MATUMIZI YA LUGHA
Kiimbo
- Jinsi sauti inavyopanda na kushuka mtu anapoongea.
- Huibua maana halisi ya maneno yanayosemwa kama ifuatavyo:
- Sentensi za taarifa
- Mtoto anaandika barua.
- Sentensi za maswali
- Mtoto anaandika barua?
- Sentensi za mshangao
- Mtoto anaandika barua!
- Sentensi za amri
- Kachezeeni nje!
- Sentensi za rai/ombi
- Nisaidie/eni.
SEE FREE PDF NOTES HERE; Free Kiswahili notes, revision questions, KCSE past Papers, Exams, Marking Schemes, Topical revision materials, Syllabus and Many more
Zoezi
- Eleza maana ya kiimbo kwa kutoa mifano.
- Tambua sentensi zifuatazo ni za aina gani kutokana na kiimbo.
- Watu wanakula nyoka?
- Watu wanakula nyoka.
- Watu wanakula nyoka.
- Tafadhali nisaidie.
Silabi
- Tamko moja katika neno/herufi moja au zaidi ambazo hutamkwa pamoja.
Miundo Miwili ya Silabi za Kiswahili
- Silabi wazi
- Huishia kwa irabu k.m. o-a, (I) i-ga (KI), mbu-zi (KKI) na u-ngwa (KKKI)
- Silabi funge
- Huishia kwa konsonanti k.m. m-tu (K)
Zoezi
- Ukitoa mifano, fafanua miundo miwili ya silabi za Kiswahili.
- Tenganisha silabi katika maneno yafuatayo:
- inkisari
Shadda/Mkazo
- Mkazo unaowekwa kwenye silabi fulani ya neno ikiwa imetamkwa kwa msisitizo.
- Alama ya ritifaa hutumiwa kutambulisha shadda.
- Huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka ya mwisho, kwenye vitenzi vishirikishi vya silabi moja au kubadilisha maana ya neno.
- ka’lamu, I’mba, thu’mni, ‘leta, n.k.
- Kitabu ‘ki mezani.
- Bara’bara (njia), ba’rabara (sawasawa), wala’kini (lakini), wa’lakini (kasoro/dosari/ila)
Zoezi
- Weka shada katika maneno haya:
- imba
- baba
- Onyesha kwa kupiga mstari iliko shada katika maneno yafuatayo:
- malaika
- nge
Sauti za Kiswahili
- Kuna makundi mawili ya sauti za kiswahili:
- Irabu
- Sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa katika ala za sauti.
- Konsonanti
- Sauti ambazo wakati wa kutamkwa hewa huzuiliwa katika ala za sauti.
- Aina za Ala za Sauti
- Ala tuli
- Ambazo hazisogei mtu akitamka k.m. meno, ufizi, kaa kaa gumu, kaa kaa laini na koo/koromeo.
- Ala sogezi
- Ambazo husogea mtu akitamka k.m. midomo na ulimi.
Matamshi/Uainishaji wa Irabu
- a ni ya katikati na chini kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
- e ni ya mbele na kati kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
- i ni ya mbele na juu kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
- o ni ya nyuma na kati kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
- u ni ya nyuma na juu kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
Zoezi
- Taja makundi mawili ya sauti za Kiswahili.
- Yatofautishe makundi ya sauti za Kiswahili uliyotaja katika (a)
- Toa mifano miwili miwili ya irabu ambazo hutamkwa:
- midomo ikiwa imeviringa
- midomo ikiwa imetandazwa
- Eleza jinsi irabu /e/ inavyotamkwa.
- Taja aina mbili za ala za kutamkia na utoe mfano mfano mmoja mmoja.
Matamshi/Uainishaji wa Konsonanti
MAHALI AINA | MIDOMO | MDOMO MENO | MENO | UFIZI | KAAKAA GUMU | KAAKAA LAINI | KOROMEO |
VIPASUO (H) (GH) | p b | t d |
| k g | |||
VIPASUO (GH) KWAMIZO (H) | ch j | ||||||
NAZALI (GH) (VING’ONG’O) | m | n | ny | ng’ | |||
VIKWAMIZO (H) (VIKWARUZO)(GH) | f v | th dh | s z | sh | gh | h | |
KITAMBAZA | l | ||||||
KIMADENDE | r | ||||||
NUSU IRABU VIYEYUSHO | w | y |
- Huainishwa kulingana na inapotamkiwa, kuwepo au kutokuwepo kwa mtetemeko katika nyuzi za sauti na jinsi hewa inavyozuiliwa katika ala k.m. /p/ ni ya midomo, kipasuo na sighuna.
- Vipasuo
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, huzuiliwa kabisa na kuachiliwa kwa ghafla na mpasuko mdogo kutokea.
- Vikwamizo/Vikwaruzo
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa kukwamizwa.
- Vipasuo kwamizo/kwaruzo
- Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiliwa kabisa halafu mwanya mdogo huachwa hewa ipite kwa kukwamizwa.
- Nazali/Ving’ong’o
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa kuna kiasi cha hewa huachiliwa na kupitia puani
- Kitambaza
- Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa kwa nguvu, kuzuiliwa na kuachiliwa ipite kando ya ulimi
- Kimadende
- Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, kuzuiliwa na kuachiliwa na kusababisha ncha ya ulimi kupigapiga ufizi mfululizo.
- Nusu irabu/Viyeyusho
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa ulaini kama katika utamkaji wa irabu.
Zoezi
- Tambua kikwamizo cha kaakaa laini na kiyeyusho cha midomo.
- Tambua konsonanti ambazo si za orodha hii na ueleze kwa nini: /m/, /n/, /ny/,/ng’/, /f/, /b/
- Tofautisha konsonanti /p/ na /dh/.
- Taja konsonanti mbilimbili ambazo hujulikana kama:
- viyeyusho
- vikwaruzo
Aina za Maneno
Nomino (N)
- Neno linalotaja kiumbe, kitu, hali, mahali, tendo, dhana, n.k.
Aina
- Nomino za Pekee
- Ambazo hutaja kitu kwa kutumia jina lake/ambazo hutambulisha upekee wa kitu hicho.
- Mwanzoni huandikwa kwa herufi kubwa.
- majina ya watu k.m. Kamau
- mahali k.m. Mombasa
- siku k.m. Alhamisi
- miezi k.m. Disemba
- miaka k.m. 1930
- milima k.m. Kilimanjaro
- Mito k.m. Tana
- maziwa k.m. Victoria
- bahari k.m. Hindi
- Mabara k.m. Africa
- Nomono za Kawaida/Jumla
- Majina ya jumla ya viumbe/vitu vinavyoonyesha umbile la jinsi moja k.m. mtu, gari, kalamu, n.k.
- Nomino za Jamii
- Majina ya makundi ya viumbe au vitu k.m. bunge, jamii, halaiki, bunda n.k.
- Nomino za Wingi
- Majina ya vitu vitokeavyo kwa wingi japo kimsingi hazina umoja au wingi k.m. maji, mate, maziwa, mahubiri, marashi, mchanga, ngeu, poda, unga, n.k.
- Nomino za Dhahania
- Majina ya viumbe au mambo ya kudhani/yasiyoweza kugusika k.m. k.m ujinga, werevu, malaika, shetani, amani, imani, roho, wazo, dhana, n.k.
- Nomino za Vitenzi Jina
- Vitenzi vyenye kiambishi awali ku ambavyo huweza pia kutumika kama nomino k.m. Kucheza kwake kunaudhi.
Zoezi
- Sahihisha jedwali lifuatalo
nomino | aina |
Juma kisu maziwa bunda amani kuomba | wingi dhahania pekee kitenzi jina kawaida/jumla wingi |
- Bainisha nomino katika sentensi ifuatayo
- Kuendesha baiskeli kwa kasi kulimfanya Hasani aangushe bunda la noti alilokuwa anaenda kununulia mchanga.
Sentensi ya Kiswahili
- Sentensi ni fungu la maneno linalojitosheleza kimaana linalotumiwa katika mawasiliano.
Sifa
- Huwa na ujumbe uliokamilika.
- Huwa na mpangilio maalum wa maneno.
- Huwa na muundo wa kiima na kiarifu.
Aina
- Sentensi Sahili
- Sentensi rahisi au nyepesi.
Sifa
- Huwa fupi.
- Huwa na kitenzi kimoja pekee.
- Huwasilisha dhana moja.
- Yaweza kuwa ya neno moja au zaidi.
- Yaweza kuwa na kiima kilichododoshwa.
- Watoto wawili wanaelekea uwanjani.
- Gachiku ni msichana mtiifu.
- Sentensi Ambatano
- Inayoundwa kwa kuunganisha sentensi sahili mbili.
Sifa
- Huwa na vishazi huru viwili.
- Huwa na kiunganishi.
- Huwa na vitenzi viwili au zaidi.
- Hutoa zaidi ya wazo moja.
