na wenzake?’’
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Eleza madhara ya vita katika jamii
- ‘’ Ni sandarusi ambazo hutumiwa kama misala bwana’’
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Eleza sifa na umuhimu wa msemaji
- Eleza ukweli wa kauli hiyo
- ‘’ Sasa ni wakati wa kila mtu na malaika wake’’
- Eleza kilichofanya nafsineni kusema maneno hayo
- Jamii ya wahafidhina matatizo ya baada ya uchaguzi ni kioo cha bara Afrika
SURA YA TATU
Sura hii inaanza kwa kuonyesha Ridhaa akiwa ameketi katika chumba cha mapokezi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Rubia. Ana hamu kuu ya kumwona Mwangeka akiwa mzima. Macho yake ameyatunga kwenye dari ya chumba hiki. Anagota sakafu kwa viatu vyake kana kwamba anataka kupata habari fulani kutoka kwayo. Ridhaa anakumbuka kuwa siku ya kuhawilishwa kutoka Msitu wa Mamba baada ya kukaa kule kwa miezi sita na kubahatika kurudi nyumbani kufuatia mradi wa operesheni rudi Kanaani, hakuwa na matumaini ya maisha bora kwani hakuwa na mwenzi wala mtoto wa kuendea.
Wengine kama Selume(mke wa mpinzani wa Mwekevu ) walikuwa wakilia kwa kuwa hawakujua waende wapi kwani mme wake amekwisha kuoa msichana wa kikwao na Babake alimkatalia katakata. Ridhaa alimfariji na kumwomba asilie kwani mwana wake yu hai tena ana kisomo na amehitimu kama mkunga, anaweza kujitegemea. Selume hakuwa ametoka katika jamii moja na mpinzani wa Mwekevu. Ndipo Ridhaa akamwahidi warudipo nyumbani, angemtambulisha Selume kwa mkuu wa Idara ya Afya ya Jamii katika Hospitali Kuu ya Tumaini na labda angepata kazi katika idara ile.
Hata , Ridhaa anapowaza haya, Selume amekwisha kuajiriwa kama muuguzi katika hospitali ndogo iliyojengwa karibu na kambi ya WWHN. Ridhaa anakumbuka mambo mengi kama vile kadhia iliyompoka familia yake ndiyo ilimkutanisha na watu kama Selume ambao angewaita ndugu na kumfanya kusahau msiba wa kuipoteza akraba yake. Kutangamana na wakimbizi kukamfunza thamani ya binadamu. Sasa amejifunza mengi kama Vile uzima ni upande mwengine wa mauti. Kwenye Msitu wa Mamba, Ridhaa alipata huduma za ushauri na uelekezaji kutoka kwa wataalamu mbalimbali na akaweza kuudhibiti ugonjwa wa shinikizo la damu ambao ulitokana na mshtuko wa kupoteza jamaa yake na mali yake dafrao moja.
Ridhaa alipotoka kwenye msitu wa mamba alikuwa mtulivu wa akili huku akijihisi kiumbe kipya kwani wapwa zake- Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu na dada yake Subira ametibiwa akapona. Mwamu wake Kaizari- amepona donda lilitokana na kuwaona binti zake wakibakwa. Ridhaa anamwona Kaizari ni afadhali kwani heri nusu Shari kuliko Shari kamili kama iliyompata kwa kupokwa familia yake yote.
Aidha anapomngojea mwanawe Mwangeka pale uwanja wa ndege , anapitiwa na kumbukumbu za jinsi alivyohisi aliporudi tena kwenye ganjo lake siku ile. Anakumbuka
kuwa alipozinduka alijipata pale pale katikati mwa kiunzi cha sebule lililokuwa kasri lake. Eneo hili ndipo wanawe Tila na Mwangeka walipokuwa wadogo walipenda kumkimbilia kila mara alipotoka kwenye shughuli zake za kikazi. Hapo ndipo kijukuu chake kilipozoea kutembea tata na kumwita “bubu” naye alipenda kukirekebisha na kukiambia “sema babuu”. Na kitoto kwa utukutu wa kitoto kingesema ‘’bubuuuu’’Hayo yote hayapo sasa, hata zile pambaja za mkewe Terry na utani wake hamna. Akiwa yu pale katika kumbukumbu zake, polepole kwenye jukwaa la akili yake kunaanza kuigizwa mchezo wa maisha yake kabla ya dhiki iliyomfika. Anamwona Tila akitoka shuleni na kuuweka mkoba wake juu ya meza. Katika mazungumzo yao mambo yafuatayo yanabainika;
- Tila alidhamiria kuwa siku moja atakuwa jaji katika mahakama kuu na kusafisha uozo
- Kuna washukiwa wengi rumande ambao wanahitaji haki ya kesi zao
- Kubadilika kwa mifumo ya uzalishaji mali kuanzia wakati wa ujimia, ukabila, ubwenyenye, ujamaa hadi sasa
- Kura ya maoni kuonyesha kuwa asilimia kubwa ilikuwa inamuunga mkono Mwekevu
- Tila anaonyesha amezinduka anasema kuwa wao hawahitaji kiongozi mwanamke ila kiongozi ambaye ataielekeza jahazi visiwa vya
- Tila anaonyesha kuna uongozi mbaya umaskini, ufisadi, ukosefu wa gharama za matibabu ya kimsingi na ukosefu wa lishe
- Kazi nyingi za serikali kupeanwa zabuni kwa kapuni za kigeni ambao wanajilimbikizia mali ya
Ridhaa aliona kuwa utabiri wa mwalimu wa Tila ulikuja kutimia kwani viongozi wa awamu ya awali walibwagwa chini na vijana chipukizi. Kinaya ni kuwa wengi walishindwa kabisa kukubali kushindwa hasa yule aliyekuwa akigombea kilele cha uongozi. Kulingana naye nafasi hii iliumbiwa mwanamume na kumpa mwanamke ni maonevu yasiyovumilika. Kiongozi huyu alipita kila mahali akitoa kauli ambazo ziliwajaza hamasa wafuasi wake nao wakaanza fujo zilizoangamiza juhudi za miaka hamsini za raia za kuijenga jamii yao.
Hatimaye ndege kwa jina PANAMA 79 iliyotarajiwa kufika saa tatu unusu sasa ndio inalikanyaga sakafu. Abiria waliposhuka, Ridhaa na Mwangeka walitazamana kimya. Ridhaa
alihisi kana kwamba anauona mzuka wa Mwangeka, hakuamini kuwa angerudi nyumbani akiwa hai. Hatimaye baada ya shaka kumwondokea, alimkumbatia mwanawe. Mwangeka akajitupa kifuani mwa babake kwa furaha. Ridhaa alimkaribisha Mwangeka nyumbani na kumtaarifu kuwa hakujua kuwa watawahi kukutana akiwa hai.
Ridhaa alimweleza mwanawe yaliyoisibu familia yao. Mwangeka alipomtazama babake akaona kuwa amekonga zaidi na sasa ameshabihi mno babu Mwimo. Baada ya kumbukumbu zake kumkumbusha ya awali Mwangeka alimshukuru babake na kumweleza kuwa alipoipata habari ya machafuko ya baada ya kutawazwa kwa kiongozi, alijawa na kihoro kisicho kifani. Aidha tunarifiwa kuwa , Mwangeka alikuwa akifuatilia matukio kwa makini kwani hata kura zilipohesabiwa upya kisha mpinzani wa Mwekevu kukubali kushindwa na kutoa wito kwa raia kusahau yaliyopita, alijua kuwa nchi imepiga hatua moja katika safari ndefu ya kupata afueni kutokana na tufani za baada ya kutawazwa. Mwangeka aliendelea kuwapa heko vijana wenzake kwa kugundua kuwa wanatumiwa vibaya na viongozi wenye tamaa.
Mwangeka akawa sasa anakubaliana na usemi wa Tila kuwa “usi cheze na vijana, wao ni kama nanga. Huweza kuizamisha marikebu ” Japo Ridhaa aliyaitikia maneno ya Mwangeka kwa mgoto, alijua kuwa palikuwa na kazi ngumu ya kujenga upya ukuta ambao ufaa wake ulikuwa umepuuzwa. Akawa anakubaliana na sera ya bintiye marehemu, Tila kuwa Vijana wanafaa kuelimishwa zaidi kuhusu amani kwani ndio wengi na ndio mhimili wa jamii yoyote ile. Hatimaye, Ridhaa alishusha pumzi na kumkabidhi mkono mwanawe na kumtaka waende ili akajipumzishe kutokan na adha za anga Mengine watazungumza baadaye.
Maswali ya ziada:
- Ni kweli, lakini kumbuka kampuni hizi zimebuni nafasi za
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Taja tamathali za usemi zilizotumika
- Jadili umuhimu wa nafsinenewa
- Jadili mbinu ya kinaya, kisengere nyuma na semi zilivyotumika katika sura
- FOR MORE RELATED LEARNING MATERIALS, 0714497530
- ‘’ Usilie mwenzangu’’
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Eleza kinachomliza nafsinenewa SURA YA NNE
Mwandishi anatuonyesha Mwangeka akiwa ameketi mkabala mwa kidimbwi cha kuogelea, nje ya jumba lake la kifahari ambalo yeye aliliona kama makavazi ya kumtonesha donda lililosababishwa na kifo cha mke wake Lily Nyamvula. Siku ile baada ya kutoka kwenye uwanja wa ndege walifululiza moja kwa moja hadi kwenye gofu la baba yake Ridhaa. Majivu yaliyokuwa mabaki ya kilichokuwa kwenye kasri lile yalibaki pale pale. Majivu hayo miili ya mama yake yaani Terry, wanuna wake Tila na Mukeli, mkewe lily na mtoto wake Becky.
Mwangeka hakuelewa ni kwa nini babake hakuyaondoa mabaki hayo na ni kwa nini hakushirikiana na majirani kuchimba kaburi la jumla (mass grave) kuyazika majivu hayo. Baba mtu alimkazia tu macho. Machozi mazito ya machozi yalitunga machoni mwa Mwangeka, akayaacha yamcharaze yatakavyo. Wakati huu hata nyanya yake angekuwapo kumwonya dhidi ya kulia kama msichana angempuuza. Alihitaji kulia ili kuliondoa komango ambalo lilikuwa limefunga mishipa ya moyo wake. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa machozi haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani akali. Kilio cha heri.
Mwangeka akakumbuka methali isemayo wino wa Mungu haufutiki. Methali hii ambayo mpinzani wake aliishi kumtolea kila mara Mwangeka alipomshinda. Sasa ndio Mwangeka anauona wazi ukweli wa methali hiyo. Hata hivyo alizidi kujiuliza iwapo binadamu aliandikiwa kumpoka binadamu mwenzake uhai.
Siku ile baada ya wao kutoka kwenye uwanja wa ndege, Ridhaa alimwelezea Mwangeka mambo yalivyojiri. Alimweleza kuwa maisha yalibadilika Pindi tu Mwangeka alipoondoka. Waliandamwa na msiba baada ya mwingine. Mwanzo, Ridhaa akapoteza majumba yake mawili. Miezi mitatu baadaye ami yake Mwangeka aliyeitwa Makaa alichomeka asibakie chochote alipokuwa aakiwaokoa watu ambao walikuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori lililokuwa limebingiria. Makaa alizikwa pamoja na mabaki ya wahasiriwa wote katika kaburi moja kwani serikali iliwatayarishia mazishi ya umma.
Baada ya Ridhaa kushusha pumzi, aliendelea kumweleza Mwangeka kuwa mambo hayo yote aliyakabili kwa msaada wa wanuna wa Mwangeka, mamake Mwangeka na mkaza mwanawe. Akaanza kuyajenga upya maisha yake hadi Siku ile ambayo aliitazama familia nzima ikimponyoka. Daktari Ridhaa anakumbuka jinsi ambavyo amewaokoa wagonjwa
wengi kutokana na magonjwa sugu lakini siku hiyo alishindwa kuuzima moto uliokuwa ukiiteketeza nyumba yao. Lakini, hakushindwa kwani hakuwepo tendo lenyewe likitendeka. Alikuwa ameenda kumfanyia majeruhi mmoja upasuaji. Ridhaa alipokuwa akirejea nyumbani akasikia sauti ya kite ya mamake Mwangeka, kisha mlipuko mkali. Yote yakaisha. Hadi hapo, ameyaishi maisha ya kinyama kupigania chakula na wahitaji wenzake. Ameonja shubiri ya kuwa mtegemezi kihali na mali.
Lakini katika hayo yote amejifunza thamani ya maisha, udugu na amani. Alimhurumia Mwangeka ambaye mkasa huo ulimfanya mjane hata kabla ya ubwabwa wa Shingo kumtoka. Baada ya kurejea kwake Mwangeka hakuishi na babake kwa muda mrefu. Mwanzo, hakuweza kustahimili uchungu uliosababishwa na kuamka kila asubuhi kutazama mahali ilipoangamia aila yake. Alimrai babake kila siku akibomoe kiunzi kile cha nyumba lakini babake alikataa katakata. Lilikuwa kaburi la ukumbusho wa familia yake. Sababu ya pili ni kuwa lazima Mwangeka angeyaanza maisha yake upya. Atafute ushauri kutoka kwa wataalamu, auguzie moyo wake mbali na babake.
Mwangeka aliporejelea shughuli zake za kawaida kazini alitafuta kiwanja cha kujengea nyumba. Babake akamtahadharisha kufanya uchunguzi kabla ya kuanza ujenzi wenyewe. Baada ya Mwangeka kuhakikisha uhalali wa stakabadhi alipata kipande cha ardhi karibu na ufuo wa bahari. Kazi ya ujenzi ilianza na baada takriban mwaka mmoja na unusu akahamia kwake. Hata anapokitazama kidimbwi hiki, mawazo yake yako mbali alikoanza maisha. Anazikumbuka changamoto za ukuaji wake. Anawakumbuka wanuna wake: Kombe, Mukeli na Annatila(Tila). Anapomkumbuka Tila anatabasamu kisha tone moto la chozi linamdondoka. Kumbukumbu ya Annatila inavuta taswira ya mnuna wake mkembe Dede aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka sita wakati ule Mwangeka akiwa na umri wa miaka kumi na miwili tanzia ile ilipowafika.
