• Thu. May 8th, 2025

    Newsblaze.co.ke

    A site providing Education, TSC, Universities, Helb, Sports and Kuccps news

    MWONGOZO WA TUMBO LISILOSHIBA

    ByHillary Kangwana

    Mar 24, 2025

    Yaliyomo

    Tumbo Lisiloshiba Said A. Mohamed………………………………….1.
    Mapenzi ya Kifaurongo KennaWasike……………………………………. 17
    /Shogake Dada ana Ndevu Alifa Chokocho ………………………………….31
    Shibe Inatumaliza Salma Omar Hamad ……………………………41
    Mame Bakari Mohammed Khelef Ghassany……………….45
    Masharti ya Kisasa Alifa Chokocho ………………………………….53
    Ndoto ya Mashaka Ali Abdulla Ali ……………………………………62
    Kidege Robert Oduori ……………………………………70
    Nizikeni Papa Hapa Ken Walibora ……………………………………76
    Tulipokutana Tena Alifa Chokocho…………………………………. 82
    Mwalimu Mstaafu Dumu Kayanda…………………………………. 88
    Mtihani wa Maisha Eunice Kimaliro………………………………… 96
    Mkubwa Ali Mwalimu Rashid ………………………….104
    iii.
    1. TUMBO LISILOSHIBA
    Historia ya Mwandishi.
    Hadithi hii imeandikwa na Prof. Said Mohammed, mwandishi
    mtajika ambaye amewahi pia kuandika vitabu vingine vitajika
    kama vile Riwaya ya Utengano. Mwandishi huyu bila shaka ni gwiji
    katika ulingo huu kwani amewahi kuandika kazi zingine za fasihi
    andishi zikiwemo tamthilia, mashairi na hadithi fupi.
    Dhamira
    Dhamira ni funzo kuu litokanalo na kazi ya sanaa au lengo kuu la
    mwandishi. Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshoba alidhamiria
    kufunua uozo unaoletwa na ubinafsi na tamaa katika jamii. Aidha
    anawajasirisha wanaoathiriwa kuwa wanaweza kukubali madhila
    wanayofanyiwa ama kupinga dhulma hizo na kusimama wima na
    kutetea haki zao.
    Ufupisho wa Hadithi.
    Hadithi hii inaangazia maisha ya watu wanaoishi katika mtaa wa
    Madongoporomoka, mtaa ambao umepakana na jiji linalokuwa
    kwa kasi mno. Jiji hili limeshiba kwa wingi wa mijengo iliyojengwa
    k i a s i c h a k u a n z a k u t i s h i a u we p o wa m t a a d u n i wa
    Madongoporomoka. Uvumi unawakia wanamadongoporomoka
    kwamba mtaa wao utanyakuliwa ili upanuzi wa mji ukie eneo hilo.
    Mwanzoni ulianza kama tu uvumi uliokuja na kupita bila ya
    wanamadongoporomoka kuwa na uhakika nao. Ingawa uvumi huo
    u l i i s h i a k u t ow e k a , M z e e M a g o k a t u h a k u wa r u h u s u
    wanamadongoporomoka kutupilia mbali wazo la uvumi huo kutimia
    na wao kuishia kufurushwa. Anawaleta pamoja wanakijiji wenzake
    ili kutafuta suluhishi kwa tatizo lililokuwa limewakodolea macho.
    Kwa pamoja wanakijiji wote wanakubaliana kutoondoka na liwe
    liwalo. Hata ikiwa watafurushwa, wanaamua kutetea mtaa wao na
    kusalia.
    Kisadfa, bwana mmoja mwenye tumbo kubwa anawasili kwenye
    mkahawa wa Mzee Mago na kutaka kupewa chakula chote
    kilichoandaliwa. Ajabu ni kuwa anapokabidhiwa chakula hicho,
    1.
    anafyeka chote fyuu! Ni ajabu kwani huyu jamaa ana “Tumbo
    lisiloshiba”. Baada ya kula na kutoa bweu kubwa lenye harufu
    mbaya, jitu linalipa na kuahidi litarejea siku iliyofuatia.
