MWONGOZO WA BEMBEA YA MAISHA UTANGULIZI
VIGEZO MUHIMU KATIKA UCHAMBUZI WA TAMTHILIA HII
- Dhamira/ Lengo/ Mintarafu/ Kusudi: Nijambo linalokusudiwa na mwandishi/ lengo kuu la
- Maudhui: Jumla ya maswala yanayozungumziwa na mwandishi
- Falsafa: Msimamo wa mwandishi kuhusu jambo fulani
- Muwala: Mtiririko wa vitushi/ mawazo katika kazi ya
- Usuli: Asili /hali inayomzunguka mwandishi na ambayo humchochea kuandika kazi ya fasihi k.m. usuli wa mwandishi waweza kuwa anazungukwa na jamii iliyojaa uongozi mbaya / ufisadi ndiyo maana anaandika kuhusu maudhui
- Mandhari: Mahali ambapo wahusika wanatekelezea kazi ya K.m. njiani, shuleni n.k.
- Wahusika: Ni viumbe ambao huendeleza mawazo ya mwandishi katika kazi ya Wahusika waweza kuwa binadamu, Wanyama, viumbe halisi au wa kidhahania (wa kufikirika tu).
AINA ZA WAHUSIKA KATIKA FASIHI
- Wahusika wakuu
- Huchukua nafasi kuu na kukuza kazi ya
- Matendo yote muhimu
- Dhamira kuu ya mwandishi na falsafa/ msimamo wake hudhihirika kupitia kwa wahusika
2)ย ย ย Wahusika wadogo
- Hawana nafasi
- Aghalabu husaidia hadhira kujua zaidi mhusika mkuu na dhamira
3)ย ย ย Wahusika wasaidizi
- Hujenga wahusika wakuu na kukuza Aghalabu huja na kutoweka baada ya muda mfupi.
- Uainishaji Mwingine wa Wahusika
4)ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย ย Wahusika bapa/ Wahusika wa mraba mmoja
- Huwa hawabadiliki katika hulka/ sifa
- Mhusika bapa anaweza kuwa na tabia nzuri au hasi kuanzia mwanzo hadi
5)ย ย ย Wahusika duara/ wahusika wa miraba minne
- Huweza kubadilika
- Huwa na sifa
- Wahusika bapa vielelezo
- Huwa na tabia za kubadilika ila hujikita katika mtazamo wa mwandishi na hadhira
- Aghalabu huwa wahusika wakuu na hutumiwa na mwandishi kuendeleza suala fulani.
6)ย ย ย Wahusika bapa sugu
- Wana sifa ya kutobadilika ila huwakilisha walio na tabia potovu katika Mhusika bapa sugu anayeweza kuwa mhusika mkuu.
7)ย ย ย Wahusika hasidi/ wapinzani
- Hulka zao ni kinyume na mtazamo wa maadili ya
- Humpinga mhusika
8)ย ย ย Mhusika nguli
- Ni mhusika anayekinzana na mhusika hasidi kwani anawasilisha maadili katika kazi ya fasihi. Aghalabu huwa mhusika mkuu au mmoja wa wahusika wakuu.
9)ย ย ย Mhusika shinda
- Hukuza wahusika wengine kwa kuwa hupelekwa mbele kwa usaidizi wa wahusika wengine.
- Huwa chini ya kivuli cha mhusika
- Kupitia kvake ndipo hadhira inapata sifa bayana za wahusika
FANI ZA FASIHI/ MITINDO KATIKA FASIHI
Fani ni mbinu ambazo hutumiwa na mwandishi anapoiandika kazi ya fasihi. Fani hujumuisha:
- Mitindo ya lugha: Pia huitwa matumizi ya lugha, mitindo ya lugha, tamathali za lugha, mbinu za lugha au tamathali za
- Mintindo ya uandishi: Pia huitwa fani za mwandishi, mbinu za uandishi, mbinu za sanaa au mbinu za
FANI ZA LUGHA (TAMATHALI ZA USEMI)
Ni maneno, sentensi au misemo inayotumiwa kuwasilisha kazi ya fasihi. (Senkoro; 1982). Zinajumuisha:
- Takriri/ Uradidi (Repetition): Takriri ni mbinu ya lugha ambayo kwayo maneno au silabi fulani Lengo kuu la takriri huwa ni kusisitiza jambo fulani na kuwavutia wasomaji wawazie jambo hilo.
- Maswali Balagha/ Mubalagha (Rhetoric; questions): Haya ni maswali ambayo hayahitaji majibu. Jibu la swali la balagha huwa akilini mwa anayeulizwa au anayesoma kazi fulani ya fasihi au huwa tayari analijua. Dhima ya maswali balagha huwa kutoa mawazo au hisia za ndani za mhusika au kuweka jambo fulani Aidha hulenga kusisitiza usemi fulani na kuwasilisha maudhui.
- Methali: Ni kauli fupi ya kimapokeo inayosheheni maana na ujumbe na ambayo huwa na mizizi katika jamii. Methali huwa na wingi wa hekima na hutumiwa kupigia mfano. Huwa na maana
- Tanakali ya sauti: Ni mbinu ambapo mwandishi huiga tendo fulani na kulipa matamshi au
- Tashbihi/ Tashbiha/ Mshabaha: Ni ulinganishi/ umithilishaji (usio wa moja kwa moja) wa kitu na kingine kwa kutumia maneno kama vile: ja, mfano wa, mithili ya, kama, sawasawa, ungedhani ni k.
- Istiara/ Sitiari: Ni ulinganisho wa kitu na kingine kwa njia ya moja kwa mojae Ulinganishi huu hufanywa bila kutumia
- Nidaa: Ni maneno ambayo hutumiwa kuonyesha hisia za Hutumika kuonyesha hisia za furaha, huzuni, masikitiko, mshangao, mshtuko n.k.
- Jazanda: Mwandishi hutaja kitu fulani ambacho kwa kawaida kinaweza kuonekana kuwa na maana ya kawaida ila kinapochunguzwa zaidi kinaonekana kuwa na maana ya ndani kuliko ile ya kawaida. Jazanda ni sawa na kilichositiriwa ndani mwa neno au maneno
- Mdokezo: Mbinu ambapo mhusika mmoja hutaja jambo kisha mwenzake hulikamilisha au mhusika hutoa wazo/ jambo na kumwacha msomaji Aidha, mdokezo waweza kutokea palipo na upinzani ambapo mhusika mmoja anaweza akatoa jambo huku mwenzake akilikamilisha atakavyo kwa kumpinga au kumkejeli.
- Tabaini: Tabaini ni mbinu ya lugha ambapo mwandishi hutumia maneno kueleza jambo linaloeleweka waziwazi na Ni maelezo ya kina kuhusu j ambo. Waandishi wengi hutumia takriri/ neno moja ili kuibua tabaini. K.m. urudiaji wa ‘ni’ na ‘si’. K.v. Walifika watu wa janibu mbalimbali: si wanawake, si wanaume, si vijana, si watoto โ wote walijumuika kumuaga gwiji wa taarabu.
- Taniaba: Taniaba yatokana na ‘kwa niaba ya’. Kitu/ Jambo hutumiwa kuwakilisha au kufanya kwa niaba ya kitu/ jambo K.m. chaki ni taniaba ya mwalimu; jembe ni taniaba ya mkulima ilhali bunduki ni taniaba ya askari.
- Utohozi: Ni mbinu ya kuswahilisha maneno ya lugha nyingine ili yatumike kama ya K.m. skwota โ Squatter, ekisirei X-ray n.k.
- Tasfida/ Tauria/ usafidi (Euphemism): Matumizi ya lugha ya adabu/ ya sitara/ ya nidhamu. K.m. Natoka kutabawali (Haja ndogo) badala ya natoka kukojoa; Alijifungua badala ya alizaa k.
- Chuku/ Udamisi (Exaggeration/ Hyperbole): Mbinu ya kuongeza chumvi katika jambo. Mwandishi hueleza jambo kwa namna inayozidi hali halisi ya jambo K.m. watu waliohudhuria matanga walikuwa wamcjaa pomoni hivi kwamba hapakuwa na nafasi ya nzi kupita.
- Ucheshi/ Kichekesho (Humour): Maneno yanayozua furaha. Msomaji hucheka kutokana na namna mwandishi alivyolieleza
- Kejeli: Pia huitwa dhihaka, kebehi, stihizai au Ni kumfanyia mtu, jambo au kitu dhihaka au kumdunisha mtu au kitu kwa kuonyesha kuwa anachosema hakina thamani.
- Lakabu: Mbinu ya mhusika kupewa au kubandikwa jina na wahusika wengine au yeye mwenyewe kujibandika jina linaloambatana na sifa
- Kuchanganya ndimi (Code mixing): Pia inaitwa kuchanganya lugha, kuchanganya msimbo au ndimi Ni mbinu ya kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. K.m. Sina time ya wanawake.
- Kubadili msimbo (Code switching): Pia huitwa kuhamisha msimbo, kuhamisha ndimi au kuhamisha Ni mbinu ya kuchopeka sentensi ya lugha
nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Utofauti kati ya kuchanganya ndimi na kubadili ndimi ni kuwa katika kuchanganya ndimi, mwandishi huchanganya maneno ya Kiswahili na lugha nyingine katika sentensi moja ila katika kubadili ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi sanifu za Kiswahili.
- Ritifaa: Ni mbinu ya kuzungumza na mtu asiyekuwepo au K.m. Mbona umeamua kuniacha duniani?
- Taashira (Symbolism): Ni mbinu ya kutumia lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani.
- Majazi: Mwandishi huwapa wahusika majina yanayoambatana na tabia au hulka
FANI ZA UANDISHI (MBINU ZA SANAA)
- Taharuki (Suspense): Ni mbinu ya kumpa msomaji hamu/ tamaa ya kuendelea kusoma ili kujua kitakachofanyika
- Sadfa (Coincidence): Matukio mawili hutokea kwa wakati mmoja bila kutarajiwa, kupangwa au
- Barua/ Waraka: Wahusika huandikiana Nyimbo na Mashairi
- Ndoto/ Njozi/ Ruiya: Maono ya mhusika akiwa
- Uzungumzi nafsia/ Mjadala nafsia: Mhusika hujizungumzia
- Mbinu rejeshi/ Kisengere nyuma: Mwandishi hurejelea mawazo ya msomaji kwa matukio ya awali hasa kupitia kwa
- Kinaya: matukio katika kazi ya fasihi kuwa kinyume na matarajio ya msomaji au hali
- Usemaji kando: Mhusika anayezungumza na wenzake hutafuta faragha labda kwa kuzungumza bila kumhusisha mwenzake au kupinda kichwa. Mhusika mmoja anaweza kuwa anamsengenya mwenzake/ au anapinga maoni ya mhusika
- Tadmini: mbinu ya kuchukua mtindo wa lugha au maneno kutoka kwa matini nyingine na kuweka katika matini fulani. Kwa mfano kuchukua vifungu vya Biblia kutoka matini ya Biblia na kuyatumia katika K.m. Amini amini nakwambia. (Kigogo).
- Hotuba: mazungumzo ambayo hutolewa kwa hadhira na mtu Mazungumzo haya aghalabu huhusu jambo maalum.
- Tashihisi: pia huitwa uhuishi, uhaishaji au uhuishaji. (Personification): Ni mbinu ya kuvipa vitu visivyo na uhai sifa za au kutenda kama kitu kilicho na
- Utabiri/ ubashiri: Ni mbinu ya kueleza kuhusu mambo ambayo yatatokea
- Mhusika ndani ya mhusika: mhusika fulani huiga maneno au matendo ya mhusika mwingine na kutenda kama
- Mbinu maarifa mtambuka: Msanii kuingiza maarifa ya taaluma (uwanja mwingine wa kitaaluma) katika kazi yake.
- Taswira: Ni mbinu ya mwandishi kutoa maelelzo kuhusu jambo au mtu yanayojenga picha (Mawazo ya akilini) ya jambo au mtu huyo hivi kwamba msomaji huona picha kamili ya kitu/ jambo au mahali Dhima ya taswira huwa kumwezesha msomaji aelewe zaidi jambo husika.
Aina za taswira
- Taswira muonjo/ mwonjo: msanii anaweza kutueleza namna chakula kilionjwa hadi msomaji akataka adondokwe na mate.
- Taswira oni: msanii hutoa maelezo hadi msomaji akaona picha ya kitu/ jambo fulani
- Taswira hisishi: msanii anaweza kueleza hisia za mhusika fulani kama furaha, majonzi n.k.
- Taswira msanii anaeleza jinsi ambavyo alisikia jambofulani kwa
- Taswira mnuso: msanii anaeleza mambo kuhusu harufu anayoingiamua kupitia pua,
- Taswira mguso; msanii anaeleza alivyohisi kwa
Katika maandalizi ya kuukabili mtihani(kuyajibu maswali), ni vyema mwanfunzi azingatie mambo yaliyo hapa chini ili aweze kuyamudu maswali yatakayotokana na kazi anazozishughulikia.
Isome kazi mara kadhaa ili kuifahamu kazi husika ndani nje. Kuisoma kazi mara moja na kujidanganya kuwa umeielewa si vyema. Hakikisha kuwa umeyafahamu mambo yote muhimu katika kazi ya fasihi na kuyahifadhi katika ncha za kucha zako(yakumbuke kwa urahisi).
Wakati wa kusoma kazi hizi, hakikisha kuwa una penseli ili kupiga nmstari mambo yote muhimu k.m mbinu za lugha, wahusika, nk. Vile vile hakikisha unaongeza pembeni mambo yote muhimu yanayojitokeza unapoendelea kutagusana na kazi. Fahamu kuwa sehemu hizi tatu hutahiniwa. Kila sehemu hubeba alama 20.
Wakati wa kuyajibu maswali ya mtihani, mwanafunzi achague maswali ambayo anayamudu vilivyo ili kujizolea alama nyingi zaidi.
Mwanafunzi vilevile asipuuze mambo mawili yafuatayo wakati wa kuukabili mtihani;
Hati
Hati ni mwandiko yaani namna mtu anavyoandika. Hati huwa kigezo muhimu sana katika mtihani. Ni vyema mwanafunzi aandike kwa hati inayosomeka vyema kwa urahisi. Ukiandika kwa hati ‘nadhifu’ mtahini hatatatizika kuisoma kazi yako wala kutumia muda mwingi akijaribu kuisoma kazi yako. Ni vyema uzingatie namna ulivyofundishwa kuandika herufi katika chekechea. Herufi zingine zisizoeleweka ambazo wanafunzi huweza kuandika si za Kiswahili na hazina maana katika Kiswahili, ziepuke.
Makosa ya kisarufi
Japo makosa haya hayaadhibiwi katika karatasi hii ya 102/3, ni vyema mwanafunzi ayaepuke mno. Makosa haya yakikithiri yanaweza kuupotosha usahihi wa jibu kiasi cha mtahini kuamua kukuadhibu na bila shaka utakuwa umepoteza alama. Makosa mengine ya kuingiza herufi zisizo za Kiswahili kama vile ‘X’, ‘C’ nek katika kuendeleza maneno ya Kiswahili visivyo pia hupotosha umantiki na usahihi wa jawabu.
JINSI YA KUKABILIANA NA MASWALI
Baada ya kuisoma kazi yoyote ile ya Fasihi Andishi, mtihani hufuata. Kwa hivyo ni vyema kujihama na mbinu za kuyakabili maswali.
Mwanzo, fanya utafiti zaidi kuhusu usuli wa kazi unayasoma, falsafa au mtazamo wa mwandishi n.k. Ihakiki kazi yenyewe kwa undani ili kuhakikisha umeelewa maudhui, wahusika, matumizi ya lugha, mandhari na fani nyingine zilizomo. Ili kujitayarisha kuyajibu maswali katika mtihani wa fasihi, ni muhimu kuelewa kuhusu Uteuzi wa maswali.
Tatizo kubwa linalowakumba watahiniwa katika mtihani wa fasihi ni uteuzi wa maswali. Kati ya maswali saba yanayotahiniwa, mtahiniwa anatakiwa kuchagua maswali manne.
Ikumbukwe kuwa Riwaya, Tamthilia na Hadithi Fupi ni kati ya maswali haya saba yaliyotahiniwa. Kwa hivyo, hakikisha unaangazia yafuatayo katika sehemu hii;
- Uzito wa swali – kadiria uzito wa maswali kwa kuangalia alama zinazotolewa kando ya Swali la alama 20 linahitaji hoja kumi zilizojadiliwa vyema.
- Hoja za kutosha. Usivamie maswali bila kuwa na hakika kama una hoja za kutosha kuyajibu kwani huenda utakwama Kama swali lina alama 20, hakikisha una hoja kumi zenye uzito.
- Kulielewa swali – Elewa swali na kuangalia kama lina vijisehemu. Iwapovijisehemuvyake vinahusiana na sehemu ya kwanza, jihadhari usije ukakosa kuonyesha uhusiano chukua muda kuchagua swali, kwa
- Kuchagua swali kuandika vidokezo vya kulijibia kando ya swali Ni vyema kuchagua swali ambalo utapata zaidi ya alama 15.
- Kuyaelewa maagizo kumbuka kuwa, maswali hutungwa ili kujibiwa kwa kuzingatia maagizo. Unapaswa kulichukua jukumu la kusoma, kuelewa na kufuata Kwa mfano, kuna maswali ambayo ni ya lazima, na maswali ya kuchagua. Kadhalika, maagizo hufafanua jinsi ya kuchagua maswali, k.v. jibu swali la tatu au la nne. Usijibu maswali mawili kutoka kitabu kimoja na kadhalika.
- Kuuelewa msamiati wa swali — pamoja na maagizo, zingatia pia msamiati wa Kwa mfano unapoambiwa – taja na ueleze, lazima uelewe kwamba, mtahini katika mwongozo wake wa kusahihisha, atakuwa na tuzo yakutaja mambo manne, kwa mfano, aghalabu utakuta neno manne limekolezwa wino.
Hakikisha kuwa una hoja nne zilizo sahihi. Iwapo utaandika hoja zaidi ya nne, mtahini atachukua hoja nne za mwanzo tu, hata kama umezikosea na hatatuza hoja zinazofuata japo zitakuwa sahihi.
AINA ZA MASWALI
Kuna aina mbalimbali za maswali. Kila moja yazo huwa na mahitaji yake. Kuna aina mbili za maswali yanayotokea katika tamthilia na vitabu vingine viteule: maswali ya insha na maswali ya muktadha wa dondoo.
Maswali ya insha huandikwa kwa nathari. Jiepushe na kudondoa hoja au kuziorodhesha. Wakati ambapo maswali ya insha yanahitaji majibu ya kina na hoja zilizofafanuliwa kikamilifu, yale ya muktadha yanamhitaji mtahiniwa awe ameielewa tamthilia kwa undani ili aweze kufafanua muktadha wa dondoo alilopewa bila kukatizika. Hii itamwezesha kulitambua dondoo lilikotolewa kwa urahisi.
Katika kufafanua muktadha wa dondoo, mtahiniwa anahitajika kujibu maswali manne kwa usahihi:
- Nani anaongea?
- Anaongea aongea na nani?
- Wakiwa wapi au katika hali gani?
- wanaongea kuhusu jambo gani?
JALADA LA BEMBEA YA MAISHA
Jalada ni sehemu iliyoko juu ya kitabu Huwa ni mambo yaliyo muhtasari wa kile msomaji anataraji ndani. Jalada huwa kuwili yaani, jalada la mbele na la nyuma. Kunavyo vipengele muhimu hasa rangi za michoro na maandishi.
Jalada la tamthilia ya Bembea ya Maisha limechorwa mwanamume na wanawake wawili wakiwa wamekumbatiana. Watu hao wameketi kwenye bembea. Mwanamume huyo anawakilisha Yona na wanawake hao wanawakilisha Sara na Neema.
Wote wanaonekana kufunga macho kuonyesha wako katika hali ya utulivu wa moyo. Hali hii ya kukumbatiana inadhihirisha kwamba kuna upatanisho wa familia ambayo ilikuwa imeyumbishwa na bembea ya maisha.
ANWANI YA TAMTHILIA
- Bembea ni kifaa kama vile ubao, kamba au chuma inayoninWinia baina ya chuma au mti ambacho hutumiwa kuchezea aghalabu na
- Bembea huenda juu na chini au mbele na Ili mtoto aweze kucheza na bembea, wakati mwingine kuna anayeisukuma bembea hiyo.
- Bembea ya maisha ni namna maisha yanavyoendesha
- Katika tamthilia hii, maisha yamesawiriwa kama Kuna wakati maisha ya wahusika yamejawa na furaha na mafanikio tele na kuna wakati maisha ya wahusika yanaenda chini, wanakumbwa na shida na matatizo.