- Yaweza kuwa na viima vilivyododoshwa.
- Mwanafunzi alipita mtihani ingawa hakuwa anasoma kwa bidii.
- Maria aliendelea kupika kwa utaratibu huku akiimba wimbo.
- Sentensi Changamano
- Ambayo huwa na kishazi tegemezi kilichochopekwa ndani.
Sifa
- Huwa na kishazi tegemezi chenye kitenzi kinachovumisha nomino kwa kuirejelea.
- Huwa na kishazi huru kimoja au zaidi.
- Huwa na virejeshi (amba na O) au –enye.
- Tunda alilonunua jana limeoza.
- Mwizi aliiba pesa zilizokuwa kabatini.
Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT)
- Kundi Nomino ni sehemu katika sentensi inayoarifu kuhusu nomino na hutokea mwanzoni mwa sentensi.
- Kundi tenzi ni sehemu katika sentensi inayoarifu kuhusu kitenzi na hutokea mwishoni mwa sentensi.
Virai
- Vikundi vya maneno vitumiwavyo na binadamu visivyo na maana kamili.
- Tungo zinayoundwa kwa maneno aghalabu mawili au zaidi yanayoashiria kitu kimoja na inayojengwa juu ya neno kuu.
Aina
- Kirai Nomino (Kn)
- Kirai Kitenzi
- T
- T+E
- T+N
- T+N+T
- TS+T
- t+N
- t+V+E
- Kirai Kivumishi(Kv)
- V+E
- V+U+V+E
- V+V+U+V+E
- V+N+V+E
- Kirai kielezi (Ke)/Chagizo
- E
- E+E
- E+E+E…
- Kirai Kihusishi (Kh)
- H+N
- H+N+V
- H+N+V+E
Zoezi
Bainisha virai katika sentensi ifuatayo
- Mzazi na watoto wawili werevu sana waliwasili shuleni leo asubuhi kabla ya mwalimu.
Vishazi
- Kundi la maneno lenye kiima na kiarifu likiwa ndani ya sentensi kuu.
Aina
- Vishazi Huru
- Vifungu vya maneno katika sentensi ambavyo hutoa maana kamili.
- Vishazi Tegemezi
- Vifungu vya maneno katika sentensi ambavyo havitoi maana kamili.
Aina
- Vishazi tegemezi vya viunganishi k.m. Alimwadhibu ingawa hakuwa na makosa.
- Vishazi tegemezi vya virejeshi k.m. Polisi walimpata mtoto aliyekuwa amepotea.
- Vishazi Viambatani
- Vinavyoundwa kwa vishazi huru viwili vikiwa vimeunganishwa k.m. Baba analala na mama anapika.
- Vishazi Viambatani
Zoezi
Bainisha Vishazi Katika Sentensi Zifuatazo
- Mwalimu amewasili.
- Amina ambaye ni daktari atakuja.
- Ametajirika japo hakupata elimu.
- Mwalimu anafundisha na wanafunzi wanaandika.
- Tumeanzisha shirika ili tunyanyue hali zetu.
- Unaweza kuamua kunyamaza au kujitetea.
Shamirisho/Yambwa
Aina
- Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa
- Nomino inayoathiriwa na kitenzi.
- Shamirisho Kitondo/Yambwa Tendewa
- Nomino inayotendewa kitendo.
- Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi
- Chombo kinatumiwa kufanyia kitendo fulani.
Mifano
- Mama alimpikia baba chakula kwa sufuria.
- Baba alipikiwa chakula na mama kwa sufuria.
- Sufuria ilitumiwa na mama kumpikia baba chakula.
- Chakula (Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa)
- Baba (Shamirisho Kitondo/Yambwa atendewa)
- Sufuria (Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi)
Ngeli za Nomino
- Makundi ya nomino katika lugha ya Kiswahili yenye sifa zinazofanana kisarufi.
- A-WA
- Huwa na majina ya watu, vilema, viumbe, vyeo na viumbe vya kiroho, n.k.
- Huchukua miundo kama vile M-WA, M-MI, KI-VI, n.k.
- mtu-watu,
- mkulima-wakulima
- mtume-mitume
- mkizi-mikizi
- kiwete-viwete
- kibyongo-vibyongo
- nabii-manabii
- kuku-kuku
- Waziri-Mawaziri
- U-I
- Huwa na majina ya mimea, sehemu za mwili, vifaa, matendo, maumbile, n.k.
- Huchukua muundo wa M-MI.
- Mchungwa-michungwa
- Mkoko-mikoko
- mkono-mikono
- mfupa-mifupa
- msumari-misumari
- mgomo-migomo
- mwendo-myendo
- msukosuko-misukosuko
- mlima-milima
- mwamba-myamba
- U-YA
- Huwa na majina ya hali, matendo, n.k.
- Huchukua muundo wa U-MA.
- Ugonjwa-magonjwa
- upana-mapana
- uasi-maasi
- uchungu-machungu
- ulezi-malezi
- uovu-maovu
- uhusiano-mahusiano
- YA-YA
- Huchukua muundo wa MA-MA.
- Huwa na nomino zipatikanazo kwa wingi.
- Hazibadiliki katika umoja na wingi.
- manukato
- mauti
- maziwa
- marashi
- mahubiri
- majira
- maradhi
- maafa
- mazingira
- KI-VI
- Ni majina ya vifaa, sehemu za mwili, vitu, udogo, lugha, n.k.
- Huchukua miundo KI-VI na CH-VY.
- kisu-visu
- kitabu-vitabu
- chakula-vyakula
- chanda-vyanda
- kijitu-vijitu
- kigombe-vigombe
- kiguu-viguu
- kidovu-vidovu
- LI-YA
- Huwa na majina ya sehemu za mwili, dhana, vifaa, ukubwa, n.k.
- Huchukua muundo wa JI-MA, JI-ME, JA-MA, JE-MA n.k.
- jicho-macho
- jina-majina
- jitu-majitu
- goma-magoma
- jambo-mambo
- janga-majanga
- jembe-majembe
- jeneza-majeneza
- wazo-mawazo
- tunda-matunda
- jua-majua
- ziwa-maziwa
- ua-maua
- I-I
- Huwa na nomino dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
- Hazibadiliki katika umoja na wingi.
- sukari
- amani
- chai
- mvua
- Imani
- chumvi
- subira
- imani
- amani
- furaha
- I-ZI
- Huhusisha nomino dhahania na vitu.
- Hazibadiliki katika umoja na wingi.
- nyumba
- baiskeli
- karatasi
- redio
- meza
- dini
- dawa
- ndizi
- jozi
- U-ZI
- Huchukua miundo W-NY, U-NY, U-F, n.k.
- wayo-nyayo
- wakati-nyakati
- uso-nyuso
- ufa-nyufa
- ufunguo-funguo
- ufagio-fagio
- wembe-nyembe
- uwanja-nyanja
- ujumbe-jumbe
- ukoo-koo
- waraka-nyaraka
- waya-nyaya
- U-U
- Huwa na nomino za dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
- Hazibadiliki kimaumbo.
- Huchukua U au W.
- Ujinga
- Ulafi
- Ulaji
- Werevu
- Unga
- Uji
- Ugali
- udongo
- KU
- Nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi k.m. kuomba kwake kumemsaidia.
- PAKUMU
- Ngeli ya mahali.
- Huwa na nomino moja ‘mahali’.
- PA (mahali karibu au panapodhihirika) k.m. Kitabu kipo pa
- KU (mahali mbali au kusikodhihirika) k.m. Mahali kule ku
- MU (ndani ya) k.m. Mahali mle mna siafu.
Zoezi
- Tunga sentensi ukitumia nomino kutoka katika ngeli ya U-ZI.
- Andika kwa wingi. Makaribisho aliyopewa yalimfurahisha.
- Andika katika ukubwa wingi: Paka mweupe amenaswa mguuni.
- Andika katika wingi wa hali ya udogo: Mtu aliumwa na mbwa.
- Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya LI-YA.