    Siku iliyofuata wanamadongoporomoka wanagutushwa na
    maporomoko yanayotokana na vibanda vyao kubomolewa na
    mabuldoza. Wanafurushwa wote kwa nguvu. Vibanda vyao
    vinabomolewa na wao kuishia kufukuzwa. Ajabu ni kwamba
    “Bwana Tumbo” anarejea kama alivyoahidi. Ila wakati huu yuko
    ndani ya gari kubwa na dereva anayemwamrisha. Hivyo amerudi
    kula kila kitu kama alivyoahidi ila wakati huu amekuja kula
    m a s h a m b a y a o . M z e e M a g o a n a w a s h a w i s h i
    wanamadongoporomoka kutoondoka, licha ya dhulma hizo.
    Umoja wa wanakijiji hawa unawaokoa kwani muda mfupi
    baadaye, vibanda vyao vinaanza kuota tena. Wanafaulu kuzuia
    tamaa ya tumbo kubwa lisiloshiba la mji kutokula mashamba yao.
    MAUDHUI
    Baadhi ya maudhui yanajitokeza katika hadithi hii ni kama vile:
    a) Ubinafsi na tamaa
    b) Unyanyasaji
    c) Utetezi wa haki
    d) Umaskini
    e) Utabaka
    f) Migogoro
    a) Ubinafsi na tamaa (Tumbo lisiloshiba)
    Haya ndiyo maudhui makuu katika hadithi hii. Maudhui haya
    yanajengeka kwa kutazama jinsi ambayo wahusika fulani
    hawatosheki na mengi waliyokuwa nayo na hivyo basi kutamani
    vidongo vya wengine na kutaka kuwahini. Wakubwa wa jiji
    wanadai kwamba jiji limejaa tayari hadi Pomoni. Halijaacha hata
    nafasi ya mtu kuvuta pumzi.
    2.
    Jiji lenyewe limekuwa limesheheni usa, ujumi na tamaduni mbali
    mbali. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, departmental stores, casinos,
    viwanja vya gofu, viwanja vya tenisi, voliboli, mpira wa vikapu,
    raga, kabumbu, vyuo vikuu, mahakama, hospitali, majumba ya osi
    na mengine mengi. Haya yote yamekuwa yamesimama wima jijini.
    Hapajasalia hata nafasi kidogo ya kuvuta pumzi. Hivyo basi
    wakubwa wa jiji waonelea vyema kwa ardhi ya watu wa
    Madongoporomoka kutwaliwa. Hii ni tamaa ya hali ya juu.
    Wanataka wajenge majumba ya kifahari huko. Hawataki kuwalipa
    wenye ardhi hiyo dhamana inayofaa bali wanataka tu kuwafurusha
    wanamadongoporomoka.
    Mhusika “Bwana Tumbo” anaingia kwenye mkahawa wa Mzee
    Mago. Ukubwa wa tumbo lake unashangaza wengi. Ni dhahiri kuwa
    huyu mtu ni mlaji hodari. Jamaa huyu anaishi kuulizia chakula
    kilichopo kwenye mkahawa na kukila. Anakula chakula chote
    kilichoandaliwa kwa walaji wengine wote. Anamaliza chakula na
    kuongezewa kingine. Anakula nyama ya kuchoma, mchuzi wa
    nyama, wali wa nazi, samaki wa kukaanga, chapatti kadhaa na
    kuishia kuteremshaa na chupa mbili za Coca cola. Anafagia
    mkahawa wote. Anaahidi kurejea siku itakayofuata na kutaka
    chakula kipikwe mara mbili Zaidi ya kile kilichopikwa siku hiyo. Hii ni
    tamaa ya ajabu. Watu waliokuwepo kwenye mkahawa wanabaki
    kushangaa ni vipi mtu anakula chakula chote kilichoandaliwa walaji
    wote kwenye mkahawa?
    Bwana mwenye tumbo ana tamaa ya mashamba. Anajaribu
    kuwafurusha wanamadongoporomoka kutoka kwenye makaazi
    yao. Anawarausha asubuhi na mapema kwa mabuldoza
    yanayobomoa makaazi yao. Inakusudiwa kuwa majengo
    yatajengwa katika ardhi hii inayotamaniwa sana na wenye jiji.
    Anwambia Mzee Mago kuwa amekuja kula mashamba yao. Hii ni
    tamaa ajabu ya mashamba yaliyo na wenyewe.
    3.