Kwa mfano:
Maisha ya familia ya Sara na Yona yanaleta taswira ya bembea. Mwanzoni, ndoa ya Sara na Yona inaonekana yenye furaha. Hii ina maana kuwa, kama bembea inavyokuwa juu, maisha yao yalikuwa yenye mafanikio na furaha. Maisha yao yanaingiwa na dosari wakati wawili hao wanakosa mtoto baada ya kipindi kirefu katika ndoa. Zaidi ya hayo, wanajaliwa na watoto wa kike watatu. Hawajaliwi na mtoto wa kiume, kinyume na matarajio ya jamii. Wanachekwa, wanasutwa na kukejeliwa.
Bembea ya maisha yao inarudi chini. Sara anaanza kuchapwa kichapo cha mbwa na bwana yake Yona. Yona anaidharau familia yake na kuingilia ulevi, ulevi uliomfanya kupigwa kalamu kazini. Sara anasema, japo kuna wakati maisha yanabwagwa na bembea ya maisha, lazima maisha hayo yaendelee. Hata kama kamba, chuma au minyororo ya maisha inakatika, hawana budi kujiinua na kuendelea na maisha (uk. 20-21). Hivyo basi Sara anasimama na familia yake kidete akifahamu kuna siku atafanikiwa na maisha yao yatakuwa mema tena.
Maisha ya familia ya Yona yanabadilika kutoka kuwa maisha ya kukosa mahitaji ya kiuchumi. Bembea yao ya maisha ilionekana kuwachini. Baada ya Neema kufanikiwa na kupata kazi, bembea ya maisha yao inakuwa juu. Wanafanikiwa kujengewa nyumba, wanapata wafanyakazi wa kuwasaidia nyumbani na hata kuwa na jiko la gesi la kupikia.
Bembea ya maisha ya Neema inaonekana kusukumwa na Bunju mumewe. Kwanza Bunju alimsaidia Neema alipokuwa amepata ajali. Bunju alimtumia flying doctors ili aweze kupata matibabu zaidi (uk. 41).
Bunju anasaidia kuisukuma bembea ya maisha ya Neema kwa kumsaidia kuwasomesha dada zake. Vilevile, anamsaidia kuwajengea wazazi wa Neema nyumba.
Maradhi ya Sara yanaifanya bembea ya maisha ya Sara kuwa kama iliyokatika na kuwa chini. Sara anakosa matumaini ya kuishi na kutamani kufa.
Bembea ya maisha ya mjini huwa juu kutokana na maendeleo. Kuna maendeleo ya barabara, magari mengi, majengo mengi na hata sekta ya matibabu imeimarishwa.
Watu mjini wanapokea matibabu ya hali ya juu ilhali, bembea ya maisha ya kijijini huwa chini kwa sababu ya kukosa maendeleo hasa katika sekta ya matibabu na barabara nzuri. Sekta ya matibabu ya kijijini inamfanya Neema kumtafutia mamake hospitali ya mjini sababu zile za kijijini hazimpi mtu matumaini ya kutoka akiwa mzima ilhali za mjini zinampa mgonjwa matumaini ya kutoka akiwa buheri wa afya.
Dhamira ya mwandishi
ย
Dhamira huelezwa kama lengo au shabaha ya mwandishi wa kazi ya fasihi.
Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha anadhamiria:
ร kuonyesha masaibu ya pombe katika maisha ya familia
ร kuonyesha kuwa ili kujenga jamii mpya, mapinduzi ni muhimu na ni lazima wanajamii wajitolee kupinga tamaduni zisizo na umuhimu wowote katika maisha ya wanajamii
ร kutuonyesha kuwa watoto wa jinsia zote ni sawa na hawafai
ร kutenganishwa kwa mila na tamaduni za jamii
ร kutuonyesha kuwa hakuna lililo na mwanzo lisilokuwa na mwisho.
MTIRIRIKO WA MAONYESHO
Sehemu I Onyesho I
- Nyumbani kwa Sara, Sara ameketi kwenye kochi baada ya kumeza vidonge vya dawa kwa sababu ya maradhi Yona anayeonekana mchovu na mwenye kukinai anaingia kwa nyumba.
- Onyesho linaanza kwa kuonyeshwa namna Yona asivyofurahia hali katika nyumba yake. Analalamikia Sara kuwa hajamwandalia chakula. Yona hababaishwi na hali ya Sara ya ugonjwa, haja yake ni chumba kivuke Sara anamweleza namna mwili wake ulivyo, hapo mazungumzo kuhusu mwana wao, Neema, yanaanza. Yona anatoa wazo lake kwa Sara amwite bintiye aje ampeleke hospitalini. Sara anakataa wazo hilo kwa kukiri kuwa bintiye ana familia yake ambayo anafaa kuishughulikia.
- Maoni ya Sara yanazua mgogoro baina yake na Yona kuhusiana na mtoto wao Yona anashikilia kuwa ni jukumu la bintiye kuwajibikia matibabu ya mamake, naye Sara anashikilia kuwa bintiye ana majukumu ya kwake na tayari amewafanyia mengi, kwa hivyo, awachwe apumzike.
- Mgogoro huu unasawazishwa onyesho linapoelekea Sara na Yona wanakubaliana kuwa wanafaa kumpa binti yao baraka zao.
- Onyesho linamalizika kwa kuonyeshwa Yona akirejelea suala la Sara anamweleza asubiri kwa kuwa amempelekea Dina salamu aje awafanyie chochote.
Masuala makuu
- Onyesho hili linakunjua jamvi la mjadala kuhusiana na majukumu ya watoto kwa wazazi wao. Inabainika kuwa katika jamii nyingi watoto wa kiume ndio wanaotarajiwa kuwatunza wazazi
- Inachukuliwa kuwa watoto wa kike walioolewa wanapaswa kupewa fursa ya kushugulikia jamii za kule walikoolewa. Ingawa Neema ni mtoto wa kike, anaonekana kuyamudu majukumu yake kama ambavyo mtoto wa kiume angaliweza Msemo wa ‘kutoa ni moyo usambe ni utajiri’
unadhihirishwa na matendo ya Neema. Mazungumzo baina ya Sara na Yona yanadhihirisha kuwa hata ajira za kiwango cha chini kama zile za kufanya kazi shambani na nyumbani pia huwa na changamoto zake. Baadhi ya waajiriwa huwaibia waajiri wao huku wengine wakidhihirisha hali za uvivu na kushindwa kutekeleza wajibu wao kama inavyotarajiwa.
Onyesho Il
- Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Kiwa alikuwa amefika nyumbani kumjulia hali mama yake.
- Onyesho hili linaanza kwa kuonyeshwa namna Kiwa anavyogusagusa chakula na kudai ametosheka. Katika harakati ya mazungumzo juu ya chakula, Dina na Siwa wanajikuta wakizungumza kuhusu familia ya Yona na Sara. Dina anamweleza mwanawe Kiwa namna familia hiyo ilivyodunishwa na wanajamii kwa kukaa muda mrefu bila kujaliwa na watoto na hata baada ya kufanikiwa na watoto wasichana, jamii iliendelea kuwasuta na kuwakejeli kwa kuwa hawakujaliwa na mtoto wa kiume atakayerithi fimbo ya baba yake. Kusemwa huku na wanajamii kunasababisha Yona kuingia katika ulevi, ulevi ambao unamsukuma kumdharau na kumchapa bibi yake kichapo cha
- Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Dina akimuaga Kiwa ili aweze kwenda kumsaidia Sara katika harakati ya mapishi kwa kuwa Sara alikuwa
Masuala makuu
- Onyesho hili linamulika masuala matatu muhimu. Taasubi ya kiume na mila potovu, ukosefu wa ufahamu kuhusu chanzo cha jinsia ya watoto na umuhimu wa bidii Kulingana na somo la Biolojia, chembechembe za kromosomu zinazofanya uamuzi wa jinsia ya mtoto hutokana na wazazi wa kiume ambao wamebeba kromosomu aina ya Y isababishayo kuzaliwa kwa mtoto wa kiume. Mwanamke hana uamuzi kuhusiana na jambo hili. Hali ya kuwafedhehesha na kuwanyanyasa wanawake kutokana na kuzaliwa kwa watoto wa kiume halina msingi wowote. Tatizo hili linatokana na ubabe dume na taasubi ya kiume. Hali hii inatiliwa mbolea na utamaduni potovu wa jamii kutaka kumrithisha mtoto wa kiume na kumkandamiza mtoto wa kike. Suala la bidii maishani linajitokeza kama kiungo muhimu cha ujenzi wa maisha.
- Dina anajitolea kuwasaidia Sara na Yona katika kazi za nyumbani kutokana na hali mbaya ya afya ya rafikiye Sara. Tendo hili linadhihirisha udugu na ujirani
Onyesho III
- Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, jikoni. Dina yupo katika harakati ya mapishi naye Sara amejikunyata kwenye kibao. Mchuzi u tayari. Sara anamshukuru Dina kwa kufika kumsaidia. Dina anapokea shukrani na kumpa Sara maneno ya kumtia Dina anamweleza Sara kuwa kila kitu hufanyika
kwa mpango wa Manani. Anamweleza atazame faraja ilivyovuka kwake kwa vile watoto wake wamefaulu maishani. Anampa matumaini kwamba atapona kwa kuwa hospitali ambayo Neema anampeleka ina watalaamu.
- Mazungumzo ya matumaini yanaendelea kunoga huku Dina akiendelea na Dina anauliza Sara alikokwenda Yona na hapo mazungumzo kuhusu mwanamume na utamaduni yanazuka.
- Tunaelezwa namna utamadumi ulivyowajenga wanaume kama watu wasiofaa kuingia jikoni.
- Onyesho hili linatimia Sara akimweleza Dina kuhusu mipango iliyopangwa na Neema kuhusu namna atakavyorudi kliniki kupata matibabu.
Masuala makuu
Katika onyesho hili inadhihirika wazi kwamba taasubi ya kiume imemtawala Yona na kumfanya kutoona hali ya unyonge wa mkewe.
Inamlazimu Sara kuomba usaidizi kwa jirani ndipo waandaliwe chakula ilhali ni kazi ambayo Yona angeifanya bila malalamishi na kuficha siri ya familia yake.
Suala la wanaume kutosaidia katika shughuli za nyumbani hutokana na mila na desturi ambazo zinamdhalilisha mwanamke. Mwanamume anapomsaidia mkewe jikoni huona ni kama kwamba hadhi yake imeshushwa.
La kutia moyo ni kwamba, ingawa jamii inamdhalilisha mwanamke, ni dhahiri kuwa mwanamke wa sasa amejizatiti na kujiinua na kufikia kiwango cha kutajika. Neema anakuwa mfano mzuri katika jamii kwa kuyabeba majukumu yake binafsi na yale ya nyumbani alikotoka.
Anahakikisha mama yake anatibiwa na kumfanya Yona amuonee fahari si tu kama msaidizi bali nguzo muhimu ya kutegemewa hata ingawa ni mtoto wa kike, tena aliyeolewa.
Umuhimu wa ujirani mwema pia unazungumziwa. Dina anajitokeza kuwa jirani na rafiki wa kutegemewa wa Sara. Ni wazi kuwa Sara na Yona wanaishi vizuri na majirani wao.
SEHEMU II
Onyesho I
- Nyumbani kwa Neema, Neema na mamake wameketi ukumbini Sara amefika mjini kwa ajili ya matibabu na amechoka kutokana na safari ndefu.
- Neema anashangazwa na kuchelewa kwa Lemi kutoka Anakumbushwa na Bela kuwa Lemi anajiandaa kwa hafla itakayofanyika shuleni na ambayo Neema ameisahau kwa sababu ya
- Neema anamsaili mamake kuhusu sababu za vurumai za mara kwa mara za Sara anamweleza kuwa vurumai hizo zilizomsababishia maradhi ya moyo zilitokana na ulevi; kwamba Yona alitaka amzalie mtoto wa kiume. Jamii nayo ilimsukuma Yona aoe mke mwingine ili azaliwe mtoto wa kiume ambaye Sara hakufanikiwa kupata. Yona aliposhindwa kuhimili shinikizo hizo aliingia katika
ulevi hadi akafutwa kazi. Mbali na haya, Sara anamtetea Yona kwa hali na mali kuhusu tabia yake ya ulevi na vurumai.
- Ni katika onyesho hili tunapomwona Neema akilalamika kuhusu Bunju, Kulingana na Neema, Bunju anaonekana mgumu wa pesa. Anajitetea kwamba amebanwa na mahitaji mengi ambayo hayamwachi na fedha za ziada.
- Tathmini
- Kupitia kwa mazungumzo haya, masuala kadhaa yanajitokeza yakiwemo maeneo ya mashambani yaliyopuuzwa kimaendeleo, bidii maishani, taasubi ya kiume pamoja na athari za uraibu wa pombe. Usemi ‘mrina haogopi nyuki,'(uk. 18) unaotumiwa na Sara unaelezea bidii inayohitajika ili mtu afaulu maishani. Kwamba, sharti mtu akabiliane na magumu anayokumbana nayo. Sara anayasema haya anapogundua kuwa Lemi ana kazi nyingi za kufanya huko Kwa sababu ya kazi hizo, inakuwa vigumu kwa Sara kuonana na mjukuu wake.
- Suala la uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa linajitokeza pia. Suala hili linaangaziwa kupitia usafiri unavyotatizwa na miundo misingi duni katika sehemu za
- Inabainikakwambayonaanajitokomezaulevinikutokananamsukumo wa wanajamii kwa kukosa kuzaa mtoto wa Huu ni utamaduni uliopitwa na wakati. Pombe inakuwa kimbilio la kumsahaulisha malengo aliyoshindwa kuyafikia. Sara anasisitiza kwamba wazazi wana wajibu wa kumlea mtoto wa jinsia yoyote ile bila ubaguzi.
Onyesho Il
ร Onyesho hili linafanyika nyumbani kwa Neema akiwa na Bela, mfanyakazi wake.
Kupitia mazungumzo yao inabainika kwamba maisha ya leo yana changamoto nyingi kiasi kwamba wazazi hawatangamani na watoto wao jinsi inavyotakikana. Hali hii inaonekana kuwakera wazazi.
ร Suala la shughuli nyingi kazini linaonekana kuhitilafiana na shughuli ya malezi.
Katika sehemu hii inabainika kuwa Neema haonani na Lemi kwa sababu kila afikapo nyumbani mtoto huwa amelala.
ร Suala la mila pia linaibuka. Wazazi wa Sara hawawezi kulala kwa mtoto wao aliyeolewa. Neema analizungumzia jambo hili kwa mshangao. Hili ni jambo la kutatiza kwa sababu mara kwa mara mamake Neema huenda mjini kwa shughuli za matibabu na huwa anahitaji mahali pa kulala.
ร Isingekuwa kwamba Asna anaishi mjini na kwamba anaweza kumuauni mamake, basi ingempasa Neema kumkodishia chumba mamake, jambo ambalo Kiafrika ni makosa. Suala la utandawazi linajitokeza na ni dhahiri kwamba baadhi ya mila zimepitwa na wakati na zinapaswa kutupiliwa mbali kama Bela anavyoeleza:
ร Hayo ni ya kale…na ya kale hayanuki. Wengi hawafuati tena mila hizo.
Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24). Kauli hii inaonyesha namna
mabadiliko ya kijamii yamefanya baadhi ya mielekeo ya kitamaduni kupuuziliwa mbali.
Masuala makuu
Sehemu hii inadhihirisha jinsi hali za maisha ya kisasa zinavyowatatiza wanajamii. Wanalazimika kufanya kazi mchana kutwa ili kujikimu na kuzifaa familia zao. Matokeo ni kwamba hawapati nafasi ya kutangamana na familia zao ipasavyo. Ni bayana kwamba bado wanajamii wamefungwa na mila ambazo kwa hakika ni vigumu kuzitii kwa sababu ya maisha ya kisasa. Mfano mzuri ni miko inayowazuia wakwe kutolala katika makaazi ya wana wakwe zao.
Onyesho Ill
ร Katika onyesho hili Bunju yuko tayari kuondoka kwenda kazini asubuhi.
Mazungumzo na mkewe Neema yanahusu matokeo ya mitihani ya Lemi, mtoto wao. Huku Neema akionekana kuridhishwa na matokeo hayo Bunju anamtaka Lemi kujitahidi zaidi ili apate matokeo ya kuridhisha zaidi. Mgogoro baina ya wazazi kuhusu masomo ya watoto wao unajitokeza. Hali ya Neema na Bunju kutokubaliana kuhusu bidii ya mtoto wao inaweza kuzua msukosuko.
ร Neema anapomwelezea Bunju kuwa mamake tayari ameshafika mjini kwa matibabu, anakataa kutoa pesa za kusaidia matibabu hayo. Bunju anadai kuwa ana majukumu mengi. Kwamba anagharamia mahitaji yote ya nyumbani, yakiwemo karo ya shule, kodi ya nyumba na amemnunulia Neema gari.
Anamtaka Neema awajibike kwa sababu amemruhusu kutumia mshahara wake kwa mahitaji ya familia yake.
ร Bunju anasisitizia ile dhana ya kutomruhusu mama mkwe kulala nyumbani kwao. Mila na desturi hizo zinamkera Neema sana. Kwa Neema, hizo ni mila na desturi zilizopitwa na wakati.
Tathmini
- Onyesho hili linazungumzia mambo muhimu ya kifamilia, hasa malezi na elimu. Neema anaridhishwa na matokeo ya mwanawe, ila Bunju anamtaka Lemi aongeze bidii masomoni. Hayo yakijiri, inaonekana kana kwamba ni Neema pekee anayejitahidi kushughulikia matakwa ya Lemi Bunju analipa karo na kutekeleza majukumu mengine ila kazi yake imembana hadi hana muda wa kutangamana na familia yake ipasavyo. Mfumo wa uchumi umewagandamiza raia na kuwalazimisha kufanya kazi masaa mengi kupindukia.
- Mfumo wa elimu unawapa watoto shinikizo la kujibidiisha zaidi masomoni, jambo ambalo linaweza kusababisha msukumo wa kiakili miongoni mwa Ni bora wazazi wakiwa na msimamo mmoja kuhusu masuala yanayohusu elimu ya watoto wao.
- Mchango wa mwanamke katika ndoa unamulikwa. Bunju analipa kodi ya nyumba, karo na hata kamnunulia mkewe Je, mchango wa mkewe katika
majukumu ya kifamilia ni upi? Ni muhimu mwanamke anayefanya kazi kuwekeza kiwango fulani cha pato lake katika mali ya familia ili kupata heshima na pia kama njia mojawapo ya kujifunza kuimudu familia ikiwa ataondokewa na mumewe mapema.
Onyesho IV
& Mjini, nyumbani kwa Asna. Asna anamwandalia mamake kiamshakinywa. Mama mtu anashangaa mbona bintiye anaishi katika chumba kidogo. Bintiye anajitetea kuwa chumba hicho kiko katika mtaa wa kifahari na anakifurahia. Sara analinganisha maisha ya mjini na ya kijijini na kuona kuwa yale ya mjini yanaudhi, afadhali ya kijijini.
& Anasema kwamba, watu wa mjini wako mbioni kila wakati na mapato yao ni haba.
Asna hakubaliani na mamake; kwake, kiwango chake cha elimu hakimruhusu kwenda kukaa kijijini.
& Sara anamsihi Asna aolewe amletee mjukuu. Asna hakubaliani na jambo hilo.
Kulingana na Asna, ndoa ina matatizo mengi kama yale anayopitia Neema, dada yake, ambaye ingawa amesoma na kupata shahada mbili, hazimsaidii kupigana na msimamo wa kitamaduni alionao Bunju, mumewe. Badala ya kupigania mabadiliko ya msimamo wa Bunju, Neema anaonekana kuukubali kwa sababu ya uhuru wa matumizi ya mshahara wake aliopewa na Bunju.
& Utepetevu kazini unazungumziwa kupitia madaktari na utendakazi wao. Baadhi ya madaktari daima wako mbioni kutoka hospitali moja hadi nyingine ili kuchuma hela za ziada bila kuwazingatia wagonjwa wao kikamilifu.
Masuala makuu
ร Kuna mambo muhimu yanayojadiliwa katika onyesho hili. Jambo la kwanza ni hadhi. Ile hali ya kutaka kuishi sehemu za kifahari hata ingawa pato ni dogo. Asna anaishi maeneo ya juu ingawa mazingira ya nyumba yake ni duni.
Anajikakamua kulipa kodi ya juu ya nyumba bila kujali mazingira anamoishi.
ร Jambo la pili linaakisi athari za elimu ya juu dhidi ya mila na desturi za Kiafrika.
Inasahaulika kwamba,elimu pekee bila uelewa haiwezi kubadilisha dhana na fikra za kitamaduni. Bunju ana elimu lakini elimu yake haijamtoa katika mila na desturi za jamii yake. Neema ana elimu lakini haimsaidii kuelewa chanzo cha mila na desturi za Bunju. Jambo la tatu ni kutosheka kwa mwanamke. Neema anaonekana kutosheka na hali ya mumewe ya kumruhusu kutumia pesa zake atakavyo. Hafikirii kuwa huenda ikawa ni mtego. Mara nyingi mwanamke anapopata uhuru wa aina hii, huweza kubugikwa na akili asiweze kufikiria kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kisha mambo yanapoharibika hujikuta hana lolote la kutegemea.