- Tambua ngeli/viwakilishi ngeli vya nomino zifuatazo:
- chakula
- shairi
- mtwana
Uundaji wa maneno
- Nomino kutokana na mzizi wa kitenzi
- danganya-kudanganya, mdanganyifu,udanganyifu
- soma-kusoma, masomo,msomi,usomaji
- unda-kuunda, muundaji,uundaji,muundo
- funika-kufunika, kifuniko, mfunikaji, ufunikaji
- Kitenzi kutokana na mzizi wa nomino
- mlo-kula
- mlevi-kulewa, kulevuka
- mwimbaji-kuimba
- fikra-kufikiri
- malezi-kulea
- fumbo-kufumba, kufumbua
- Nomino kutokana na mzizi wa nomino
- mwimbaji-kuimba, wimbo, uimbaji, kiimbo
- mchezo-kucheza, uchezaji, mchezaji
- ulaghai-kulaghai, mlaghai
- hesabu-kuhesabu,uhesabu
- mdhalimu- kudhulumu, dhuluma, udhalimu
- Nomino kutokana na mzizi wa kivumishi
- -refu-mrefu, urefu, urefushaji
- -baya-mbaya, ubaya
- -zuri-mzuri, uzuri
- -kali-mkali, ukali
- -eupe-mweupe,weupe
- Kivumishi kutokana na mzizi wa nomino
- ujinga -jinga
- werevu -erevu
- mzuri -zuri
- mpumbavu -pumbavu
- mpyoro -pyoro
- Kitenzi kutokana na mzizi wa kivumishi
- haramu-kuharamisha, kuharamika
- halali-kuhalalisha, kuhalalika
- -fupi-kufupisha, kufupika
- bora-kuboresha, kuboreka
- -refu-kurefusha, kurefuka
- sahihi-kusahihisha, kusahihika
- -sikivu-kusikia
- -danganyifu-kudanganya
- Kivumishi kutokana na mzizi wa kitenzi
- dunisha – duni
- Haramisha – haramu
- fupisha -fupi
- sahilisha -sahili
- tukuka -tukufu
- fahamu -fahamivu
- teua -teule
- nyamaza -nyamavu
- ongoka -ongofu
- sahihisha -sahihi
- danganya -danganyifu
- Kitenzi kutokana na kielezi
- haraka-harakisha
- zaidi-zidisha
- bidii-bidiisha
- hima-himiza
Zoezi
- Unda neno ulilopewa katika mabano kutokana na maneno yafuatayo:
- zingatia (kivumishi)
- sahili (kitenzi)
- taliki (nomino)
- Unda nomino kutokana na mizizi ya maneno yafuatayo kisha utunge sentensi.
- -kali
- lia
Vitenzi
- Kitenzi ni neno linaloeleza kuhusu jambo linalofanywa.
Aina za Vitenzi
- Kitenzi halisi
- Kinachofahamisha tendo halisi.
- Hutokea peke yake k.m. Boke anacheza
- Kitenzi kikuu (T)
- Kinachoeleza tendo kuu katika sentensi.
- Hutokea pamoja na kitenzi kisaidizi k.m. Baba anataka kulala.
- Kitenzi Kisaidizi (Ts)
- Kinachosaidia kitenzi kikuu
Maneno yanayoweza kutumiwa kama vitenzi visaidizi
- ngali
- kuwa
- taka
- pasa
- bidi
- huenda
- kuja
- weza
- kwisha
- stahili
- wahi
- maliza
- Vitenzi Sambamba
- Vinavyofuatana moja kwa moja/vinavyotokea kwa mfululizo.
- Hutumika kutoa maelezo kuhusu tendo moja maalum kwa uwazi zaidi.
- Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo.
- Vitenzi Vishirikishi (t)
- Vinavyoshirikisha vitu kihali, kitabia au kimazingira.
Aina
- Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu
- Ambavyo huchukua viambishi.
- Mama alikuwa mgonjwa/jikoni/muuguzi.
- Aisha angali kitandani/mkaidi/ mwanafunzi.
- Vitenzi Vishirikishi Vipunguvu
- Ambavyo havichukui viambishi
kuyakinisha | kukanusha |
ni/niko ndiko yuko li/liko | si/siko siko hayuko hali/haliko |
Viwakilishi (W) na Vivumishi (V)
- Viwakilishi ni viambishi au maneno yanayotumiwa badala ya nomino.
- Vivumishi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu nomino.
VIVUMISHI | VIWAKILISHI | ||||||||||||
Viulizi | Viulizi | ||||||||||||
G Maneno ya kuulizia. G Mizizi ni –pi, -ngapi na gani. ü Amechukua kitabu kipi?(V. kiulizi)
| ü Kipi kimepotea? (W. Kiulizi) ü Amenunuliwa mangapi? ü Gani imefungwa? | ||||||||||||
a-unganifu | a-unganifu | ||||||||||||
G Maneno yanayoundwa kwa viwakilishi ngeli na kiishio a. G Hutoa maana ya umilikaji ü Mtoto wa shangazi amelala. (V. a-unganifu) | ü Wa Juma analia. (W. a-unganifu) ü Cha mlevi huliwa na mgema. | ||||||||||||
Vimilikishi | Vimilikishi | ||||||||||||
G Hutoa maana ya umilikaji. Mizizi
ü Kiatu changu kimepotea. (V. kimilikishi). | ü Usichukue chake. (W. kimilikishi) | ||||||||||||
Sifa | Sifa | ||||||||||||
G Maneno ya kusifu au kueleza jinsi nomino ilivyo k.m. -fupi, -baya, -kali, -dogo, n.k. ü Mti mrefu umeanguka. (V. sifa) | ü Alichukua cheupe. (W. Sifa) | ||||||||||||
Vionyeshi/viashiria | Vionyeshi/viashiria | ||||||||||||
G Maneno ya kuonyesha nomino ilipo. G Huwa za karibu, wastani na mbali k.m. hili, hilo, lile. ü Kiatu hiki kimechafuka. (V. kionyeshi/kiashiria) | Hii ni ya nani? (W. kionyeshi/kiashiria) | ||||||||||||
Viashiria visisitizi | Viashiria visisitizi | ||||||||||||
G Maneno ya kutilia mkazo nomino yakizingatia ilipo. G Huwa ya karibu, wastani na mbali. G Huundwa kwa kutumia kiwakilishi ngeli katika kionyeshi cha kwanza k.m. kiki hiki-vivi-hivi, lili hili-yaya haya, n.k. ü Chumvi ii hii ilimwagika. (V. kisisitizi) | ü Kuku huku ndiko kulinyesha. (W. kisisitizi) | ||||||||||||
Virejeshi | Virejeshi | ||||||||||||
G Hurejelea nomino au kukumbusha kuihusu. G Huwa amba- na -o- rejeshi. ü Mtoto ambaye analala ni wake. ü Watoto wanaolala ni wao. (V. kirejeshi) ü Mnyama ambaye huwindwa ni nguruwe. ü Mnyama awindwaye ni nguruwe. | ü Ambaye aliniibia ninamjua. ü Aliyeniibia ninamjua. ü Ambaye hula nyasi ni ng’ombe. ü Alaye nyasi ni ng’ombe.
| ||||||||||||
Idadi | idadi | ||||||||||||
G Hutaja idadi ya nomino Aina a) Idadi halisi (iliyo dhahiri) k.m. -moja, sita, n.k. b) Idadi ya jumla (isiyo dhahiri) k.m. -chache, -kadha –ingi, n.k. ü Mwalimu mmoja na wanafunzi sita wameenda. (V-idadi halisi) ü Vitabu vichache vimechukuliwa na watoto kadha. (V. idadi ya jumla) | ü Nipe kumi na kimoja. (V. idadi halisi). ü Amechukua machache tu. (V. idadi ya jumla)
| ||||||||||||
Pekee | Pekee | ||||||||||||
G Hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino kwa njia ya pekee. a) –enye (umilikaji) ü Msichana mwenye maringo ni yule. (V. Pekee) b) –enyewe (halisi au kusisitiza) ü Barua yenyewe niliipeleka posta. c) –ote (bila kubakisha) ü Chakula chote kimeliwa. d) -o-ote (bila kubagua) Mtu yeyote anaweza kuugua. e) -ingine (sehemu ya baadhi ya vitu) ü Mikufu mingine imeibwa. f) -ingine-o (mbali na/zaidi ya) ü Nyuzi nyinginezo zilikatika. | ü Mwenye macho haambiwi tazama. (W.pekee) ü Yenyewe yaliiva jana. ü Kiliharibika chote. ü Popote paliposafishwa pamechafuka. ü Ametorokea kwingine. ü Nyingineyo niliweka katika chakula. | ||||||||||||
Nomino/majina | W | ||||||||||||
Þ Nomino/majina ambayo hutumika kama vivumishi ü Mtu mzee hutembea kwa mkongojo. (V. jina/nomino) |
| ||||||||||||
W | Ngeli | ||||||||||||
| Viwakilishi ngeli ambavyo huwakilisha nomino k.m. Liliiva jana-Yaliiva jana. | ||||||||||||
W | Nafsi | ||||||||||||
Þ Maneno au viambishi vinavyotajia nafsi. Aina a) Nafsi huru Þ Maneno ya kutajia nafsi.
ü Yeye ni mtiifu. (W. nafsi huru) b) Nafsi tegemezi/viambata Þ Viambishi ambavyo hutaja nafsi.
ü Walisahau kumwambia. (W. nafsi tegemezi)
|
Vielezi (E)
- Viambishi au maneno yanayoeleza zaidi kuhusu kivumishi, kitenzi au kielezi kingine.
- Yeye ni mweupe sana/ajabu/kwelikweli/kupindukia/pepepe.
- Alikula pole pole sana.