    Jiji lina tumbo ambalo halishibi. Jiji hili limepambwa vyema na
    majumba ya kifahari. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, departmental
    stores, casinos, viwanja vya gofu, viwanja vya tenisi, voliboli, mpira
    wa vikapu, raga, kabumbu, vyuo vikuu,mahakama na hata
    hospitali. Ajabu ni kuwa jiji hili halijatosheka kwa usa wake. Jiji
    linataka kupanua tumbo lake hadi katika mtaa wa
    Madongoporomoka.
    a) Unyanyasaji
    Hii ni hali ya wahusika kuhiniwa haki ambayo wanastahili na
    badala yake wengine kupewa haki hiyo kwa haramu.
    Wanamadongoporomoma wananyanyaswa na viongozi wa jiji.
    Licha ya wao kuwa wamiliki halisi wa mashamba yao,
    wanapangiwa hila ya kunyang’anywa vipande vyao vya ardhi.
    Ardhi hiyo inapangiwa njama ya kunyakuliwa bila ya wao kulipwa
    dia inayostahili. (Uk 4)
    WanaMadongoporomoka pia wananyanyaswa kisheria. Ni mujibu
    wa sheria kuwatetea watu wote ambao wamehiniwa au kutendewa
    isivyo haki. Mzee Mago anafahamu vyema kwamba kuna
    uwezekano mkubwa wa wao kupokonywa mali zao ilhali sharia
    itumiwe kuwakandamiza yeye na maskini wenzake.Anaomba
    waishie kumpata hakimu ambaye ni mpenda haki ili haki isiuliwe na
    asiyestahili kuishia kutetewa na sharia mbovu. (Uk 2)
    Majengo makubwa yaliyoko jijini yananuia kuwanyanyasa
    wanamadongoporomoka na kumeza vipande vyao vya ardhi.
    Vipande hivi vya ardhi vinanuiwa kutumika ili kuwahi kujenga
    majengo bora Zaidi.
    b) Utetezi wa haki
    Mzee Mago ametumiwa na mwandishi kama kielelezo cha mtetezi
    wa haki ya wakaazi wa kijiji wa madongoporomoka. Mhusika huyu
    anawatetea madongoporomoka kutokana na maonevu ya wakuu
    wa jiji.alijitahidi kuzuia njama ya watu wakubwa kutaka kuchukua
    ardhi za watu wadogo. Mzee Mago aliwafuata wengine ili
    kuzungumza kuhusu haki ya unyang’anyaji wa mashamba yao. Yeye
    hupiga mbio huku na kule kujaribu kuzuia haki isiangamizwe. (Uk 2)
    4.
    Kwa kuwa Mzee Mago anafahamu kwamba haki inauzwa na
    kupewa watu wasiostahili. Anajua kuwa haki itauzwa. Anafahamu
    kwamba haki itapewa wengine wasiostahili. Hivyo basi anamtafuta
    wakili mzuri ambaye hatasaidiana na viongozi dhalimu ili kuwahini
    mashamba yao.
    Mzee Mago anawahamasisha wanamadongoporomoka kutokubali
    kufurushwa kutoka maeneo yao. Hawaruhusu watu kusahau uvumi
    wa wao kufurushwa. Anawaita katika kikao na kuwakumbusha
    uwezekano wa hao kufurushwa. Anawaongoza kutokubali
    kufurushwa ikiwa wakubwa wa jiji watakuja kuwaondoa kwenye
    makaazi yao. Baadaye wanamadongoporomoka wanapovamiwa,
    wanakataa kuondoka hadi wiki tatu baadaye ambapo makaazi
    yao yanarudi kuchomoza kama uyoga. (Uk 11)
    a) Umaskini
    Ni hali ya kukosa mali/hali ya ufukara au ukata. Umma wa
    Madongoporomoka unaishi katika hali mbaya ya kimaskini.