Sehemu III Onyesho I
ร Nyumbani kwa Neema na Bunju. Neema yuko nyumbani anafanya usafi.
Anafikiria jinsi ugonjwa wa mamake ulivyomfanya fukara. Bunju anapoingia chumbani, Neema hamsikii, anashtuka. Kwa mara nyingine, anakataa kumsaidia Neema kugharamia ugonjwa wa mamake.
ร Anasema kwamba anafanya majukumu yote ya pale nyumbani na haoni ni kwa nini Neema hawezi kuupangia mshahara wake ili uweze
ร kuyakidhi mahitaji yake. Neema anahuzunishwa na msimano wa Bunju lakini pia anakumbuka maneno ya mamake kuwa Bunju ni zawadi kwake, jambo ambalo linampa heri kidogo.
Masula makuu
ร Onyesho hili linampa msomaji au mtazamaji nafasi ya kuelewa mahusiano katika taasisi ya ndoa. Wanandoa hao wawili wanashikana mkono kuendeleza maslahi ya jamii yao. Mume anaheshimu rai ya mkewe ya kutumia hela zake kushughulikia wazazi wake ambao ni wahitaji.
ร Mama ni mgonjwa na baba yake amepoteza ajira. Tofauti ya matumizi ya pesa kati ya mwanamke na mwanamume yanajitokeza. Mwanamume anajenga na mwanamke anapamba. Mambo yanapoharibika, mwanamke huachwa bila makao kwa sababu ya dhana kuwa hakuwekeza katika
ร ujenzi wa nyumba. Hili ni jambo linalohitaji mjadala zaidi. Bunju anajitokeza kama mwanamume anayefanya majukumu yote ya kifamilia, hali ambayo haimtayarishi mkewe kwa maisha ya baadaye iwapo mambo Kuna pia suala la matumizi ya pesa ili kutibu magonjwa. Familia nyingi yataharibika. hazina bima ya matibabu. Magonjwa yanapobisha hodi basi huziacha baadhi ya familia hizo katika hali ya umaskini. Wengi huitisha michango kama Neema anavyoitisha msaada kutoka kwa Bunju.
ร Katika mazungumzo yao, pia inadhihirika wazi kwamba mapato ya kazi moja hayatoshi kamwe. Umuhimu wa kujishughulisha zaidi ili kuweza kuyamudu mahitaji unajitokeza.
Onyesho II
ร Sara yuko hospitalini ambako amelazwa. Neema na Asna wamefika kumwona. Sara anataka kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa sababu gharama ya hospitali inaendelea kupanda. Sara analinganisha huduma za matibabu za kule kijijini na za mjini. Hospitali za mjini ni kama hoteli ilhali za kijijini ni kama seli ambako mtu akilazwa hata matumaini ya kupona hudidimia.
ร Sara anataka atoke hospitalini arudi kijijini kwenda kumsaidia Yona ambaye alimwachia kazi zote za nyumbani. Bunju anafanya shughuli zake bila kupita hospitalini kumjulia hali Sara. Jambo hili linamkera Asna ambaye anamwona Bunju kama mchoyo na asiyewajibika kuhusu mkwe wake. Neema anamtetea Bunju.
ร Anasema kwamba tabia yake inatokana na jinsi alivyolelewa, kwa hivyo wasimlaumu.
Masuala makuu
ร Mazungumzo haya yanaibua mambo matatu muhimu kuhusu hospitali aliyopeIlekwa Sara. Mosi, malazi na chakula ni vya hali ya juu. Pili, gharama ya huduma ni ya juu mno. Tatu, hospitali hiyo ina aina nyingi za wataalamu. Hali hii inakinzana na hali ilivyo katika baadhi ya hospitali nchini ambazo ni duni na hutoa huduma mbovu zinazomfanya mgonjwa kutamauka na kukata tamaa.
ร Hospitali za kibinafsi hutoa mazingira mema zaidi ya kimatibabu na ni mwafaka zaidi kwa wale wanaoweza kulipia gharama zake, Mazingira ya hospitali za umma ni duni, nyingi zikiwa hazina huduma bora, hazina madaktari na hata dawa za kutosha.
ร Pia, mwanamume angali anapewa hadhi ya juu kuliko mwanamke. Jamii haimruhusu mwanamume kufanya kazi za jikoni kwa sababu kazi hizo huchukuliwa kuwa ni za kike. Ndiposa, ingawa Sara angali mgonjwa, bado ana ari ya kurudi nyumbani kumshughulikia Yona, mumewe.
ร Bunju amechorwa kama mtu asiyemjali mama mkwe. Ingawa Neema haridhishwi na hali hiyo, anashindwa kumkabili na kusingizia malezi.
ร Heshima anayopewa mwanamume na mwanamke katika onyesho hili, inawekwa kwenye mizani.
Onyesho III
ร Neema anamsaidia Lemi katika masomo yake. Lemi analalamika kwamba kwa muda mrefu wazazi wake hawajampeleka ziara. Neema anamweleza kuwa hataweza kumpeleka ziara kwa sababu anamrudisha bibi kijijini. Lemi haelewi ni kwa nini bibi yake hakuja kumsalimia.
ร Neema anamwomba Bunju ampeleke Lemi kwenda kuogelea kwa kuwa yeye anapanga kumrejesha mama yake nyumbani. Bunju anakataa kwa sababu ya gharama na pia anasema anaenda kutafuta riziki. Analalamika kuwa Neema mara nyingi yuko nje kikazi na anamwachia majukumu yote ya nyumbani.
ร Bunju analalamika kwamba hakujulishwa kuwa mama mkwe ametoka hospitalini na kwamba atasafirishwa kijijini. Neema anamwambia Bunju kuwa mkewe hakutaka kumsumbua na mambo ya kwao nyumbani.
ร Kulingana na Bunju, Neema ameanza kumdharau. Bunju anamkumbusha Neema alivyokuwa mahututi wakati alipompata. Suala hili linamhuzunisha Neema hata anaanza kulia. Bunju anamhurumia na kumwambia atulie asilie mbele yake.
Tathmini
Katika onyesho hili, suala la mivutano baina ya wanandoa kuhusu majukumu ya familia yao linajitokeza. Ni bayana kwamba suala hili linahitaji tahadhari ili lisiwe chanzo cha mafarakano katika ndoa. Pia, kuna suala la gharama za kulea watoto. Ni lazima wazazi
wawape muda wana wao kama Neema anavyomsaidia Lemi na kazi za shule. Lakini pia kuna gharama nyingine za kuwafurahisha watoto ambazo zinahitaji pesa na mara nyingi pesa hizo hazipo. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na maelewano baina ya wazazi na watoto kuhusu mambo hayo ili kusiwe na mikurumbano. Ni vyema pia wazazi kuwaeleza watoto kuhusu gharama hizo ili wazielewe mapema. Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Asna. Sara na Asna
Onyesho IV
- Mazungumzo ya mama na bintiye yanagusia masuala mengi. Inabainika kuwa Asna hana imani na ndoa. Anaridhika na maisha ya kuishi bila mume ingawa amefikia umri wa kuolewa. Kulingana na Asna, ndoa ya Neema ina doa. Hii ni kwa sababu Bunju ni bahili na hapendi wazazi wa Neema walale nyumbani kwake. Pili, anaonelea kuwa, Sara pia aliteseka sana katika ndoa yake. Hata ugonjwa alionao ulitokana na kero za Yona, baba yao. Asna anaamua kuishi nje ya ndoa kwa sababu ya mifano ya ndoa hizo mbili zisizoridhisha. Katika onyesho hili, Sara anapata muda wa kumzungumzia Asna masaibu ya ndoa yake na babake na jinsi yalivyoanza.
- Sara na Asna wanazungumzia juhudi za Dina na wanawe ambazo zimewasaidia kujitoa katika lindi la
Masuala makuu
ร Kulingana na Asna, taasisi ya ndoa ina uwezo mkubwa wa kumletea binadamu shida nyingi. Anamweleza mama yake kwamba msongo wa moyo alionao unatokana na matatizo yaliyo katika ndoa yake. Pia, anaona kuwa ndoa ya Neema ina matatizo.
Kwamba Bunju ni mchoyo na hajali ugonjwa wa mama yao, hali inayomfanya Neema kutokuwa na raha katika ndoa yao. Mifano hiyo miwili inamfanya Asna kutoridhishwa na asasi ya ndoa na hivyo, kuikinai. Lakini Sara anamweleza kuwa ingawa ndoa huwa na changamoto nyingi, uvumulivu huwasaidia wanandoa kukabiliana na changamoto hizo.
ร Kulingana na Sara, bidii ni silaha inayoweza kumkomboa mwanadamu kutoka umaskini. Familia ya Dina inatumika kama mfano wa familia ambayo awali ilikuwa maskini lakini ikafaulu kujinyanyua kutoka hali hiyo ya umaskini na kujikimu ipasavyo.
ร Sara anamweleza Asna kuwa hata yeye (Sara) na mumewe Yona walikuwa maskini lakini hawakusita kufanya bidii. Waliungana katika juhudi zao ili kujimudu katika kuwatunza na kuwasomesha watoto wao hasa wakati Yona alipopoteza kazi yake ya ualimu. Hatimaye, watoto wao waliweza kuhitimu hadi Chuo kikuu. Inamsikitisha kuwa wanajamii bado waliwachukulia kuwa maskini wa kutojaliwa kupata mtoto wa kiume hata baada ya kufanya juhudi hizo zote. Suala la unyanyapaa dhidi ya
familia za walevi linajitokeza pale ambapo familia ya akina Asna inadharauliwa na kunyimwa hadhi katika jamii kwa sababu ya ulevi wa Yona.
Sehemu IV Onyesho I
ร Kijijini nyumbani kwa Luka. Luka anawakaribisha Beni na Yona kwa sherehe ya kufurahia mazao yake. Beni anazungumzia jinsi watu walivyozitupa mila zao kabisa. Anasema kwamba vizazi vijavyo havitakuwa na mila na desturi. Katika mazungumzo yao, wazee hao watatu wanakubaliana kuwa vizazi vya siku hizi vinafikiria kuwa uzungu ndio ustaarabu. Jambo hilo linatokana na malezi ya mjini ambayo mara nyingi yameachiwa wafanyakazi wa nyumbani. Wazazi wanaraukia vibaruani asubuhi na kurudi usiku watoto wakiwa wameshalala.
ร Luka anawakumbusha wenzake kuwa mila za zamani hazikuwaruhusu watoto wa kike kwenda shuleni wala kurithi mali ila walitegemea usaidizi wa waume zao. Lakini anakubali kuwa thamani ya mtoto wa kike imepanda na nafasi yake kupanuka. Watoto wa kike wa Yona wanamulikwa katika mazungumzo haya. Japo walidharauliwa hapo awali, sasa wamekuwa nyota ya jaha. Ni wazi kwamba wao sasa ndio wanaogharamia matibabu ya mama yao katika hospitali za hali ya juu huko mjini.
ร Hata hivyo, fikra za kitamaduni bado zinatawala. Beni anamlaumu Sara kwa kumwacha Yona peke yake akifanya kazi zote za nyumbani. Luka anapinga kauli ya Beni ya kuwadunisha watoto wa kike na mwanamke kwa jumla.
ร Katika onyesho hili, masuala ya ulevi na athari zake, taasubi ya kiume, usawa wa kijinsia na mabadiliko yanaangaziwa.
Masuala makuu
Suala la utamaduni linajitokeza wakati wazee wanapotoa rai kwamba dini za kisasa zimewafanya watu kudharau utamaduni wao.
Yona na Beni wanalalamikia kukengeushwa kwa wanajamii. Wanaeleza kuwa watoto wa siku hizi hawazifahamu lugha zao za kiasili, kwamba wamezama katika Kiswahili na Kiingereza. Wanashindwa kutofautisha hata wanyama wa kufuga kama vile mbwa, mbuzi na kondoo. Suala la usawa wa kijinsia linazungumziwa kupitia maelezo kuwa wanawake wa zamani waliwategemea waume zao lakini sasa jinsia zote zinachuma na kushirikiana katika malezi ya watoto. Neema, anakuwa mfano mwema wa mwanamke aliyefaulu maishani na ambaye anachuma na kuwatunza wazazi wake kama vile mtoto wa kiume angalivyoweza kufanya. Nafasi ya mtoto wa kike katika maendeleo ya familia inajitokeza. Ni wazi kwamba tofauti na zama za kale, watoto wa kike wa sasa wamesoma na kuajiriwa, na kuwa tegemeo muhimu katika familia zao na jamii nzima kwa jumla.
Aidha, suala la chanzo cha ulevi wa kupindukia linamulikwa. Ni wazi kuwa vijana wengi huingizwa kwenye mitego ya ulevi wanapotangamana na wenzao
chuoni. Kwa wengine, mbegu hiyo ya ulevi huota na kuwa chanzo cha vurugu na maangamizi maishani. Kutangamana kwa vijana katika taasisi za elimu kumeleta athari nzuri na mbaya kutegemea jinsi wanavyotumia uhuru wao.
Onyesho Il
ร Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, kijijini. Sara na Neema wanajadiliana kuhusu suala la utamaduni na mabadiliko ya kijamii.
ร Neema anasema ulimwengu unakwenda mbio ilhali watu wengine wamebaki nyuma katika mielekeo ya kijadi ya kubugia pombe bila kikomo.
ร Sara anamtetea Yona kwa kutowajibika ipasavyo na majukumu ya nyumbani hasa yale ya mifugo. Kulingana na Sara, mwanamume hawezi kuwekwa katika kiwango kimoja na mwanamke. Anasema
ร Yona anatekeleza majukumu yake ipasavyo. Hizo ni fikra za kitamaduni. Kwa Sara, mwanamume ana nafasi yake katika jamii na hapaswi kumsaidia mwanamke kazi za nyumbani. Kufanya hivyo ni kualika minong’ono ya wanajamii na kuwakosesha wanawe waume wa kuwaoa.
ร Sara anatunza heshima ya ndoa yake ili watoto wake wapate fanaka maishani licha ya mateso anayopata kutoka kwa mumewe. Sara anampa Neema ushauri unaoweza kuifanikisha ndoa yake. Anamshauri Neema azungumze na baba yake kwa hekima ili amsaidie kubadilisha msimamo wake, hasa kuhusiana na ulevi.
Masuala makuu
ร Kwa mara nyingine, taasisi ya ndoa inazungumziwa. Ingawa wanandoa wanapaswa kusaidiana, ni wazi kuwa jamii za Kiafrika bado zinatilia mkazo mgawo wa kazi katika jamii. Kuna majukumu mengine ambayo jamii haitarajii yafanywe na mwanamume mwenye mke, na iwapo ataamua kuyachangamkia, basi inakuwa ni kama yanampunguzia hadhi katika jamii. Ingawa fikra hizo zimepitwa na wakati na jamii imebadilika, bado jamii inatumia vigezo vya tamaduni hizo kumwekea mipaka mwanamke. Hata hivyo, Sara anamuasa Neema kuzitilia maanani tamaduni hizo ili kudumisha ndoa yake.
ร Onyesho hili pia linazua suala la ukoloni mamboleo. Kutokana na mazungumzo ya Sara na Neema, ni wazi kwamba matatizo ya kiuchumi ya mataifa machanga yanasabishwa na hali ya mataifa hayo kuendelea kuwa masoko ya bidhaa za nchi za nje. Yamebakia tu kuwa masoko ya bidhaa zitokazo ng’ambo badala ya kujibidiisha kuzalisha bidhaa zao.
Onyesho III
- Onyesho linafanyika asubuhi pale kijijini. Yona yuko peke yake sebuleni. Ugonjwa wa mkewe unamhuzunisha na anajutia maisha yake ya awali yaliyomletea mkewe Neema anampata babake akiwa katika hali ya mawazo mengi. Yona anashangaa kumwona bintiye amekonda.
- Yona anamwelezea Neema jinsi maradhi ya Sara yalivyoathiri mji wake. Anamshukuru kwa kumshughulikia Yona anakumbuka maisha yake ya chuoni na jinsi alivyokuwa mwerevu. Neema anapata mshangao anapogundua kuwa babake ameandaa kiamshakinywa mapema, yeye na mama yake wakiwa bado wamelala. Neema anafurahi na kumshukuru babake kwa wema wake.
- Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Yona akiomba msamaha kwa Neema kwa makosa aliyowafanyia wakiwa wangali Yona anatumai kuwa mabinti wake wengine watamsamehe siku moja. Yona pia anaomba msamaha kwa mke wake na kumwahidi kuwa asitie shaka atakuwa naye katika kila hali. Taa zinazima na wote watatu wanakumbatiana kuonyesha hali ya kusameheana na kuja pamoja kwa familia hiyo.
Masuala makuu
Katika onyesho hili, Yona anapata fursa ya kujirudia na kufikiria maisha yake ya siku za usoni. Anatambua kuwa mke wake ni mgonjwa kwani sasa maisha yake yanaendeshwa na madawa. Anaamua kuacha kunywa pombe kabisa. Uamuzi wa Yona una umuhimu mkubwa kwa sababu anakubali kuwa alimkosea mkewe na kwamba umefika wakati wa kujutia makosa hayo na kuanza upya. Kupitia kwa Sara na Neema, anaonekana kuomba msamaha familia yake kwa yote aliyowatendea na kuwaomba wampe nafasi ya kuanza maisha yake upya. Hii ni hatua kubwa na mwafaka katika maisha ya Yona na familia yake. Anaahidi kumtunza mkewe kikamilifu.
MSUKO
Kazi ya fasihi huwa imepangwa kwa muundo maalumu. Muundo huu huitwa msuko. Msuko ni mtiririko wa matukio katika kazi ya fasihi, Ni namna kazi ya fasihi huwa imepangwa kutoka mwanzo hadi mwisho.
Msuko huwa na sehemu tatu kuu ambazo ni:
- utangulizi/ mwanzo/ ufunguo
- kati/ sehemu ya pili- kilele na mpomoko
- hitimisho/ mwisho
a)ย Utangulizi/mwanzo
- Mwanzo katika tamthilia hii unaanza kwa kueleza uhusiano uliopo bainaya Hivyo basi, utangulizi huu unatusaidia kujua uhusiano wa wahusika. Kwa mfano, mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ameonyesha uhusiano wa wahusika kama vile: Sara na Yona ambao ni mke na mume na waliobarikiwa na watoto watatu wa kike ambao ni
- Neema, Asna na Salome. Mhusika Dina ameelezwa kama mama yake Kiwa na rafikiye Bunju ni mumewe Neema; wamejaliwa na watoto wawili ambao ni Mina na Lemi. Beni na Luka wanatajwa kama wazee wa kijiji.
- Utangulizi au mwanzo wa tamthilia ya Bembea ya Maisha unamsaidia msomaji kujua uhusiano uliopo bainaya wahusika najinsi wanavyoshiriki katika
- Sehemu ya utangulizi pia humsaidia msomaji kujua mahali na wakati mchezo Tamthilia ya Bembea ya Maisha ni mchezo/kazi ya fasihi inayofanyika katika eneo la Afrika wakati wa jana na leo.
- Utangulizi katika tamthilia hii pia unamwezesha msomaji kupata kiini cha Kiini katika tamthilia ya Bembea ya Maisha kinajitokeza katika onyesho la kwanza na la pili. Kulingana na tamthilia hii, kiini chake ni pamoja na namna utamaduni, mila na desturi za jamii husika zinavyoweza kuidunisha familia.
b)ย Kati/sehemu ya pili
ร Sehemu hii huwa imegawika katika sehemu mbili ambazo ni kilele/ upeo na mpomoko. Msomaji hupata mivutano au migogoro baina ya wahusika. Sehemu hii inasaidia kuibua maudhui katika kazi ya fasihi.
ร Katika tamthilia ya Bembea ya Maisha, sehemu ya kati inajidhihirisha katoka sehemu ya Il kuendelea.
ร Mivutano baina ya wahusika inajidhihirisha kupitia wahusika kama vile Sara na Asna kuhusu suala la ndoa. Wawili hawa wana mitazamo tofauti kuhusiana na suala la ndoa. Asna ana mtazamo hasi ilhali Sara ana mtazamo chanya. Sara anamtaka Asna aolewe ili amletee mjukuu ampakate kwa mikono yake kabla hajaaga dunia. Hata hivyo, Asna anaona ndoa kama suala la kuleta matata katika familia. Mtazamo huu unachochewa na jinsi ndoa ya wazazi wake na ile ya dadake zinavyojidhihirisha. Asna anaona kuwa ndoa imemuweka mama yake katika hali ya ugonjwa atakaoishi nao milele (uk. 54). Vilevile, kulingana na Asna, ndoa imemfanya Neema kutokwa na hali ya ukakamavu na kujiamini kwa dhati (uk. 54).