Katika jamii ya Mwangeka, kifo kilifuatwa na viviga vya aina mbalimbali yakiwemo maombolezi. Basi baada ya kifo cha mtoto huyo majirani walikuja kuifariji familia ya Bwana Ridhaa. Wiki mbili baada ya mazishi ya ndugu yake, Jumamosi moja Mwangeka alimpata Tila na wenzake nyuma ya nyumba wakimngojea. Tila alimvuta na kumnong’oneza kitu sikioni kisha akavuta boksi lililokuwa limetiwa mwanasesere wao kwa jina Dedan Kimathi lakabu waliokuwa wamempa marehemu ndugu yao. Walianza kulia na kuomboleza kifo cha Dedan Kimathi. Wakaimba mbolezi. Katika hali ile ya kuomboleza, watoto hawa hawakujua kuwa baba yao alikwisha kuja dakika thelathini zilizokwisha. Akawa anawatazama watotohawa wakiigiza mazishi ya ndugu yao Dede.
Alibanwa na hasira na kuutwa mshipi wake kutoka kiunoni, akamshika Mwangeka na kumwadhibu vikali. Akamkemea Mwangeka kwa kuwa bendera inayofuata upepo badala ya kuwa kielelezo bora kwa mnuna wake Tila. Mwangeka anapokumbuka kisa hiki anajutia ni kwa nini hakukiomboleza kifo cha Tila. Baada ya kipigo hiki, Mwangeka aliwajibika zaidi akayavalia masomo yake njuga hadi chuo kikuu ambako alisomea uhandisi. Hapo ndipo alipokutana na mke wake Lily Nyamvula. Nyamvula alikuwa akisomea uanasheria. Mwangeka alihitimu masomo yake na kujiunga na kikosi cha wanamaji, jambo hili liliwashangaza wengi kwani ungewauliza marafiki wa chuoni wa Mwangeka wangekuambia Mwangeka ksajiunga na vikosi vya usalama na kuipoka taaluma ya uhandishi. Hata hivyo, Mwangeka alitamani kutoa huduma yake ya uhandishi katika vitengo vya usalama.
Mwangeka anakumbuka kuwa mkewe Lily Nyamvula alipingana na hatua ya Mwangeka. Kwake kazi ya askari ilikinzana na imani yake hasa kwa vile Nyamvula alikuwa born again. Alishikilia kuwa haihalisi muumini wa kweli kumpoka binadamu mwenzake uhai. Hata hivyo alipoona kuwa msimamo wa Mwangeka hautetereki, aliridhia shingo upande. Mwangeka anajuta kama angesikiza ushauri wa mkewe angeweza kuiokoa aila yake na kumwona mwanawe ambaye aliwahi kumwona tu kwa picha ambazo tausi wake alimtumia.
Maswali ya ziada:
- ‘’ msiba huandamwa na mwingine”
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Eleza mikasa yote aliyoelezewa msemewa
- “ mwenye macho haambiwi tazama’’
- Eleza yaliyokuwa yakitazamwa
- Eleza maudhui ya kazi, ukabila na elimu
- Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wa sura hii
- ‘’Umewaacha na ndugu kwa ukiwa”
- Tia dondoo katika muktadha wake
- Eleza tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo
- Eleza umuhimu wa mbinu ya nyimbo ilivyotumika katika sura hii
SURA YA TANO
Msitu wa Mamba uligeuka kuwa nyumbani kwa maelfu ya watu waliogura makwao bila tumaini la kurudi. Walijipa moyo na kusema kuwa hata walikokuwa wakiishi hakukuwa kwao, walikuwa maskwota. Wakaamua kula asali na kuyanywa maziwa ya Kanaani hii mpya isiyokuwa na mwenyewe. Matokeo ya maamuzi haya yalikuwa kukatwa kwa miti kwa ajili ya kupata mashamba ya kupandia vyakula na kwa ajili ya ujenzi. Kabla ya miaka miwili kuisha, pahali hapa palikuwa pamepata sura mpya- majumba yenye mapaa ya vigae, misitu ya mahindi na maharage, maduka ya jumla, viduka vya rejareja kila mmoja akijibidiisha kufidia kile alikuwa amepoteza. Familia ya Bwana Kangata ilikuwa miongoni mwa zile zilizoselelea(zilizoishi) kwenye msitu huu. Kwa Kangata na mkewe Ndarine hapa palikuwa afadhali. Awali wakiwa wamelowea katika shamba Ia mwajiri wao aliyekuwa akiishi jijini. Waliishi pale kwa muda mrefu hata watu wakadhani kuwa ilikuwa milki yao.
Wengine wakidhani Kangata na familia yake walikuwa akraba ya mwajiri wao. Hata wana wa Kangata walipokwenda shuleni walijisajilisha kwa jina Ia tajiri wa baba yao. Walikuwa wakiitwa Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri. Kiriri likiwa jina Ia Mwajiri wa Kangata. Kangata na mwajiri wake walikuwa wamesekuliwa kutoka mtaa wa Matunda katika zile patashika za baada ya kutawazwa. Kiriri aliiaga dunia muda mfupi kutokana na kihoro cha kufilisika na ukiwa aliokuwa ameachiwa na mkewe Annette na wanawe. Walipata Green Card na kuhamia ughaibuni. Hivyo basi, juhucii za Kiriri kumshawishi mkewe asimnyime ushirika wa Wanawe ziliaangukia moyo wa Firauni. Mkewe Kiriri alikuwa ashaamua kuwa hapa hapamweki tena. Kazi aliyokuwa akiifanya katika afisi za umma kama mhazili mwandamizi kwa miaka mingi ilikuwa inamfanya kusinyaa, akawa hana hamu akahisi kinyaa. Wanawe walipoenda kusomea Ng’ambo – wafanyavyo wana wa viongozi kwa kuwa wanaiona elimu ya humu kama isiyowahakikishia mustakabali mwema raia wake, yeye alistaafu mapema na kuchukua kibunda cha mkupuo mmoja almaarufu Golden Handshake akachukua Green Card na kuwafuata na kumwacha mume wake akiwa mpweke. Baada ya wana wa Kiriri kumaliza masomo yao walibakia huko huko Uzunguni kufanya kazi.
Walipuuza rai ya baba mtu ya kurudi nyumbani ili kuziendesha baadhi ya biashara zake. Kila mmoja akajishughulisha na mambo yake. Kifungua mimba wa Kiriri kwa jina Songoa alisema kuwa nchi yao haina chochote kumfaa kwa hata walio na shahada tatu bado wanalipwa mshahara mdogo sana, akaona heri awekeze huko mbali aliko na imani nako.
Kabla ya kifo chake, Kiriri alikuwa akiibua mijadala nafsi akilini mwake kuhusu Waafrika ambao ni kama waachao mbachao kwa mswala upitao. Akawa anajiuliza maswali mengi kama vile ni nini huwavutia raia kuhamia ughaibuni? Je ni hiyo mishahara minono wanayolipwa? Je, ni hizo kazi za kujidhalilisha za kwenda kuwauguza maajuza waliotelekezwa na aila zao? Au ni zile ndoa kati ya vijana wakembe wa Kiafrika na vikongwe vilivyochungulia kaburi? Kiriri aliendelea kushangaa ikiwa mkewe amegeuka wale wake pindi wafikapo ng’ambo hufunga ndoa na waume wengine kwa kuwa ndio njia pekee ya kuufukuza upweke na kupata riziki au kwa kutaka kujikwamua kwenye tope la uhawinde?
Kutokana na uzoefu wake katika kilimo, Kangata alipofika katika Msitu wa Mamba aliweza kuendeleza kilimo chenye natija. Kwa sasa, miaka mitano imepita na Kangata na Ndarine wameipa dunia kisogo. Lucia Kiriri-Kangata ameolewa katika ukoo wa Waombwe ambao awali walikuwa maadui sugu wa ukoo wa Anyamvua. Ndoa hii ilipata pingamizi sana kutoka kwa ukoo mzima lakini kutokana na Msimamo imara wa Kangata ndoa hii ilisimama.
Watu wa ukoo wa kina Kangata walishangaa ni kwa nini mwana wao akaozwa kwa watu ambao huvaa nguo ndani nje na pia huzaa majoka ya mdimu ambayo ni machoyo kupindukia. Kangata aliyatupilia maneno ya watu wa ukoo wao kwani Kiriri aliyadhamini masomo ya mabinti zake hata ingawa walikuwa wa ukoo tofauti na wake. Watu wa ukoo wa Kangata walikuwa wakipinga elimu ya msichana na kutoa rai kama kumuelimisha msichana ni kufisidi raslimali. Kangata anashangaa wakat mwanawe amelimika na kuishi maisha ya heri ndio wakati jamaa zake wameona tofauti za kiukoo. Hatimaye ukoo wa Kangata ulikubali muungano huu wa ndoa na ukawa umeyeyusha tofauti na chuki iliyokuwa baina yao. Nasaba hizi mbili zikawa sasa zinapikia chungukimoja.
Naye Akelo Kiriri-Kaango habari yake haijulikani. Baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne, alipata kuolewa na dereva wa malori yanayosafirisha bidhaa hadi Zambia. Jina la dereva huyo ni Kaango. Alipomwoa Akelo Kiriri, alimjengea nyurnba katika gatuzi la Mbuyuni na tetesi zinasema kuwa walipata watoto wawili. Mmoja kwa jina Ngaire na mwingine Mumbi. Hakuna ajuaye walikopelekwa na misukosuko ya miaka mitano iliyopita.
Lunga Kiriri — Kangata ndiye anaishi katika milki ya babake katika Msitu wa Mamba. Yeye amesomea kilimo. Awali alikuwa ameajiriwa kama afisa wa kilimo nyanjani. Alikuwa akiwaelimisha raia kuhusu mbinu bora za kilimo kama vile watu wasilime karibu na mito, watu wachimbe mitaro kuzuia mmonyoko wa udongo na watu wapande miti inayostahimili ukame. Alikuwa amirijeshi wa uhifadhi wa mazingira. Alipokuwa shuleni ndiye aliyekuwa
mwasisi wa chama cha watunza mazingira wasio na mipaka.
Kila ijumaa wakati wa gwaride ungemsikia akihutubia wanafunzi wenzake kwa mhemko.Kimondo (mwanafunzi mwenzake Lunga) alikuwa haishi kushangazwa na I-unga kwani mtu akimsikiliza Lunga hangedhani kuwa amekulia mazingira sawa na wale wanyonge ambao uwepo wao huamuliwa na matajiri. Ilishangaza kuwa Lunga hakuwazia kwamba alikolowelea baba mtu palikuwa msitu tu, tajiri wake akapabadilisha. Babake Lunga haswa ndiye aliyeliendeleza shamba lile. Aliendelea kumuuliza iwapo hajui kwamba umaskini unaweza kuupujua utu wa mtu akatenda hata asivyokusudia kutenda. Iunga hangeweza kujua kwani hajawahi kulala njaa akakosa usingizi kutokana na mkato wa njaa ilhali baba mtu anavuna kahawa katika shamba kubwa Ia Mzungu.
Mzungu huyu mwenye shamba akiwa anapata mamilioni ya pesa lakini anawapunja wafanyakazi wake kwa kuwalipa kishahara duni kiasi cha wao kushindwa kuwanunulia wana wao sare mpya. Kimondo anaendelea kumwambia mwenzake Lunga kuwa hajawahi kuamka asubuhi huku anakeng’etwa na tumbo na homa ya matumbo inamwandama. Mwalimu anapokupa barua ili ukatibiwe kwenye kituo cha afya kilichoko ndani ya kijiji ambacho mwenye kahawa amewajengea wafanyakazi, Daktari mwafrika anakataa kukupa huduma kwa kuwa wazazi wako hawajawekewa bima kutokana na kijishahara duni
wanacholipwa. Sasa Lunga ni mkulima stadi. Ametononokea si haba katika msitu huu. Hakumbuki kuwa msitu huu unafaa kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Kabla ya shida kumleta hapa mstakabali wa maisha ya Lunga ulitishia kuporomoka. Alikuwa ameipoteza kazi yake ya Ukurugenzi katika kampuni ya Maghala ya Fanaka alikopinga kitendo cha raia kuuziwa mahindi ambayo yalikuwa yameagizwa kutoka ughaibuni.
Mahindi ambayo licha ya kuwa na rangi ya njano, yalihofiwa kuwa yameharibika. Yalikotolewa yalisemekana kuwa hatari kwa usalama hata wa panya. Lunga alipopinga uuzaji wa mahindi haya kwa raia vijisababu vilitolewa na vigogo wenye shehena za mahindi haya. Walidai kuyakataa mahindi haya ni kama kuidhinisha kifo cha mamilioni ya raia ambao hawamudu kujinunulia hata kibababa cha unga. Hata hivyo, rai za wakubwa ziliambulia patupu kwani Lunga alikataa katakata.
Lunga akawa amehiari kupoteza kazi yake ili kuyaokoa maisha ya wanyonge wasio na hatia. Baada ya mwezi mmoja Iunga akiwa ofisini mwake alitumia barua ya kumstaafisha kwani shirika hili lilikubwa na changamoto ya kifedha na hivyo halmashauri ikachukua hatua ya kupunguza idadi ya wafanyakazi. Lunga alipoisoma barua hii mara mbili
alishangazwa na ukosefu wa fadhila wa waajiri wake. Kweli asante ya punda ni mateke. Lunga alipokuja katika Msitu wa Mamba alikuwa na azma ya kumhamisha babake na kuwachia wanyama Edeni pao lakini aliyoazimia siyo aliyotenda.
Lunga alipokutana na ekari thelathini na tano za mahindi aliingiwa na tamaa na uchu akausaliti uadilifu wake. Tamaa ya kulima maekari na maekari zaidi ikamkumbatia akakata miti zaidi. Alipoulizwa ilipofia jadhba ya kupigania uhifadhi wa misitu alisema mungu mwenyewe alitupa ulimwengu tuutawale, sio ututawale. Siku zilivyosonga, mashamba ya Lunga na wenzakeyakendelea kutoa mazao mengi nayo jamii ya Msitu wa Mamba ikazidi kupanuka nazo tofauti za kitabaka zikazidi kujionyesha. Kundi Ia kwanza la wakimbizi Ridhaa, Kaizari na Kangata hamkuwa na tofauti kubwa. Mpito wa wakati ukazaa matajiri kama Lunga ambaye alikuwa akiwakumbusha wenzake kuwa alitokana na jadi ya kifahari ya Kiriri. Kulikuwa pia na maskini ambao kupata kwao kulitegemea utashi wa matajiri. Polepole uhasama ulianza kutishiakuisambaratisha jamii ya Msitu wa Mamba.