Aina
- Vielezi vya Namna/Jinsi
- Ambavyo hueleza vile jambo lilifanyika.
Aina
- Vielezi namna mfanano
- Vinavyoeleza vile jambo lilifanyika kwa kufananisha na nomino au vivumishi.
- Huchukua viambishi KI na VI.
- Anakula ki
- Tulifanya kazi vi
- Vielezi namna viigizi
- Maneno ambayo kiasili ni vielezi k.m. sana, haraka, ghafla, mno, kabisa, pole, barabara n.k.
- Mwenda pole
- Vielezi namna hali
- Hueleza hali ya tendo.
- Alilelewa kwa shida.
- Alilewa chakari
- Maneno ambayo kiasili ni vielezi k.m. sana, haraka, ghafla, mno, kabisa, pole, barabara n.k.
- Vielezi namna vikariri
- Huelezea vile jambo lilifanyika kwa kurudiwarudiwa
- Alinijibu
- Tembea
- Yeye hufanya kazi yake hivi hivi/ovyo ovyo
- Mbwa alibweka bwe! Bwe! Bwe!
- Vielezi namna ala
- Walimpiga Stephano mawe/kwa mawe.
- Vielezi Namna Viigizi
- Hueleza vile kitendo kilitendeka kwa kutumia tanakali.
- Mbuni alianguka majini chubwi!
- Vielezi vya Idadi/Kiasi
- Maneno ambayo hutaja kitendo kimetendeka mara ngapi.
Aina
- Vielezi vya idadi halisi
- Tulivamiwa mara moja.
- Vielezi vya idadi ya jumla
- Alitoroka mara kadha/nyingi/chache.
- Vielezi vya mahali
- Hutaja mahali kitendo kilitendekea.
Aina
- Vielezi vya mahali vya maneno kamili
- Ndege ilipofika Nairobi, ilitua chini.
- Vielezi vya mahali vya aina ya viambishi
- Ni viambishi po, ko, mo na ni.
- Alipolala palikuwa na siafu.
- Wanacheza uwanja
- Vielezi vya wakati
- Hutaja kitendo kililifanyika wakati gani.
Aina
- Vielezi vya wakati vya maneno kamili
- Rais atawasili kesho/mwaka ujao.
- Kielezi cha wakati cha kiambishi (po ya wakati)
- Nililala nilipofika nyumbani
Viunganishi (U)
- Neno au fungu la maneno la kuunganishia.
Aina
- Vya kujumuisha pamoja
- na
- aidha (pia)
- isitoshe
- kadhalika (pia))
- tena
- mbali na
- fauka ya (zaidi ya)
- Vya kukatiza ili kupambanua
- walakini (lakini)
- bali (lakini)
- ijapokuwa (hata kama)
- ingawa (hata kama)
- Vya kuonyesha kinyume cha mambo
- ilhali
- licha ya
- Kuonyesha masharti
- budi (lazima)
- lazima
- sharti
- ikiwa (kama)
- bidi
- Vya sababu
- kwa
- kwa sababu
- maadamu (kwa kuwa)
- madhali (kwa kuwa)
- kwa vile/maana
- kwa ajili/minajili ya
- mintaarafu (kutokana na)
- Vya kuonyesha Chaguo
- au
- ama
- wala
- Viunganishi vingine na maana zake
- ila (isipokuwa)
- laiti (kama)
- lau (kama)
- mradi (bora)
- angalau (bora zaidi)
- bighairi (bila ya kujali) k.m.Minghairi vitu vilivyo kwenye kabati vinginevyo unaweza kuvichukua.
- seuze/sembuse (kulinganisha ili kuonyesha tofauti)
- labda (pengine)
Vihusishi (H)
- Maneno yanayoonyesha uhusiano.
Aina
- Mahali
- juu ya, miongoni mwa, katika, mpaka, hadi
- Wakati
- kabla ya, baada ya, tangu, hadi, mpaka
- Sababu
- kwa, kwani, kwa sababu, mintaarafu ya
- Ala
- Alimkata kwa
- A-unganifu
- Simu ya rununu inalia.
- Jumba la mikutano limeandaliwa.
- Kiatu cha ngozi hudumu.
- Kikome cha plastiki ni duni.
- Ulinganisho
- Zaidi ya, kuliko, kuzidi, kushinda.
- Kiwango
- Zaidi ya, kati ya, takriban, karibu
- Vya hali
- Mithili ya, kwa niaba ya
Vihisishi (I)
- Maneno yanayotoa hisia za moyoni.
- furaha
- Hoyee! Haleluya! Alhamdulilahi!
- hasira
- Kefle! Ah! He!
- majuto
- Kumbe! Jamani! Ole wangu! Laiti
- huzuni/huruma
- Pole! Ole! Maskini!
- kuitikia
- Bee! Labela! Naam! Ehee! Ahaa!
- mshangao/mshtuko
- Eti! Salaale! Ajabu! Msalia mtume! Lahaula!
- kubeza
- Mawe! Ngo! Mmm! Mwangalie!
- kusisitiza
- Hata
- kutakia heri
- inshallah
Mwingiliano wa Maneno
- Hali ya maneno kuwa na matumizi tofauti mifano:
- W kuwa V
- Huyu
- Mtoto huyu
- V kuwa W
- Vikombe vizuri vitavunjika.
- Vizuri
- V kuwa N
- Mti mrefu
- Mrefu alikufa jana jioni.
- V kuwa E
- Viatu vibaya
- Uliifanya kazi
- Mtu mjinga ni huyu.
- Anaongea
- N kuwa V
- V kuwa E
- Tajiri alimdharau Razaro.
- Mtu tajiri
- N kuwa E
- Nairobi ni mji mkuu.
- Amewasili
- Kitoto
- Unaongea
- Haraka haina baraka.
- Fanya haraka tuondoke hapa.
- Sindano ya babu imepotea
- Alidungwa sindano/kwa sindano na daktari.
- E kuwa N
- Niliwasili jana.
- Jana yangu haikuwa nzuri.
- T kuwa N
- Nataka kulala
- Kulala kwake kunaudhi.
- N kuwa U
- Ila yake imemwathiri sana.
- Watu wote ila yeye walikwenda.
- Kichwa changu kina walakini.
- Nimekula walakini
- E kuwa I
- Mwenda pole
- Pole! Usijali utapona.
- Amepaka rangi sawasawa.
- Sawasawa! Siku moja tutakutana.
- H kuwa E
- Paka amepanda juu ya mti.
- Ameingia katika choo.
- T kuwa E
- Mtoto akilia
- Aliingia akilia.
- N kuwa I
- Gege anacheza ala yake ya muziki.
- Ala! Waniwekea uchafu katika chakula?
Mofimu
- Kipashio kidogo zaidi katika lugha kisichoweza kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana yake.
Aina
- Mofimu huru
- Neno lisiloweza kugawanywa katika vipande mbalimbali na linalojisimamia na kuwa na maana kamili.
- Kuku, baba, mama, sana, labda, jana n.k.
- Mofimu tegemezi
- Isiyoweza kujisimamia na kujitosheleza kisarufi, mifano:
- Mzizi (Sehemu ya neno inayobeba maana kuu na isiyoweza kubadilishwa)
- m–tu, samahe-k-a, n.k.
- Nafsi
- Tumesahau
- Ngeli
- Li
- Ya
- Kikanushi
- Sikumpiga
- Ha
- Hu
- Njeo/wakati
- Lili
- Ana
- Tuta
- Alipo
- Hali
- Me, nge, ngali, hu, ki, ka, n.k.
- Mahali
- Alipo
- Aliko
- Alimo
- Virejeshi
- Lililo
- Aliji
- Mtendwa/watendwa/kitendwa/vitendwa/shamirisho
- Virejeshi
- Alichiki
- Kilichowa
- Mnyambuliko/kauli
- Alimpigi
- Alimlilia
- Alinikose
- Alimtole
- Kiishio
- a, e, i, u
Viambishi
- Viungo vyenye maana vinavyofungamanishwa na mziziwa neno ili kulipa maana mbalimbali.
Aina
- Viambishi Awali
- Ambavyo hutokea kabla ya mzizi.
- A-li-ye-ku-kata-a
- Viambishi Tamati
- Ambavyo hutokea baada ya mzizi k.m. ki-pig-ishw-a-cho
Mnyambuliko wa Vitenzi
- Kunyambua kitenzi ni kukiongeza viambishi tamati ili kukipa maana tofauti.
Aina za minyambuliko/kauli za vitenzi
- Kutenda
- Hali ya kawaida ya kitenzi.
- Kutendatenda
- Hali ya kitenzi kurudiwa.
- Kutendea
- Kwa niaba ya
- Badala ya
- Sababu
- Kuonyesha kitumizi
- Mwendo wa kitu kuelekea kingine
- Kutendwa
- Huonyesha nomino iliyoathiriwa na kitenzi.