ร Maudhui yanayojitokeza katika sehemu hii ni ndoa, utamaduni, taasubi ya kiume, nafasi ya mwanamke na mengineyo.
Kilele/ Upeo
- Kilele katika tamthilia ni sehemu ambayo matukio yanafanyika katika hali ya Msomaji akifika katika sehemu hii, hupatwa na mshawasha wa kutaka kusoma ili apate ujumbe kamili.
- Katika tamthilia hii ya Bembeaya Maisha, sehemu ya kilele inajitokeza katika mazungumzo ya Dina na Sara. Ni baada ya mazungumzo hayo, ndipo msomaji atapata hamu ya: kutaka kujua namna walivyofanikiwa, kujua kama ugonjwa wa Sara utapona, kujua kama ulevi wa Yona ulipungua au ulifikia kikomo. Msomaji anapata hamu ya kujua kama mtazamo wa jamii kuhusu familia ya Yona na Sara ulibadilika au uko
Mpomoko
ย
ย
Hii ni sehemu ambayo mhusika mkinzani anashindwa. Katika sehemu hii, tensoni/msuko wa tamthilia unashuka.
Mpomoko katika tamthilia hii ya Bembea ya Maisha unajidhihirisha wakati Yona anapokuwa akijizungumzia na kujilaumu kwa kukosa kumshughulikia mkewe Sara (uk. 70). Yona anakata shauri ya kutoshiriki katika unywaji wa pombe. Anasema kuwa atatumia siku zake kumwangalia mke wake mgonjwa. Hapa ndipo msuko wa tamthilia unashuka kwa kuwa msomaji ameshapata suluhu ya tensoni au taharuki aliyotaka kujua itaishia wapi.
c)ย Mwisho/Hitimisho
Hii ni sehemu ya mwisho katika msuko wa tamthilia. Sehemu hii inamwezesha msomaji kujenga au kupata suluhu ya suala kuu linalojitokeza katika tamthilia. Mwisho wa mchezo wa Bembea ya Maisha unajitokeza Yona anapoomba msamaha kwa mwanawe Neema na kutumainia kuwa wanawe wengine watakuja kumwelewa. Aidha, anaomba msamaha kwa mkewe kwa kutomjali siku za awali. Anamwahidi kuwa atasimama naye katika kila hali (uk. 74).
MAUDHUI NA DHAMIRA
Maudhui ni masuala muhimu ambayo mwandishi anayachanganua Maudhui katika kazi yake; yale mambo muhimu anayoyaona katika jamii na anayotaka kuyaeleza kisanaa katika kazi yake, bila kujali utanzu anaotumia kumulikia masuala hayo. na namna mwandishi anavyoyajadili. Msomaji anaweza kuelewa lengo la mwandishi na funzo la kazi yake kupitia jinsi anavyochanganua masuala
Katika tamthilia hii, mwandishi ameshughulikia masuala yafuatayo: mbalimbali. mabadiliko, migogoro, ndoa na mahusiano katika ndoa, nafasi ya mwanamke katika jamii, tamaduni, maadili ya kazi, ulevi, maendeleo, malezi na bidii maishani.
1.ย Nafasi ya mwanamke
Haya ni maudhui yanayonyesha namna mwanamke amesawiriwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
ร Mwanamke amesawiriwa kama mwerevu na mwenye maarifa, hekima na busara. Kwa mfano, katika uk. 6 Kiwa anasema kuwa Sara amebarikiwa na watoto wenye akili nzuri. Wote wamehitimu vizuri na kuleta faraja. Tunaona Neema amesoma na kuhitimu Chuo kikuu na ana kazi nzuri. Asna na Salome vilevile wamefanikiwa kusoma hadi Chuo kikuu. Salome alipita mtihani kwa kupatafirst class. Alibahatika kwenda nwambo kuendeleza masomo yake (uk. 28).
ร Mazungunzo ya Sara katika tamthilia hii yanaonekana kuwa yenye wingi wa hekima na busara. Anatoa ushauri katika masuala mbalimbali kama vile: masuala ya ndoa, maisha, heshima na mengineyo.
ร Mwanamke anaonekana kama mzazi anayestahili kujifungua watoto wa kike na wakiume na hasa watoto wa kiume. Asipopata watoto wa kiume, anasutwa na kukejeliwa.
ร Tunaelezwa kwamba Sara alisutwa na kutukanwa na wanajamii kwa kukosa mtoto wa kiume hata baada ya kujaliwa na mabinti watatu baada ya muda mrefu bila watoto (uk. 6,7).
ร Mwanamke amesawiriwa kama mtu mvumilivu na anayestahili kuvumilia mateso na bughudha za ndoa. Kwa mfano, Sara anavumilia ndoa yake ambayo ilikuwa na changamoto nyingi. Aidha anavumilia mumewe Yona baada ya kumtesa na kumchapa kichapo cha mbwa.
ร Neema anapewa mawaidha na mama yake kuhusu kuzidi kuvumilia ndoa yake.
Kudhihirisha suala hili la uvumilivu wa ndoa tunamwona
ร Neema akimweleza mumewe kwamba anakubaliana na wazo kuwa hawaishi katika ndoa ya raha mustarehe mia fil mia (uk. 48). Wazo hili linaonyesha kuwa Neema pia anavumilia ndoa yake na Bunju.
ร Mwanamke ameonyeshwa kama mtu anayestahili kujukumika katika majukumu ya nyumbani. Anasawiriwa kama mtu mwenye majukumu ya shambani, jikoni na nyumbani kwa jumla. Yona anapomkuta Sara ameketi, analalamika kuwa hajaandaliwa chochote. Inambidi Sara amtumie salamu Dina ili aje amsaidie kupika. Hali hii inaonyesha kuwa ni jukumu la mwanamke kupika na kuandaa chakula kwa mumewe.
ร Kizazi cha jana kimemsawiri mwanamke kama mtu asiyestahili kupata elimu. Sara anasema kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanywa bezo. Yeye aliachia darasa la saba (uk. 33).
ร Mwanamke amesawiriwa kama kiumbe dhaifu. Kiumbe ambacho hakifai kushindana na mwanamume. Sara anamwambia bintiye
ร Neema kuwa utamaduni ungali una nguvu na hawezi kushindana na mwanamume (uk. 66).
ร Wanawake katika tamthilia hii wameonyeshwa kama watu wenye msimamo dhabiti. Sara na binti zake wamesawiriwa kama wenye msimamo imara. Kwa mfano, Sara anasimama na familia yake hata baada ya kutukanwa na kukejeliwa na wanajamii. Hakuwacha familia yake, alisimama nayo hadi wakati wa mwisho. Asna pia ana msimamo wake kuhusu ndoa (uk. 53). Anashikilia msimamo kuwa ndoa ni taasisi inayomkandamiza mwanamke na kuwa haifai.
Mabadiliko
Mabadiliko ni hali ya kutoka katika hali moja hadi nyingine.
- Mabadiliko yanajitokeza pale ambapo Yona anatueleza kuhusu maisha yake ya ujana alipokuwa mwalimu. Anatueleza namna alivyokuwa akiamka alfajiri na mapema kiboko mkononi na mwanafunzi aliyekuja baada yake angepokea Anasema kuwa siku hizi huwezi kumnyoosha mtoto kwa kiboko. Suala hili linamaanisha kuwa kuna mabadiliko ya sheria na kanuni za shuleni (uk. 62).
- Suala la mabadiliko linadhihirika wakati Yona anakubaliana na Mtazamo wa Yona kwa Sara unabadilika. Alikuwa hana huruma kwa mkewe Sara alipokuwa mgonjwa. Katika onyesho la kwanza, Yona analalamika kwa sababu Sara alikuwa hajamwandalia chakula. Yona alikuwa hana huruma hata baada ya Sara kumwelezea kuwa alikuwa hajaandaa chakula kwa sababu ya maumivu (uk. 1).
- Mabadiliko yanajitokeza wakati Yona anaonekana kuhuzunishwa na maradhi ya mke Anasema aliona hapo awali kama maradhi yale yalikuwa mchezo lakini sasa anatamani angeishi tofauti. Yona anasema hawezi kuendelea kuishi kama zamani, ni lazima angefuata mkondo mpya wa maisha. Anataka kuzitumia siku zake za uzee kumshughulikia mkewe (uk. 70). Anamwambia Sara pole na kusema kuwa taabu zake Sara zitakuwa taabu zake (uk. 74).
- Yona amesawiriwa kukuza maudhui ya mabadiliko. Mwanzoni, ameonyeshwa kama mtu mzuri, baada ya kusutwa na kudharauliwa kwa kukosa mtoto wa kiume anabadilika na kuwa mlevi na kupoteza upendo kwa familia yake. Tunamwona akimpokeza bibiye kichapo cha mbwa hadi kusababishia bibiye maradhi ya moyo. Yona anabadilika kutoka hali hiyo ya ulevi kwa kuamua kuchukuwa mkondo mpya wa maisha (uk. 70). Anasema kwamba pombe imemchezesha kama mwanasesere na kumnyima fursa ya kuilea familia
- Kuna mabadiliko ya mitazamo ya utamaduni wa jamii ya kizazi cha jana na ya kizazi cha leo. Mabadiliko haya yanajidhihirisha kupitia suala la mtoto wa kike na mtoto wa kiume. Mtazamo wa mtoto wa kike katika kizazi cha jana umebadilishwa na utamaduni wa kizazi cha leo. Kizazi cha jana kinamwona mtoto wa kike kama mtoto asiyekamilika na asiyestahili kusomeshwa wala kurithi mali ya familia (uk. 60). Wazo hili linabadilishwa na kizazi cha leo ambacho kinamwona mtoto wa kike sawa na mtoto wa kiume. Kwa hivyo, kama mtoto wa kiume, yeye pia anaweza kurithi mali ya familia na vilevile kusomeshwa.
- Mabadiliko ya utamaduni pia yanajitokeza katika suala la Sara anamweleza Asna kuwa zamani, wasichana walikuwa wakiozwa punde tu walipobaleghe (uk. 52). Mtindo huu unabadilika miongoni mwa kizazi cha leo kwani wasichana wanaolewa wakati watakapo.
- Mabadiliko ya utamaduni yanadhihirika kutoka kwa mhusika Yona ambaye, hapo awali, hangeweza kuingia jikoni kumpikia mkewe Sara. Baada ya kugundua kuwa hayo ni mambo yaliyopitwa na wakati, tunamwona akiandaa kiamshakinywa kwa familia yake. Pia, anamhakikishia Sara kuwa atamshughulikia kwani hali yake Sio nzuri (uk. 62).
- Kuna mabadiliko ya mitazamo au uonevu wa mambo katika tamthilia Neema anabadilisha mtazamo wake kuhusu baba yake (uk. 72).
- Bunju pia anabadilisha mtazamo wake wa kutomsaidia Neema kugharamia matibabu ya mamake Sara. Anamwambia anaenda kukutana na mkurugenzi wa kampuni na kuwa akipata hela, atampiga jeki katika suala la matibabu ya mama yake (uk. 40).
- Tamthilia ya Bembeaya Maisha inaangazia mabadiliko ya Mabadiliko haya yanajitokeza kupitia familia ya Yona. Kwanza, maisha ya Sara, mkewe Yona, yanabadilika kutoka kuwa ya afya njema na kuwa yenye afya duni. Afya ya Sara inazorota kutokana na ugonjwa wa moyo ambao ataishi akimeza vidonge vya dawa maisha yake yote (uk. 71).
- Pia, mtazamo wa wanajamii kuhusu familia ya Yona unabadilika pia. Wanajamii sasa wanaiheshimu familia ya Yona ambayo ilikuwa imedharauliwa na kudunishwa hapo mbeleni. Familia hii haisutwi wala kutukanwa kwa sababu ya mafanikio na elimu ya mabinti Jambo hili linadhihirishwa kupitia maneno ya Luka wakati walikuwa wakiongea na Beni na Yona.
Ndoa
Mwandishi amesawiri suala la ndoa kupitia wahusika wafuatao:
ร Yona na Sara, Neema na Bunju na hata Asna. Kupitia ndoa za wahusika hawa masuala mengi ya mahusiano katika ndoa yanajadiliwa.
ร Ndoa ya Yona na Sara inasawiriwa kama ndoa ya kizazi cha jana.Inaonyesha matarajio ya ndoa kulingana na jamii yao. Inaakisi malezi, majukumu ya mke na mume na matarajio ya wanajamii kuhusiana na watoto. Inachora picha ya majukumu kama yalivyopangwa na jamii ya Yona na Sara.
ร Kulingana na jamii katika tamthilia ya Bembea ya Maisha, mwanamke anapoolewa anahitajika kuanzisha familia na mumewe. Anatarajiwa kujifungua watoto wa kike na vva kiume. Katika ndoa ya Yona na Sara, tunafahamishwa kuwa wanajamii waliwasema na kuwatafuna kama chingamu huku Yona akiitwa gumba na Sara kuitwa tasa. Hii ni baada ya kuoana na kukaa kwa muda mrefu bila kujaliwa na watoto (uk. 6). Ni wazi kwamba ndoa ya Yona na Sara imenyimwa hadhi katika jamii kwa kukosa mtoto wa kiume (uk. 7).
ร Kulingana na kizazi cha jana, mke anatarajiwa kujifungua watoto wa kike na wa kiume na hasa wale wa kiume. Ndoa ya Yona na Sara inasutwa na kukejeliwa na wanajamii kwa kukosa mtoto wa kiume ambaye aliaminika angekuwa mrithi wa Yona (uk. 8). Wanajamii walimtaka Yona kumwoa mke ambaye angemzalia watoto wa kiume. Kulingana nao, Sara alikuwa ameshindwa kumzalia mtoto wa kiume. Unyanyapaa huu ulimsukuma Yona kuupokea ulevi na kuanza kumpiga Sara kipigo cha mbwa kwa kuwa hakumzalia mtoto wa kiume (uk. 9-10).
ร Ni wazi kwamba ndoa ya Yona na Sara imenyimwa nafasi na hadhi katika jamii kwa kukosa mtoto wa kiume.
ร Ndoa pia imesawiriwa kama kitu chema ingawa chenye changamoto zinazoweza kuvumiliwa. Sara anasema kuwa ndoa ni uvumilivu na wala Sio watoto na hakuna ndoa isiyokosa doa. Sara anaivumilia ndoa yake na Yona. Anavumilia kuchapwa, kudharauliwa na kudhulumiwa. Sara anamvumilia mumewe hata baada ya dhiki hizo. Fauka ya hayo yote, anamshauri Neema aivumilie ndoa yake na Bunju. Vilevile, anamshauri Asna kumtafuta mume aolewe (uk. 33, 67).
ร Ndoa huakisi suala la malezi. Yona na Sara wanaonyesha malezi kwa kuwalea mabinti wao. Sara anawafurahia watoto wake na kujitahidi kuwalea ipasavyo.
ร Ndoa ya Neema na Bunju ni ya kizazi cha leo. Neema na Bunju wamesoma, wamehitimu na wameajiriwa na kuanza familia yao. Wanashirikiana katika masuala ya matumizi ya pesa. Bunju anashughulikia majukumu ya familia yake na Neema. Amemruhusu
ร Neema kutumia mshahara wake kuwasaidia wazazi wake. Ndoa katika tamthilia hii imesawiriwa kama uhusiano unaofaa kuleta heshima na uvumilivu. Bunju anamlalamikia Neema kwa kukosa kujulishwa kuwa mama mkwe wake anarejea kijijini bila yeye kujulishwa. Suala hili linamkera sana Bunju na kumuona Neema kama mke asiye na heshima (uk. 48).
ร Neema anasisitiza kuwa amempa mumewe heshima ya kutosha (uk. 49). Jambo la ndoa limesawiri majukumu ya mke na mume. Katika ndoa
ร ya Bunju na Neema, mume ana majukumu ya kulipa karo, kulipa kodi ya nyumba na majukumu mengine. Jambo hili linaonyesha kuwa Bunju ni mume aliyewajibika. Kwa upande mwingine, Neema ana jukumu la kuwatunza wazazi wake.
ร Katika ndoa ya Sara na Yona, Yona anasawiriwa kuwa na jukumu la kuwasomesha wanawe. Hata baada ya Sara kwenda mjini kwa ajili ya matibabu, Yona anachukua majukumu nyumbani kama vile kushughulikia mifugo na kuondoa mtama shambani. Katika mwisho wa tamthilia, Yona anamwahidi Sara kuwa atayachukua majukumu yote kama mumewe na atamshughulikia katika kila hali. Yona pia anaonyeshwa kuwa na jukumu la kumjuza Sara kuhusu mikutano ya vyama vya kina mama.
ร Ndoa pia imesawiriwa kama jambo lililojaa bughudha. Kulingana na Asna, ndoa ina mateso na imejaa masharti mengi. Asna anaona ndoa ya dadake Neema imejawa na matatizo yasiyoweza kuvumilika. Anasema kuwa Bunju ni mchoyo na asiyetaka kumsaidia mtu (uk. 33, 45). Asna vilevile anaiona ndoa ya wazazi wake kama iliyojawa na mateso.
ร Anamweleza mamake kuwa amedhoofishwa na mateso aliyoyapata katika ndoa yake (uk. 53). Hali hii inamfanya Asna kusawiriwa kama msichana anayetaka kuyajenga maisha yake bila mume.
Ulevi
ร Maudhui ya ulevi yameangaziwa kupitia mhusika Yona. Tunaelezwa kuwa Yona alijiingiza katika ulevi baada ya kushinikizwa na wanajamii kumuoa mke mwingine atakayemzalia mtoto wa kiume. Shinikizo hili lilimfanya kuingilia ulevi kwa hali ya juu zaidi.
ร Kutokana na ulevi, alianza kumpa mkewe Sara kichapo cha mbwa (uk. 10).
Tatizo hilo la ulevi linamwingiza kwenye matatizo chungu nzima.
ร Yona pia alifutwa kazi kwa sababu ya ulevi (uk. 56).
ร Ulevi uliyamega maadili ya Yona na kumpokonya uwajibikaji wa familia yake. Katika jamii yoyote ile, uraibu wa pombe uliopindukia unaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi katika familia. Yona anafutwa kazi na kuingia katika limbi la uchochole.
ร Anaanza kumdhulumu mke wake hadi kumsababishia maradhi ya moyo. Kwa kifupi, pombe inayavuruga maisha yake kama mfanyakazi na kama mume aliyetegemewa na jamaa yake.
Teknolojia na Maendeleo
- Suala la teknolojia na maendeleo limeonyeshwa na mwandishi kupitia maelezo ya wahusika kama vile: Neema, Asna, Sara, Luka na wahusika
- Maendeleo ya mjini na kijijini yamedhihirishwa kupitia mazungumzo ya Neema na Sara. Sara alikuwa amewasili mjini kwa ajili ya
- Neema anasema kuwa maendeleo mjini ni ya hali ya Anasema kuwa watu hufika mjini kutoka mashambani ili kupata jambo au kitu kizuri.
- Anasema kwao maendeleo bado na yanakuja kwa kudoda (uk. 17). Hali kadhalika, maendeleo ya kijijini yamedorora kwa sababu ya ahadi Sara anasema kuwa tangu wakiwa watoto maendeleo yamekuwa yakija hadi walipokuwa wazima na kujaliwa na watoto na ahadi hii ya maendeleo imebaki kuwa tu ahadi isiyotimizika wakati wa uhai wao (uk. 17).
- Katika mazungumzo ya Dina na Sara pale jikoni, Dina anasema kuwa anasikia mjini kuna magari mengi, majengo makubwa, barabara nyingi na pia watu wengi (uk. 15). Mazungumzo hayo yanaonyesha namna mjini kulivyoendelea. Dina anasema kuwa anasikia watu wa mjini wameendelea sana hata wametengeneza magari yatembeayo
- Maendeleo katika hospitali za mjini yamesawiriwa katika mazungumzo ya Sara. Anasema kwamba kwenye hospitali aliyokuwa amelazwa, huduma za huko ni nzuri sana mpaka anashindwa kuamini kama kweli yuko Anasema kuwa kuna kitanda kizuri, godoro nzuri na shiti nzuri zilizoplgwa pasi. Anasema kuwa madaktari hawakawii kuzibadilisha shiti hizo. Anasema hospitali za mjini si kama za kijijini ambazo amezisawiri kama seli na ukilazwa katika hospitali hizo tayari wewe ni kama mahabusu. Asna anasema kuwa hewa katika wodi za hospitali za kijijini huwa zimejaa harufu ya dawa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zimekagura. Anasema kuwa hospitali hizo hazimpi mtu matumaini ya kutoka akiwa bora na kumbidi mtu kuweka tumaini lake katika sala (uk. 42).