    Mandhari ya kijiji hiki ni ya kimaskini na kufedhehesha mno. Kuna
    mashonde na vinyesi. Kuna vibanda vya uchwara vinavyozungukwa
    na uoza na bubujiko la maji machafu. Kuna uvundo unaopasua
    mianzi ya pua. (Uk 4). Bila shaka, mandhari haya sio ya mahali
    ambapo mtu anaweza kufurahia kuwa. Ni mandhari ya mahali
    ambapo ni masikini tu ndio wanaishi.
    b) Utabaka
    Hii ni hali ya wahusika kugawika katika makundi tofauti tofaauti
    kulingana na uwezo wao wa kiuchumi. Kuna tabaka la matajiri na
    masikini. Kila tabaka limejikita katika shughuli zao wenyewe za
    kutetea matumbo yao. Masikini wanapigania kutetea makaazi yao
    ya kimaskini. Wanakataa kata kata kuhiniwa na wachache matajiri
    ambao wanamiliki mali nyingi. Kwa upande mwingine, matajiri
    wana matumbo yasiyoshiba. Wananyakua mashamba ya masikini
    kwa minajili ya kutaka kuendeleza ujenzi wa majumba ya kifahari.
    Hivyo basi, matajiri wanaishi kuwafurusha masikini kutoka kwenye
    makaazi yao. (Uk 10-11)
    5.
    a) Migogoro
    Katika hadithi hii panazuka migogoro mbali mbali baina ya
    wahusika tofauti. Kuna tofauti nyingi ambazo zinazuka kati ya
    wahusika mbali mbali katika hadithi. Baadhi ya migogoro hii ni
    kama vile:
    a) Mgogoro baina ya Wakuu wa Jiji na wanakijiji wa
    Madongoporomoka.
    Mgogoro huu unatokana na hali ya jiji kupanuka na
    kusheheni kila aina ya majumba kiasi cha kukosa nafasi ya
    mtu kuvuta pumzi. (Uk 4)Kutokana na hali hii, wakuu wa jiji
    wanaonelea kuwa mahali pazuri pa kupanua shughuli za jiji
    lile ni huko Madongoporomoka. Huko ndiko kuna vijishamba
    ambavyo havina kazi. Vishamba ambavyo vinapaswa
    kupambwa na majumba mazuri ya kifahari. Kwa upande
    mwingine, maskini hawa wanaenzi vijumba vyao pamoja na
    mazingira yao na hawako tayari kuondoka kwa njia yoyote
    ile. Hali hii inazua mgogoro kati yao na wakuu wa Jiji.
    b) Mgogoro baina ya Bwana mwenye tumbo na wana-
    Madongoporomoka.
    Bwana Mwenye tumbo ananuia kula mashamba ya wana-
    Madongoporomoka. Kwa upande mwingine, wanakijiji hawa
    wanakaidi amri ya kuondoka, pamoja na madhila ya
    kubomolewa makaazi yao wanamoishi. Licha ya mateso yote
    wanayoelekezewa wana-Madongoporomoka, wanakataa
    kuondoka katika mashamba yao na kuruhusu ujenzi wa
    majumba ya kifahari kutekelezwa. Ni wazi kuwa huu ni
    mwanzo tu wa mgogoro kati ya wahusika hawa hawa na
    mporaji huyu wa ardhi.
    6.
    MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI.
    Hizi ni mbinu ambazo mwandishi hutumia ili kuleta mvuto katika kazi
    yake. Mbinu za uandishi ni sawa na mtindo wa mwandishi. Hizi
    zinahusu upekee wa mwandishi kwa namna anavyoichora kazi
    yake. Mbinu za uandshi ni mbinu ambazo mwandishi hutumia ili
    kutupa sisi wasomaji ujumbe wa ziada. Mbinu hizi ni kama vile
    matumizi ya ndoto, barua, mbinu rejeshi,n.k. mbinu zilizotumiwa
    katika hadithi hii ni pamoja na:
    1. Takriri
    Takriri ni mbinu ya kifasihi ya kurudiarudia neno au kifungu cha
    maneno ili kusisitiza au kulitilia mkazo. Mifano ya takriri ni kama
    ifuatayo:
    a) Ulianza uvumi. Uvumi ukageuka nong’ono. Nong’ono
    zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. Wasiwasi ukawa
    hofu… (Uk 1).
    b) …gwa sahau hiyo ni tokeo la lile lile la umoja katika uwili.