- Kutendewa
- Humaanisha kitendo kimetendwa na mtu badala au kwa niaba ya mtu mwingine.
- Kutendana
- Unamtenda mtu jambo naye anakutenda jambo lilo hilo.
- Kutendeana
- Kutendana
- Unamtendea mtu jambo naye anakutendea jambo lilo hilo.
- Kutendeka
- Uwezekano wa kitendo kufanyika
- Kutendesha
- Mtu au kitu kusababisha kufanyika kwa kitendo.
- Kutendeshea
- Kutendeka
- Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mwingine.
- Kutendeshwa
- Kusababishwa kufanya jambo.
- Kutendeshewa
- Mtu kusababishwa kitendo kitendeke kwa niaba yake.
- Kutendeshana
- Kusababisha kitendo kitendeke kwa mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwako.
- Kutendesheana
- Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwa niaba yako.
- Kutendesheka
- Kitendo fulani kinaweza kusaababishwa.
- Kutendama
- Kuwa katika hali fulani bila ya mabadiliko.
- lala-lalama
- ficha-fichama
- shika-shikama
- ganda-gandama
- chuta-chutama
- funga-fungama
- kwaa-kwama
- unga-ungama
- andaa-andama
- saki-sakama
- Kutendata
- Hali ya mgusano au kushikanisha vitu viwili.
- paka-pakata
- fumba-fumbata
- kokoa-kokota
- okoa-okota
- kama-kamata
- Kutendua
- Hali ya kiyume
- choma-chomoa
- funga-fungua
- Kutenduka
- Kuweza kufanyika kwa hali ya kinyume.
- Kutenduka
- chomoka
- funguka
Vinyume vya vitenzi
- komea-komoa
- bariki-laani
- patana-kosana
- angika-angua
- mwaga-zoa
- ziba-zibua
- tatiza-tatua
- funika-funua
- tega-tegua
- tawanya-kusanya
- ugua-pona
- nasa-nasua
- kwamiza-kwamua
- kosa-kosoa
- pakia-pakua
- twika-tua
- paa-tua
- cheka-lia
- anika-anua
- simama-keti
- fukia-fukua
- inama-inuka
- funga-fungua
- furahi-huzunika
- kumbuka-sahau
- oa-taliki
- choka-pumzika
- uliza- jibu
- jenga-bomoa
- ishi-kufa/hama
- kufa-kufufuka/ishi
- lewa-levuka
- anza-maliza/isha
- saza/bakiza-maliza
- meza-tapika/tema
- ingia-toka
- dharau-heshimu
- kweya-teremka
- panda-shuka
- sifu-kashifu
- chimba-fukia
- chafua-safisha
- cheka-lia
- panda-shuka
- babaika-tulia
- pokea-aga
- zama-elea
- vaa-vua
kitenzi | tendea | tendwa | tendewa | tendana | tendeka | tendeana | tendesha | tendeshea | tendesheka |
cha ü ogopa | chia | chwa | chiwa | chiana | chika | chiana | chisha | chishia | chishika |
cha ü pambazuka | chea | 0 | chewa | 0 | 0 | 0 | chesha | cheshea | chesheka |
chwa ü jua kuanza kutua | chwea | 0 | chwewa | chweka | 0 | 0 | chwesha | chweshea | chwesheka |
fa ü tokwa na uhai | fia | 0 | fiwa | fika | 0 | fiana | fisha | fishia | fishika |
gwa ü anguka | gwia | 0 | gwiwa | 0 | 0 | gwiana | gwisha | gwishia | gwishika |
ja ü sogea karibu | jia | 0 | jiwa | jika | 0 | jiana | jisha | jishia | jishika |
la ü tia chakula kinywani na kumeza | lia | liwa | liwa | lika | lana | liana | lisha | lishia | lishika |
nya ü enda haja kubwa ü anguka matone | nyea | nyewa | nyewa | nyeka | 0 | nyeana | nyesha | nyeshea | nyesheka |
nywa ü tia kitu majimaji kinywani na kukimeza | nywea | nywewa | nywewa | nyweka | 0 | nyweana | nywesha | nyweshea | nywesheka |
pa ü kabidhi | pea | 0 | pewa | peka | pana | peana | pesha | peshea | pesheka |
pwa ü maji toka ufuoni hadi mbali ya bahari | pwea | 0 | pwewa | pweka | 0 | 0 | pwesha | pweshea | pwesheka |
ta ü taga | tia | o | tiwa | tika | 0 | 0 | tisha | tishia | tishika |
wa ü tokea | wia | 0 | wiwa | wika | wana | wiana | wisha | wishia | wishika |
Matumizi ya Maneno na Viambishi Maalum
Maneno Maalum
- ila
- isipokuwa
- Watu wote ila yeye wameenda.
- kasoro
- Hakuna kizuri kisicho na ila.
- labda (pengine/shaka)
- Haonekani siku hizi labda amepata uhamisho.
- ikiwa
- (kama/shaka)
- Tutamkuta nyumbani ikiwa amepewa likizo.
- masharti
- Mgonjwa atapona ikiwa atakunywa dawa ipasavyo.
- walakini
- dosari
- Ghorofa limebomolewa kwa sababu lilikuwa na walakini.
- lakini/bali
- Nimekula walakini
- ingawa/ingawaje (hata kama)
- Nilijilaza kitandani ingawa sikuwa na usingizi.
- ijapokuwa/japo (hata kama)
- Usicheze na nyoka ijapokuwa ni mdogo.
- jinsi
- njia/utaratibu wa kufanyia jambo
- Sijui jinsi ugali unavyopikwa.
- aina/namna/sampuli
- Siwezi kula chakula jinsi
- kulingana na/kama
- Alikuja jinsi
- kwa
- jinsi
- walakini
- mahali
- Ameenda kwa
- jinsi
- Alisoma kwa
- sehemu ya kitu kisima/akisami
- Amepata alama moja kwa tano katika mtihani.
- pamoja na
- Harusi ilihudhuliwa na wazee kwa vijana na tulikula wali kwa
- kuonyesha kitu kilitumiwa kama kifaa
- Alikata mkate kwa
- sababu
- Aliugua kwa kunywa maji machafu.
- kuunganisha vipashio viwili
- Leo ndiwe utapika kwa hivyo tayarisha viazi.
- muda/kipindi
- Alilia kwa nusu sana.
- kufanya jambo bila kupoteza wakati
- Baada ya kula, tulienda moja kwa moja kulala.
- kivumishi cha a-unganifu cha ngeli ya KU
- Kucheka kwa Maria kunaudhi.
- umiliki wa mahali
- Twende nyumbani kwangu.
- na
- kiunganishi
- Mama na baba wanalima.
- umilikaji
- Kamau ana kitabu kizuri.
- wakati uliopo
- Anaandika barua.
- kauli/mnyambuliko
- Kamau na Juma wanapigana.
- kuonyesha tofauti
- Kiatu hiki ni tofauti na
- mtenzi
- Alipigwa na
- kuonyesha ufupisho wa nafsi
- Alisaidiwa nao.
Zoezi
- Eleza matumizi ya na katika sentensi zifuatazo:
- Baba na mama wanapigana kwani ana tabia ya kulewa.
- Mtoto aliteswa na mama yake kwa kuwa tofauti na wengine nami kikamkanya.
- wala (kukanusha)
- Sikumtusi wala
Viambishi Maalum
- me/ja (hali timilifu/kitendo kutendeka na si muda mrefu uliopia)
- Mama ame
- Mama haja
- hu
- mazoea/jambo hutokea kila wakati
- Yeye hulala mapema.
- kikanushi
- Hukutibiwa vizuri.
- li
- wakati uliopita
- Alitupatia zawadi.
- ngeli
- Tunda li
- kitenzi kishirikishi kipungufu
- Jembe li
- ni
- nafsi ya kwanza umoja
- Niliwasili jana.
- mahali
- Twende kanisani.
- kitenzi kishirikishi kipungufu
- Yeye ni
- wingi
- Tokeni
- ndi- (kitenzi kishirikishi kipungufu)
- Yeye ndiye aliniibia pesa.
- ji
- udogo
- Kijitu kimeanguka.
- ukubwa
- Jibwa limebweka.
- kirejeshi
- Alijipalia makaa.
- nafsi ya pili
- Jichukulie upendacho.
- kiambishi tamati cha kuunda nomino.
- Mwimbaji
- Ki
- kitendo ki katika hali ya kuendelea
- Tulikuwa tukila alipoingia.
- masharti/kitendo kinategemea kingine
- Utapita mtihani uki
- udogo
- Kitoto kinalia.
- ngeli
- Kitabu ki
- kitenzi kishirikishi kipungufu
- chakula ki
- kielezi namna mfanano.
- Yeye hula ki
- kitendo hakifanyiki kamwe
- Chai hii hainyweki.
- ku
- kikanushi cha wakati uliopita
- Hakumpiga kwa jiwe.