Mawaidha au Wosia
& Suala la mawaidha au wosia katika tamthilia ya Bembea ya Maisha linakuzwa na wahusika kama vile Luka, Yona, Sara na Neema. Sara anamwambia Neema kuwa asishindane na mwanamume hasa nyumbani ila wanaweza shindana kazini au
hata masomoni. Sara anawapa Neema na Asna mawaidha kuwa ni vyema wamheshimu Bunju kama ndugu yao.
& Sara anawapa mawaidha wanawe wamheshimu baba yao aliyewalea na kuwasomesha. Sara anawashauri Asna na Neema kuziheshimu na kuzitii mila na desturi za jamii yao. Luka anawashauri Beni na Yona kuhusu I-muhimu wa elimu ya mtoto wa kike katika jamii. Anadai kuwa tamaduni, mila na desturi zinazidi kubadilika na wanapoyapuuza hayo yote ni kazi bure (uk. 60). Luka awafundisha Beni na Yola kuhusu usawa kati ya watoto wa kike na wa kiume (uk. 60).
& Kuna mawaidha Sara anayompa Neema kwa njia ya mafumbo kuhusiana na maisha. Sara anamweleza Neema kuwa hakuna kizuri kinachokuja kwa urahisi. Analinganisha maisha na mbegu iliyopandwa. Mbegu hiyo hukua na kutoa mche wenye umbo la kupendeza hata baada ya kuoza. Vivyo hivyo, maisha hukumbwa na pandashuka lakini huzidi kuendelea. Anawataka Neema na dada zake warudi kijijini kuotesha mbegu zingine zitakazokua na kuwa miche ya kupendeza kama wao (uk. 68).
& Sara anampa bintiye Neema mawaidha ya jinsi ya kuelimisha wanakijiji na kuwapa maarifa ya kisasa. Anamwambia anaweza kuanza kwa kumshawishi baba yao badala ya kumkabili kumwelewa ndiposa aweze(uk. 69).
Malezi
ร Suala la malezi limejitokeza kupitia kwa wahusika Yona na Sara, Bunju na Neema na hata Bela. Yona na Sara wanajikakamua kuwalea watoto wao kwa njia inayostahili. Wawili hao walikuwa hawajiwezi kiuchumi hasa baada ya Yona kufutwa kazi kutokana na ulevi. Wanajitahidi kuwasomesha watoto wao.
Kifungua mimba wao, Neema, alisoma hadi Chuo kikuu na kupata shahada mbili. Wanawalea mabinti hao badala ya kuwaelekezea ndoa za mapema kama njia moja ya kutoroka uhitaji wa kiuchumi waliokuwa nao.
ร Neema na Bunju wanaonyesha malezi kwa kuwasomesha ndugu za Neema hadi kuhitimu Chuo kikuu. Bunju anasema kuwa waliishi na Salome huku wakimlipia karo ya shule ya upili na chuoni (uk. 28). Bunju na Neema vilevile wanamlea mtoto wao Lemi. Wanamsaidia kufanya kazi ya ziada ya shule.
ร Bunju na Neema wanasawiriwa kama wazazi ambao hawajawajibika katika kuwalea watoto wao kikamilifu. Wanamwajiri Bela ili awasaidie katika ulezi wa Lemi na shughuli za pale nyumbani. Mtoto wao Mina anasoma katika shule ya bweni, kwa hivyo mara nyingi hayuko nyumbani bali yuko shuleni. Hii ina maana kuwa malezi ya Mina yanatekelezwa na walimu wake. Vilevile, Neema anahuzunishwa na jinsi anavyokosa muda wa kuonana na mwanawe Lemi. Mara nyingi akitoka asubuhi Lemi huwa amelala na akirudi vilevile huwa amelala (uk. 22).
ร Bunju anasema kuwa mara nyingi Neema hayupo nyumbani na kuwa yeye ndiye humsaidia Lemi kufanya kazi ya ziada (uk. 49).
ร Bela anakuza maudhui ya malezi kwa sababu ameajiriwa kama mfanyakazi nyumbani kwa Neema. Bela ameiacha familia yake na kuja kuifanya kazi ya kumlea Lemi. Bela amezoeana sana na Lemi kuliko alivyozoeana na mamake Neema. Bela anamfahamisha Neema jinsi Lemi anavyoendelea. Anamwambia kuwa Lemi alikuwa amekula na keshalala kwa sababu ya uchovu uliotokana na mazoezi ya shuleni. Bela anasema kuwa kila baada ya kutoka shule, Lemi humwonyesha jinsi walivyocheza shuleni. Hii ina maana ya kuwa Bela ndiye aliyekuwa mlezi wa karibu wa Lemi.
ร Yona anamsifia Sara kwa kumsaidia katika kuwalea na kuwasomesha mabinti wao. Anasema alikuwa akiwaangalia ng’ombe shambani huku Sara akipeleka maziwa na kuuza bidhaa walizozalisha sokoni (uk. 62).
ร Malezi katika maisha ya mjini yanasawiriwa kama ya ajabu. Yona anasema kuwa malezi mjini ni magumu sana. Watu wa mjini huraukia vibarua na kurudi watoto wakiwa wamelala. Wanaishi wiki nzima hawajaonana na watoto wao. Malezi yameachiwa yaya. Yaya ambaye anaweza kumfundisha mtoto lugha au tabia aitakayo. Ulezi umejaa mashaka (uk. 59).
Taasubi ya Kiume
- Taasubi ni hali ya jamii kuthamini jinsia moja kuliko Jamii katika tamthilia ya Bembeaya Maisha imemthamini mwanamume kuliko mwanamke kwa njia zifuatazo.
- Mwanamume amesawiriwa kama mtu anayeweza kurithi mali ya Hii ni kuonyesha kuwa mwanamume tu ndiye mwenye uwezo huo (uk. 2).
- Sara anasema fimbo hurithiwa na watoto wa kiume wala si wa kike. Jamii inamshinikiza Yona kuoa mke mwingine ili aweze kumzalia mtoto wa kiume ambaye atakuwa mrithi wa fimbo
- Mwanamume ameonyeshwa kama mtu asiyestahili kuhusika na kazi ambazo zinaaminika ni za Kazi kama vile kupika na kuteka maji kisimani ni kazi ambazo zinaamika kuwa kazi za wanawake.
- Beni anamwambia Yona amekaa muda mwingi kama mkewe hayuko nyumbani. Beni anamuuliza Yona nani anayempikia muda wote huo kwani umri wake si wa kuingia jikoni kujipikia (uk. 61).
- Sara naye anamkaripia mwanawe Asna ambaye anasema haoni ubaya wa baba yake kwenda kujitekea maji kisimani. Sara anasema kwamba itakuwa aibu kubwa na wanajamii watamtazama Yona kwa dharau (uk. 44-45).
- Katika uk. 1, tunamwona Yona aliyekinai na kukasirishwa na Sara ambaye ameketi palepale ilhali hajamwandalia Yona hajali kuwa mkewe anaugua, haja yake ni chakula. Kwa sababu ya mila za jamii, Yona hawezi kuingia jikoni kuandaa chakula. Inamlazimu Sara kumwita Dina ili aje amsaidie katika maandalizi ya chakula. Suala hili limetiliwa mkazo katika mazungumzo ya Sara na Dina (uk. 14), kuwa mwanamume hawezi kusaidia katika kazi zozote za jikoni.
Utamaduni
- Utamaduni una nafasi muhimu katika jamii ya Sara na Wanajamii wanaamini kuwa kuna mafunzo mengi ambayo yanatokana na mila na desturi za jamii hiyo.
- Katika jamii ya Yona na Sara, kuna msisitizo mkubwa kwamba kila familia sharti iwe na mtoto wa kiume. Familia zenye watoto wa kike peke yake zinadhihakiwa na kudharauliwa kama ilivyofanyiwa familia ya Yona na Sara. Luka anapinga mwelekeo huu na kuwathamini watoto wa jinsia ya kike (uk. 60).
- Utamaduni unajitokeza katika baraza la wazee: Luka, Beni na Yona. Luka anawaalika wazee wenzake ili kunywa, kucheza na kufurahia mazao yao (uk. 64).
- Luka anataja kuwa mavuno ya kwanza huonjwa na wazee na kutoa baraka (uk. 58).
- Utamaduni unasawiriwa kama jambo lililopitwa na wakati kulingana na ulimwengu wa leo. Kwa upande mwingine, utamaduni unazidi kutiliwa mkazo katika ulimwengu wa jana. Bunju anakubaliana na utamaduni wa kutowakubali wazazi na wakwe zake kulala nyumbani kwake.
- Bela na Neema kwa upande mwingine wanapinga mawazo hayo na kusema kuwa utamaduni huo umepitwa na wakati na kuwa hauna nafasi katika ulimwengu wa leo uliojaa mabadiliko ya kila aina (uk. 24, 29).
- Asna anasema kuwa dunia imebadilika, ya zamani yamepita (uk. 36).
- Mila na desturi za jamii huwa na mafunzo ya Sara aliishi wakati wa jana na leo. Anatoa mafunzo kwa wanawe kuhusu utamaduni wa jana. Wakati Asna na Neema wanamwambia kuwa hakuna tatizo lolote anapolala nyumbani kwa Neema na Bunju, anadai kuwa mila zina mahali pake (uk. 36).
- Kulingana na mila na desturi za kizazi cha jana, msichana akisha baleghe, sharti aozwe (uk. 52).
- Mila na tamaduni za kizazi cha jana kinawajenga wanaume kama watu wasioweza kusaidia katika kazi za Kazi zote za jikoni zimeachiwa wanawake. Hata mume anapomsaidia mkewe kazi hizo, anaonekana kushushwa hadhi yake (uk. 14).
- Inasemekana kuwa watu watamcheka na kusema amekaliwa (uk. 66).
Elimu
Suala la elimu limepewa kipaumbele katika tamthilia ya Bembea ya Maisha hasa na kizazi cha leo. Maudhui haya yamekuzwa na Yona, Mina, Lemi, Sara na watoto wa Dina.
Yona ni mwenye elimu kwa sababu alikuwa mwalimu. Yona anasema kuwa wakati alipokuwa mwalimu, alikuwa akienda skuli wakati wa majira ya alfajiri, kiboko mkononi. Anasema kuwa siku nzima ilikuwa kazi tu, jioni ni darasani tena.
Alipotoka shule, alikuwa akivifunga vitabu kwenye baiskeli kwenda kuvisahihisha wikendi (uk. 62).
Yona amesoma hadi Chuo kikuu. Alikuwa mtu wa kwanza pale kijijini kufuzu kutoka chuoni.
Mabinti wa Yona na Sara wanasawiriwa kama watoto walio na elimu.
Elimu ya Neema inadhihirishwa tunapoambiwa kuwa amesoma hadi Chuo kikuu na kuhitimu shahada mbili. Bunju anasema kuwa Asna amesoma hadi Chuo kikuu alikohitimu digrii vilevile. Salome naye ameishi nyumbani kwa Bunju na Neema huku akisoma Shule ya upili.
Baadaye anafanikiwa kwenda Chuo kikuu alikopita na kupata first class. Alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kuendeleza masomo yake ng’ambo (uk. 28).
Elimu imeonyeshwa kupitia watoto wa Neema na Bunju: Mina na Lemi. Mina anasemekana kuwa anasomea Shule ya bweni. Lemi naye anakuza elimu kwa jinsi anavyoshiriki katika kazi yake ya ziada baada ya kutoka shuleni. Bela anamweleza Neema jinsi Lemi hujinengua anapocheza nyimbo za shuleni. Elimu imesawiriwa kama nguzo ya ufanisi katika maisha ya leo. Wahusika waliosoma na kuhitimu kama vile Yona, Neema na Sara wanafanikiwa kupata kazi na kuwa mwanga wa kijijini.
Migogoro
- Migogoro ni hali ya mvutano au kutoafikiana baina ya pande mbili au zaidi. Migogoro katika tamthilia huzuka kwa sababu ya mambo mbalimbali Katika tamthilia hii kuna migogoro ya kitamaduni kati ya wanausasa na wanakizazi cha jana, migogoro katika ndoa, maisha na maendeleo ya mjini na kijijini.
- Kuna mgogoro wa kitamaduni kati ya kizazi cha leo na kizazi cha jana kinachoshikilia imani zilizopitwa na wakati. Kwa mfano, Asna anamwona babake angali kijana na ana uwezo wa kutekeleza majukumu ya nyumbani kama vile kuteka maji kisimani. Wazo la Asna linaleta mvutano baina yake na mamake. Sara analiona wazo hilo kama bovu na lisiloweza kutekelezwa na mumewe kwa sababu ya jinsi wanajamii watakavyomchukulia. Sara anasema kuwa wanajamii watamshushia hadhi na watamtazama kwa sini ya dharau (uk. 44-45).
- Utamaduni unazua mgogoro kati ya Asna na Kulingana na Sara, utamaduni wa jamii unamtaka kila msichana aliyebaleghe aozwe.
- Asna anapinga utamaduni huo na kudai kuwa, hilo ni jambo lililopitwa na Asna anadai kuwa msichana anaweza kuolewa au kukosa kuolewa. Na anapotaka kuolewa, anaweza kuolewa kwa wakati autakao yeye bali Sio kwa wakati wanaotaka wanajamii.
- Mgogoro unajitokeza baina ya mawazo ya Bunju kuhusu mila zinazowakataza wazazi kulala nyumbani kwa mkwe na mawazo ya Neema, Asna na Bela. Neema anapinga mawazo hayo na kusema kuwa mila hizo hazina thamani wala nafasi tena katika dunia ya sasa (uk. 29). Asna naye anayapinga mawazo hayo kwa kusema kuwa dunia imebadilika (uk. 36). Bela vilevile anapinga wazo hilo kwa kusema kuwa hayo ni ya kale na kuwa watu wengi hawafuati mila hizo kwani ulimwengu umebadilika (uk. 24).
- Kuna migogoro ambayo inazuka katika asasi ya ndoa. Ndoa ya Sara na Yona ni yenye Yona anasababisha mgogoro baina yake na Sara kwa kumchapa na kumkosea hadhi Sara kwa kukosa mtoto wa kiume.
- Mgogoro huu unasababisha Sara kupatwa na maradhi ya moyo na kumfanya mwanawe Asna kuona ndoa kama
- Ndoa ya Bunju na Neema ina mvutano kuhusu suala la matumizi ya pesa na suala la malezi ya mtoto wao Lemi. Bunju ana msimamo wake kuhusu majukumu yake kwa familia yake na kusema gharama ya matibabu ya mamake Neema Sio jukumu
Neema anahisi kuwa
- Bunju anaweza kumsaidia katika matibabu ya mama Wawili hao wanavutana kuhusu suala hilo. Wazo la Bunju linamfanya kumuona kama mkono birika na asiyetaka kuwasaidia.
- Neema na Bunju wanavutana vilevile kuhusu suala la kumpeleka Lemi kwenda kucheza na kuogelea na Neema anamsihi Bunju ampeleke Lemi kujivinjari lakini Bunju anasema kuwa hawezi kwenda huko badala ya kwenda kuvuta riziki. Isitoshe, anadai kuwa michezo hiyo hununuliwa si kama ya zamani (uk. 48).
- Bunju anasema kuwa Neema anapenda kukana na lazima abishe jambo ambalo litamfanya kuonekana mbwa
- Kuna mgogoro baina ya wanajamii na familia ya Mvutano unazuka wakati ndoa ya Yona na Sara inakosa kujaliwa na mtoto.
- Wanajamii wanaikejeli na kuisuta ndoa hii na kumuita Yona gumba na Sara tasa. Hata wanapopata watoto wasichana bado jamii inawasuta kwa kukosa mtoto wa
MBINU ZA LUGHA NA MBINU ZA KIMUUNDO
Mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ametumia mbinu mbalimbali za lugha na za kimuundo ili kuwasilisha dhamira na maudhui yake.
Mbinu za lugha
- Lugha ya kitamthilia ni lugha maalumu. Hii ni kwa sababu inatumika katika utanzu wa kijukwaa. Jukwaa la uigizaji humpatia mwandishi fursa ya kutumia lugha ambayo sharti iambatane na uigizaji. Vilevile, kuna lugha ya uigizaji ambayo inaweza kuhusisha uteuzi wa maneno wenye urari kama katika
- Katika tamthilia ya Bembeaya Maisha, mwandishi ametumia lugha kwa njia mwafaka ili kutekeleza malengo yake. Tamathali za usemi zimetumika kwa
Taswira
- Twasira ni dhana ambayo hutumia maneno ili kumchorea msomaji picha fulani katika fikira au akili yake. Pia huitwa
- Inawezekana mwandishi kutumia taswira za kimaelezo au zile zilengazo hisi za mwanadamu kama vile joto, mnuso, mguso na
Mifano
ร Taswira inajitokeza kwenye maneno yaliyo kwenye mabano au yaliyoandikwa katika hati ya kiitaliki. Maelezo hayo yanatuchorea picha akilini mwetu.
Yanatufahamisha na kutujulisha dhahiri wakati, mahali na matendo yanapofanyikia.
ร Kwa mfano, katika onyesho la kwanza sehemu ya kwanza maneno yaliyo kwenye mabano yanatuonyesha kwamba onyesho linafanyika wakati wa alasiri, mahali ni nyumbani kwa Sara, tunaona Sara akichukua vidonge vya dawa na kuvimeza
ร kabla ya kuketi kwenye kochi jipya. Tunaona namna ukuta wa nyumba ya Sara umepambwa na picha za familia. Takriban maneno yote yaliyo kat:ika hati ya kiitaliki yanatuchorea picha fulani akilini, hivyo yanajenga taswira.
ร Taswira katika tamthilia hii pia imejidhihirisha kupitia kwa maneno yanayosemwa na wahusika. Kupitia usemaji wa wahusika, msomaji anapata taswira fulani kuhusiana na namna mhusika anavyozungumza. Kutokana na maneno yao, msomaji hupata taswira sikivu ambayo inamdhihirishia toni au kiimbo anachotumia mhusika lengwa.
ร Katika Onyesho I Sehemu I; mazungumzo kati ya Sara na Yona yanatuonyesha taswira sikivu ya toni wanayotumia, Yona anatumia toni ya juu naye Sara anatumia toni ya chini. Maneno Yao yanatuchorea picha akilini kuhusu wanavyozungumza.
Taswira ya aina hii ndio inayowezesha tamthilia kuigizwa jukwaani kwa kutumia toni au kiimbo kinachofaa.
ร Anwani ya tamthilia hii inatuchorea picha akilini. Neno bembea linarejelea kifaa ambacho mara nyingi hutumika na watoto kuchezea. Kifaa hiki huenda juu na chini na kurudi nyuma na mbele. Hivyo basi,
ร BEMBEA YA MAISHA ni taswira fikirivu, msomaji anaposoma anwani hii anapata mawazo mengi kuhusu maisha ambayo anayalinganisha na bembea. Msomaji anatarajia kupatana na maisha ambayo yana panda shuka au ambayo yanayumbisha anaposoma tamthilia nzima. Hali hii inadhihirika wazi kwa kuwa anwani Bembea ya Maisha imejidhihirisha katika maelezo na matendo ya wahusika katika tamthilia nzima.
Mifano ya taswira inayojitokeza katika dondoo
- …Miaka inaposonga ..kama..kama vile tambara bovu. Tambara lisilomjia hata mpiga deki akilini (uk. 4). Maneno haya yanatumiwa na Yona yakielekezewa mkewe. Maneno haya yanaonyesha namna wanaume hawana umuhimu wowote kwa wanawake katika jamii ya tamthilia hii.
- …Wewe unaona rangi ya mwisho wa kinachoelea. Kabla kielee kimepigwa shoka, kimeonja misumeno aina aina, kimetambaliwa na randa, kimestahimili makali ya patasi na kupapaswa na mikwaruzo ya msasa (uk. 10). Haya ni maneno ya Dina akimweleza Kiwa kuhusu maisha ya mabinti wa Yona na Sara. Maneno haya yanatujengea taswira ya Msomaji anaposoma maelezo haya anaona picha ya watu walioishi kuteseka, kunyanyaswa na kwa jumla watu walioishi maisha magumu sana kisha kufanikiwa baadaye.
- …Nilikuwa kimbaumbau mwiko wa pilau. Upepo mchache tu ungeniyumbisha kamajani kavu wakati wa kipupwe (uk. 10). Haya ni maneno ya Sara akimweleza Maneno haya yanatuonyesha taswira ya maono. Tunaona namna mwili wa Sara ulikuwa umedhoofika na afya yake kuzorota kwa kukondeana kama ngonda hadi kufikia kiwango cha kupeperushwa na upepo.
- …Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka (uk. 18). Haya ni maneno ya Sara ya kumpongeza Neema kwa juhudi zake za kujiendeleza kimaisha. Analinganisha hali hii na ya mkulima ambaye amelazimika kufanya kazi ngumu shambani na kupata vuno zuri. Ili afanikiwe sharti nguo zake zichafuliwe na udongo na Kama angaliogopa kuchafuka basi mkulima asingelifanikiwa.