    (Uk 1)
    c) Mzee Mago kajifunza kutosahau. Kutosahau hamkumpi hata
    kidogo… (Uk 2)
    d) Itikadi ya wakubwa ilikuwa bado ni ile ile. (Uk 2)
    e) Hawawezi…hawawezi, hawawezi, kabisa hawawezi! (Uk 5)
    2. Kinaya
    Kinaya ni hali ambayo mhusika anasema au kutenda kinyume
    na matarajio. Mifano ya kinaya ni kama ifuatayo:
    a) …maana siku hizi wanasheria waaminifu ni adimu kama
    haki yenyewe. (Uk 2)
    b) Ilishikilia kwamba jiji halina nafasi tena. Yaani limejaa kila
    pahala. Limejaa hiki na kile, hili na lile. Limejaa hadi
    pomoni. (Uk 3-4)
    7.
    c) Halikuacha hata nafasi ya kuvuta pumzi. (Uk 4)
    d) “sharia gani hiyo iko mikononi mwetu?” Aliuliza Mzee
    Mago. “Sheria kila wakati iko mikononi mwao.” (Uk 6)
    a) “Nitakula chakula chako chote ulichopika kuwauzia
    wateja wako leo.” (Uk 8)
    1. Taswira
    Taswira ni maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika akili za
    msomaji. Mifano ya taswira ni kama ifuatayo:
    a) Kuna mashonde na vinyesi. Kuna vibanda vya uchwara
    vinavyozungukwa na uozo na bubujiko la maji machafu. Kuna
    uvundo unaopasua mianzi ya pua. (Uk 4).
    b) Wakati huu ndipo pua za wazungumzaji hawa ziliponasa
    harufu za vyakula vilivyotoka jikoni. Harufu mchanganyiko
    zilizowaingia puani na kukaanza kulambatia na kukaza mate
    vinywani mwao. (Uk 6)
    c) Jitu lilikuwa limevaa suti nyeusi na shati jeupe. Limekabwa
    shingoni na tai ya buluu iliyozama kwenye misuli ya shingo
    fupi nene…(Uk 7)
    d) Naam. Vyakula vilipakuliwa. Wali na nazi. Mchuzi na nyama.
    Nyama ya kuchoma kwa mkaa na bakuli la kachumbari.
    Samaki wa kukaanga. Chapatti kadhaa za duara… (Uk 8)
    1. Maswali ya Balagha
    Balagha ni mbinu ambapo mwandishi huuliza maswali yasiyohitaji
    majibu. Maswali haya hulenga kumfanya mhusika au msomaji kukiri
    kwa kina. Kwa mfano:
    a) Aaa, kuna jabu gani lakini mvua ikinyesha? Si kila siku
    huanguka kupunguza joto …? Si huanguka kuburudisha nafsi
    zinazohaha na kukata tamaa? (Uk 1)
    b) Nani angewashauri wao mburumatari? Sauti zao hazikustahi
    kusikika, seuze kusikizwa? (Uk 3)
    8.
    c) Kwani si kila mtu anafaa kujua kuwa kimya kirefu kina
    mshindo mkuu? (Uk 3)
    d) Tuondoke twende wapi? (Uk 5)
    e) Kuwe na mazungumzo gani hasa yatakayomchangamsha
    kila mtu wakati huu kuliko uvumi ulioanza tena kuvuma? (Uk 5)
    f) Aaa, nani anayejua hatimaye? Kesho yenyewe haijazaliwa
    seuze fumbato ndani ya kesho yenyewe?
    g) Chupa mbili za Coca cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo?
    (Uk 8)
    h) Wakawa wanatazamana kwa wakionyesha hawaamini nini
    kinachotokea. Itawezekanaje?
    1. Kuchanganya Ndimi
    Hii ni mbinu ya uandishi ambapo wahusika huzungumza kwa
    kutumia lugha zaidi ya moja ili kuonyesha hali yao na hisia zao
    katika mazungumzo. Mbinu hii humwezesha mhusika kujieleza
    vyema Zaidi kwa kutumia msamiati ambao hauko katika lugha
    fulani. Kwa mfano:
    a) Chupa mbili za Coca cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo?
    (Uk 8)
    b) Jitu hilo lilikuwa limeketi nyuma ya gari kubwa aina ya Audi
    Q7…(Uk 10)
    c) Simama kidogo Chauffer… (Uk 11)
    9.