- nafsi ya pili umoja.
- Alikupigia simu jana.
- mahali
- Huku ku
- ngeli
- Kuugua ku
- mwanzo wa kitenzi
- Ameenda kusafisha nyumba.
- ka
- mfuatano wa matukio
- Tulikula chakula, tukanywa chai kisha tuka
- vichwa vya habari
- Mwizi kapigwa mawe
- kutoa amri
- Kachezeeni nje!
- kitendo fulani ni tokeo la kingine
- Tulisoma kwa bidii tukapita mtihani.
- kutoa nasaha/shauri
- Kamwombe babako msamaha.
- a
- Hali isiyodhihirika ya wakati uliopo
- Watoto wacheza uwanjani.
- vichwa vya habari
- Waziri aaibishwa na wananchi.
- kitendo kinaendelea
- Twaenda sokoni.
- nafsi ya tatu umoja
- Yeye aliudhika sana.
- ngeli
- Mbuzi yule atachinjwa kesho.
- kiishio
- Mtoto amekula
- nge/ngali (masharti yanayowezekana au yasiyowezekana)
- Ningekuwa na pesa, ningenunua kiatu.
- Laiti ningalijua nisingaliingia katika hilo basi.
- po
- wakati
- maalum
- Yeye anapolala hukoroma.
- Wowote/mazoea
- Mwalimu aingiapo wanafunzi husimama.
- mahali
- Paliposafishwa pamechafuka.
- masharti
- Mtoto aamkapo, mpe uji.
- kikanushi cha ki ya masharti
- -asipokula.
Viakifishi
- Alama za usemi(“”)
- Usemi halisi
- “Njoo kesho,” mama akamwambia.
- Lugha ngeni
- “Ninunulie jarida la ‘Parents’”, babake akamwambia.
- Vipindi, filamu, makala
- “Vioja Mahakamani”
- Semi
- “kumwaga zigo”
- Dukuduku (…)
- maneno yameachwa ya kutangulia, kati au ya mwisho. Yaweza kuachwa kwa kuwa makali
- Nyani haoni…
- kukatizwa usemi/kauli
AMINA: Mama ni…
MAMA: Kwanza watoka wapi usiku huu?
- maneno yanaendelea
- Alimwambia ajihadhari anapovuka barabara…
- Koma/mkato/kipumuo( , )
- pumziko fupi katika senyensi
- Tulipofika sokoni, tulinunua mboga.
- kuorodhesha
- Alinunua mboga, samaki, nyanya na viazi.
- kuonyesha mwanzo au mwisho wa usemi halisi
- “Njoo kesho,”mama akamwambia.
- kuandika anwani
- Shule ya upili Gatwe, S.L.P 160, Kerugoya.
- baada ya kutaja jina la mtu anayepewa habari
- Daktari, ningependa kukuona.
- kutenganisha sentensi zenye masharti
- Usipofanya kazi, usile.
- kuandika tarehe
- Alizaliwa mwezi wa Julai, tarehe 18, 1999.
- kuandika tarakimu zinazozidi elfu
- 1,000, 13,000, n.k.
- Ritifaa/kibainishi( ’ )
- herufi imeachwa
- wal’otutuma
- shadda/mkazo
- `iba, ka`lamu
- katika sauti ya king’ong’o
- Ng`ombe amekufa.
- Kufupisha
- Tu’shasafisha nguo.
- katika kuandika miaka yenye namba izilizoachwa
- `73-`99.
- Mshazari/mkwaju(/)
- Tarehe
- Alizaliwa tarehe 5/6/1998.
- kuonyesha kumbukumbu
- KUMB 1/2009
- kuonyesha visawe
- Nenda katika shule/skuli.
- Kuonyesha au
- Wanawake/wanaume wataajiriwa.
- Kistari kifupi( – )
- kuandika tarehe
- 5/6/2006
- kuonyesha silabi, viambishi au mofimu
- sa-la-mu na imb-a.
- kuonyesha neno linaendelea katika mstari unaofuata.
- Usitenganishe sauti za silabi.
- Kuonyesha mzizi wa neno
- -ma,-bwa
- kuonyesha kudumishwa kwa sauti
- Lo-o-o-o!
- Hadi/ kipindi cha tukio fulani
- 1999-2008.
- Kutenganisha usemi na msemaji
- Huo ni upumbavu-Kibaki
- Kistari kirefu( )
- kutenganisha usemi na msemaji
- kuonyesha mabadiliko ya ghafla
- Wanafaunzi ni wajinga-samahani, simaanishi wote.
- kutangulia maelezo ya ziada
- Walisaidia nchi za Afrika Mashariki- Kenya, Uganda na Tanzania kwa msaada
- Mstari( )
- kusisitiza
- Jibu maswali mawili
- kuonyesha aina za maneno
- Mtoto wangu analala (V. kimilikishi).
- kuonyesha vitabu, majarida na magazeti
- Chemchemi za Kiswahili, “True Love”, n.k.
- kuandika anwani/kichwa
- Mwanafunzi Adhibiwa/Kaadhibiwa Vikali
- Kikomo/kitone/nukta (.)
- mwishoni mwa sentensi.
- kuandika tarehe
- 3.2013
- kuonyesha ufupisho wa maneno
- ,Bw.,Bi.,C.C.M
- kuonyesha takwimu
- 5, 86.27, n.k.
- kutenga shilingi na senti
- 50-shilingi sita na senti hamsini
- juu ya herufi j na I
- Nusu/semi koloni/nukta na kituo (:)
- kugawa sentensi mbili zinazoweza kujisimamia bila ya viunganishi
- Wasichana walifuata maagizo waliyopewa; wafulana waliyagomea.
- kama kipumziko katika sentensi ndefu
- Alipochunguza ile hati aliyokabidhiwa na wale wafanya biashara aliona kuwa si nzuri; akaamua kujitenga nayo.
- Vifungo/mabano/paradesi( )
- kuzingira nambari au herufi katika orodha
- (i),(a)
- kuonyesha maelezo ya vitendo vya msemaji katika mazungumzo, mahojiano au tamthilia
- MAMA :( ) Hebu njoo haraka.
- kutoa maelezo zaidi
- Ema (kifungua mimba changu) chaja leo kutoka marekani.
- kuonyesha visawe
- Mamba (ngwena) huliwa.
- Herufi kubwa(H)
- mwanzoni mwa sentensi.
- kuandika anwani
- L.P 1000, Bura.
- mwanzoni mwa usemi halisi
- “Twendeni zetu,” akatwambia.
- baada ya kiulizi (?) na hisi (!)
- Lo! Ulienda? Hebu niambie yaliyojiri.
- mwanzoni mwa nomino za pekee
- Musa
- ufupisho wa maneno
- C.M (Chama cha Mapinduzi)
- mwanzoni mwa majina ya vitabu, majarida, magazeti, vipindi, filamu, n.k.
- kuandika sifa inayotokana na jina la pekee
- Kiganda, Kikristu.
- Koloni/ Nukta mbili ( : )
- kuorodhesha
- Ukitaka kuandaa samosa, unahitaji vitu hivi: unga, nyama, chumvi, mafuta na kitunguu
- kutangulia usemi halisi
- Alimwangalia kisha akamtupia: “mshenzi.”
- kuandika mazungumo, mahojiano au tamthilia
- MAMA :( Akiinuka.) Umechelewa wapi?
- kutenganisha dakika na sekunde
- 25:05
- kutangulia maelezo fulani
- Alipofungua mlango alishtuka: mizoga ya punda ilikuwa imetapakaa nje.
- Hisi/mshangao (!)
- kuamrisha
- Kachezeeni nje!
- Kamau! Unafanya nini?
- baada ya vihisishi
- Masalaale! Pesa zangu zote zimeibwa.
- baada ya sentensi iliyo mshangao
- Gari langu limeibwa!
- kusisitiza
- Kesho msichelewe kuwasili shuleni!
- kudharau/kubeza
- Mwangalie! Kichwa kama jiwe.
- baada ya tanakali
- Mate yalimdondoka ndo! Ndo! Ndo!
- Kiulizo (?)
- mwishoni mwa sentensi iliyo swali
- mwishoni mwa methali zenye muudo wa swali
- Pilipili usiyoila yakuwashiani?
- kuonyesha shaka
- Kenyatta alizaliwa mwaka wa 1945(?)
- kuonyesha mwaka wa kuchapishwa kwa kitabu haujulikani
- Mlacha J (?) Tujijue Ipasavyo
- Herufi nzito (h)
- kusisitiza
- Jibu maswali manne
- kuonyesha wakati/njeo au hali
- Nilicheza,Nimelima
- kuonyesha umoja na wingi
- mtoto-watoto
- kuonyesha aina ya neno katika sentensi
- Mtoto wake amelala (kivumishi)
- Herufi za mlazo/italiki(h)
- kuonyesha aina ya kiambishi au mofimu
- Ki-li-cho-ib-w-a (kirejeshi).