- …Mwanangu usitake kuhoji alacho Utachafukiwa roho umchukie kuku bure. Wala usitake kujua asali ameitengenezea nini nyuki. Hutaila. Maadamyameshakujayapokee (uk. 20). Kupitia maneno haya, Sara anampatia Neema moyo ili ajikaze na kumvumilia mumewe kwa kupuuza udhaifu wake kwani asipofanya hayo ndoa yake na Bunju inaweza kuingia doa.
- … Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa Huungwa na mchezo kuanza tena (uk. 21). Sara analinganisha mchezo wa watoto wa kubembea na maingiliano ya ndoa. Mchezo wa bembea humalizika kwa sababu bembea imekatika na uhusiano wa ndoa hutatizika wanandoa wanapokosa kuvumiliana.
- Ni kama mti mchanga kwenye chaka la miti mikubwa Unaishi kutapia
hewa na jua. Unajitahidi kutoa Shingo kila wakati kuung’ang’ania mwanga huo. (uk. 26) Haya ni maneno ya Neema akimweleza Bela namna watu wa tabaka la chini hulazimika kufanya bidii ili kujinyanyua kutokana na mnaso wa umaskini. Hali hii inalinganishwa na jinsi miti michanga inavyong’an<ana kuufikia mwanga porini.
Misemo
Misemo ni aina ya semi fupi zenye ukweli ambazo hutumiwa kuelezea mambo yenye kuafiki ukweli huo. Mwandishi ametumia mifano kadhaa ya misemo katika tamthilia hii.
Mifano
- Kutupigajeki (uk. 3) – Kumpa mtu msaada au
- Kuadimika kama wali wa daku (uk. 5) – Ni kutoonekana kwa muda mrefu
- Kufanya nongwa (uk. 12) – Kusongwa na moyo kutokana na jambo
- Kila limfikalo mwanadamu ni mpango wa Manani (uk. 12) – Imani kuhusu majaaliwa ya kwamba tunayokutana nayo ni mpango wa Mwenyezi
- Kupiga makasia chombo kinapopungukiwa na upepo (uk. 14) Kutoa msaada wakati hali ngumu inapomkabili
- Kichwa kimeudara mto (uk. 1) – Kichwa kimelala juu ya
- Tiwa vinywani (uk. 6) – Semwa sana na
- Bongo za sumaku (uk. 7) – Bongo zinazoweza kushika mambo kwa
- Sisimkwa na malaika (uk. 12) – Kuwa na
- Nisiyatie machungu moyoni (uk. 12) – Nisihuzunike, nisiwe na
- Watoto ni baraka (uk. 18) – Watoto ni majaliwa ya Mwenyezi
- Fungulia milangoya heri (uk. 18) – Achilia
- Ingiajakamoyo (uk. 44) – Patwa na
- Ponza roho (uk. 44) – Jiingize katika
- Ana bidiiya mchwa (uk. 45) – Bidii
- Kutokuwa na kabaya ulimi (uk. 48) Kutojizuia, kusema sana na kila
- Kuwa chiniya amri (uk. 49) – Kuwa
- Ujana ni moshi (uk. 52) – Ujana ni sawa na moshi ambao ukienda
- Ndoa ni mtihani mkubwa (uk. 53) – Ndoa ina matatizo mengi; inahitaji
Nahau
Nahau ni aina ya semi ambazo huundwa kwa fungu la maneno ya kawaida yanayozua maana tofauti na ile ya maneno hayo. Nahau ni maneno ya busara ambayo hutumiwa kueleza kitu kutokana na mifano katika maisha. Ni bayana kwamba nahau hutokana na mazingira ya watumiaji wa lugha husika. Nahau hutumiwa kupamba lugha na kupunza ukali wa maneno.
Mifano
- Kutupa jogoo na mti wake (uk. 3) – Inamaanisha kuachana na jambo Sara anarejelea jinsi ambavyo baadhi ya wasichana wanavyowasahau ndugu zao wanapoolewa.
- Bahatiya mtende (uk. 3) – Ni kubahatika sana kwa njia
- Kushindana na ng’onda (uk. 5) – Kukonda
- Kikapu cha mama kimejaa ndago (uk. 6) – Usemi unaoashiria mtu aliyefanikiwa. Usemi huu unamrejelea Sara ambaye alikuwa na uhitaji siku za nyuma lakini sasa bintize wanamfaa kwa hali na
- Maji kuzidi unga (uk. 11) – Hali kuwa tatizi au ngumu kukabiliana
- Utakuwa unajivulia nguo (uk. 14) – Utakuwa
- Nyotayajaha (uk. 19) –
- Tumeyaacha maji ya mbizi tukaingia maji ya mbuzi (uk. 20) Tumetoka kwenye hali ngumu na sasa tumeingia kwenye hali
- Taaridhi isiyo kifani (uk. 24) – Udadisi; hali ya kuuliza uliza au kuchunguza
- Bora punda afe mzigo ufike (uk. 27) – Kutomjali mfanyakazi bora tu kazi Hata anayeifanya akidhurika Sio hoja.
- Fanya ajizi (uk. 1) – Legea, kuwa mvivu, Zika katika giza la kina cha moyo (uk. 7) – Nyamazia jambo au fanya kuwa siri.
- Angukiwa na nyotayajaha (uk. 19) –
- Piga kalamu (uk. 19) – Achisha
- Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24) – Watu wamebadilika; wameachana na ya kitambo na wanafuata ya Akili za madongo kuinama (uk. 23) – Akili hafifu zisizo imara.
- Mchele umeingia mchanga (uk. 26) – Mambo
- Poa moto (uk. 26) – Tuliza hasira; kuwa
- Bunju ni mkono wa birika (uk. 33) – Ni
- Chombo kingezama (uk. 62) – Mambo
- Kujipiga kifua (uk. 63) –
- Kata shauri (uk. 70) –
- Sikuwa na picha nzima (uk. 74) – Sikuwa na ufahamu wa
Mbinu ya majazi
Majazi ni mbinu ambayo mwandishi hutumia kuwapa wahusika majina kulingana na tabia zao. Mbinu hii inadhihirika kupitia kwa wahusika kama vile:
ร Bunju – jina Bunju ni la kimajazi. Bunju alipewa jina hili lililolinganishwa na mnyama mwenye sumu lakini sumu hiyo huondoka baada ya kusafishwa. Bunju ana tabia mbaya inayolinganishwa na sumu ya mnyama huyo. Kwa mfano, alionekana kuwa na ukali kwa mambo ya kusaidia Neema katika matibabu ya mama mkwe (Sara). Baada ya kushawishiwa kwa muda na Neema, ukali huo unamwondoka na kumweleza Neema kwamba atamsaidia kulipa gharama ya matibabu ya mama yake (uk. 40). Anamwambia atampiga jeki.
ร Neema – Neema ni jina la kimajazi. Neno neema lina maana ya kufanikiwa au kustawi. Mwandishi amempa Neema jina hili kutokana na sifa za kustawi na kufanikiwa maishani. Neema amefanikiwa kusoma hadi Chuo kikuu na kustawi kwa digrii mbili, amefanikiwa kupata kazi nzuri, amefanikiwa kupata mume anayemjali na kushughulikia maisha ya familia yake na pia amefanikiwa kuwalipia karo dada zake hadi Chuo kikuu. Kwa kifupi, mhusika Neema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa maishani.
ร Sara – mhusika Sara amepewa jina hili kutokana na namna alivyosemwa na wanajamii. Neno sara lina maana ya kutapakazwa au kuenezwa kila mahali. Jina la Sara lilienezwa na wanajamii kila mahali. Alisemwa sana na kutukanwa kwa kuwa hakuwa na watoto wa kiume (uk. 13). Alisemwa kotekote ikiwemo makanisani na magengeni. Kwa sababu hii mwandishi akampa mhusika huyo jina, Sara.
Lakabu
- Lakabu ni mbinu ambayo mwandishi hutumia kuwapa wahusika majina mbali na majina yao Lakabu huwa ni jina la kupanga au jina la kutania. Mhusika ametumia mbinu hii kuwarejelea wahusika kama vile:
- Kalasinga – hili ni jina alilojipa baba yake Yona. Alijipa jina hili kwa kuwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kufanya kazi kwa Mhusika huyo alijifunza
Kihindi na kufanikiwa kukimudu vizuri baadaye akajipa jina Kalasinga. Kalasinga si jina lake halisi ila ni jina la kupanga.
Tasfida
Tasfida ni matumizi ya maneno yanayoficha ukali wa hali fulani. Mwandishi anatumia mbinu hii kupitia kwa mifano ifuatayo:
ร Sara: Hata nikiitwa nitaondoka nikiwa nimeridhika (uk.13). Haya ni maneno ya Sara akirejelea ufanisi wa watoto wake ambao walikuwa wanachekwa na majirani kutokana na fikra kuwa hawawezi kufaulu kwa sababu ya uhitaji wa wazazi wao. Sara anamaanisha kwamba hata
ร akiaga dunia atakuwa ametekeleza azimio lake la kuwasaidia watoto wake kufaulu maishani.
ร Bunju: Unataka nifurahi ghaya wakati huna kamba ya ulimi (uk. 48). Haya ni maneno ya Bunju kwa Neema. Bunju anatumia tafsida kwa kutumia neno”kamba ya ulimi,” kuficha ukali fulani. Maneno haya yanamaanisha kwamba Neema anaongea sana au anaropokwa na maneno.
ร Dina: wewe umekua ukampata Yona kipenzi cha maji (uk. 10). Kipenzi cha maji ni maneno yenye maana ya mtu anayependa pombe; mievi
ร Sara: watt/ walituona masikini wa watoto. Maskini wa kizazi (uk. 55). kupindukia. Maneno haya yametumiwa kurejelea mtu asiye na uwezo wa kupata mtoto, badala ya kutumia maneno ya moja kwa moja na makali kama vile gumba au tasa.
Kuchanganya ndimi
Kuchanganya ndimi ni mbinu inayotumiwa na mwandishi kuonyesha hali ya kuzungumza lugha mbili au zaidi kwa pamoja. Mwandishi wa tamthilia hii ametumia mbinu hii katika uandishi wake kama ishara ya maudhui ya elimu na pia kusawiri hadhi ya wahusika fulani kama walioelimika.
Mifano:
- Culture shock (uk. 46) – Usemi huu unamaanisha hali ya kushangazwa na mienendo ya watu ambao wana utamaduni tofauti au mazoea tofauti na yale ambayo mtu
- Homework (uk. 40). Asna anasema Lemi amempa homework. Hii ina maana kuwa amempa kazi ya Pia ukurasa 49, Bunju anasema kuwa “ninamsaidia kufanya homework”.
- Boarding school (uk. 27). Usemi huu una maana ya shule ya
- First class(uk. 28). Usemi huu unamaanisha kiwango cha juu zaidi cha kupita mtihani wa Chuo
- Flying doctors (uk. 41). Usemi huu unamaanisha madaktari ambao husafirishwa kwa ndege ili kufika haraka mahali penye wagonjwa
- My foot (uk. 26). Mwandishi ametumia usemi huu kukejeli. Bunju anatumia usemi huu kumkejeli mke wake Ni usemi unaotumiwa katika jamii ya kisasa na vijana kwa lengo la kutupilia mbali mawazo ya watu wengine.
- Hii Servant Quarter inanitosha (uk. 31). Asna anatumia neno servant quarter kurejelea chumba anamoishi Chumba cha aina hii aghalabu hutumiwa na wafanyakazi wadogo kwenye boma la mwajiri wao. Kwa hivyo, iwapo Asna anaishi mtaa wa kifahari, hana nyumba ya kifahari huko bali anaishi katika chumba kidogo tu.
- I wish wangeelewa (uk. 72). Neema anatumia maneno I wish kuonyesha matamanio yake kwa wale wanaopewa kibarua kujua kuwa waajiri wao wanapitia magumu ili kupata mali kidogo waliyonayo.
- Sharp (uk. 73). Katika muktadha wa matumizi usemi huu una maana ya kuelewa mambo kwa upesi au kwa
- Mum (uk. 47). Lemi anatumia jina hili kumwita mama Mum ni jina la Kiingereza linalomaanisha mama.
- Kesho una time umpeleke huyu out? (uk. 48). Katika muktadha wa matumizi, neno out lina maana ya ‘ziara’. Yaani kwenda kuburudika na kujivinjari. Lemi alitaka kupelekwa out wakacheze na kuogelea pamoja na watoto Nalo neno time limetumiwa kuonyesha ‘nafasi’.
- Tomboy (uk. 52). Hii ina maana ya msichana anayeishi na kutenda mambo kama
Kubadili msimbo
Hii ni mbinu ya kubadilisha lugha wakati wa mazungumzo na kuanza kutumia lugha nyingine tofauti na ile ya kwanza. Mwandishi ametumia mbinu hii katika tamthilia kuonyesha hekima au elimu..
Mfano;
If wishes were horses beggers would ride (uk. 72). Maneno haya yalisemwa na Yona kwa Neema. Mhusika Yona anabadili msimbo kutoka kwa lugha ya Kiswahili hadi lugha ya Kiingereza kwa kutunga sentensi nzima. Ni kauli inayodhihirisha majuto na nia ya mabadiliko kwa upande wa Yona.
Maswali ya balagha
Hii ni njia ya usemi ambayo hutumia maswali yaliyokusudiwa kusababisha athari fulani bila kutarajia majibu.
Mtindo huu umetumiwa na Sara anayeuliza:
(Kwa ukali.) Hivi mtoto una akili wewe? Babako aende kuteka maji kisimani? Wazee wenziwe watamwonaje? Kijiji kitasema nini? Kwamba
amesomesha watoto ambao wameniweka jijini ili baba yao ataabike2 hiyo ndiyo heshima?(uk. 44)
Sara alikusudia kuonyesha hisia zake kuhusu kuendelea kukaa kwake mjini na kumsababishia mumewe izara. Usemi huu pia unaendeleza maudhui ya utamaduni, migogoro, na nafasi ya mwanamke katika jamii pamoja na kusawiri sifa za Sara.
Mbinu hii imetumika pia katika mazungumzo nafsia ya Neema (uk. 41). Anajiuliza: Leo tungekuwa wapi bila Bunju? …Mtu huyo atakosaje kuwa zawadi kwako? Maswali haya yanadhihirisha mabadiliko katika hisia za Neema juu ya mumewe Bunju. Anaanza kumthamini zaidi.
Utohozi
Utohozi ni mbinu ya kubadili maumbo ya maneno ya lugha moja na kuyafanya yachukue muundo wa lugha nyingine. Mwandishi ametumia majina ya kutoholewa kutoka lugha ya Kimombo hadi lugha ya Kiswahili. Mifano
ร Hospitali (uk. 51) – neno hili limetoholewa kutoka kwa neno la Kiingereza hospital.
ร Familia – limetokana na neno la Kiingerezafamily.
ร Skuli – limetoholewa kutoka neno la Kiingereza school.
ร Presha (uk. 11) – limetoholewa kutoka neno la Kiingereza pressure.
ร Daktari (uk. 12) – limetoholewa kutoka neno la Kiingereza doctor.
ร Afisini (uk. 27) – limetokana na neno la Kiingereza office.
ร Kliniki (uk. 14) – neno hili limetokana na neno la Kiingereza clinic.
ร Hoteli (uk. 42) – jina hili limetoholewa kutoka kwa neno la Kiingereza hotel.
ร Rekodi (uk. 73) – neno lililotoholewa kutoka neno la Kiingereza record.
Tashbihi
Huu ni usemi wa ulinganisho au ufananisho wa vitu viwili au zaidi kwa kutumia maneno ya ulinganishi: kama vile, kama, mithili ya, mfano wa na kadhalika.
Mifano
- Tafunwa kama chingamu (uk. 6); kusemwa sana na
- Kutuona kama tambara bovu (uk. 4); ni kuonekana vibaya au kitu kisicho na
- Hayayalikuwa kama vishindo vya mashua na Sisi kama bahari (uk. 56); maana ya tashibihi hii kulingana na matumizi ya muktadha ni kwamba matatizo ya maisha yao yanafananishwa na hali ya mashua kupita kwenye bahari na kwamba walistahimili na .
- Tunaendeshwa kama tiara (uk. 23); kuendeshwa Kazi kama safari ya ahera (uk. 23); kazi ambayo inachosha; isiyokamilika.
- Ni wazi kama mchana (uk. 3) – jambo lisilofichika, lisilo
- Mwili mzima mfano wa bua (uk. 4) mwepesi – mwili hauna nguvu, ni
- Ni kama msafiri katikajangwa (uk. 7) – mtu mwenye kiu au tamaa ya kupata kitu
- Mwanadamu sawa na tumbo, hakinai (uk. 8) – mwanadamu
- ponyoka kama maji kwenye viganja (uk. 10) – jambo lisiloweza
- Upepo ungeniyumbisha kamajani kavu (uk. 12) – upepo ungempeleka kokote ufanyavyo majani
- Maisha yamekuwa mfano wa gurudumu kwenye gari la masafa marefu (uk. 23). Hata gurudumu likichoka halina hiari. Litaenda tu namna Watu hawana chaguo ila kuendelea na maisha yajavyo.
- Kujisikia kama abiria kwenye gari liendalo kasi (uk. 29) – kuwa na wasiwasi; kutotulia.
- Konda kama ng’onda (uk. 32) – konda Mwoga kama kunguru (uk. 34) – mwoga sana.
- Safi kama pamba (uk. 35) โ bila doa, uzuri Hospitali za kijijini ni kama seli (uk. 42) – hali yake ni mbovu.
- Watoto wa siku hizi wanakua mithili ya mchicha (uk. 43) wanakua kwa
- Ana moyo kamajiwe (uk. 45) – ana moyo mgumu; si mwepesi wa kutoa; ni
- Kuteleza kama sabuniya povujingi (uk. 56) – kushindwa kumudu hali
Methali
Methali ni aina ya semi ambayo huwa na muundo maalumu. Hueleza ukweli fulani wenye maana pana na unaoweza kufasiriwa kwa njia mbalimbali.
Methali hukusudia kuonya, kuelekeza, kuadhibu, kusuta, kulaumu, kushauri na kadhalika. Methali huwa imebeba maana pana kuliko maneno yenyewe.
Tamthilia ya Bembea ya Maisha imetumia mbinu ya methali kwa wingi. Mifano:
- Mungu hamwachi mja wake (uk. 8).
- Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu ki uchungu (uk. 63).
- Baada ya dhiki faraja (uk. 6).
- Njia haimuagulii msafiri (uk. 6).
- Binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe (uk. 5).
- Mlango mmoja ukifunga, macho huiona mingine mingi (uk. 56).
- Mwacha mila ni mtumwa (uk. 58).
- Mgala muue na haki yake mpe (uk. 66).
- Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi (uk. 67).
- Kutoa ni moyo, usambe ni utajiri (uk. 2)
- Mtu hujikuna ajipatapo (uk. 2)
- Mungu si Athumani (uk. 10)
- Mungu hamtupi mja wake (uk. 10)
- Leo kwangu kesho kwal<0 (uk. 11)
- Mungu hamwachi mja wake (uk. 11)
- Safari ya kesho huungwa leo (uk. 16)
- Mrina haogopi nyuki (uk. 18)
- Papo kwa hapo kamba hukata jiwe (uk. 21)
- Mwana wa yungwi hulewa (uk. 21)
- Kipendacho roho hula nyama mbichi (uk. 21)
- Ya kale hayanuki (uk. 24)
- Mapema ina sudi (uk. 25)
- Afikaye kisimani mapema hunywa maji maenge (uk. 25)
- Samaki hukunjwa angali mbichi (uk. 26)
- Msafiri kafiri angawa tajiri (uk. 31)
- Mwindaji huwa mwindwa (uk. 32)
- Ng’ombe halemewi na nunduye (uk. 35)
- Mali ya bahili huliwa na mchwa (uk. 45)
- Mgala muue na haki umpe (uk. 66)
Methali katika tamthilia ya Bembeaya Maisha zimetumika kutekeleza yafuatayo:
ร Kupamba lugha na kuipa mvuto wa kisanaa.
ร Kuendeleza maudhui na dhamira ya mwandishi, hasa kuhusu suala Zima la bembea ya maisha.
Sitiari
Ni mbinu ya lugha inayotumia ulinganisho wa moja kwa moja wa kitu na kingine. Kitu kimoja husemwa kuwa kingine. Mifano ya sitiari katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
- Mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani yake akijua itamfaa (uk. 1-2). Yona analinganisha wanawe (Asna na Neema) na mbegu, mazao yake, na mavuno. Pia, anawalinganisha na sahani ambayo aliitakasa imfae.
- Katika 2, Sara anasema kuwa Neema ana ‘mzigo’ wa familia yake. Mzigo umetumiwa kama sitiari ya majukumu mengi au mazito.