Vlongozi nao kwa kuhofia mambo kuharibika, walianza kampeni za kuwaelimisha raia kuhusu umuhimu wa kuishi kwa amani licha ya tofauti zao za kiusuli. Hata hivyo juhudi hazikufua dafu kwani awamu ya kwanza ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ilianza. Walinda usalama walipokuja kudumisha amani, walitumia bunduki zao na kuwaacha wengi wakiwa wafu nao watoto wakabaki wanawakiwa. Kisa hiki kiliwafungua macho viongozi wakatambua kuwa wakazi hawa walikuwa wakiishi hapa kiharamu. Vyombo vya habari vikatoa wito kwa chama tawala kuwatafutia mahali kwingi, vidonda vya zamani vikanza kutoja damu. Juhudi zao za kuandama ya uamuzi wa kuhamiShwa kwao hazikufua dafu. Wachache walifanikiwa kurudi kwao katika awamu ya pili ya Operesheni Rudi Kanaani.
Wengine kama Lunga ambaye hakujua kitovu chake hasa walitimuliwa pamoja na familia zao. Baada ya miezi mitatu Lunga aligundua kuwa amerudishwa kwenye Mlima wa Simba ambako inaaminiwa mababu zake walikuwa wamehamia kutoka Kaoleni, siku za biashara ya watumwa. Msitu wa Mamba ulibaki tasa. Mto uliokuwa hapo karibu, ambao ulikuwa umeanza kukauka sasa ulianza kutiririsha maji. Jambo la kushangaza ni kwamba, hata baada ya tangazo kutolewa kuwa msitu huu ni marufuku kwa binadamu, usiku wa manane kulisikika milio ya malori na matrekta yakibeba shehena za mbao, makaa na mahindi. Moshi pia hufuka mle mara kwa mara.
Maswali ya ziada
- Eleza sifa za wahusika hawa: (alama 10)
- Lunga b. Kimondo c. Kangata
- Kuukata mkono niliostahili kuubusu yalinifika ya kunifika “
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Eleza namna msemaji alivyoukata mkono aliostahili kuubusu (a!ama 6)
- Fafanua mambo mawili yaliyomfika msemaji (alama 2)
SURA YA SITA
Sura hii inapoanza tunampata Mwalimu Dhahabu akimtaka Umulkheri kuyarudisha mawazo yake darasani.Mwalimu huyu kwa kawaida ni mcheshi. Umu(ufupi wa Umulkheri) aliyarudisha macho yake darasani yakatazamana na ya Mwalimu Dhahabu bila yeye Umu kumwona mwalimu mwenyewe. Tangu Umu kujiunga na Shule hii katika kidato cha pili anajihisi kama samaki aliyetiwa kwenye dema. Haya mazingira ni mageni kwake na hakuja hapa kwa hiari. Baridi ya mahali hapa inamsinya kwani si kama kwao ambako kulikuwa na hari. Ukweli ni kuwa Umu alikuwa na kwao ila sahii hana.
Amebaki kuishi kwa hisani ya mkuu wa aliyeshauriwa na Wizara ya Elimu kumsajili umu na wengine watano. Umu ni mwana wa pili wa Bwana Lunga Kiriri —Kangata. Uongozi ulipoamua kuwahamisha mlima wa simba. Kule kuhamia Mlima wa Simba hakukumkalia vyema Lunga. Aliona kuwa ameyapoteza mengi maishani. Watoto wake walikuwa wakisomea katika Shule za kifahari na sasa fidia aliyopewa na serikali haitoshi hata kuwapeleka wanawe katika Shule za watu wa kima wastani.Lunga alipohamia Mlima wa Simba mke wake Naomi naye hakuwekwa na mazingira haya mapya.
Asubuhi moja alimtumia Lunga ujumbe na kumtaarifu kuwa ameondoka ili akatambe na ulimwengu na huenda akaambulia Cha kumsaidia Lunga kuikimu familia.Akawaacha Lunga na wanawe.Pigo hili la tatu lilimuuma Iunga sana kwani alijisabilia kwa hali na mali
kumpendeza mkewe. Naomi alilipa penzi lake na kumwachia Lunga adha za malezi jambo ambalo Lunga hakustahimili. Mwaka mmoja wa kwanza ulimwia Lunga mgumu mno kwani ilimlazimu Lunga kuwa mama na baba wa watoto wake. Katika hali hii Iunga aliingiwa nawahaka na kihoro na hatimaye ugonjwa wa shinikizo Ia damu ukampata.
Kabla ya mwisho wa mwaka huo Lunga alifariki na kuwaacha watoto wake mikononi mwa kijakazi wao. Asubuhi moja Umu aliamka na kujipata yu pweke nyumbani mwao. Ndugu zake wawili, Dick naMwaliko walikuwa wametoweka. Umu alijaribu kumwita kijakazi Sauna kumjuza lakini alisalimiwa na cheko la mwangwi wa sauti yake katika sebule. umu alimaka, hajui awafuate wapi ndugu zake wakembe.Dick alikuwa darasa la saba naye mwaliko alikuwa katika darasa Ia kwanza. Picha ya watoto waliotekwa nyara ilimjiaUmu akilini mwake ikakifanya kichwa chake kumwanga kwa maumivu. Mwishowe alipiga ripoti katika kituo cha polisi alikoulizwa maswali mengi kuhusiana na kukosekana kwa ndugu zake.
Baada ya kuripoti habari hiyo Umu alijizoazoa na kujiendea zake nyumbani. Maisha ya Umu sasa yalichukua mkondo mpya. Siku ile baada ya kuwapigia polisi ripoti,ilibainika wanuna wake walikuwa wametekwa nyara na Sauna kwani hayo ndiyo yalikuwa mazoea yaSauna. Sauna alikuwa akijifanya mwema kwa waajiri wake ili aaminiwe ili naye apate fursa ya kuwaiba watoto na kuwapeleka kwa bibi mmoja ambaye aliwatumia katika biashara zake na katika ulanguzi wa dawa za kulevya.
Machozi ya uchungu yalimtiririka Umu na hakuamini kuwa nduguze wadogo walikuwa mali ya mtu atakayewatumia kama kitega uchumi. Baada ya kutia na kutoa, aliona kuwa hapo hapamweki tena akaamua kuondoka. Asubuhi moja Umu alifika kwenye kituo cha garimoshi. Sasa yu katikati mwa jiji la Karaha. Woga mkubwa ukamkumbatia kwa kutojua alikokuwa kwani mji huu ni mpya kwake. Hajawahi kutembea hapa peke yake. Hata hivyo, Umu yu tayari kuanza maisha upya katika jiji hili. Hajui vipi lakini penye nia ipo njia. Baada ya kuwaza na kuwazua, Umu alijikokota na kuchukua njia iliyoelekea kushoto. Alipofika Church Road mara moja aliikumbuka njia hii.
Aliwahi kupitia pale zama za utukufu wa babake. Anakumbuka akiwapata ombaomba wengi karibu na kanisa Ia Mtakatifu Fatma. Anakumbuka namna alivyomsihi mamake kumpa noti ya shilingi mia moja ili amkabidhi mmoja wa ombaomba wale. Mama mtu alikatalia ombi Ia Umu lakini hatimaye baada ya Umu kusisitiza mno, mamake alimkabidhi shilingi ishirini naye umu akaongeza mapeni aliyokuwa akipewa na babake na kumkabidhi ombaomba mmoja shilingi mia mbili. Ombaomba huyo alimshukuru na kumwita sistee na
kuahidi kuwa siku moja atamsaidia Umu. Leo hii Umu anashangaa iwapo bahati itamvutia usaidizi hata kutoka kwa yule maskini wa Mungu. Akipewa msaada wowote hata kama ni jamvi la kuuweka ubavu wake usiku kwenye mitaa atashukuru.
Alielekea kwenye mkahawa mkubwa mkabala mwa kanisa. Aliwaona vijana wengi wa mitaani. Umu akayaangaza macho yake kuona kama atampata rafiki yake. Hakumpata wala hakuona yule aliyekaribiana naye. Alikataa tamaa. Aliamua kuendelea na safari yake, huenda atampata kanisani. Kisadfa, kabla hajatembea hatua chache kutoka pale aliskia sauti ikiita “kipusa”. Alipogeuka alimwona yule kijana kazaliwa upya! Nadhifu! Meno meupe. Alijitambulisha kwake Umu kama Hazina. Serikali ilimwokoa kutokana na kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati. Akapelekwa shuleni akasoma. Walijengewa makao ambapo yeye na wenzake wanaendelea kusaidiwa na kupewa mbinu za kukabiliana na maisha.
Hazina alibahatika kujifunza upishi na huduma za hotelini na sasa hivi anafanya kazi kama mhudumu katika hoteli hiyo. Hazina alimwomba Umu waende akanywe chai. Umu alimtazama Hazina huku kaduwaa. Akamfuata hotelini alikokula shibe yake. Alimsimulia Hazina mkasa huku mito ya machozi ikiwatiririka wote wawili. Hazina alimwonea imani umu kwa kuharibikiwa na maisha katika kipindi ambapo anahitaji hifadhi ya wazazi. Umu machozi yake yalikuwa mchanganyiko wa furaha na majonzi. Furaha kwa kuona kuwa rafiki yake amefaulu kujitoa katika hali ya utegemezi. Huzuni kwa sababu anahisi kuwa ndugu zake wawili huenda ndio walichukua nafasi ya Hazina katika mitaa ya miji. Hazina alimwahidi kuwa atamsaidia. Akampeleka moja kwa moja hadi kwenye makao yao na kumjulisha kwa Julida mama aliyesimamia makao haya. Julida alimkaribisha na kumtaka asijali. Hapo pangekuwa nyumbani mwao kwa muda kisha Julida wangewasiliana na Idara ya Watoto kuhusu suala la ndugu zake Umu.
Ndugu zake wangetafutwa na wangepatikana. Mwezi mmoja baadaye, Umu alijiunga na Shule ya Tangamano akajiunga na kidato cha pili ambako alijipata kuwa mgeni. Mwalimu Dhahabu akatambua kwa wepesi unyonge aliokuwa nao Umu. Mwalimu huyu akataka pia kujua usuli wa Umu kutoka kwa mwalimu wa darasa la Umu. Mwalimu huyu wa darasa alipoyahadithia masaibu ya Umu kwa Mwalimu Dhahabu, Bi Dhahabu akawa haishi kumhimiza Umu kuwa jasiri kukabiliana na hali yake hii mpya.
SURA YA SABA
Hata hivyo ilimwia vigumu Umu kusahau yaliyopita. Hata hivyo, Umu aliendelea kuhimizwa na wenzake ayazoee maisha haya mapya. Siku moja Kairu alimweleza Umu kuwa ana bahati sana kwani yeye hakupitia waliyoyapitia wao. Wao walitendwa ya kutendwa. Wao walipofurushwa kwao siku hiyo hakujua waendako. Mama akiwa mbele nao kina Kairu nyuma. Mama yao alikuwa amembeba kitindamimba ambaye alijifia mgongoni mwa mamake. Baada ya kuuzika mwili wa ndugu yao, kina Kairu waliendelea na safari wasiojua mwishowake. Hatimaye nguvu ziliwaisha mama yao akawaashiria kuketi kando ya njia, wakawa wanangojea kifo. Mara waliwajia watu waliokuwa wamevaa mavazi yaliyoandikwa IDR,wakasombwa na kutiwa kambini walikokuwa wamejaa sana watoto kwa watu wazima.
Hali hapo ilikuwa ngumu. Miiko ilivunjwa. Walivumilia wakawa wanaishi kwa tumaini wakidhani hali itatengenea. Wakatumaini kwamba wangerudi kwao. Lakini kinyume na matarajio, uongozi mpya hukuleta ahueni yoyote katika maisha yao. Kilichobadilika ni kuwa walipewa ardhi zaidi ya kujenga mabanda zaidi ili kupunguza msongamano katika mabanda ya awali. Sasa wako pale pale. Kairu alikwenda pale akiwa darasa la sita na sasa ako kidato cha pili. Wangali wanasubiri kurudi nyumbani ila yeye haoni kama mna nyumbani pema zaidi ya hapo kambini ambako wanaishi bila kujali mtu alikotoka. Kairu alimsihi Umu kuvumilia na kuzingatia masomo kwani ndiyo yatakayomtoa katika lindi hilo la huzuni. Kairu aliendelea kumweleza Umu kuwa ana bahati kupata mfadhili. Yeye Kairu, mzazi wake wa pekee ni mama ambaye ni muuza samaki na baada ya ule mzozo wa ni nani kamiliki Ziwa kuu, biashara yao imedidimia sana.
Samaki wamekuwa adimu sokoni na bei yake imepanda. Mamake Kairu hana mtaji wa kuanzisha biashara nyingine kwa kuwa yeye ni maskini. Maisha yamemwia magumu kwani hata karo yake Kairu imembidi amlilie mwalimu mkuu amruhusu alipe kidogokidogo hadi mwisho wa mwaka. Katika mazungumzo ya Kairu inabainika kuwa babake yu hai na ana familia nyingine na kuwa Kairu alizaliwa nje ya ndoa. Umu anapoyaweka masaibu ya Kairu kwenye mizani anaona kuwa anaona msiba wake kuwa mwepesi sasa. Mwanaheri naye alianza kusimualia na kusema kuwa baada ya kurudishwa nyumbani kutoka Msitu waMamba baba yakeMwanaheri- Mzee Kaizari, aliweza kuyajenga maisha yao upya.
Akajenga myumba kufu yao pale kwenye ganjo lao Yeye na dadake Lime walirudi shuleni
mlemle kijijini mwao tu. Ikawa rahisi kuyazoea maisha kwani wanafunzi wenzao waliwapenda sana. Lime alikuwa hodari katika michezo ya kuigiza- ile ya kitoto. Alikuwa mcheshi mno na kutokuwapo kwake shuleni kuliwafanya watoto kumpeza. Majirani wao nao wakamsaidia baba yao kukabiliana na hali hii mpya ya maisha hata hivyo baba mtu alikuwa na hofu kuwa huenda wangeshambuliwa tena, nao majirani walimhakikishia kuwa hawangeruhusu jambo lolote kuusambaratisha tena udugu baina yao.