- kusisitiza
- Jibu maswali mawili.
- kuonyesha jina la kitabu
- Nyota ya Rehema
- kuonyesha maneno ya kigeni
- Napenda
- kuonyesha maelezo ya vitendo vya mhusika katika mazungumzo, mahojiano na tamthilia
- AMINA: (Akiinuka) Mama ameenda kwa Farashuu.
- Kinyota(*)
- kuonyesha neno limeendelezwa vibaya
- *kitaabu
- kuonyesha sentensi haina mpangilio sahihi wa maneno
- *Kisu cha hiki ni nani?
- kuonyesha tanbihi (maelezo ya neno yanapatikana chini mwa ukurasa)
- idhibati*
- kuonyesha sentensi ina makosa kisarufi
- *Kuku hii ni ya nani?
Usemi Halisi
- Maneno halisi kama yanavyotamkwa na msemaji.
- Huandikwa bila kugeuza chochote.
- Huanzia kwa herufi kubwa.
- Hunukuliwa kwa alama za usemi ambazo huandikwa zikiwa mbili mbili na moja moja katika dondoo ndogo k.m. “Mwambie ‘ugua pole’ ukimuona,” baba aliniambia.
- Koma hutumiwa mwanzoni au mwishoni mwake.
- Msemaji mpya anapoanza kusema, unapaswa kufungua aya mpya k.m.
Alimuuliza, “Huendi kwa nini?”
“Sikupewa ruhusa,” alijibu Zahara.
- Baada ya (?) na (!) na (.) maneno huanzia kwa herufi kubwa k.m. Lo! Unatoka wapi saa hii? Aliniuliza.
Usemi wa Taarifa
- Ripoti kuhusu mambo yaliyosemwa na mtu mwingine.
- Si lazima maneno yatokee yalivyosemwa. Yanaweza kubadilishwa mradi ujumbe ubakie ule ule.
- Alama za mtajo, kiulizi na hisi hazitumiki.
- Maneno “kwamba’ na ‘kuwa’ hutumiwa.
- Baadhi ya maneno na viambishi hubadilika k.m.
usemi halisi | usemi wa taarifa |
-angu -etu -enu -ako wiki ijayo kesho leo sasa huyu hii ta/ki ni na jana Lo! ?
| -ake -ao -ao -ake wiki iliyofuata siku iliyofuata siku hiyo wakati huo huyo hiyo nge a li siku iliyotangulia alishangaa alitaka kujua |
VITATE T/D
Tata
- hali ya kutoeleweka
- sentensi hii ni
- fundo katika uzi
- uzi umeingia tata/umetata.
Dada
- ndugu wa kike
Tua
- shuka kutoka angani
- ndege ilitua
- weka chini k.v. mzigo
Dua
- maombi kwa Mungu
- omba dua
- piga dua –apiza/laani
Toa
- ondoa kitu ndani ya kinginea
- kinyume cha jumlisha
Doa
- alama yenye rangi tofauti na mwili wa kitu
- dosari/ila/walakini
Ndoa
- arusi/makubaliano rasmi ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mke na mume/chuo
Tundu
- uwazi mdogo wa mviringo kwenye kitu k.v. sindano
- kitu maalum cha kuwekea ndege kilichotengenezwa kwa mabati, matete n.k.
Dundu
- mdudu anayebeba uchafu
- rundo la vitu /mtumba
Tuma
- peleka kitu k.v. barua kwa njia ya posta
- agiza mtu kufanya jambo
Duma
- mnyama mkubwa mwenye umbo kama la paka
- kamata, hasa katika vita
K/G
Kuku
- aina ya ndege anayefugwa nyumbani
Gugu
- mmea unaoota mahali usipotakiwa
- mmea wa mwituni mfano wa unyasi
Kuni
- vipande vya mti vya kukokea moto
Guni
- shairi la arudhi lililokosa kutosheleza kanuni moja au zaidi ya uandishi
Kuna
- kwaruza kwa kucha /kitu chenye menomeno
Guna
- toa sauti ya kuonyesha kukataa, kutoridhika, au kuchukia jambo.
Kenge
- mnyama kama mjusi mdogo
Genge
- kundi la watu
- pango/shimo
Kesi
- daawa/mashtaka yanayosikilizwa mahakamani
Gesi
- hewa inayotumiwa kupikia au kutiwa katika vinywaji
- hewa ambayo haigeuki na kuwa majimaji katika joto la kawaida
CH/J
Changa
- toa kitu ili kukusanya kwa kusudi fulani
- siokomaa
- chanja/pasua vipande vipande vidogo vidogo k.v. kuni
Janga
- hatari/balaa
Chema
- kizuri
Jema
- zuri
Chini
- kwenye ardhi/sakafu
Jini
- shetani/ mtu muovu
Choka
- pungukiwa na nguvu baada ya kufanya kazi
Joka
- nyoka mkubwa sana
Chungu
- chombo kinachofinyangwa cha kupikia
- kinyume cha tamu
- idadi kubwa (chungu nzima)
- mdudu mdogo wa jamii ya siafu
Chambo
- kinachowekwa kwenye mtego kunasia wanyama,samaki n.k.
Jambo
- habari,tukio shughuli
Kucha
- elekea asubuhi
- ogopa
Kuja
- hali ya kusogea karibu
Chuma
- pata mali
- madini magumu yanayotumiwa kujengea na kuundia vitu
- tungua matunda au maua kutoka mtini
Juma
- wiki
- jina la mtu
Chenga
- hepa kwa hila
- mchele uliovunjikavunjika(mchele wa chenga)
Jenga
- aka nyumba
- fanya madhubuti/imarisha
Mchi
- mti wa kupondea kwenye kinu
Mji
- makazi ya watu wengi kulikojengwa nyumba nyingi
- mahali kaburini anapowekwa mauti
- sehemu ya kati ya chupa ya mwanamke mja mzito inayounganisha mtoto na mwili wa mama
Kichana
- kitu cha kuchania nywele
Kijana
- mtu wa makamo mwenye nguvu/mtoto wa kiume kabla ya kubaleghe
F/V
Faa
- kusaidia
- kuwa vizuri
Vaa
- eneza kitu katika mwili ili kufunika sehemu fulani
Fua
- safisha nguo
- tengeneza kitu kutokana na madini
- toa maji katika chombo
- fua maji
- Hakufua (hakufaulu)
Vua
- pata samaki kwa kutumia wavu, mshipi, ndoana n.k.
- ondoa nguo mwilini
- nusuru, okoa, ponya
- vua macho (tazama)
Fika
- wasili mahali
- bila shaka/kabisa
Vika
- valisha
Fuka
- toa moshi bila kuwaka
- uji wowote mwepesi (uji fuka)
Vuka
- enda upande wa pili
Fuma
- piga kwa mkuki
- ona kwa ghafla bila kutazamia mtu anayetenda jambo ovu
- tengeneza kitu kwa kusokota nyuzi,ukindu n.k
Vuma
- julikana kwa watu wengi k.v. habari, mtu n.k.
- toa sauti nzito v. simba,.upepo mkali,.ngoma n.k.
Afya
- hali nzuri ya mwili/siha
Avya
- toa mamba
- tumia ovyoovyo mali, pesa, n.k.
Fito
- vipande vya miti au chuma vya kujengea nyumba
Vito
- mawe ya thamani
Fuja
- tumia vibaya
- haribu mali, nguo ,chakula n.k.
Vuja
- pita kwa kitu mahali penye upenyo
- Gunia hili lina
Vunja
- fanya kitu kigumu kuwa vipande vipande
- badilisha pesa ziwe ndogondogo
- enda kinyume na kanuni
Futa
- pangusa
- chomoa kisu
- toa maji nje ya chombo/fua maji
Vuta
- fanya kufuata/burura
- ingiza hewa au moshi mapafuni
Wafu
- waliokufa
Wavu
- utando wa nyuzi wa kufulia samaki,kutegea wanyama,kuweka golini/kimiani n.k
CH/SH
Chaka
- mahali penye miti iliyosongamana
- msimu wa kaskasi/joto na ukavu wa ardhi
Shaka
- wasiwasi
- tuhumuma
Chali
- lala mgongo juu kichwa chini
- mtu anayechekesha watu kwa kuwatolea mkasa
Shali
- kitambaa cha begani cha shehe
Shari
- balaa (pata shari)
Chati
- mchoro unaotoa maelezo Fulani
Shati
- vazi la juu la mwili lenye mikono
Sharti
- lazima
Choka
- pungukiwa na nguvu baada ya kufanya jambo kwa muda mrefu
Shoka
- kifaa cha kukatia na kupasulia miti
Chombo
- ala ya kufanyia kazi
Shombo
- harufu mbaya ya samaki
Chokoa
- tia kitu chenye ncha kwenye tundu au shimo ili kutoa kitu k.m chokoa meno
Shokoa
- kazi ya kulazimishwa (fanyishwa shokoa)
- shamba lililolimwa na kuachwa kumea nyasi
TH /DH
Thamini
- tia maanani, heshimu
Dhamini
- toa pesa maakamani ili mshtakiwa asitiwe korokoroni
Thamani
- kima
Dhamana
- malipo ya kortini
Thibiti
- kuwa ya kweli/kuaminika
- Habari ime
Dhibiti
- tia mkononi
- Nikidhibiti pesa zangu kutoka kwake nitanunua baiskeli.