- Vilevile, kwenye 2, Yona anasema kuwa fimbo ya mzee hurithiwa na mtoto wa kwanza. Fimbo ni sitiari ya nafasi ya mzee katika familia.
- Ukurasa wa 3, Sara anasema kwamba wachapakazi hodari ni njozi Hii ina maana kuwa hawapatikani.
- Mimi mzigo (uk. 4) – mtu ambaye ni tatizo kwa jamaa zake, anayetekelezewa majukumu yake yote.
- Amekuwa na kimo cha sindano (uk. 5) – amekuwa mwembamba
- Neema ni chuma cha reli (uk. 6) – Neema ana nguvu za kustahimili changamoto za
- Katika 8, mvua ya baraka iliwanyea Yona na Sara. Mvua ya baraka ni sitiari ya watoto ambao Yona na Sara walibarikiwa kuwapata.
- Dina anaeleza kuwa watu walimtaka Yona kutafuta mtoto wa kiume ili “utambi wa ukoo wake usizime” (uk. 10). Utambi wa ukoo ni sitiari ya kizazi cha
- Ukurasa wa 11, dunia ni nyumba ya mitihani. Hii ina maana kuwa dunia ni mahali pa changamoto
- Sara anasema kuwa alipoanza kuugua alikuwa kimbaumbau mwiko wa pilau (uk. 12) – hii ina maana kuwa alikuwa mwembamba na mithili ya mwiko wa kupikia
- Safari hii ni maji ya mbizi (uk. 16) – safari ni ndefu Maisha ya siku hizi si maji ya kunywa (uk. 23). Maisha si rahisi au
- Mamangu mzazi ni mboni ya jicho kwetu (uk. 30) – mama mzazi ni mwangalizi
- Nyumbani, hiki ni kizimba cha kuku (uk. 31) – ni chumba kidogo na
- Maisha ni mshumaa usio mkesha (uk. 32) maisha ni mafupi na hayapo
- Sara na Bunju ni chanda na pete (uk. 36) – wanalingana katika maoni yao, ni
- Mifuko inazidi kuwa king’onda (uk. 41) – inaendelea kuishiwa
- Akili za Yona zinatajwa kuwa sumaku (uk. 43) – zinashika mambo
- Nina jeshi lake (uk. 46) – nina watoto
- Bunju anamweleza Neema kuwa kuwa yeye (Bunju) ni kichwa na Neema ni shingo (uk. 49). Hii ina maana kuwa Bunju ndiye kiongozi wa nyumba naye Neema ni msaidizi wake.
- Ujana ni moshi (uk. 52) – ujana ni kitu kinachopita na kikienda
- Ndoa ni mtihani mkubwa sana (uk. 53) ndoa ina majaribu
- Luka anamrejelea Neema kama ‘simba wa kike anayenguruma’ (uk. 61). – hii ina maana kuwa Neema ana sauti, usemi au hadhi sawa na ya mtoto wa
- Watoto walikuwa nyota ya jaha (uk. 61) โ ina maana kuwa watoto wa Sara na Yona walikuwa bahati kubwa
- Mwanamume ni mto wa kifuu (uk. 67) – ina maana kuwa mwanamume amesawiriwa kama mtu
- Sasa rudini mzalishe mbegu nzuri (uk. 68) – wawasaidie watoto wengine kukua vyema kama wao; wawe mfano kwa
- Shikeni usukani muwe marubani wa kweli ili ndege ipae angani (uk. 68) – chukueni nafasi ya kuleta maendeleo
Tashihisi
Tashihisi ni mbinu ya mwandishi kuvipa viumbe visivyo na uhai sifa za uhai au za kibinadamu. Pia huitwa uhuishi.
ร Katika uk. 5, Kiwa anasema kuwa mvua yenyewe imefanya ugeni. Kiwa analinganisha mvua na mgeni, na hivyo kuipa mvua sifa za uhai.
ร Katika uk. 6, Dina anasema kuwa maradhi yamemgeuza Sara kuwa ngoma.
Katika mfano huu, maradhi yamesawiriwa kuwa yenye uwezo wa kumpiga Sara kama vile mtu anavyopiga ngoma.
ร Katika uk. 9, Dina anamweleza Kiwa kuwa “dunia mwanangu imetufunza Sisi wazee wenu”. Katika mfano huu, dunia imepewa uwezo wa kutoa mafunzo. Hii ina maana kuwa matukio mbalimbali duniani yana uwezo mkubwa juu ya maisha ya mwanadamu.
ร Tashihisi pia imetumika katika uk. 38. Neema analalamika kuhusu maradhi yasiyosikia dawa. Anasema, maradhi “yakitaka huzichezea dawa mwajificho. Dawa zikiingilia huku, maradhi hutokezea pale, hali pesa zinakwenda, shughuli zinasimama”. Vitu hivi vitatu: maradhi,pesa na shughuli vinasawiriwa kuwa na uwezo fulani ambapo maradhi yanazidi uwezo wa vyote viwili.
ร Vilevile, tashihisi imetumika katika uk. 39 ambapo Bunju anamwambia Neema kuwa “chumba chenyewe kinajisemea”. Hii ni baada ya Bunju kufika nyumbani kwake na kupendezwa na uzuri wa chumba hicho. Mfano huu una athari ya kusisitiza uzuri wa chumba hicho usiofichika.
ร Mbinu hii pia imetumika katika uk. 56 ambapo Sara anasema kuwa agongo liliyamega maadili” ya Yona kimyakimya na taratibu uwajibikaji wake ukawa umemponyoka. Gongo ni aina ya pombe kali.
ร Mwandishi wa Bembea ya Maisha ameisawiri pombe hii kuwa na uwezo juu ya mwenendo wa maisha ya mtu na kuweza kumdhuru mtu huyo.
ร Vilevile, katika uk. 62, Beni anasema kuwa Yona alikuwa mwalimu mwenye bidii kabla “tembo kunyoosha mikono yake na kumdaka”. Mfano huu, sawa na ule uliotangulia hapo juu, unadhihirisha uwezo mkubwa wa pombe kumteka na kumyumbisha mtu.
Mbinu za kishairi
Mbinu za kishairi ni sehemu muhimu ya matumizi ya lugha katika tungo za kitamthilia. Miongoni mwa mbinu hizo muhimu ni takriri.
Takriri
Takriri ni urudiaji wa sauti, silabi, neno au sentensi za namna moja zinazofuatana kwa karibu. Takriri hupamba lugha katika fasihi na pia kuvuta nadhari ya msomaji au msikilizaji.
Mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ametumia mbinu ya takriri katika kazi yake. Mifano:
& Sara: … Ulikuwa umenila kiasi cha kuniacha chicha. (uk. 2).
& Kiwa: Dunia ya leo haithamini kimo, inathamini akili. Haitaki kututumua misuli, inataka tambo la fikira. (uk. 5).
& Dina: Dunia hii sasa tunaishi katika hofu. Tunahofu hata tusichokifahamu. (uk.
9).
& Dina: Wewe unaona rangi, tena rangi ya mwisho wa kinachoelea. Kabla kielee kimepigwa shoka, kimeonja misumeno ainaaina, kimetambaliwa na randa, kimestahimili makali ya patasi, na kukapaswa na mikwaruzo ya msasa. (uk. 10).
& Sara: Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si magengeni. (uk. 13). Sara: Tena hodari wa misemo na nahau. Wala hawana simile
& kutuloweka kwenye misemo na nahau zao. Hawana simile mwanangu!
& Sara: Tumeyaacha maji ya mbizi na kuingia kwenye maji ya mbuzi. (uk. 20).
& Neerna: Kikijanjaruka hakitakuwa na budi ila kurauka. (uk. 25).
& Neema: Usingepikika, usingelika. (ul<. 41).
& Neema: Mwenyewe huyo analipia kila kitu. Ninakwambia kila kitu! (uk. 41).
& Asna: Ndoa imeyatia doa maisha yako. (uk. 53).
& Sara: Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. (uk. 54).
& Asna: Elimu ni muhimu mama. (uk. 55).
& Sara: Mungu hakupi yote. Akikupa hiki, anakunyima kile.
& Akikupa yote yatakushinda. (uk. 55). Sara: Watu walituona maskini wa watoto.
Maskini wa kizazi. (uk. 55).
& Sara: Wakatulaumu na kutusema bila simile. Bila simile! (uk. 56).
& Yona: Malezi yameachiwa yaya. Nyumba ni ya yaya. (uk. 59).
& (xviii) Yona: Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri, kiboko mkononi…
& Jioni darasani tena, kiboko mkononi. (uk. 62).
& Yona: Nilishindwa kuingia kazini kila siku. Nilishindwa kuishi bila kulewa. (uk.
62).
& Yona: Yabarikiwe mashamba yetu.
& Beni: Ibarikiwe mimea yetu.
& Luka: Vibarikiwe vizazi vyetu. (uk. 64).
& Neema: Kwenye hujuma na kuchimbana, kwenye ugomvi na mivutano, kwenye chuki na uhasama wa kitoto, kwenye tembo na gumzo lisiloisha, penye uchimvi na kusutana (uk.65).
& Sara: Anza polepole. Anza na baba yenu. Badala ya kumkabili, mshawishi.
Atakuelewa. Akikuelewa atauendeleza ujumbe. (uk. 69).
& Yona: Siku zangu za uzeeni lazima nizitumie kumwangalia mke wangu mgonjwa.
Lazima nimshukuru kwa vitendo kwa jinsi alivyojitolea kuijenga familia yetu. Kwaheri pombe. Buriani. (uk. 70).
Ishara na taashira
Ishara katika fasihi hutumiwa kurejelea kitendo, hali au kitu kinachodokeza au kuonyesha dalili ya kitu kingine. Nayo taashira ni alama mahususi ambazo huhusishwa na hali fulani katika jamii.
- Katika 1, Yona analalamika kuwa nyumba haifuki moshi. Kufuka kwa moshi ni ishara ya upishi. Kutokuwepo kwa moshi ni ishara na pia taashira kuwa hakuna kinachopikwa.
- Mwangaza hafifu unaotokana na taa ya sola katika chumba cha Asna mjini ni ishara ya maisha ya Asna. Mwangaza huu hafifu unaashiria kuwa ingawa Asna anaona anaishi maisha mazuri na katika mtaa wa kifahari, mazingira anamoishi si mazuri sana. Uzuri wake ni hafifu. Chumbani humo hamna vitu vya thamani vinavyoendana na maisha ya kifahari. Ishara hii ni kama kejeli kwa maisha anayoishi
- Katika uk. 6, Dina anasema kuwa njia, sawa na moyo wa mwanadamu imejaa Mfano huu unatumia giza kama ishara au taashira ya mambo yasiyojulikana au yasiyoweza kutabirika.
- Katika uk. 61, Luka anaeleza kuwa kijiji kina mwanga kutokana na ufanisi wa watoto wa Katika mfano huu, mwanga umetumiwa kuashiria maendeleo yanayotokana na elimu. Baadhi ya maendeleo hayo ni watoto kupata kazi, kuwajengea wazazi wao nyumba na kununua gari na kuenda nalo kijijini.
- Vilevile, mbinu ya ishara imetumika katika uk. 15 ambapo Dina anapika kwa kuni mbichi zinazomfanya Sara kuondoka nje kwa sababu ya moshi. Kuni mbichi zinaashiria umaskini na hali ngumu ya maisha ya kijijini. Pia, ni ukosefu wa Hali hii inaweza kutofautishwa na mjini ambako watu wanapika kwa kutumia jiko la gesi.
- Ishara pia imetumika pale ambapo tunaelezwa kuwa Salome alipata First Class katika mtihani wake wa Chuo kikuu (uk. 28). First Class imetumika kama ishara ya hekima na bidii masomoni.
- Katika 33, Sara anamwambia Asna kuwa Bunju ashanunua leso yake akavaa mpaka ikazeeka. Leso ni ishara ya zawadi au kirimu kwa mama mkwe. Hivyo basi, Sara anamtaka Asna atafute mume amletee zawadi au amkirimu.
Tabaini
Ni mbinu ya fasihi ambapo jambo husisitizwa kwa kutumia kikanushi ‘si’. Mbinu hii imetumiwa na mwandishi wa Bembea ya Maisha mara kadhaa. Mifano:
ร Asna: …nyumbani pakigeuka kuwa kambi ya jeshi nitafanyaje! Amri si amri, masharti si masharti! Asna anasisitiza hali ya ndoa anayoiona kuwa haifai.
ร Sara: Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si magengeni. Sara anasisitiza kuwa watu waliwasema kila mahali, hata makanisani, mahali pasipofaa kusengenywa mtu.
Tanakuzi
Ni tamathali ya usemi inayolinganua mawazo kwa kutumia mkinzano wa maneno, virai au sentensi kwenye miundo yenye usambamba.
ร Katika uk. 1, Yona anasema kuwa “njaa haileti shibe”. Hapa kuna mkinzano baina ya njaa na shibe.
ร Katika uk. 9, Kiwa anasema kuwa dunia imekuwa ngumu kama “mwanga uletao kivuli”. Mkinzano upo baina ya mwanga na kivuli.
MBINU ZA KIMUUNDO
Mbinu za kimuundo hutumiwa na mwandishi kuendeleza msuko wa kazi ya fasihi. Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu kadhaa za kimuundo kujenga msuko wa tamthilia yenyewe.
Mifano Uzungumzi nafsia
Ni aina ya monolojia itolewayo na mhusika mmoja akiwa jukwaani pekee yake. Mbinu hii hutumiwa kuwasilisha maoni, hisia na fikra za mhusika kuhusu jambo fulani.
ร Mbinu ya uzungumzi nafsia imetumika (uk. 38) ambapo Neema anazungumza pekee yake na kudhihirisha hisia zake kuhusu maradhi yasiyosikia dawa.
Anasema maradhi hayo yanamfukarisha mtu. Mtu huwa hana la kufanya ila kumwomba Mungu amwepushie. Ni wazi kuwa maradhi yana uzito usiostahilimika.
ร Mbinu hii pia imetumika katika (uk. 41) kwenye mazungumzo ya kibinafsi ya Neema. Neema anajisemea kuhusu Bunju. Anasema kuwa Bunju ni zawadi kwake kwa kuwa alimsaidia wakati alipatwa na ajali na kuwachwa katika hali mahututi. Tunamwona pia akikumbuka maneno ya mamake kuhusu Bunju, kuwa Bunju ni mmoja wao. Anakiri kuwa zamani hakuona hivyo kwa kuwa mtazamo wake kuhusu mumewe ulikuwa hasi. Sasa, kwa sababu ameahidiwa kusaidiwa kulipa gharama ya hospitalini ya Sara, mtazamo wake kuhusu Bunju unabadilika na anmuona kama zawadi kwake.
ร Uzungumzi nafsia pia unatokea katika mazungumzo ya Yona (uk. 70). Yona anamhurumia mke wake Sara kwa sababu ya ugonjwa uliodhuru. Anasema awali aliona kuwa ni kama mzaha kuwa mkewe anaugua. Anajilaumu kuwa angejua hangemfanyia madhila mkewe, angemtunza na Silesi za maisha wangezila zijavyo. Tunapata nia na mwelekeo wa Yona kwa kurejelea mazungumzo yake.
Anasema ni lazima awache njia zake za awali za unywaji pombe na kutoshughulikia familia yake.
ร Mkondo anaochukuwa ni kubadilisha tabia na kuahidi kwamba siku zake za uzeeni atazitumia kumwangalia mke wake Sara.
Usemaji-kando
ร Hii ni mbinu ambayo mhusika mmoja anasema maneno kwa hadhira au mhusika mwingine huku wenzake kwenye jukwaa wakijifanya kutosikia anachosema mhusika huyo.
ร Mbinu hii humsaidia msomaji kuelewa nia na kuibua msimamo wa mhusika kuhusu mhusika mwingine, wazo au kitu fulani kinachozungumziwa katika kazi ya fasihi kinyume na anayosema au kufanya akiwa na wahusika wengine.
Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu hii katika kazi yake.
ร Mbinu hii imetumika katika mazungumzo baina ya Bela na Neema (uk. 24). Bela anaposisitiza kumwuliza Neema sababu ya kutowacha Sara alale kwake ili wapige gumzo, Neema anageuka kando na kuuliza kwa nini Bela aendelee kuulizia kuhusu hilo. Ni wazi kuwa Neema hataki kuzungumzia suala hilo lihusulo mila na tamaduni. Ana hisia hasi nalo.
ร Mbinu ya usemaji-kando pia imetumika katika uk. 29-30. Neema anainuka na kuihutubia hadhira. Analalamikia hali ngumu ya maisha yanayokwenda mbio kama gari liendalo kwa kasi. Anashangaa iwapo Bunju anamwelewa kama ilivyokuwa hapo awali kwa kuwa hataki kumsaidia kumlipia mama yake matibabu. Anajiuliza iwapo anaweza kumwacha mamake ateseke kwa sababu ya ugumu wa maisha.
Mbinu rejeshi
ร Mbinu rejeshi ni sehemu katika kazi ya fasihi inayozungumzia matukio katika wakati uliopita. Pia huitwa kiangaza nyuma. Mbinu hii imetumika katika sehemu mbalimbali katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Kimsingi, mbinu hii imetumika kutofautisha maisha ya jana na ya leo, kuendeleza maudhui ya utamaduni na mabadiliko. Dina anaturejesha nyuma kiwakati katika mazungumzo yao na Siwa ambapo anasimulia kuhusu maisha ya awali ya familia ya Yona na Sara (uk. 7). Kupitia mbinu hii, tunapata kuelewa shida ambazo Sara na Yona walipitia, hasa masimango ya watu waliowasema kwa kukosa kupata watoto.
ร Katika (uk. 51) Bunju na Neema wanaturejesha nyuma kwenye ajali iliyompata Neema. Bunju anasema alimpata Neema akiwa mahututi.
ร Neema anakiri kuwa ilikuwa ajali mbaya sana ambayo ilisababisha vifo vingi. Hata hivyo, Neema alinusurika baada ya kupangiwa matibabu na Bunju. Mfano huu unaendeleza sifa ya utu na ukarimu alionao Bunju.
ร Mbinu rejeshi pia imetumika katika uk. 62 kupitia mazungumzo baina ya Beni, Luka na Yona. Hususan, Yona anakumbuka maisha yake ya awali alipokuwa kijana na mwalimu. Yona anaeleza kuwa alikuwa anarauka kwenda shuleni, akiwa na kiboko mkononi na hakupenda wanafunzi kuchelewa kufika shuleni. Vilevile, anakumbuka namna alivyovibeba vitabu kwenye baiskeli yake kwenda kuvisahihisha wikendi. Mfano huu unadhihirisha bidii yake kabla pombe haijamwathiri na kumbadilisha.
ร Mfano mwingine wa mbinu rejeshi umetumika katika uk. 64 ambapo Neema anakumbuka usafiri wa zamani kabla mabadiliko ya kiteknolojia. Anasema kuwa zamani wangechukua siku tatu kupambana na barabara ya vumbi, na mvua
Sadfa
iliponyesha, kulikuwa hakuendeki mpaka barabara ikauke ndipo safari iendelee. Sara anachangia na kusema kuwa mwendo ulikuwa wa kobe na safari ilikuwa ya kuchosha. Mfano huu unaendeleza maudhui ya mabadiliko ya kiteknolojia na mgogoro baina ya jana na leo.
Sadfa katika fasihi ni hali ambapo matukio mawili hutokea kwa wakati mmoja bila kupangwa na kwa namna ya kushangaza au inayoashiria bahati.
Mbinu ya sadfa imetumiwa mara kadhaa katika tamthilia ya Bembeaya Maisha.
ร Kwanza, mbinu ya sadfa imetumiwa katika (uk. 34) ambapo Sara na Asna wanazungumza kuhusu ndoa ya Neema na Bunju wakiwa nyumbani kwa Asna mjini. Ghafla, na bila kutarajiwa, Neema anaingia bila kubisha. Asna anashtuka.
ร Vilevile, katika (uk. 71) Sara anamweleza Neema aende kuandaa kiamshakinywa. Neema anaitikia wito wa mama yake na kusema kuwa ataandaa kiamshakinywa mara moja. Hata hivyo, Yona anawaeleza kuwa alikuwa ameshaandaa tayari. Hii ni sadfa na pia kinyume cha matarajio. Neema anaonyesha kushangazwa na kitendo hicho cha babake.
Taharuki
ร Taharuki ni hali katika kazi ya fasihi inayoibua matarajio au hali ya kutojua kitakachofanyika hatimaye.
ร Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu ya taharuki kuendeleza msuko wa tamthilia yenyewe na kumpa msomaji hamu ya kusoma zaidi kujua kitakachotokea.