Kwa hivyohali ya utulivu ilitawala tena.Uhusiano kati ya marehemu mamake Mwanaheri na mavyaa yake ulikuwa umeingia ufa. Mama mkwe daima alikuwa kwa kumwona aliyekuja kumbwakura mwanawe. Hali hii ikawa imezidishwa na tofauti zakikabila kati ya mamake Mwanaheri na babake.Mamake ametoka kwenye jamii ya Bamwezi. Daima anachukuliwa kama mgeni, si katika boma lao tu, bali katika kijiji kizima. Uhasama ulizidi baada ya vurugu za miaka mitano iliyopita. Nyanya yao akimwona mamake Mwanaheri kama chanzo cha kuharibiwa mali yao, kwamba ndiye aliyewafanya majirani kuwachomea boma Iao.
Mamake Mwanaheri alidhoofika kiafya kwa majonzi ya kutengwa na wale aliowadhania kuwa wa aila yake. Siku moja waliamka na kupata kibarua juu ya meza dogo iliyokuwa chumbani mwa Mwanaheri.Mwanaheri alipofungua barua hii alipata kuwa mama mtu alihiari kuondoka kwa kubaguliwa,kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyotenda.Mwanaheri aliendelea kuwahadithia wenzake nakusema kuwa baada ya miezi miwili babake alienda kumtafuta mamake kwao asimpate. Baada ya kujuzwa kuwa mama mtu alikuwa ameenda mjini kuzumbua riziki, babake Mwanaheri alifululiza mjini kwenda kumtafuta mke wake akiwa mwenye majuto. Alimtafuta na kumtafuta mwezi baada ya mwezi na alipompata alikuwa amejifia chumbani mwake baada ya kutumia kinywaji kikali. Baba mtu alifanya juhudi na mabaki ya mamake Mwanaheri kuzikwa. Mwanaheri alipomaliza kuhadithia kadhiayake, matone mazitomazito ya machozi yalikuwa yakimdondoka.
Umu na Kairu walimwacha autue mzigo wake. Sasa Umu alianza kuhisi mzigo wake ulikuwa mwepesi sana.Mwanaheri aliendelea kuhadithia kuwa mara nyingi mwalimu anapofundisha mawazo yake hutangatanga. Yeye hujiuliza ni kwa nini mamake akakitekeleza kitendo hicho cha ubinafsi. Kwa kuwa maji yamekwishamwagika, sasa ameamua kuufuata ushauri wa MwalimuDhahabu wakuandama elimu kama ya kumwezesha kuleta mabadiliko katika jamii. Mwanaheri anasema kuwa iwapo mamake angefuata mikakati bora zaidi ya kuhusiana na wakwe zake badala ya kukata tamaa,huenda maisha yake Mwanaheri na ndugu zake yangekuwa bora zaidi.
Zohali naye alikuwa akiusikiliza utambaji wa marafiki zake nacho kilio kikawa kinamwandama. Baada ya kuwaza ikiwa atawatolea wenzake dukuduku lake hatimaye aaliamua kuwasimulia. Yeye alikuwa motto wa nyumba kubwa. Babake alikuwa mkurugenzi katika Shirika la Utoaji wa Huduma za Simu na mamake alikuwa mwalimu mkuu wa Shule maarufu ya kitaifa. Wazazi wake walikuwa walezi wema.Zohali na nduguze hawakupungukiwa na chochote.Maisha yake Zohali yalianza kwenda tenge alipojiunga na kidatocha pili.Mtafaruku wa kihisia katika umri huo ulimfanya kufanya mambo kwa papara na kutahamaki akawa ameambulia ujauzito.
Mwalimu mkuu alimtaarifu dadake Zohali kuwa alikuwa mjamzito na alifaa kurejeshwa nyumbani na akisha kujifungua wazaziwake waweze kumtafutia Shule nyingine.Tima(dadake Zohali) alimaka. Kutoka siku hiyo maisha ya Zohali yalichukua mkondo mpya. Amewahi kulala katika barabara za jiji pamoja na watoto wengine wa mitaani, amewahi kutumia gundi ili kujipurukusha,amewahi kupigana na majitu yaliyokuwa yakitaka kuuhujumu utu wake kwa kumnyanyasa kijinsia.Wakati wenzake waliona siku zake za kujifungua zimekaribia za kujifungua walimpeleka kituo chaWakfu wa Mama Fatma. Alikuwa ameyapitia mengi.Zohali anamshukuru Mtawa Pacha aliyemwokoa kutokana na kinamasi cha unguliko la moyo. Baada ya Zohali kumweleza kadhia yake, Mtawa Pacha alitikisa kichwa na kumwahidi kwamba baada yakujifungua angemrejesha shuleni. Sasa hivi na ulezi ulimpotezea miaka yake miwili.
Huwa anatamani sana kumwambia Mtawa Pacha ukweli wa mambo kuwa ana wazazi lakini moyo wake hukataa katakata. Atamwambiaje kuwa ana wazazi ilhali waliisha kumkana alipohitaji pendo lao?Anaendelea kusema kuwa madhila aliyoyapitia nyumbani kwao hayaelezeki. Baba yao alisema kuwahakuwa na pesa za kulipa kijakazi tena. Kazi zote za nyumbani zikawa za Zohali. La kusikitisha zaidi ni, mama mtu ambaye anajua uchungu wa kulea mimba hakutoa sauti yakumtetea. Baada ya Zohali kuyakamilisha masimulizi yake aliyaondoa machoyake kwenye ukuta yalikokuwa yameganda.Chandachema alifuata kusimulia kadhia yake. Kisa chake kikiwa na mshabaha na kile cha Zohali.Alilelewa na bibi yake aliyefariki Chandachema akiwa darasa la kwanza. Habari ilisema kuwa baba yake Fumba alikuwa amehamia Uingereza na familia yake na ni mhadhiri katika Chuo kikuu. Baada ya nyanyake kuiaga dunia, mambo yake Chandachema yalijaa giza.
SURA YA NANE
Ni alasiri moja ya joto kali. Mwangeka na Mkewe Apondi wameketi kwenye behewa la
nyumba yao.Wameyaelekeza macho yao kwenye kidimbwi ambamo wanao watatu Sophie,Ridhaa na Umulkheri- wanaogelea.Ukichunguza kwa makini utapata kwamba wawili hawa hawaoni chochote japo wanatazama. Kila mmoja,Apondi na Mwanageka, amepotea kwenye ulimwengu wake. Mwangeka anapomtazama Apondi anatabasamu. Kisa cha kukutana kwao kilikuwa kama ifuatavyo:Mwangeka , babake Mwangeka alikuwa akiishi nyumbani kwa Mwangeka kwa muda. Walikuwa wajane wawiliwaliokomaa. Hitaji la Mwangeka kuwa na mshirika wa kumwondolea ukiwa lilimwandama.
Baba mtu alimtaka Mwangeka kuwazia suala hili, Alijua kuwa wakati ndio mwamuzi,ipo siku atakapotokeza hurulaini wake Mwangeka.Ataifungua kufuli kubwa iliyoufunga moyo wake na hiyo itakuwa siku ya kumwaga chozi la heri. Baba mtu akaendelea kungojea kwa matarajio makuu, kila jioni akimchunguza mwanawe kuona kumetokea badiIiko lolote. Siku moja alikutana na RachaelApondi ambaye alifanya kazi katika Wizara ya Vijana na Masuala ya Kijinsia. Apondi alikuwa na shahada katika masuala ya kijamii. Apondi alikuwa mmoja wa wawasilishaji na ilipowadia zamu yake kuwasilisha aliwasisilisha kwa ustadi wa hali ya juu. Akautekanyara moyo wa Mwangeka. Apondi alipotoka jukwaani alisindikizwa na makofi ya hadhira yake.
Mwangeka akamsindikiza na macho zaidi ya makofi. Moyo wake uliokuwa umejaa barafu ukayeyuka na kutwaa uvuguvugu. Binti huyu alimkumbushaMwangeka marehemu mke wake Lily. Mwangeka naApondi walipata kujuana vizuri zaidi wakati wa chamcha. Huu ukawa mwanzo wa usuhuba na uchumba wa mwaka mwaka mmoja ambao kilele chake kilikuwa kufunga ndoa. Apondi alikuwa mjane wa marehemu Mandu. Mzee Mandu alijifia ughaibuni katika shughuli za kudumisha amani. Kifochake Mandu kikamwachia Apondi na Sophie mwanawe wa miaka miwili kilio kisichomithilika.
Apondi akawa mwoga, akachelea kuhusiana na mwanamume mwingine asije akamwachia ufa wamoyo. Miaka sita baada ya kufiwa ndipo alipokutana naMwangeka na penzi likazalika, wakapanga kuoana.Alipojifungua mtoto wa kiume alimwita Ridhaa. Ridhaa ni bavyaa yake aliyemkubali katika familia yake licha ya kwamba koo zao ni tofauti. Akawa nafuraha tele kwa kuwaSophie amepata mwenzake naye Baba Ridhaa amepata fidia japo kidogo kwa familia yake iliyoteketea.Mwangeka na Apondi walikuwa wameamua kuwa watoto wao wawili walitosha kukamilisha familia yao.
Lakini, ukarimu wao ulifanya kuzaliwa kwa Umulkheri katika familia yao.Baada ya Umu kujiunga na Shule ya Tangamano, waliishi alishirikiana na mwalimu mkuu wa Tangamano
mfadhili. Apondi alikuwa rafiki wa utotoni wa Mwalimu Dhahabu. Alipompigia simu na kumweleza kadhia ya Umu Apondi alikubali kumchukua Umu kama mtoto wake wa kupanga.Baada ya kuwasiliana na Mwangeka, Mwangeka hakuwa naPingamizi yoyote kuhusu kuwa mlezi wa Umulkheri.
Mwangeka alimwambia mkewe kuwa umu ni baraka kwa Mwenyezi Mungu na kuwa Mungu amemfidia mwanaye aliyekufa umu akapata wazazi wapya.Wakawa wanamlipia karo umu mwanzoni alikuwa na shaka lakini baadaye alikuja kuwapenda kwa dhati.Upendo alioupata kwa wazazi hawa wapya uliponya donge chungu lililokuwa moyoni mwake.Akawa sasa yu tayari kumsamehe mamake hapa duniani na ahera. Akawazia pia kumsamehe Sauna. Hata hivyo alibaki kujiuliza maswali mfululizokuhusiana na walikotokomea ndugu zake.
SURA YA TISA
Siku hii Dick alihisi kuwa uwanja wa ndege ulikuwana baridi na mzizimo kuliko siku nyingine zote. Dick mlolongo mkubwa wa watu ambao walingoja kuingia akawa anakumbuka siku alipoanza kusafiri kwa ndege. Siku hiyo alijawa na kiwewe kwani biashara haramu ya kubeba dawa za kulevya aliyokuwa amejiingiza kwayo ilikuwa imewaingiza wengi kwenye mikono ya polisi, wakatiwa mbaroni.
Siku hizo alikuwa mwanagenzi katika uga huu kwani alikuwa na umri wa miaka kumi tu. Zipo siku alipotetemeka karibu ajisaliti lakini hatimaye alizoea kujipa moyo. Sasa miaka kumi ya adha imepita. Haukuhitaji mnyonge. Dick alitoswa katika kinamasi cha kuuza dawa za kulevya na Sauna- kijakazi wao.Dick amesafirisha maelfu kwa maelfu ya vifurushivya dawa hizi. Mwanzoni akawa si mraibu wa dawa hizi lakini ilibidi ajizoeshe kwa usalama wake mwenyewe, kwani mara nyingi alilazimika kuzimeza dawa zenyewe ili kwenda kuzitapika kwenye masoko ya ughaibuni.
Jambo hili lilichangiwa na uwepo wa mashine zenye uwezo mkubwa wa kung’amua shehena za dawa zilizofichwa kwenye chupi. Siku ile baada ya kijakazi Sauna kumwiba Dick baba mmoja tajiri ambaye alijitia kumpeleka shuleni.Kumbe alikuwa amempeleka katika biashara yakuuza dawa za kulevya. Buda ( lakabu ya tajiri wakeDick) alipoona Dick akitaka kukataa kushiriki biashara hii, alimtishia Dick kuwa angetupwa nje, asingiziwewizi na bila shaka Dick alijua malipo ya wezi ni kutiwa tairi na kuchomwa moto. Wazo la kupata adhabu ya aina hii lilimtetemesha Dick. Akambuka rafiki yake Lemi alivyofishwa kwa njia hii. Kisa cha Lemi kilimfanya kuunasihi moyo wake kuingilia biashara hii haramu ili mwenye nguvu
asije akamtumbukiza akajisemea kuwa huenda siku moja akapata mbinu ya kujinasua.
Sababu nyingine iliyomfanya Dick kuingilia biashara hii ni kuwa alihitaji chakula na mahitaji mengine. Akasema potelea mbali kwa lisilobudi hutendwa. Alipojitosa katika biashara hii haramu aliingilia kwa hamasa za ujana. Miaka mitano ya kwanza ikawaimejaa hekaheka kwani alisafiri kwingi na kuona mengi. Akaweza kuchuma pato Si haba, pato aliloliona ni halali yake baada ya ulimwengu kumpoka maisha yake. Hata hivyo asubuhi moja aliamka baada ya kuamua kuwa hakuumbiwa uhalifu,dhamiri yake ikamsumbua na moyo wake kumsuta.
Mawazo mengi yakawa yamempitikia akilini na ya kamsukuma kuufikia uamuzi wa mkataa,akajinasua kutoka kucha za mwajiri wake huyu. Akaacha biashara ile haramu na kuanzisha biasharaya kuuza vifaa vya simu. Leo hii amejiajiri. Ashaamua kuufungua ukurasa mpya katika maisha yake. Amekwisha kuhitimu masomo katika Chuo cha ufundi ambako alijifunza teknolojia ya mawasiliano ya Simu. Sasa amepanua mawanda yake ya kibiashara. Anauza vifaa vya simu. Husafiri ng’ambo mara kwa mara kununua bidhaa ili kuyauzia mashirika yanayotoa huduma za mawasiliano. Asubuhi hii Dick na kijana mwenzake (mwajiriwa wake) walikuwa katika safari ya kawaida.
Alinuiwa kuabiri ndege ya saa moja asubuhi kuelekea ughaibuni ambako alizoea kununua mali yake. Huku akingoja afisi kufunguliwa,akayakunjua maisha yake ya siku za Mlima wa Simba.Akamwazia mama yake kwa masikitiko makuu. Akashanga jinsi ulimwengu unavyoweza kummeza mwanadamu akawacha kuwaazia hata wana wake.