- weka chini ya mamlaka
Ridhi
- kubali
- pendezwa na jambo
Rithi
- miliki kitu kutoka kwa mtu aliyekufa ama uliye na uhusiano naye
- pata jambo au ujuzi kutoka kwa mtu mwingine
A/H
Apa
- tamka jina aghalabu la Mungu kuthibitisha jambo Fulani
Hapa
- mahali karibu
Ama
- au
Hama
- toka mahali fulani ili kwenda mahali pengine kuishi (gura)
Adimu
- -a shida kupatikana,nadra
Hadimu
- -mtumishi (mahadimu)
Ajali
jambo la madhara au hatari
Hajali
- kinyume cha jali
Auni
- saidia
Launi
- rangi
L/R
Lahani
- tuni
Rahani
- chumba maalum katika nyumba au chombo cha kuwekea vitu
Lea
- tunza mtoto
Rea
- ghadhibika
Lemba
- nyanganya kwa hila,punja
Remba
- pamba, rembesha
Fahali
- ng`ombe dume
Fahari
- -a kujivuniwa kwa watu
Mahali
- sehemu ambapo mtu au kitu huweza kukaa
Mahari
- mali au fedha inayotolewa na mwanamme kupewa wazazi wa mwanamke anayetaka kumuoa
S /SH
Saba
- namba inayoonyesha idadi
Shaba
- madini yenye rangi ya manjano
Saka
- tafuta,winda
Shaka
- wasiwasi
- tuhuma
- kutokuwa na hakika
Suka
- tikisa kitu
- pitisha kitu kama nywele baina ya zenyewe kupata mfumo fulani
Shuka
- enda chini kutoka juu ya kitu
- kitambaa cha kujifunga kiunoni
Soga
- mazungumzo ya kupitisha wakati
Shoga
- jina waitanalo wanawake marafiki
- msenge
Sababu
- kinachofanya jambo kutokea,chanzo
Shababu
- kijana
J/NJ
Jaa
- tosha
- tapakaa kila mahali
- mahali pa kutupia taka
Njaa
- hali ya tumbo kutaka kupata chakula
- ukosefu mkubwa wa chakula
Chema
- kizuri
Jema
- zuri
Njema
- nzuri
Jia
- sogelea karibu
Njia
- barabara
- namna au jinsi ya kufanya jambo
Jozi
- vitu viwili vinavyofanana vilivyo pamoja
Njozi
- maono yatokeayo usingizini;ruia
Jana
- siku kabla ya leo,mwaka kabla ya huu
- buu la nyuki-kama kiluwiwi cha nzi
Njana-samaki mwenye rangi nyekundu
D/ND
Dege
- eropleni kubwa
- ndege mkubwa
- ugonjwa wa watoto unaosababishwa na homa kali
Ndege
- mnyama aghalabu anayeruka kwa mabawa
- eropleni inayosafiri angani
- ndege mbaya/mzuri (bahati nzuri/mbaya)
Duni
- kitu chenye thamani ya chini
Nduni
- ajabu/lisilo la kawaida
B/MB
Basi
- gari la abiria
- kisha
Mbasi
rafiki
Buni
- gundua
- unda
- tunga
Mbuni
- ndege asiyeweza kuruka lakini huenda mbio sana
- mkahawa au mti uzaao kahawa
Bali
- lakini
- sijali wala sibali (kusisitiza kutojali)
Mbali
- si karibu
- tofauti
Mbari
- ukoo
Bega
- sehemu ya mwili juu ya mkono na chini ya shingo
Mbega
- nyani
- manyoya ya ndege wanayojifunga wachezaji ngoma (jifunga mbega)
Iba
- chukua kitu cha mtu mwingine bila ruhusa
Imba
- tamka maneno kwa sauti ya mziki
G/NG
Gawa
- tenga katika sehemu mbalimbali
- aina ya ndege wa usiku;kirukanjia
Ngawa
- mnyama afananaye na paka
Guu
- mguu mkubwa sana
Nguu
- kilele cha mlima
- nguru_aina ya samaki
Goma
- kataa kufanya jambo mpaka masharti fulani yatimizwe
- ngoma kubwa sana
- duwi (aina ya samaki)
Ngoma
- ala ya mziki inayotengenezwa kwa kuwambwa ngozi kwenye mzinga (piga ngoma)
- mchezo wa kufuata mdundo wa ngoma (cheza ngoma)
Koma
- alama ya kituo
- acha kufanya jambo
P/B
Pata
- kuwa na jambo, hali au kitu
- kuwa kali
- Kinolewacho hupata.
Bata
- ndege mwenye vidole vilivyotandwa aghalabu akaaye majini
Papa
- samaki mkubwa
Baba
- mzazi wa kiume
Pana
- kinyume cha –embamba
Bana
- finya
Bango
- uwazi ulio ardhini,mtini au jabalini
Bango
- kipande cha karatasi ngumu kama kadi
- bati linalozuia matope juu ya gurudumu la gari au baiskeli
Pacha
- watoto wanaozaliwa kutokana na mamba moja
Bacha
- tundu kwenye ukuta; shubaka(closet)
Paja
- sehemu ya mguu kati ya goti na nyonga
Pania
- kazana ili kufanya jambo lililokusudiwa
Bania
- zuia kitu bila ya kutaka kukitumia (bania pesa)
Pima
- tafuta urefu, uzito n.k.
Bima
- mkataba na shirika wa kulipa pesa ili kupata fidia mtu anapofikwa na hasara
Punda
- mnyama
Bunda
- fungu la karatasi,noti,ngozi n.k
Panda
- enda juu
- kifaa cha kurushia vijiwe; manati
- baragumu
- tia mbegu ardhini ili zimee
Banda
jengo kubwa la kuwekea vitu au wanyama
Pasi
- fuzu/faulu
- hati inayomruhusu mtu kusafiri nje ya nchi/pasipoti
- chombo cha kunyooshea nguo
Basi
- gari kubwa la abiria
Mbasi
- rafiki
T/D
Tamu
- enye ladha ya kuridhisha mdomo
Damu
- maji mekundu yanayozunguka mwilini
- ukoo
Taka
- kuwa na haja ya jambo fulani
- uchafu
Daka
- pokea kwa mikono kilichorushwa
- tunda bichi (nazi daka/danga)
Tokeza
- fanya kuonekana
Dokeza
- toa habari za siri kwa uchache
Tai
- ndege mkubwa mwenye makucha marefu alaye mizoga (vulture)
- kitambaa kinachovaliwa kwenye ukosi wa shati
Dai
- taka kupewa kilicho chako
- habari inayosemwa na haijathibitishwa
K/G
Kamba
- uzi mnene
- samaki mdogo
- mnyama wa baharini mwenye miguu mingi ambaye huliwa
- kata kamba (kimbia)
Gamba
- ngozi kama pembe ya kasa, samaki ,kasa au kobe(scales)
Konga
- kuwa mzee
- kusanya vitu au watu mahali pamoja (kongamano)
- meza maji kidogo ili kupunguza kiu (konga roho)
Gonga
- kutanisha kitu kimoja na kingine kwa kuvipiganisha
Koti
- vazi zito livaliwalo juu ya nguo
Korti
- mahakama
Goti
- kiungo cha mguu kinachounganisha paja na muundi
Mfugo
- mnyama anayefugwa nyumbani kwa ajili ya kuliwa au biashara
Mfuko
- kitu cha kitambaa cha kutilia vitu
Tegua
- fanya mtego usifanye kazi
- ondoa chombo kama chungu mekoni
- fanya kiungo cha mwili kifyatuke
Tekua
- angusha kwa kusukuma
- ng`oa kwa nguvu k.v. mmea
Mkuu
- kiongozi
- wenye hadhi kubwa
Mguu
- kiungo cha binadamu au mnyama cha kusimamia au kutembelea
Oka
- tia ndani ya tanuu kitu ili kiive au kikauke k.v unga uliokandwa au matofali
Oga
- safisha mwili
- enye hofu
Pika
- weka kitu k.v. chakula sufuriani juu ya moto ili kiive
Piga
- kutanisha vitu kwa nguvu
- piga chafya, maji, hodi n.k.
Ukali
- hali ya kutokuwa mpole
- hali ya uchungu (ladha)
Ugali
- chakula kinachopikwa kwa unga wa mahindi na kusongwa na maji moto hadi yakauke