Mifano
- Katika onyesho la kwanza sehemu ya kwanza (uk. 1-2), mwandishi anaeleza kuhusu ugonjwa wa Sara. Pia, Asna anaeleza kuwa Sara ataishia
- kumeza vidonge maisha yake yote kwa sababu ya ugonjwa huo. Kisha, mwandishi anaonyesha Sara akisafirishwa mjini na kulazwa katika hospitali ya bei ghali iliyo na huduma bora na wataalamu hodari kuliko hospitali za kijijini. Mwandishi anampa msomaji hamu ya kuendelea kusoma kujua iwapo ugonjwa wa Sara
- Katika uk. 10, Dina anamweleza Kiwa kuhusu namna Yona alivyoanza kulewa kupindukia na kuanza kumpiga mkewe Sara kipigo cha Hali hii ya Yona na Sara pia inamulikwa kupitia kwa mazungumzo ya Asna na mamake Sara. Msomaji anapata hamu ya kutaka kujua iwapo ulevi wa Yona ulipungua au ulifikia kikomo.
- Katika 28, mwandishi anadokeza kuhusu mgogoro baina ya Neema na mumewe Bunju. Bunju anakataa kumsaidia Neema kulipia gharama ya hospitalini kwa ajili ya matibabu ya Sara. Hata hivyo, katika
- 40, Bunju anabadilisha msimamo na kuahidi kusaidia “baadaye”, kisha anaondoka. Msomaji anapata hamu ya kutaka kujua iwapo Bunju alitimiza ahadi hiyo.
- Mfano mwingine wa taharuki unazuliwa na mgogoro baina ya Asna na mamake Sara kuhusu haja ya ndoa (uk. 52-53). Asna anasema kuwa kuolewa ni hiari ya mtu, na kuwa ndoa ni dhuluma. Kwa upande mwingine, Sara anamhimiza Asna kutafuta mchumba aolewe amletee wajukuu na zawadi kutoka kwa mumewe. Msomaji anapata hamu ya kujua iwapo Asna aliishia kuolewa au
WAHUSIKA
Yona
Ni mume wa Sara na pia ni mmoja wa wahusika wakuu. Anatambulika kama mhusika mkuu kwa sababu anahusika na takriban masuala yote yanayojadiliwa katika tamthilia hii. Ni kama kwamba kila kitu katika tamthilia hii kinamhusu.
Sifa zake:
- Mwenye bidii: Alikuwa mwalimu hodari aliyesifika kazini na udumishaji wa nidhamu Aliijali kazi yake na hakusita kufunga vitabu kwenye baiskeli yake ili avisahihishe anapofika nyumbani hata siku za wikendi.
- Mtamaduni: Licha ya kujaliwa na mabinti waliofanikiwa maishani na kuiletea fahari jamii yake, msukumo wa wanajamii wa kumhimiza apate mtoto wa kiume Alikosa furaha kwenyenndoa yake kwa sababu ya kuamini mila na desturi za jamii yake.
- Mwenye rabsha: Yona alipoingilia ulevi wa kupindukia alibadilika kwa njia Alianza kumpiga mkewe hata akazirai na kumwagiliwa maji. Alishindwa kutekeleza wajibu wake kazini na hatimaye akafutwa.
- Mwenye majuto: Mwishoni mwa tamthilia anajirudi na kujisuta kuhusu matatizo aliyoisababishia familia yake na hasa mke wake na kuamua kuacha kunywa
- Mlevi: Yona aliposhinikizwa na wanajamii kuoa na kutafuta mtoto wa kiume aliingilia ulevi wa kiwango cha
- Katili: Yona ni katili na hana utu kwa sababu hata baada ya kumkuta bibi yake akiwa katika hali mbaya ya ugonjwa, anamuuliza kwa nini hajamwandalia Hakusaidia bibi yake katika mapishi.
- Ni msomi: Amesoma hadi Chuo Alikuwa mtu wa kwanza pale kijijini kufuzu kutoka chuoni.
Umuhimu wake
ร Yona anadhihirisha masaibu ya uraibu wa pombe unaoweza kuvuruga maisha ya mtu yeyote pasipo kujali nafasi yake katika jamii. Pia, anadhihirisha kwamba vita dhidi ya uraibu wa pombe vinaweza
ร shindwa ikiwa mikakati bora itatumika. Anadhihirisha ukweli wa methali kuwa muwi huwa mwema.
Sara
Sara ni mke wa Yona. Yeye pia ni mhusika mkuu kwa sababu anahusika na karibu masuala yote ya tamthilia hii. Ndoa yake ilikuwa na changamoto nyingi zikiwemo mahitaji ya kiuchumi, fujo za mumewe ambaye alikuwa akishiriki ulevi na ugonjwa wa moyo uliomkaba.
Sifa zake:
- Mvumilivu: Sara alivumilia mateso ya mume wake ambaye alimlaumu kwa kutopata mtoto wa Mume wake alimtesa kutokana na kosa ambalo kwa hakika halikuwa lake.
- Mpatanishi: Sara ni mpatanishi kwa kuwa alimshauri bintiye amwelewe mume wake ambaye alitii utamaduni uliomfanya asimkubali mkwe wake alale nyumbani kwao. Pia, alimshauri bintiye amshukuru mumewe kwa kumruhusu kutumia hela zake kumtibu yeye aliyekuwa
- Mwenye utu: Sara aliijali ndoa yake na kumpenda mumewe licha ya fujo Alikataa kukaa mjini na binti yake ili kumwepushia mume wake fedheha ya kujifanyia kazi zilizohusishwa na wanawake kama vile kuchota maji kisimani.
- Mwenye hekima: Maneno anayozungumza yana wingi wa hekima na busara. Anamweleza Asna asicheze na akili zake ijapokuwa hakupata elimu
- Mlezi mwema: Anawalea wanawe kwa kuwapa mawaidha ya Anawanasihi kuheshimu ndoa, utamaduni na baba yao.
- Mtamaduni: Neema anatilia maanani tamaduni za jamii yake. Kwanza tunamwona akisema kuwa fimbo hurithiwa na mtoto wa kiume. Tena tunamwona akimtetea bwana yake kuhusiana na suala la kazi za jikoni na kuteka maji kisimani.
- Mwenye uhusiano mwema: Sara alikuwa na uhusiano mwema na Dina. Anapougua, Dina anakuja kumsaidia kwa kuwa walikuwa na uhusiano
- Mwenye msimamo thabiti: Hata baada ya kusutwa na kukejeliwa na wanajamii hakuyumbishwa na maneno yao. Aliwapenda mabinti zake kwa dhati. Hata ingawa anachapwa kichapo cha mbwa na bwana yake, hakutoka nyumbani kwake, alisimama kidete na familia
Umuhimu wake
ร Sara anakuwa kielelezo chema cha wanawake walio katika ndoa zenye misukosuko. Anavumilia na kufaulu kuwalea na kuwasomesha wanawe ingawa mumewe anamdhulumu.
ร Anaendelea kumtii mumewe na kumshauri bintiye amnasihi baba yake dhidi ya ulevi kwa heshima.
Neema
Neema ambaye ni binti wa Yona na Sara ni mhusika mjenzi. Neema ni mke wa Bunju. Wasifu wa Neema unadhihirika kutokana na kauli zake na za watu wengine pamoja na matendo yake. Neema anadhihirisha sifa kadhaa:
- Mwenye bidii: Anadhihirisha mwelekeo wa mtu mwenye bidii tangu alipokuwa Licha ya kwamba wazazi wake walikuwa hawajiwezi, alisoma kwa bidii na kufaulu katika masomo yake hadi Chuo kikuu.
- Mwenye moyo wa kujitolea: Neema aliipenda familia yake hata alipoolewa. Tofauti na wasichana wengine ambao hujitenga baada ya kuolewa, Neema aliendelea kuwa nguzo imara katika familia Alijitolea kumpeleka mama yake hospitali na kugharamia ada iliyohitajika. Pia aliajiri wafanyakazi wa kuwasaidia wazazi wake.
- Mwenye busara: Neema alidhihirisha busara katika ndoa yake kwa kumheshimu mumewe na kushirikiana naye katika malezi ya watoto wao tofauti na baadhi ya wake ambao huvuruga ndoa zao kwa mivutano mambo yanapokuwa
- Mwenye Hakujibizana na Asna dada yake wakati alikuwa akizungumza vibaya kuhusu ndoa yake na Bunju.
- Amekengeuka: Neema amezinduka kwa kujua kwamba kuna tamaduni ambazo hazifai kutiliwa maanani katika kizazi cha leo. Anamwambia Bunju kwamba kumkataza mama yake kulala kwao ni utamaduni uliopitwa na
- Mwenye heshima: Neema anamheshimu baba yake hata baada ya kuwatesa walipokuwa wachanga. Neema anamheshimu bwana yake pia. Anasema amempa heshima yake tangu walipofunga ndoa.
Umuhimu wake
ร Neema anajitokeza kuwa kielelezo chema cha akina mama wenye uwezo wa kiuchumi na kuonyesha kwamba inawezekana kudumisha amani kwenye ndoa bila ya kusababisha ushindani usio na manufaa.
ร Anadhihirisha na kuthibitisha kuwa hata mtoto wa kike anaweza kuwasaidia wazazi wake wanapotatizika hata akiwa kwenye ndoa. Hivyo basi, anasawiriwa kama nguzo muhimu ya kuupinga utamaduni unaomdhalilisha mtoto wa kike na kumtukuza mtoto wa kiume.
Asna
Bintiye Yona wa pili. Ni mdogo wake Neema. Asna ni mhusika msaidizi. Anamsaidia msomaji kuelewa baadhi ya masuala yanayojadiliwa katika tamthilia.
Sifa zake:
- Mwenye misimamo ya kipekee: Asna anasema kwamba si lazima msichana aolewe mara tu aingiapo utu Anaonelea kuwa watu wanastahili kupewa nafasi ya kufanya maamuzi. Anasema taasisi ya ndoa ndiyo taasisi pekee inayotolewa vyeti kabla ya watu kupita mtihani. Anazungumzia hali ya watu
wawili wanaotoa ahadi za maisha kabla ya kufahamu ikiwa jambo wanalojiingiza litafanikiwa au la.
- Mwenye heshima: Hata ingawa msimamo wake kuhusu ndoa ni tofauti na ule wa dadake, bado anamheshimu kama mkubwa wake na kuiheshimu ndoa ya Neema ingawa anajua ina Pia, anawaheshimu na kuwapenda wazazi wake.
- Amekengeuka: Asna anaelewa fika kwamba kuolewa ni kwa hiari ya mtu binafsi ila si kushinikizwa au kulazimishwa na
- Msomi: Asna amesoma na kuhitimu hadi Chuo
- Mwenye chuki: Asna anachukia tabia za Bunju za kujifanya kuwa hana pesa ilhali Anachukia ubahili.
Umuhimu wake
ร Asna anawakilisha vijana ambao hawana azimio la kuolewa. Wao ni sehemu ya jamii na wanastahili kukubalika kama wale wenzao wenye imani kwenye taasisi ya ndoa. Hata hivyo, anavyoeleza Sara, na anavyodhihirisha Neema, vijana hawapaswi kuwa na msimamo mkali kuhusu taasisi ya ndoa kwa sababu changamoto nyingi zilizo katika taasisi ya ndoa zinavumilika kama ilivyo katika taasisi nyingine.
Bunju
Bunju ni mumewe Neema.
Sifa zake:
- Mpenda haki: Bunju anamkubalia mke wake kutumia pesa zake kuishughulikia jamii yake ambayo ina uhitaji mkubwa baada ya Yona kufutwa kazi. Pia, mama mkwe anahitaji kutunzwa kwa hali na mali kutokana na hali yake ya kuugua kwa muda
- Mwenye mapenzi: Bunju anampenda mkewe na wanawe na kutekeleza wajibu wake wa malezi kwa
- Mwenye bidii: Anajitahidi kazini na mara nyingi hata muda wa kustarehe Bidii zake zinamwezesha hata kumnunulia mkewe gari.
- Ni mgumu wa pesa: Anajitokeza kama mwenye msimamo thabiti kuhusu matumizi ya pesa na hivyo kusawiriwa kama mtu mchoyo au
- Mtamaduni: Bunju anashikilia mila na desturi za jamii yake. Anapoziishi kwa kumkataza mama mkwe kulala nyumbani kwao, anaonekana kama mtu mchoyo na asiyejali maslahi ya mama mkwe wake. Mila na desturi zinamtawala na kumfanya asitangamane na mama mkwe hata akiwa amelazwa hospitalini. Hili Sio jambo
Umuhimu wake
ร Bunju anadhihirisha umuhimu wa kushirikiana katika ndoa. Anatoa kielelezo chema cha mume anayemjali mke wake. Ana moyo wa kusaidia.
ร Alimsaidia Neema wakati alipopata ajali na kumlipia gharama zote za matibabu.
Anamsaidia Neema kwa kumruhusu atumie mshahara wake kusaidia wazazi wake. Kwa hiyo, anampatia Neema fursa ya kusaidia jamii yake bila pingamizi. Pia, Bunju anasimamia wanarika ambao bado wanathamini mila na desturi za kwao kwani mwacha mila ni mtumwa.
- Dina
Ni mama wa umri wa makamu na jirani wa Sara na Yona.
Sifa zake:
- Mwenye moyo wa huruma: Sara anapougua, Dina anamsaidia kazi za nyumbani na kumpa moyo kuhusu ugonjwa alionao. Anamsifu Sara kwa bidii aliyonayo iliyomfanya kusomesha watoto wake hadi wakafikia Chuo kikuu licha ya masimango ya wanajamii na mateso ya mumewe.
- Mwenye ujirani mwema: Anapoitwa na Sara amsaidie kupikia bwana yake, anafika nyumbani mwa Sara kumsaidia katika shughuli hiyo.
- Mwenye roho safi: Hana kinyongo chochote kwa watoto au familia ya Anafurahia kufanikiwa kwa watoto wa Sara.
- Mwenye mapenzi ya dhati: Anamsaidia rakifi yake Sara kwa
Umuhimu wake
ร Dina anadhihirisha usemi kwamba “Kidole kimoja hakiui chawa.” Hii ni kutokana na kujitolea kwake kumsaidia Sara kazi za nyumbani anapokuwa anaugua. Ni kielelezo cha urafiki wa dhati na ujirani mwema. Ifahamike kwamba Sara asingeishi vyema na majirani, asingepata mtu wa kumsaidia.
Kiwa
Kijana wa kiume, mtoto wa Dina. Kama majirani wengine anashangazwa na bidii za watoto wa Sara na Yona.
Sifa zake:
- Mwenye heshima: Anamheshimu mama yake na kushirikiana naye licha ya pato dogo Kupitia pato lake dogo, ameweza kubadilisha hali yao ya maisha pale nyumbani na kuinua maisha ya Dina.
- Mwenye roho safi: Anashangazwa na ufanisi wa majirani zake lakini hawaonei
- Mdadisi: Kiwa anamuuliza mama yake maswali mengi kuhusu familia ya
Umuhimu wake
ร Umuhimu wa Kiwa unatokana na mambo mawili; ni kijana anayewajibika na kubadilisha maisha ya mama yake licha ya pato lake dogo. Kupitia kauli zake, anadhihirisha kuwa ufanisi maishani hautegemei jinsia bali bidii ya mtu binafsi.
Luka
Mwanakijiji ambaye ni jirani na rafikiye Yona.
Sifa zake:
- Ana busara: Anakiri kwamba siku hizi watoto wa kike wameacha kutegemea waume zao na kuanza kuwajibikia familia zao
- Mshauri mwema: Anamshauri Beni kuhusiana na masuala ya kitamaduni kwamba zamani tamaduni zilikuwa lakini sasa tamaduni zingine zimepitwa na
Umuhimu wake
Anadhihirisha kwamba hata vijijini mabadiliko ya kimawazo kuhusu mtoto wa kike yameanza kukita mizizi. Anamchora Neema kama “simba wa kike” (uk. 67).
Beni
Mwanakijiji ambaye ni jirani na rafikiye Yona.
Sifa zake:
- Mtamaduni: Anashikilia kuwa mtoto wa kiume ana manufaa kuliko wa Anadai Neema hajali maslahi ya baba yake huku akijua kuwa Neema anamshugulikia mama yake ambaye ni mgonjwa. Hajakengeuka: Beni hajazinduka kwa kuwa hajui tofauti kati ya injinia na fundi wa mitambo.
- Mchochezi: Anadai kuwa Yona anafedheheshwa kwa kuachiwa kazi za Ni kama anaelekezwa na mkewe na wanawe. Ukweli ni kwamba mkewe alisafiri mjini kwa matibabu na kukaa kwa wanawe kwa siku chache tu. Beni anatawaliwa na taasubi ya kiume na si jirani mwema kwa Yona kwa kuwa anachangia kumchanganya akili.
Umuhimu wake
ร Ni hasidi katika jamii. Watu wa aina hii huwachochea wenzao na mwisho kuwatenganisha na wake na familia zao. Yona anapuuza uchochezi wa Beni na kuonyesha kuwa sasa ameanza kupatwa na mwamko mpya.
Bela
Ni mfanyakazi wa nyumbani wa Neema.
Sifa zake:
- Mwenye busara: Anazungumza na mwajiri wake, Neema, kuhusu matatizo anayoyapitia kwenye ndoa yake kwa busara na kumsihi
- Mtu wa kutegemewa: Ni mfanyakazi wa Ana uhusiano mwema na mwajiri wake na anaelewa kazi yake barabara. Anamkumbusha Neema kuhusu
kazi za shule za Lemi kwa maana kuwa, anaelewa jukumu lake la kuwalea watoto wa Neema, anayeonekana kuwa mtu wa kazi nyingi.
- Mlezi Bela analea watoto wa Neema vizuri na kwa bidii.
- Mwenye bidii: Bela anafanya kazi ya kuwalea watoto wa Neema kwa bidii. Pia anasema kuwa mara nyingi yeye hakupatana na watoto wake kwa sababu ya shughuli ya Maneno hayo yanaonyesha alikuwa mwenye bidii hata kabla ya kuanza kufanya kazi kwa Neema.
Umuhimu wake
Anawakilisha wafanyakazi wa kiwango cha chini wanaowajibika, kuheshimu na kuthamini kazi zao.
Lemi
Ni mvulana wa miaka kumi, mwanawe Bunju.
Sifa zake:
- Mtiifu: Lemi anawatii wazazi wake na pia mlezi wake Anatii amri ya mama yake anapoambiwa aende akafue hanchifu.
- Mwenye shukrani: Lemi anamshukuru mama yake Neema wakati alikumbushwa kufua hanchifu yake (uk. 48).
- Mdadisi: Lemi anauliza mama yake maswali kuhusu mama yake na bibi Lemi anauliza mama yake (uk. 30) kwa nini hana raha na maswali mengine mengi. Pia anataka kujua ni kwa nini bibi yake hajakuja kumsalimu.
- Mwenye vipawa: Lemi ana kipawa cha kuimba na kucheza nyimbo kwa miondoko na minenguo (uk. 22).
Umuhimu wake
Lemi anawakilisha watoto wa baadhi ya wazazi ambao hawapati wakati mwingi wa kuingiliana na wazazi wao ambao mara mwingi wako kazini. Anawakilisha watoto ambao hulelewa na yaya.
Wahusika wadogo
Salome na Mina: Wahusika wadogo ambao wanatajwa tu. Hawashiriki moja kwa moja katika masuala ya tamthilia hii. Salome ni mwanawe Yona na Mina ni bintiye Bunju na Neema.
Umuhimu wao
Wanakamilisha idadi ya watoto wa Yona na Bunju mtawalia. Idadi hii ni dhihirisho la usasa ambapo wazazi hawapati watoto wengi kutokana na hali ibuka za kiuchumi na za kijamii. Pia, wanaendeleza malezi ya kisasa ambapo watoto hawaonani na wazazi wao kwa kuwa wanahudhuria masomo ya bweni au nje ya nchi.
Ushauri muhimu kwa mtahiniwa
- Mtahiniwa sharti asome kitabu husika (Bembeaya Maisha) barabara na
- Mwongozo ni kurunzi ya kumulikia njia, kwa hivyo, mtahiniwa sharti aelewe
- Ni muhimu kusoma na kulielewa swali Ni vyema kujiuliza swali lifuatalo: Mtahini anataka habari gani kutokana na swali hili?
- Usitoke nje ya muktadha wa swali na kuandaa habari ambazo hazihusiani na swali
- Ikiwezekana, toa mifano kutoka kwenye tamthilia inayohusiana na jambo unalolifafanua ili kuweka jambo hilo
PIA KUNA
- MWONGOZO WA NGUU ZA JADI
- MWONGOZO WA KIGOGO
- MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA
- MWONGOZO WA CHOZI LA HERI
- MASWALI NA MAJIBU YA MAPAMBAZUKO
- MTIHANI WA SHULE ZA KITAIFA MBALIMBALI
- MITIHANI YA KATI YA MUHULA
- MITIHANI YA MWISHO WA MUHULA
- TINI YA ISIMUJAMII, FASIHI SIMULIZI, SARUFI NA USHAIRI
- MASWALI NA MAJIBU YA CHOZI, KIGOGO NA TUMBO
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย
ย