Akamkumbuka babake katika dakika ya mwisho ya hasidi” ndio waliomsababishia uwele alionao. Dick akiishi, atawaona. Akili yake ikamtuma kumkumbuka Umulkheri- dadake. Anakumbuka alivyomwambia kuwa asijali kwani yeye angewakimu kwa viganjavyake na hawangepungukiwa na chochote. Akawa na maswali chungu nzima kuhusiana na aliko Umu.Wakati Dick alikuwa akiwaza kuhusu familia yake,hakujua kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake kapiga foleni.
Anasafiri ng’ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada yakuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni nakufuzu vyema katika mitihani yake.Kisadfa, safari ya Umu imekuwa siku hii ambapo Dick anasafiri. Dick aliposikia Mwangeka akimwita Umuna kumtaarifu kuwa ndege i karibu kuondoka,hakuamini. Mazungumzo baina ya Umu na wazazi wake yalimwamsha Dick kutoka lepe lake la muda.Aligeuka na kutazamana ana kwa ana na Umu. Mwanzoni Umu
akidhani macho yanamdanganya. Mikono yake ikamwachilia dadake Sophie, moyowake ukamwenda mbio. Ghafla Dick, alimwita dadake Umu nakumkimbilia. Wakakumbatiana.
Wasafiri wote na aila yote ikawatazama kwa mshangao. Machozi yakawadondoka wote wawili na kulia kimyakimya huku wakiambiana kimoyomoyo yote yaliyowakumba. Hatimaye sauti iliita ikitangaza kuwaabiria wa ndege Tumaini waanze kuingia. Walijua kuwa jaala ilikuwa imewakutanisha na hawatawahi kutengana tena.
SURA YA KUMI
Sura hii inaanza kwa Wimbo wake Shamsi. Leo Shamsi anaskika kama amebadilisha wimbo wake kama ana wasema Ridhaa japo kwa sauti ya chini. Wimbo huu wa leo unasikika kama wa kiumbe mwenye maumivu zaidi na mapigo yake hasa ni ya mbolezi. Huu wa leo ni tofauti na majigambo yake ya kila siku. Ridhaa alianza kuyaghani majigambo yake Shamsi kwa sauti ya chini kama anayeyatia maneno ya majigambo kwenye mizani.Ridhaa anamtazama Shamsi akipita kama afanyavyo kila siku.Mtaa anakoishi Shamsi si mbali na hapa, Shamsi na Ridhaa ni majirani. Huu ni mwezi wa tatu tangu Ridhaa kuhamia mtaa wa Ahueni. Ahueni ni mtaa wa raia wenye kima cha juu kiuchumi. Mtaa huu una sura ya mijengo ya kifahari ya ghorofa.
Daraja kubwa limeutenga mtaa huu na mtaa waKazikeni inakoishi familia ya Shamsi na nyingine za aina yake. Huku maisha ni ya kubahatisha. Huu nimtaa wa mabanda yaliyojengwa kwa udongo na mabati. Mwangeka aliamua kuhamia mtaa wa Ahueni baada
ya mjukuu wake wa mwisho kuzaliwa. Aliona ulikuwa wakati wake kuanza kuyajenga maisha yake upya. Maisha yaMwangeka sasa yalitengenea. Baada ya kuzungumza na mwanawe, Ridhaa alimwomba Mwangeka amruhusu aondoke ili akaanze kuyazoea maisha ya ujane. Aliondoka akiwa na azimio Ia kukamiIisha kukijenga kituo cha afya chaMwanzo Mpya alichokijenga kwenye ganjo lake. Kituo hicho kingewafaa raia wengi ambao hawangemudu gharama ya matibabu katika hospitali za kibinafsi.
Selume alifanya kazi katika kituo cha afya chaMwanzo Mpya. Hali katika kituo hiki ni bora kuliko ilivyokuwa katika hospitali ya umma. Huko alikuwa amechoka kutokana na kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiiShia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali. Alikuwa amechoshwa na mambo mengi. Katika kituo hiki kipya Selume aliajiriwa kama Muuguzi Mkuu naye Kaizari kama Afisa wa Matibabu. Sasa huu ni mwaka wa tatu tangu kuanza kazi hapa chini ya usimamizi wa Ridhaa ambaye ndiye mkurugenzi.Anawahudumia
wagonjwa walio na matatizo aina aina.
Kuna mgonjwa mmoja aliuguza majeraha katika mgogoro wa ardhi katika eneo la Tamuchungu. Mwingine aliyejifia ni kijana anayesomea shahada ya uzamili, alikuwa mwathiriwa wa pombe haramu. Mgonjwa mwingine wa kike kwa Jina Tuama alikuwa amejipata katika hali mbaya kwa kukubali kupashwa tohara. Alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake.Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Anaendelea kusema kuwa kupashwa tohara hakumaanishi kuacha Shule kwani dadake Hazina alipashwa tohara lakini sasa amehitimu shahada kutoka Chuo kikuu.
Mgonjwa mwingine kwa jina Pete aliendelea kupata ahueni.Yeye aliokolewa akitaka kujiangamiza pamoja nakitotO chake. Pete alizaliwa katika kijiji cha Tokasa.Yeye ndiye mtoto wa nne katika familia yenye watoto sita. Alipoutambua ulimwengu tu, alijipata kwa nyanyake mzaa mama.Sababu yake kujipata katika hali hii ni ule mtafarukuuliokuwa umetokea baina ya mamake na babakePete kisa na maana, Pete hakuwa na mshabaha hata chembe na babake. Mama yake Pete kwa kuchelea kuiharibu ndoa yake akampagaza nyanya mzigo wa malezi.
Pete hajadiriki kuonja tamu ya kupendwa na wazazi wake. Alipoanza kupata hedhi maisha yalichukua mkondo mwingine. Alipoingia darasa Ia saba alipashwa tohara naowajombake wakapokea posa na baadaye mahari
kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Alipojifungua, akaamua kwa mzee Fungo hakumweki tena. Akaondoka bila kuangalia nyuma. Akaingia jijini kuzumbua riziki. Akapata ajira ya kijishahara duni ambacho hakikutosha kugharamia mahitaji yake yote. Maisha yakazidi kuwa magumu hadi akamzaa mwana wa pili.
Kitoto alichonacho zahanatini ni cha tatu na alikipata akiwa katika shughuli za uuzaji pombe. Mamboyalipombainikia kuwa ana watoto watatu kabla yakufikisha umri wa miaka ishirini na moja, aliona niheri ajiangamize. Alimwambia jirani yake amchungie watoto kisha akaacha kikaratasi chenye anwani ya bibi yake kwenye kimeza katika chumba chake na kuondoka. Alijiambia kuwa dawa ya panya haingeshindwa kumuua yeye pamoja na kilichomo tumboni na ndipo akamimina kopo la dawa hiyokinywani. Sasa anapata ahueni katika kituo hiki cha afya.
SURA YA KUMI NA MOJA
Sauna anaamka huku akijipindua kusikiliza mlio wa kingora unaosikika kwa mbali. Sauna anajihisi mzito kama nanga na kutamani kurudi kulala. Lakini inabidi aamke ili amtayarishie Bi. Kangara kiamshakinywa. Sauna anajihisi kutokuwa na utulivu na mara polisi wanafika kumkamata sauna na Bi Kangara ambaye ni mwajiri wake. Hawa wawili wamejihusisha katika biashara ya ulanguzi wa watoto.
Sauna baada ya kumtorosha Dick na Mwaliko na kuuza Dick kwa mzee Buda anaawaza jinsi ambavyo maisha yake yamekuwa. Hakupenda kazi hii sana kutokana na kitendo cha babake wa kambo anayemhujumu kila wakati apatapo nafasi na mamake kumwonya dhidi ya kumwambia yeyote asimbujie ndoa sauna aligeuka kuwa na moyo wa ujabari. Babake Sauna (Kero) alikuwa mlevi jambo lililosababisha kupigwa kalamu. umaskini aliosababishia mamake sauna ndicho kilichokuwa kiini chake cha kuolewa na Bwana Maya. Baada ya Sauna kutoroka kwao alifanya kazi mbalimbali kabla ya kukutana na Bi Kangara. Mabibi hawa walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa ukiukaji wa haki za watoto. Mwaliko anapelekwa kwa kituo cha watoto mayatima kilichoitwa Benefactor.
Neema na mwangemi wanajadiliana juu ya kupanga motto.hii ni baada ya kujaribu kwa muda wa miaka mitano bila kupata motto. Motto wao bahati alikufa katika juma la kwanza kutokana na ugonjwa wa sickle cell.
Neema anamwelezea mmewe mwangemi jinsi mungu alimpa nafasi ya kumpanga motto kasha akaitema kama masuo. Anamwambia asubui moja miaka kumi iliyopita, akiwa anapitia katika ujia uliolekea ofisini mwake alipata kitoto kimetupwa katika karatasi ya sandarusi. Alikipeleka kitoto kile kituo cha polisi na kasha baadaye kikapelekwa katika kituo cha watoto cha Benefactor.
Neema baada ya kukubali rai ya Mwangemi ya kumpanga motto walienda katika kituo cha Benefactor na kumpanga Mwaliko. Mwaliko aliwaheshimu wazazi wake na majirani hata akamaliza masomo yake ya kidato cha nne na akajiunga na chuo kikuu kusomea shahada ya Isimu na Lugha.
SURA YA KUMI NA MBILI
Baada ya masomo ya uzamili ya Mwaliko anaajiriwa katika kampuni ya magazeti ya Tabora kamamhariri katika kitengo cha biashara. Mwaliko anakumbuka yaliyotokea kwao baada ya a kuachwa na mama yao. Mama Neema aliishi kumpa tumaini kuwa atawahi waona .
Mwaliko na babake wanaamua kwenda kujivinjari katika mji. Ilikuwa siku ya kuzaliwa ya mwangemi. Katika hoteli mwaliko anazungumzia nduguze huku akionyesha labda waliweza kujifia au labda mama yao aliwajia. Kwa upande mwingine Umu na familia yao walikuwa pia katika hoteli ya Majaliwa kusherehekea kuzaliwa kwa Umu . Umu anakumbuka siku ambayo wazazi hawa wake wa kupanga walipomkujia na ujumbe wa mwalimu Dhahabu kuwa ni watu wa imani.
Umulkheri anawashukuru wazazi wake kwa kumsomesha, kwa utu wao, kwa kumsaindikia nduguye Dick kujiendeleza katika masomo na kuwaombea thawabu kutoka kwa Mungu. Aidha Apondi anamshukuru Umu kwa ulezi wa nduguze wadogo Don Ridhaa na hasa Sophie ambaye amekuwa katika hali ya kutafuta ujitambuaji. Dick anamkumbusha nduguye Umu alipomwambia kuwa angewalea na Mwaliko kwa viganja vyake. Aidha Dick anawashukuru sana wazazi hawa kwa mashauri yao kwani alipokutana nao kwanza alikuwa na kiduka kimoja cha kuuzia vifaa vya simu , lakini sasa ni mmoja kati ya watu mashuhuri katika kuendeleza teknohama.
Mwangemi anamwita mwanawe Mwaliko ambaye Dik na Umu wote wawili walitazamana , kila mmoja akiapa moyoni kuwa amewahi kumwona kiumbe kama huyu mahali , lakini hakuna anayedhubutu kunena. Mwangeka anakumbuka maisha yake na Mwangemi ya utotoni na jinsi walivyopendana. Katika utoto wao walibuni michezo ya kishujaa ambayo kila moja alipenda kujitambulisha na majagina.
Mwaliko moyo wa udugu unamwambia kuwa hawa ndio ndugu zake . Mara mwaliko anainua macho taratibu na kumwita Umu na Dick huku akiwarifu kuwa ni yeye nduguyo. Umu na Dick wanamkumbatia na kulizana. Wanafurahi kukutana huku wakipanga kumtamfuta mamayao. Mwaliko anarudi nyumbani akiwa na hamu kuu ya kumsimulia Neema majaliwa ya siku hiyo.
3 Athari ya vita katika nchi ya Wafidhina
- watu kuuawa, kuacha makwao na kukimbilia maisha yao huku wakipoteza mali kwani waliokimbia makwao kila walichokiacha kiliteketezwa
- kupora maduka ya Kihindi, kiarabu na hata Waafrika wenzao
- Misafara ya wakimbizi ikawa kwenye barabara na vichochoro vya Wahafidhina
- Mizoga ya watu na wanyama
- magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa moto
- uharibifu wa mali na
- Nyimbo za uchochezi mpinzani wa Mwekevu anambiwa tawala wahafidhina , mwanzi wetu tawala.
- Kuchomwa kwa magari kana kwamba ni mabiwi ya taka
- Vilio kwa waliokuwa wakiteketezwa
- Kubakwa kwa mabinti wa Kaizari yaani Lemi na Mwanaheri
- Askari wa fanya fujo uone kuwafyatulia risasi vijana walioamua kufa
- Magonjwa ya homa ya matumbo
- Njaa na ukosefu wa maji safi
- Kukimbilia chakula kwa watu wazima jinsi wafanyavyo watoto
4 Dhana ya chozi katika riwaya ya Chozi la Heri
- Umu alilia sana alipowakumbuka nduguye Dick na
- Umu anahuzunika kwa kukosa kwao nyumbani
- Watoto wa Lunga Dick, umu na mwaliko walilia machozi ya heri walipopatana katika hoteli ya majaliwa
- Ridhaa analia machozi ya furaha baada ya mwanawe mwangeka kufunga ndoa
na Apondi Reachel
- Vilio vya kite vilitanda baada ya makundi mawili kukutana, yaani lililomuunga mkono mwekevu na la mpinzani wake
- Ridhaa analia baada ya familia yake na jumba lake la kifahari kuteketezwa
- Neema analia machozi ya furaha mwaliko anapokubali kuwa motto wao wa kupanga
- Neema analia kwa uchungu wakati alipokumbuka kisa cha Riziki Immaculate kitoto alichookota na akaogopa kukichukua na
- Mwangeka analia kilio cha uchungu babake alipomweleza sababu ya kutozika mabaki ya familia yake
- Umulkheri na Dick wanapokutana kisadfa katika uwanja wa ndege wanatoa machozi ya
- Selume analia inapomlazimu kuondoka na kuacha motto na nyumba yake kwa sababu ya ukabila
- Subira alipokatwa kwa sime alilia kwa kite kabla ya kufa kwake
- Subira anakilovya kifua chake machozi sababu ya mamamkwe anayemshutumu na kuacha mwanawe na mumewe
- Mwangemi walipomtania babu Msubili pamoja na Mwangeka walichapwa wakatoa machozi ya uchungu
- Kaizari alitoa machozi ya uchungu alipoona vijana wakipigwa risasi kwa kukataa kuondoka barabarani
- Ridhaa analia kwa kubaguliwa shuleni
- Abiria waliochomewa katika gari la kuabiri na vijana waasi walilia kwa uchungu
- Mwanaheri anadondokwa na machozi anapowasimlia wenzake kifo cha mamake katika shule ya tangamano
- Ridhaa alilia machozi ya uchungu alipomwelezea Mwangeka mkasa wa kupoteza mali yake
- Viongozi wanatoa machozi kikinaya kuonyesha njisi ambavyo wanawahurumia maskini
- Ridhaa akiwa katika magofu anakumbuka kilio cha Mwangeka akiwa mtoto
- Kumbukizi za maongezi kati ya Terry na Ridhaa zinamfanya atokwe na machozi
- Mwangeka na Annatila wanalia walipokuwa wakiigiza kifo cha mdogo wao Kim
- Wenyeji walilia katika mazishi ya Kim wakilizunguka jeneza
- Umulkheri analia alipoenda kuhusu kupotea kwa nduguze katika kituo cha polisi
- Umu alipokutana na Hazina alilia machozi ya mseto wa furaha na huzuni
- Kairu na mamake wanalia kwa matatizo waliyopata na kujifia kwa kitoto chao walichozika porini
5 Nafasi hasi na chanya ya mwanamke
Mwanamke ni Msomi– Umu alikuwa na shahada ya uhandisi, Tila alimudu masuala ya sheria.