    2. Taharuki
    Taharuki ni mbinu inayotumiwa na waandishi ili kuteka hisia na
    hamu ya wasomaji kutaka kuendelea kusoma zaidi. Katika
    kufanikiwa kujenga taharuki, mwandishi husuka matukio
    yalito na mshikamano na mtiririko ambao humvutia msomaji
    asiiweke chini kazi hiyo pindi aanzapo kuisoma hadi akie
    kikomo chake.
    a) Ulianza uvumi. Uvumi ukageuka nong’ono. Nong’ono
    zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. Wasiwasi ukawa
    hofu… (Uk 1). Msomaji anajiuliza, Ni jambo gani hili ambalo
    linatarajiwa kutendeka?
    b) Kwa Mzee Mago, iliyobaki sasa ni kutazamia siku ya
    kulipuka mambo…(Uk 3)
    Ni mambo yepi yatalipuka? Hii inasalia kama taharuki.
    c) Kesho nitaka hapa tena. Niwekee chakula mara mbili
    kuliko hiki cha leo…(Uk 9)
    Tunashangaa ikiwa jitu hilo kweli litarudi.
    1. Jazanda/ Istiari.
    Jazanda ni mbinu ambayo inaonyesha fumbo lililotumiwa na
    mwandishi kurejelea hali fulani kwa njia che. Istiari kwa upande
    mwingine inalinganisha moja kwa moja kitu au hali na nyingine
    lakini bila ya kutumia maneno ya ulinganisho. Mifano:
    a) Angepoaje na ule moto unaomlipukia kila mtu pale mtaani
    umeacha mpaka sasa kovu bichi moyoni…? (Uk 2)
    10.
    b) Wakubwa hawatambui kuwa kwamba jambo hilo la
    kuwafanya wao takataka tu ndilo linalowakasirisha… (Uk 3)
    c) Sahau imebaki vilevile kutanda giza na kufunga milango ya
    wasiwasi vichwani mwa watu… (Uk 5)
    d) Bweu likapasuka na kutoa uvundo wa mnyama aliyeoza…
    (Uk 9)
    Hii ni ishara ya jinsi jitu hili litawahangaisha wanakijiji hawa
    baadaye.
    2. Tashbihi/Mshabaha
    Tashbiha/Tashbihi/Mshabaha ni maneno yanayofananisha kitu,
    jambo au kitendo na kingine kwa kutumia vihusishi kama vile ‘kama’,
    ‘mithili’, ‘ja’, ‘mfano wa’ na kadhalika. kwa mfano:
    a) …maana siku hizi, wanasheria waaminifu ni adimu kama
    maziwa ya kuku! (Uk 2)
    b) Ulikuwa ukitukuta ndani kwa ndani kama moto ya makumbi.
    (Uk 3)
    c) Umebaki tu ukining’inia hewani kama mvua inayotarajiwa
    kunyesha…(Uk 4)
    d) Kauli ya jitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama mtu
    aliyechapwa na bakora. (Uk 7)
    e) Lilipokula, lililamba sahani zote kana kwamba lilikuwa na
    jukumu la kuziosha.(Uk 9)
    f) …vibanda vya Madongoporomoka viliota tena hapo kama
    uyoga. (Uk 11)
    11.
    1. Tashihisi/Uhuishaji
    Hii ni mbinu ya lugha ya kuweka hisia na uhai katika vitu
    visivyokuwa na uhai. Pia kuna uwezekano wa kuwapa wanyama
    uwezo na hulka za binadamu. Mifano:
    a) Nong’ono zikafumbua kinywa kueneza wasiwasi. (Uk 1)
    b) Maisha ndugu yangu ndiyo- maisha ndiyo yanayotukaba
    koo akina sisi! (Uk 1)
    c) Yeye hupiga mbio huku na kule kujaribu kuzuia haki
    isiangamizwe…(Uk 2)
    d) Mzee Mago lakini hairuhusu sahau iketi na kutawala
    kichwani mwake. (Uk 2)
    e) Aliwakumbusha kuwa maendeleo yanadai mchango wa kila
    mtu…(Uk 2)
    f) Kesho yenyewe haijazaliwa, seuze fumbato…(Uk 5)
    g) Sahau imebaki vilevile kutanda giza na kufunga milango ya
    wasiwasi vichwani mwa watu… (Uk 5)
    h) Kauli ya jitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama mtu
    aliyechapwa na bakora. (Uk 7)
    i) Haikuchukua muda mrefu akili zilipowaamsha kuwapeleka
    maana ya kile…(Uk 10)
    2. Chuku
    Ni mbinu ya kutilia mazungumzo chumvi ili kuyafanya yavutie
    Zaidi. Kwa mfano:
    a) K w a m i u j i z a , n d i p o j i t u l a m i r a b a m i n e
    lilipoingia…halikujulikana lilipotoka. Liliingia tu ghaa..(Uk
    6)
    b) Lile tumbo lake limezidi kufura na ndani ya tumbo, ugomvi wa
    vyakula ukawa unapwaga kwa mingurumo ya radi iliyosikika
    hadi nje. (Uk 9)
    12.