Mwanamke ni mtamaduni – Tuama anatetea tohara ya wanawake bila kuangazia matatizo inayosababisha
FOR MORE RELATED LEARNING MATERIALS, 0714497530
Mwanamke ni mwenye bidii– Apondi mkewe Mwangeka alikuwa anafanya kazi katika wizara ya vijana
Mwanamke ni mwenye tamaa – Bi Kangara anafanya kazi ya ulanguzi wa watoto ili kujilimbikizia mali
Mwanamke ni mwenye huruma– neema anakihurumia kitoto kilichokuwa kimetupwa na kukipeleka katika kitui cha polisi na kasha baadaye katika kituo cha watoto cha Bebefactor.
Mwanamke ni katili – neema anapokiokoa kitoto kilichotupwa kuna wanamwambia
asijitwike mzigo wa mwenzio. Aidha Neema akiwa chuo kikuu aliweza kuavya. Pete alijaribu kuavya mara tatu.
Mwanamke ni mwenye majuto– Naomi anaporudi katika msitu wa samba na kuona kaburi la mmewe anajutia alichokifanya.
Mwanamke ni mwenye amezinduka – Zohali anapigana na majitu yaiiyokuwo yakitaka kumnyanyasa kijinsia
Mwanamke ni mcheshi– Terry amboye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza bali alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini.
Mwanamke ni mwongo – Sauna anawahidi Dick na Mwaliko kuwatunza ila anawauza kwa Bi Kangara
Mwanamke ni mlezi mwema – Apondi anamlea Umu vyema
Mwanamke ni mwenye mashauri – Kairu anamshauri Umu kuwa asijihurumie sana kwani yeye ndiye aliyekuwa amepitia maovu mengi kumliko
6 Umuhimu wa mashirika ya misaada
- Mashirika ya kidini yanaungana pamoja kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa chakula katika kambi mbalimbali
- Kituo cha Benefactor kimeokoa maisha ya watoto wengi;
- Mwaliko
- Mtoto aliyeokolewa na Neema na watoto wengine
- Shirika la jeshi la wajane la Wakristu linasaidia maisha ya mayatima kama vile Chandachema, Umu na Mwanaheri uk95
- Shuleni tangamano iliwasaidia wanafunzi kama vile mwalimu Dhahabu anamwambia Umu arudi darasani anapoona amekumbwa na mawazo
- Mamake kairu ni maskini kwamba kulipa karo ni jambo linalomtatiza ila anaongea na mwalimu mkuu kumruhusu mtoto wake asome akilipa kidogo kidogo
- Mwalimu Dhahabu anajishughulisha kuwatafutia mayatima wazazi wa kuwapanga
- Shirika la Hakikisho la Haki na Utulivu linajishughulisha katika kusaidia watoto
kupata elimu kama ville chandachema
- Kituo cha wakfu cha mama Paulina kinamsaidia Zohali aliyepelekwa alipokaribia kujifungua
7 Matatizo ya ukabila
- Ridhaa anabaguliwa na wanafunzi wenzake kwa kutokuwa wa jamii yake jambo linalomfanya Ridhaa kulia sana na kutaka kuacha shule uk 10
- Subira analia kilio cha ubaguzi unatokana na mamamkwe
- Mamamkwe anamlaumu kuwa yenye ndiye sababu ya kuharibiwa mali yao
- Ukabila huu unasababisha kutengana kwa Subira na mmewe Kaizari
- Subira anaacha watoto wake kwa uchungu yaani lime na Mwanaheri
- Ukabila unasababisha kuwa na malezi mabaya kwani waazazi hawana utulivu wa kuwaelekeza watoto wao.
- Ukabila unasababisha kifo cha familia ya Ridhaa
- Kuharibu mali ya Ridhaa jumba lake la kifahari linachomwa
- Subira mkewe kaizari ambaye ni mbamwezi suala la kutengwa na familia yake kina msababishia kifo cha mapema uk 97
- Selume anatengwa na bintiye Sara kwa sababu ya ukabila
- Lucia kangata ndoa yake inapingwa kwa kuwa anaolewa katika jamii ambayo si yao
- Lime na Mwanaheri nduguye wanabakwa mbele ya babake
8 Malezi ya watoto
- Kuna ndoa kati ya Ridhaa na Terry inayowalelea watoto wao vizuri licha ya kuwa Terry anatengana na mmewe kwa mkasa Uk 11
- Mwangeka alimuoa Lily Nyamvula aliyekutana naye katika Chuo kikuu . walikuwa na mtoto mmoja kwa jina Malezi yao hayadumu kwani Lily na Becky
waliangamia kwenye janga la moto.
- Mwangeka hapo baadaye alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa. Aidha, Apondi anakuja na mtoto wake Sophie aliyekuwa wa Mandu mmewe wa awali kabla ya kufia ughaibuni alikokuwa ameenda kudumisha amani
- Mwangeka na Apondi wanawalea watoto wao vizuri kwa kuwapa elimu na Dick na Umu wanashukuru kwa malezi yao.
- Apondi anamshukuru Umu kwa malezi mazuri ya wadogo wake aghalabu anapokuwa mbali
- Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema hawakupata mwanao ila walipanga Mwaliko ambaye wamemlea vyema kwa kumpa elimu na kusoma hadi kitengo cha uzamili katika isimu na
- Kangata alimuoa Ndarine na kubarikiwa na; Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo waliwalea vyema kwani waliweza kuwapa elimu iliyowasaidia.
- Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Walibarika na mabinti wawili, Lime na Familia inapatwa na tatizo la kulea wanao kwa sababu ya ubaguzi wa mamamkwe kwa Subira jambo linalosababisha kifo chake.
- Lunga alimuoa Naomi walibarikiwa na watoto watatu, Umu, Dick na Mwaliko. Ndoa hii ina changamoto katika malezi kwani Naomi anamtoroka mmewe jambo linalosababisha kifo cha Lunga na watoto kama vile Dick kuingizwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya
- Familia ya Pete ilikuwa ya watoto sita baada ya kugunduliwa kuwa hakuwa na mshabaha na babake aliweza kurudishwa kwa bibi jambo linalosababisha ndoa ya mapema
- Pete aliozwa na wajombake kwa Fungo alipoingia darasa Ia saba na baada ya kupashwa tohara Pete anaozwa kwa Fungo akiwa bibi wanne. Anapogundua kuwa anapata watoto watatu akiwa chini ya miaka ishirini na moja alitamani Mtoto wake wa kwanza hakupata malezi yake kwani alimuacha kwa Fungo na kasha hawa wawili anawapata katika vibarua vya pombe.
- Kuna wazazi wengi ambao wanatupa watoto wao na pia kuavya. Tunambiwa kuwa Neema aliweza kukiokoa kitoto ambacho kilikuwa Aidha alipokuwa chuo
kikuu alikuwa ameweza kuavya
- Wazazi wa Zohali wanamkandamiza jambo ambalo linamfanya kutoroka nyumbani na kuwa mwana wa mtaani. Aidha kwake anasema kuwa hana wazazi anapohojiwa kwani walimkataa alipowahitaji zaidi
- Babake Kairu hamsaidii mkewe katika malezi jambo ambalo halimpi amani Kairu katika masomo
- Wazazi wake Chandachema yaani ndoa kati ya Rehema na mwalimu wake (Fumba) ambaye sasa ni mhadhiri hawashughuliki na malezi ya mwanao Rehema jambo ambalo linamfanya maisha yake kuwa ya
- Bwana Maya(mzazi mlezi) anamwingilia Sauna kimapenzi na kusababisha kupata ujauzito jambo linalomtia Sauna ujabali na unyama wa kujiingiza katika ulanguzi wa watoto
9) Athari za matumizi ya mihadarati
- Zohali anajiunga na kundi la vijana na kuvuta gundi inayomfanya kusahau matatizo anayopitia bila kujua mathara yake
- Pete anahamia kwa kazi ya kuuza pombe inayosababisha kupata watoto ambao anashindwa kuwalea na kutaka kujiua
- Dick anaingizwa na Sauna katika ulanguzi wa dawa za kulevya zinazohatarisha maisha ya muuzaji anaweza kamatwa na polisi na kufungwa
- Dick anashurutishwa kumeza dawa za kulevya na kasha akifika ughaibuni asitapike kutokana na uangalizi mkali katika viwanja vya ndege
- Dawa za kulevya zinasababisha vifo kijana msomi anakufa katika hospitali ya mwanzo mpya kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya
- Shamsi anawapigia kelele majirani wake katika mji wa Ahueni kutokana na ulevi wake
- Aidha ulevi unamfanya aishi katika mtaa wa makabwela wa Kazikeni
- Kapanga ananusurika kifo kwa matumizi ya kangara inayosababisha vifo vya watu sabini uk143
10) Uongozi mbaya
- Hueneza uhasama uk 21
- Viongozi kulia machozi ya mamba kuonyesha jinsi wanavyowajali maskini
- Kunyakua mashamba ya walalahoi uk 22
- Viongozi kupokea milingura kwa mabwenyenye waliokuwa wamejenga sehemu zilizotengewa barabara uko Tononokeni uk 13
- Kutoona ripoti za uchunguzi wa mashamba ya walalahoi
- Tume za uchunguzi ambazo hasiwajibiki
- Wizara ya ardhi kupeana hati miliki ghushi baada ya kuuza shamba mara ya pili
- Viongozi katika hospitali za umma wanachukua dawa na kupeleka katika hospitali zao za kibinafsi
- Watoto wa matajiri wanapewa mikopo ya elimu iliyokuwa imetengewa watoto wa maskini
- Viongozi katika forodha wanapokea rushwa Kurusu ulanguzi wa dawa za kulevya uk123
- Viongozi wanashindwa kuwapa vijana kazi baada ya Shamsi analalamika kwa kutopata ajira licha ya kupata shahada akiwa wa kwanza katika kijiji chao
- Viongozi wananyakua mali ya walalahoi huko msitu wa mamba bila kuwafidia kwa lolote jambo linalosababisha mauko ya Lunga
- Vijana saba wanakufa kwa mtutu wa bunduki kwa kutetea haki yao uk 24
- Wazungu walipoingia wananyakua mashamba yaliyotoa mazao mengi na kuchukua waafrika kuwa wafanyikazi wao
- Walitendao/ watendeao wenzao mabaya na mwishowe mabaya yale yakawafika Elezea visa vya wahusika hawa ili kughamua jibu la swali hili;
- Sauna anayewalangua watoto
- Bi Kangara aliyekuwa amempa ile kazi
- Neema kwa kuavya mimba akiwa chuo kikuu
- Pete kujiingiza kwa uuzaji wa pombe
- Zohali anapojiingiza katika raha za ujana anapata pigo la ujauzito 12)Aina za migogoro
- Mgogoro wa familia ya akina pete ambaye anaonekana hana mshabaha na babake na kupelekwa kwa bibi
- Mgogoro wa kisiasa kuna mgogoro kati ya wafuasi wa Mwekevu na wa mpinzani wake mwanamume
- Mgogoro wa kikoloni mkoloni anapuuza sera za Mwafrika.Uk 10,”Hatua ya mkoloni ya kupuuza sera za mwafrika za umiliki wa ardhi na kumchukua kama mfanyikazi wake
- Migogogo ya ukabila Subira anafukuzwa na mamamkwe kwa sababu ya kutoka jamii Ridhaa aliitwa ‘mfuata mvua’,na kutengwa na wenzake. Walimwona kama mwizi.uk 10
- Mgogoro wa nafsi pete ana mgogoro na nafsi yake jambo linalomfanya kutumia dawa ya panya
- Mgogoro wa utawala vijana wanamuua kutotoka kwa njia jambo linalosababisha kupigwa risasi na kujifia
- Mgogoro wa kiimani Lily imani yake ya kikristo inakinzana na wazo la Mwangeka kuwa uk 62
- FOR MORE RELATED LEARNING MATERIALS, 0714497530
- Mgogoro wa kiuchumi Dick anakataa kazi ya ulanguzi wa dawa za kulevya ila anashindwa atapata vipi chakula asipoikubali kazi hii
- Mgogoro wa kisaikolojia darasani Umu anaonekana kuwazia mambo mengi mwalimu anapomwambia rudi darasani. Aidha mwanaheri anasema anashindwa kumsikiliza mwalimu juu ya mawazo yanayompitia
- Mgogoro wa ufisadi watu wanapewa hatimiliki ghushi aidha maskini ambao mashamba yao yalinyakuliwa na kuundwa kwa tume za uchunguzi hawapati ripoti ya uchunguzi
- Mgogoro wa kitamaduni Tuama licha ya mathara ya tohara yanayomkabili hospitalini anatetea utamaduni wa kupasha tohara wasichana
- Mgogoro wa kitabaka matajiri wanapewa mikopo ya elimu iliyotengewa watoto wa kimaskini
- Mgogoro wa matibabu selume analalamika jinsi ambavyo viongozi katika hospitali za umma wananyakua dawa na kuacha hospitali bila dawa
- Mgororo wa ardhi serikali imaamua kuwaondosha watu kutoka msitu wa mamba bila ya
13) Uozo wa maadili
Ubakaji uk 25 genge hili la mabarobaro watano lilifululiza hadiwalipokuwa maskini mabinti zangu wawili, Lime naMwanaheri. Sikuweza kuvumilia kuona unyamawaliotendewa. Nilijaribu kwa jino na ukuchakuwaokoa lakini likawa suala la mume nguvuze!
Ulanguzi wa dawa za kulevya; Dick anaifanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine, uk 119
Uporaji; watu wanapora mashamba ambayo yalitengewa ujenzi wa barabara uko Tononekeni
Ulanguzi wa watoto; Bi. Kangara walifanya baiashara haramu ya kuwauza watoto na vijana. Uk 157;
uavyaji wa mimba ; mamake Sauna anamshurutisha kuavya mimba ili kumwondolea mmewe fedheha
Uasherati ; Pete anapata watoto wawili nje ya ndoa
Ulevi ; shamsi anajiingiza kwa ulevi akisema ndio inayompa utulivu. Watu sabini wanaangamia kwa kutumia kangaras
Ukabila ; familia ya Ridhaa inaangamia kwa sababu ya ukabila na uharibifu wa mali
nyingi
Ukatil ; polisi wanapiga vijana sabini na wawili risasi na kuwaua. Aidha wafuasi wa mpizani wa Mwekevu wanaua watu kwa kuwachoma.
14 utamaushi ; ni ile hali ya kukata tamaa kwa jambo fulani maishani. Wahusika mbalimbali waliweza kukata tamaa kwa njia moja au nyingine;
- Pete anakata tamaa maishani baada ya kupata watotto watatu akiwa chini ya miaka shirini na moja jambo linalomfanya kutaka kujiua
- Ridhaa mkewe na familia yake ilipoangamia kwa moto alikata tamaa ya mapenzi katika maisha yake
- Zohali licha ya kuzaliwa katika familia ya tabaka la juu anakata tamaa katika maisha na kuingia mtaani kutumia gundi na wenzake
- Mwangemi na Neema wanakata tamaaya kupata mtoto na kuamua kupanga Mwaliko
- Shamsi anakata tamaa ya kupata kazi na kudhamini pombe licha ya kuwa wa kwanza kuingia chuo kikuu kutoka eneo lao’
- Naomi anakata tamaa kuishi na Lunga na kuamua kwenda kutafuta kazi mjini
- Naomi anakata tamaa kuishi mjini na kurudi msitu wa samba ila anakuta Lunga aliaga na watoto wakaondoka
- Umu anakata tamaa ya kupata nduguye hasa baada ya kugundua kuwa hapati usaidizi katika kituo cha polisi
- Mwanaheri anakata tamaa baada ya kifo cha mamake Subira
- Subira anakata tamaa ya kuishi kwa Kaizari kutokana na chuki ya mamamkwe kwa kiini kuwa hawakuwa wametoka katika jamii moja
- Lunga anakata tamaa ya maisha baada ya kuachishwa kazi, kunyakuliwa kwa mazao yake na kuachwa na mkewe jambo linalosababisha kufa kwake
- Chandachema anakata tamaa baada ya nyanya yake kufariki na kunyanyaswa na jirani yake satua
MASWALI YA ZIADA YA INSHA. MAUDHUI YA:
Ufisadi, ukatili, uharibifu wa mazingirauu,ujaala, majanga, ubinafsi, ukoloni mamboleo, elimu, utabaka, nafasi ya vijana, taasubi ya kiume, ndoa, mapenzi, ushirikina, umaskini na mauti.
MAJIBU YA MASWALI YA MUKTADHA
- Msemaji ; Mwangeka Kwa ; mkewe Apondi Mahali; nyumbani kwao
Sababu; baada ya Apondi kumweleza umuhimu wa kupanga Umu
- Uk 121Msemaji ; Lemi Kwa ; dadake Tindi Mahali; sherehe
Sababu; walikuwa wamechelewa kurudi nyumbani
- Uk 122Msemaji ;uzungumzi Dick Mahali;katika biashara ya Buda
Sababu; licha ya kulazimishwa kufanya ile kazi anasema atatafuta njia ya kujitoa
- Uk 125Msemaji ; Dick anakumbuka maneno ya Umu Mahali; walipokuwa nyumbani kwao
Sababu; baada ya kuondoka kwa mama yao
- Uk 139 msenaji : Mwangeka Kwa : babake Ridhaa Mahali: kwa mwangeka
Sababu: alikuwa anataka kwenda kukamiliza kituo cha afya
- msenaji : uk 141 Selume Kwa : Meko
Mahali: hospitali ya mwanzo mpya
Sababu: alikuwa akimrejelea mgonjwa ambaye kichwa kilikuwa kimejaa damu 7 ) msenaji : uk 142 maneno ya Meko
Kwa : Selume Mahali: hospitalini
Sababu: alitaka kujua kama ni mmoja wa wale waliangamia kwa sababu ya pombe haramu
8) msenaji : uk 148 bibi Kwa : wajombake Pete Mahali: nyumbani kwake
Sababu: walitaka kumuoza Pete
- msenaji : uk 153 sauti kutoka moyoni mwa Sauna Mahali: kwa Kangara
Sababu: polisi walikuwa wamefika kuwakamata
- msenaji : uk 156 Bi Kangara kwa : Sauna
Mahali: nyumbani kwake
Sababu: baada ya Sauna kutoroka kwao
- msenaji : uk 159 mwangemi kwa : Neema Mahali:nyumabani kwao
Sababu:hakuonekana kufurahia suala la kupanga mtoto
- msenaji : uk 162 mtawa Cizarina kwa : Neema
Mahali: kituo cha Benefactor
Sababu: kwa kuokota kitoto kilichokuwa kimetupwa
13 ) msenaji : uk 163 mtawa Anastacia kwa : Neema na Mwangemi
Mahali: benefactor
Sababu: walikuwa wameomba kupanga mtoto 14)msenaji : uk 170 mwangemi
kwa : mwaliko
Mahali: nyumbani kwao
Sababu: alikuwa akimfariji juu ya nduguze
- msenaji : 174 Dick
kwa : akiambia familia ya mwangeka Mahali: hoteli ya Majaliwa
Sababu: anashukuru kwa mashauri ya Mwangeka
- msenaji : 176 Mwangemi kwa : Mwaliko
Mahali: hoteli ya majaliwa
Sababu: alikuwa anataka waonane na Mwangeka 17)msenaji : uk 179 kumbukizi za Mwangeka
Mahali: hoteli ya Majaliwa
Sababu: alikuwa anakumbuka jinsi walivyoishi na Mwangemi katika sehemu kame 18)msenaji : uk 154 Sauna
kwa : moyo wake Mahali: kwa Kangara
Sababu: hakuwa anapenda vitendo vibaya ila alitiwa ujabari na dunia
- msenaji : uk 168 uzungumzi nafsia wa Mwaliko
Mahali: nyumani kwa Mwangemi
Sababu: Neema alimtunza vyema kama mtoto wake
- msenaji : 171 mawazo ya Umu ya maneno ya mwalimu Dhahabu
Mahali: shuleni Tangamano
Sababu: Mwangeka walikuwa wamekuja kumpanga Umu
- msenaji : uk 173 Dick kwa : Umu
Mahali: hoteli ya Mjaliwa
Sababu: walikuwa wamempa mashauri mema
- msenaji : 176 maneno ya mwandishi kuhusu Umu na Dick Mahali: hoteli majaliwa
Sababu: walifahamiana na sura ya Mwaliko
- msenaji : uk 177 mawazo ya Mwangeka Mahali: hoteli ya Majaliwa
Sababu: alikuwa mtoto mtundu kulingana na babu
- msenaji : uk 180 kumbukizi za mwangeka wakiwa na mwangemi
Mahali: akiwa hoteli ya majaliwa
Sababu: majeruhi huvuja damu zaidi jua likiwa kali 25)msenaji : 184 Kumbukumbu za mwangeka ya swali la babu
Mahali: akiwa hoteli majaliwa
Sababu: babu alitaka kujua walikokuwa mama zao
- msenaji : kiongozi wa kidini aliyeongea kwa lafudhi ya kizungu kwa: wakimbizi
mahali : kambi ya wakimbizi
sababu : walikuwa wamewaletea misaada
- msenaji : uk 188 mwaliko akisema kimoyomoyo
Mahali: hoteli ya majaliwa
Sababu: alikuwa amewatambua nduguze 28)msenaji : uk 189 Umu
kwa : kwa familia yake Mahali: hoteli ya majaliwa
Sababu: alikuwa na furaha ya familia yao kupatana
- msenaji : uk 192 mwandishi akimrejelea Naomi kwa wanawe Sababu: baada ya kuwatafuta kila mahali akiwakosa
- msenaji : mwanaharakati Tetei kwa : wahafidhina
Mahali: nchi ya wahafidhina
Sababu: hakupenda mwekevu kuchukua ule wadhifa wa uongozi FOR MORE RELATED LEARNING MATERIALS, 0714497530
MAJIBU YA WAHUSIKA NA UMUHIMU WAO
RIDHAA.
Ni mumewe Terry. Babake Mwangeka Tila na Kim Mwenye bidii ni daktari ambaye alifanya kazi kwa uadilifu Msomi amesomea udaktari
Mwenye uhusiano mwema anakula pamoja na majirani Mshirikina anahusisha milio ya bundi jambo mbaya kutokea Mwenye mapenzi anawapenda wanawe sana
Mkarimu anasaidia jamii kwa kujenga hospitali
Amepevuka anasema iwapo hakutakuwa na njia madhubuti ya kusuluhisha migogoro kunaweza shuka shida tena
Mvumilivu navumilia kuona mabaki ya kuteketezwa kwa familia yake TERRY
Mcheshi mwandishi anasema hanyamazi kwa ucheshi wake Mfariji alikuwa anamfariji Mwangeka kwa nyimbo zake za kidini MWEKEVU
Amezinduka kwa kushindania wadhifa wa kisiasa na mwanamume
Ni jasiri haogopi kusemwa kwa watu
Ni mzalendo historia yake ya kazi ilionyesha kuwa anafanyia wananchi kazi vyema Mwenye maono sera zake zilipendwa na watu
Mwenye matumaini licha ya ushindi wake kupingwa ana matumaini MZEE KEDI.
Ni jirani yake Terry na Ridhaa ambaye alisababisha vifo vya familia ya Ridhaa TILA
Mwanawe Ridhaa aliyefia katika mkasa wa moto. Amepevuka anajua nguvu za vijana ni kama nanga Amezinduka anajua kuwa bado wafidhina hawajapata uhuru Ni msomi anaelewa masuala ya sharia kwa kina
Ni mzalendo anasema wanahitaji kiongozi ambaye atapeleka jahazi kwenye visiwa vya hazina
MZEE MWIMO MSUBILI.
Huyu ni babake Ridhaa.
Ni mtamaduni anaoa wake wengi
Ni mkali anaogopwa sana na Mwangemi na Mwangeka Ni mwenye bidii kwani mtu kuilisha familia kubwa NAOMI.
Alikuwa mkewe Lunga na mama wa Umu, Dick na Mwaliko
Mwenye tamaa anamuacha mmewe kwa sababu ya ukosefu wa pesa Mwenye dharau anadharau mmewe na kumwacha kwenda kutafuta kazi Mwenye bidii amefungua duka la kunukulisha karatasi karibu na chuo kikuu Mwenye majuto anajuta kwa nini alimwacha mmewe na watoto wake
Mwadilifu anakataa kufanya mapenzi na mwajiri wake LUNGA
Alikuwa mumewe Naomi
Mwenye mapenzi kwa mkewe na wanawe
Mzalendo anaamua kuachishwa kazi ili watu wasipewe unga umeharibika Mvumilivu anavumilia hali ngumu licha ya kuwa alikuwa na kazi nzuri Mlezi mwema analea watoto wake hadi mauko yake
Msomi alikuwa amesomea masuala ya kilimo UMULKHER1 (UMU)
Mtoto wake Lunga na Naomi
Ni msomi amefanya shahada ya uhandisi katika kilimo Amepevuka anaripoti kwa polisi baada ya kupotea kwa nduguye
Ni mwenyemapenzi ya dhati kwa ndugu zake na wazazi wake wa kupanga Mwenye bidii anasoma kwa makini hadi anaenda chuo kikuu
Mwenye shukrani anawashukuru wazazi wake wa kupanga Mwenye huruma anawahurumia ndugu zake
Mwenye utu anaomba mamake pesa ili amsaidie Hazina kijana wa mtaani SAUNA
Kijakazi aliyekuwa akiwaangalia Umu, Mwaliko na Dick Ni mnafiki anajifanya kuwa mtiifu ili aibe watoto
Ni katili anajiuzisha na ulanguzi wa watoto
Ni mtiifu anatii kila jambo alapewa na mkuu wake HAZINA
Huyu ni kijana ombaomba wa mitaani aliyesaidiwa na Umu Mwenye utu anawajibika kumsaidia Umu
Mwenye bidii anafanya kazi katika hoteli Ni msomi amesomea masuala ya upishi KAIRU
Ni mwanafunzi katika shule ya akinaUmu. Ni mwathiriwa wa uhasama wa kikabila. Mamake ni muuzaji wa samaki ambaye hamudu kulipa karo vizuri
Ni mwenye mashauri anamshauri Umu kuwa yeye amebahatika na hasijisumbue na mawazo
Ana uvumilivu ana vumilia kuishi maisha ya taabu na mzazi wake Mwenye matumaini anamin I kuwa elimu ndiyo itakayomwokoa Ni mwenye bidii anatia bidii masomoni
MWANAHER1
Huyu ni mwanawe mzee Kaizari nduguye Lime
Ni mpenda mashairi ana kipawa cha kughani mashairi Mwenye bidii anatia bidii masomoni
Ni mshauri anamshauri Umu na wenzake shuleni Ni msomi pamoja na wenzake kama Umu na Kairu
Ni mvumilivu anavulia kusoma licha ya uovu aliofanyiwa genge Mwenye matumaini kuwa elimu itaweza wasaidia
MWALIKO
Mwanawe Naomi na Lunga
Mwenye bidii amesoma hadi kiwango cha uzamili
FOR MORE RELATED LEARNING MATERIALS, 0714497530
Ni msomi amefanya shahada ya uzamili ya isimu na lugha Ni mtiifu anawatii wazazi wake
Mwenye shukrani anawashukuru wazazi wake wa kupanga yaani Neema na Mwangemi Mwenye matumaini kuwa siku moja atawaona nduguye
DICK
Msamehevu anamsamehe mamake na Sauna
Mwenye shukrani anawashukuru Apondi na Mwangeka Mwenye bidii anafanya kazi ya teknolojia
Mwenye mapenzi ya dhati kwa nduguze
Amezinduka anajua hatari za ulanguzi wa dawa za kulevya BWANA MAYA
Baba wa kambo wa Sauna aliyemsababishia ujauzito Ni katili analala na mtoto wake
Ni mpyoro anatumia lugha yenye matusi
Mwenye taasubi ya kiume anampiga mkewe sana MWANGEKA
Ni mwanawe Ridhaa na Terry. Ni mmewe wa lily na hapo baadaye Apondi. Ni babake Becky , Don Ridhaa na baba wa kupanga wa Sophie na Umu
Ni msomi ana shahada ya uhandisi
Ni mlezi mwema analea familia yake vizuri Ana uhusiano mwema na familia yake
Ni mzalendo anaenda mashariki ya kati kuleta amani Ni mwenye mashauri anamshauri Dick
Ni mkarimu anaonyesha ukarimu kwa umu na nduguye Dick MWANGEMI
Ni mmewe neema na baba wa kupanga wa Mwaliko
Ni mkarimu anaonyesha Mwaliko ukarimu kwa kumpanga Ni msomi ana shahada ya udaktari
Mwenye upendo kwa mkewe na Mwaliko Amepevuka anamshauri mkewe kupanga mtoto Ni mcheshi waliishi kucheza na Mwangeka utotoni
UMUHIMU WA WAHUSIKA HAWA NI KUENDELEZA MAUDHUI NA VIELELEZO VYA WANAJAMII WENYE WASIFU KAMA WAO.
MAJIBU YA MBINU ZA LUGHA NA TAMATHALI ZA USEMI JAZANDA.
- Tila anapomwambia babake kuwa nchi ya Wahafidnina ni watoto wa miaka hamsini inamaanisha wao bado ni wategemezi licha ya kupata uhuru uk 6
- Aidha Tila anamwambia babake wanahitaji kiongozi yeyote awe wa kike au kiume ila kama ataweza kulielekeza jahazi katika visiwa vya Jahazi kwa maana ya nchi na visiwa vya hazina ni kuimarika kiuchumi uk 40
- Baada ya kuangamizwa kwa familia ya Ridhaa anaelewa maana ya vijikaratasi vilivyokuwa vikisambazwa kuwa kutakuwa na gharika baada ya kuapishwa kwa musumbi uk12
- Lunga anatumia neno Eden kurejelea mahali pazuri pa wanyama
- Mamake Ridhaa anamwambia unyonge haukuumbiwa majimbi ila makoo yaani majimbi ni wanaume na makoo wake uk3
- Kuikolesha nundu mafuta kuonyesha kuwa mhafidhina hasaidiki kutokana na mzungu
- Mshahara wanaopewa wahafidhina unitwa mkia wa mbuzi yaani mdogo uk 44
- Ridhaa baada ya familia yake kuangamia haamini kuwa Mwangeka angerudi anasemekana ameumwa na bafe uk46
- Ridhaa anasema bila jamii kushirikiana amani waliyokuwa nayo ni ya kifaurongo tu uk50
- Uchafuzi uliotokea baada ya uchaguzi Ridhaa anasema vijana waliweza kuligongesha jahazi mwamba badala ya kuliongoa uk49
- Ridhaa anamwambia Mwangeka mwanya wake wa meno uliopendeza sana ndi ndoana aliyotumia kumvulia mamake uk 48
- Ridhaa alitamani mwanawe awe na mapenzi aweze kuoa tena anasema anjua siku moja atapata hurulaini ambaye ataponya kiharusi
- Aidha anasema hurulaini huyo atafungua kufuli iliyofunga moyo wake uk 111
- Selume anapolia kwa kuacha mwanawe Ridhaa anamwambia asilie kwani ata kama samba ni mkali vipi ni mhali kumrarua
TASHIHISI
- UK28 Msongamano wa vibanda kwa jitimai
- Uk 24 vifua vyao vilikabiliana na risasi zilizorashiwa vifuani mwao kama marashi
- Uk 29 matumbo yalianza kudai haki
- Uk20 vitoa machozi vinafanya kazi barabara
- Uk 19 wimbi la mabadiliko kuvamia jamii
- Uk 15 mawingu yaliyoshiba kutaka kutapika
- Uk 46 ndege ya PANAMA inapiga pambaja sakafu
- Uk 48 kudekeza fikra
- Uk 45Faili zake zitakapopatikana zilikojifungia
- Uk 85 kutafuta haki ilikojificha
- Uk 78 kuyambia macho yake yatoke uko yalikokuwa yamejificha
- Uk 85 baridi ya vuli ilikuwa ikimtafuna
- Uk 169 alikumbatwa na ukiwa na umaskini
- Uk 147 maumbile yameanza kufanya kazi yake MAJAZ1
- Nchi ya wahafidhina inamaana wasiotaka mabadiliko katika nchi hii mtu ka Tuama hataki babadiliko ya kuacha tohara kwa jinsia ya kike
- Ridhaa kwa maana ridhika mhusika huyu anaridhika na hali yake baada ya mkasa uliompata
- Shamsi ni jua la asubui linapotokea ambalo hakuna mtu ambaye huwa halioni. Mhusika huyu alipokuwa akija kila mtu alikuwa akijua amefika kutokana na nyimbo zake za majisifu
- Bw Tenge kwa maana ya kwenda Matendo yake ya ukware yanaonyesha kwenda kombo na ahadi ya ndoa yake
- Mwekevu Tendakazi ni mwanamke aliyeweza kuwatumikia watu kwa kuwafanyia kazi vizuri kuliko mpinzani wake
- Mwalimu Dhahabu kitu cha maana Mwalimu huyu amekuwa wa muhimu sana kwa kuwasaidia watoto shuleni
- Hazina ile hali ya kuhifadhi vitu vya dhamana, Umu anampa mia mbili iliyomfanya amsaidie baadaye na kumpa makao katika upweke wake
- Mtawa Cizarina Neno mtawa lina maana ya mcha Mungu . alijitolea kulea watoto waliokuwa wametupwa na wazazi
- Hoteli ya majaliwa ni mahali watoto wa Lunga wote waliweza kukutanika
- Mji wa Afueni mji ambao ulikuwa mji wa kifahari wa matajiri
- Msitu wa simba ni msitu ambao maisha ya Lunga yanaharibikia na kukata kamaba
- Msitu wa heri sehemu ambayo ilikuwa na rotuba nzuri ya kulima
- Zohali hali ya kuchelewa kufanya jambo kwa sababu ya ugumu Fulani anachelea kusema kuwa ana wazazi kwa sababu walimtesa
- Mhusika Kangata neno hili lina maana kushikilia jambo Fulani anashikilia jina la mwajiri wake ambaye ni Kiriri hadi anadhaniwa kuwa ni wa aila
- Bw Kero huyu ni babake halisi wa Sauna kwa sababu ya kero zake za ulevi wanaachana na mkewe na kwenda kuolewa na Maya
- Bw Maya maana yake ni Kitendo chake cha kulala na Sauna mwanawe na kumtia ujauzito kilimtia hamaki sana na kutoroka kwao
- Mji wa Tokosa ndiko alikozaliwa Neno hili linamaana ya kuchemsha chakula ovyo tu. Malezi yake yalikuwa ovyo hadi kufumuzwa kwake kwa kutoshabihiana na babake
- Mhusika Neema alikionea neema kile kitoto kilichokuwa kimetupwa na kukipeleka makao ya watoto baada ya kuripoti kwa polisi
TASWIRA
- Uk 13 kubomolewa kwa nyumba ishirini katika mtaa wa Tononokeni
- Uk 109 mwangeka na mkewe wakiangalia watoto wao wakiogelea
- Uk 21 gari lilichomwa na watu wakiwa ndani
- Uk 20 vijana wanabeba mabango ya mpinzani wa Bi Mwekevu
- Tindi anavyonengua kiuno katika sherehe
- Umati wa watu wanaomchoma Lemi
- Taswira ya kaburi la Lunga Naomi anaporudi kuwatafuta wanawe MASWAL1 YA BALAGHA
- Uk17 lakini ni wangapi mnatambua hata maghulamu wanalawitiwa?
- Uk 192 kipi kilichonipa kumkimbia Lunga wangu wakati ambapo alinihitaji zaidi?
- Uk 25Wapi kile kidume chako kijoga?
- Uk 12 je, si mchango tosha wa mtu kuitwa ndugu hata angawa mgeni?
- Uk40 nani kasema viongozi waliopo hawajajikuna wajipatapo?
- Uk 41 serikali haijagharamia elimu ya shule za upili kwa kugharamia karo ya shule za kutwa?
- Uk 65 kipi kinachovuta raia kuhamia nchi za ughaibuni?
- Uk 66 Mlikuwa wapi wakati huo?
- Uk 123 kwa nini akatumia kijakazi Sauna kuja kusambaratiza familia ya baba?
- Uk 78Kwetu? Kwani mimi nina kwetu tena?
- FOR MORE RELATED LEARNING MATERIALS, 0714497530
- Uk 176Mungu wangu! Huyu si ndugu yangu mwaliko?
- Uk 18Tangu lini mwanamke akashinda uchaguzi?
- Uk 164 je, ikitokea kuwa nasaba yao ni watu wenye kifafa au hata wendawazimu?
KINAYA
- Ni kinaya Sauna kujifanya mzuri ilhali anawaiba wattoto
- Ni kinaya Neema kupeleka mtoto kwa makazi ya watoto na mwishowe kwenda kupanga mtoto huko
- Ni kinaya Naomi kutoroka mmewe nawanawe ilhali hapo baadaye anajilaumu
- Ni kinaya nchi ambayo ina miaka hamsini kuonekana kama mtoto wa mika hamsini
- Ni kinaya kuwa wafrika wanakuwa wafanyikazi katika mashamba yao chini ya wakoloni
- Ni kinaya watu walioishi na Ridhaa kwa amani wanawageukia na kuchoma nyumba yake pamoja na familia yake
- Ni kinaya vijana kumbaka lime na Mwanaheri mbele ya wazazi wao
- Ni kinaya mamakwe kufukuza subira kwa kuwa hawakuwa wa jamii moja
- Ni kinaya mzee Maya kumbaka mwanawe Sauna
- Ni kinaya wazazi wa Zohali ambao ni wasomi kumtesa Zohali kwa ajili ya ujauzito
- Ni kinaya Tuama kusifu utamaduni wa tohara za kike ilhali ndio sababu ya kuwa hospitalini
- Ni kinaya watu wan chi ya Wahafidhina kumkataa kiongozi wa kike na ndiye anayewafanyia kazi
- Ni kinaya kwa pete kutaka kujia kwa kuwa na watoto watatu akiwa umri wa chini ya mia ishirini na moja
MBINU REJESHI
- UK3 Ridhaa anakumbuka mlipuko na kilio cha mkewe
- Uk 1-2 anakumbuka milio ya kereng’ende na bundi
- Uk 10 anakumbuka jinsi watoto walivyomtenga shuleni
- Uk 13ana kumbuka majumba yake yakibomolewa
- Uk 45 anakumbuka mijadala aliyokuwa akifanya na mwanawe Tila
- Uk 187 Mwangeka anakumbuka mafunzo ya dini
- Kaizari anasimulia Ridhaa jinsi familia yake ilivyovamiwa
- Uk 96 Mwanaheri anakumbuka kwenda kwa mamake kupitia barua
- Uk 177- 178 mwangeka anakumbuka maisha yake na Mwangemi utotoni
- Kijana aliyekuwa amevaa shati ambalo lilikuwa limeandikwa Hitman anaeleza jinsi ambavyo aliwandanganya vikongwe kumchagua kiboko ambaye hawakumtaka
MATUMIZ1 YA BARUA
- Uk 72 Barua iliyoachisha Lunga kazi
- uk 81 Mkewe Lunga ana mwandikia barua ya kumuaga mmewe
- UK95 Barua hii inaandikwa na Subira kwa mmewe na wanawe Mwanaheri na Lime TAHARUK1
- Anwani chozi la heri ina taharuki kwani msomaji anatakakujua nanni huyu anatokwa
na chozi la heri
- Mwandishi hatuambii baada ya kufungwa kwa Sauna na Kangara kama walibadilika
- Kuna taharuki kama Zohali aliwahai kuelezea kama alikuwa na wazazi
- Kuna taharuki kama Tuama aliweza kuamini umuhimu wa kutopaswa tohara kwa jinsia ya kike
- Kuna taharuki chandachema kama aliwahi kujiwa na wazazi wake
- Kuna taharuki kama wana wa Naomi waliwahi mkukutana naye
- Kuna taharuki kama ya wenzake Umu katika shule ya Tangamano waliweza kufaulu katika masomo
- Kuna taharuki kama Ridhaa aliweza kuoa
- Kuna taharuki kama Mwangemi na Neema walifanikiwa kumzaa mwanao
- Kuna taharuki kama Buda aliyekuwa amemwajiri Dick aliwahi kutiwa mbaroni SADFA
- Inasadifiana kuwa wakati Selume anapotaka kiacha kazi katika hospitali ya umma ndio Ridhaa anamaliza kujenga hospitali ya mwanzo mpya
- Siku ya kuzaliwa kwa Umu inasadifiana nay a Mwangemi
- Inasadifiana wakati Neema akienda ofisini anakiona kitoto kilichokuwa kimetupwa
- Umu na Dick wanakitana kisadfa katika uwanja wa ndege
- Ni sadfa Mwaliko kupangwa na binamuye mwangeka aliyempanga nduguye
- Inasadifu kuwa Dick alipokuwa akiwaza juu ya nduguye Umu alikuwa nyuma yake
- Kukutana kwa wana wa Lunga katika hoteli ya Majaliwa ni sadfa
- Ni sadfa kuwa Umu anapowaza sana juu ya maisha yake wenzake wana matatizo kumliko