    c) Mstari huo ulikuwa umefuatana na mpasuko mkali wa radi na
    umweso uliomulika mpaka ndani ya mioyo ya watu. (Uk 10)
    d) Jitu hilo lilimwaga tabasamu mfululizo iliyoenea eneo lote la
    Madongoporomoka. (Uk 10)1. Nidaa
    Ni mbinu ya kuonyesha hisia aliyo nayo mhusika. Hujulikana kwa
    kutumia alama ya hisi. Kwa mfano:
    a) Maisha ndugu yangu ndiyo- maisha ndiyo yanayotukaba koo
    akina sisi! (Uk 1)
    b) …maana siku hizi, wanasheria waaminifu ni adimu kama
    maziwa ya kuku! (Uk 2)
    c) Pale lilipoketi, lilionekana kupapa jasho ovyo! (Uk 7)
    d) Halikubakisha hata chembe moja ya chakula chochote
    alichopewa! (Uk 9)
    e) Hazitatuhamisha kabisa hizi fujo zenu! (Uk 11)
    2. Tanakuzi.
    Ni mbinu ya kutaja vitu viwili ambavyo sifa zao zimepingana.
    Kwa mfano:
    a) “Hata hivyo, kila mtu, mdogo kwa mkubwa, kike kwa kiume…
    (Uk 2)
    b) Aliwakumbusha kuwa maendeleo yanadai mchango wa kila
    mtu, maskini au tajiri. (Uk 2)
    c) Lile jitu lilimkata maneno Mzee Mago, Wakubali,
    wasikubali…(Uk 8)
    d) Watu wanakimbia huku na huku, huku na kule, mbele na
    nyuma…(Uk 10)
    e) Kike kwa kiume, vijana kwa wazee, watoto kwa watu
    wazima…(uk 10)
    13.
    WAHUSIKA NA UHUSIKA
    a) MZEE MAGO
    Huyu ndiye mhusika mkuu ambaye ametumiwa na mwandishi kama
    kielelezo cha watetezi wa haki. Ametumika kuwatetea wanyonge
    kutokana na madhila ya matajiri wanaotaka kuwapokonya
    mashamba yao. Sifa zake ni kama zifuatazo:
    i) Ni mtetezi wa haki.
    Anakataa kutazama huku wanakijiji wakihiniwa mashamba yao.
    Anamtafuta wakili ambaye hajahongwa ili kutetea haki ya
    w a n y o n g e . I s i t o s h e , a n a k a t a a k u w a r u h u s u
    wanamadongoporomoka kusahau uvumi uliokuwepo hapo awali
    kuhusu uwezekano wa vipande vyao vya ardhi kuchukuliwa.
    ii) Ni mwenye hekima/busara.
    Anafahamu vyema matokeo ya wingu linalotarajiwa kutua. Hivyo
    anajiandaa na pia kuwaandaa wanakijiji ili yatapowasili madhila,
    wawe tayari wameungana kupigania haki zao.
    iii) Ni mwenye bidii.
    Ni yeye tu aliye na mkahawa pale madongoporomoka, ishara ya
    kwamba ni mtu mwenye bidii ya mchwa.
    14.
    iv) Ni mwenye ushawishi
    Anafaulu kuwahamasisha wanakijiji wote kujiandaa ili kukabiliana
    na vita vinavyokuja vya kunyang’anywa vipande vyao vya ardhi.
    Isitoshe anawaandaa wanamadongoporomoka kupinga hila
    zitakazokuja na kukataa kuondoka kwenye mtaa wao. Hatimaye
    wanapovamiwa na kubomolewa makazi yao, wanakaidi na
    kukataa kuondoka, jambo linalowapa ushindi baadaye.
    v) Amepevuka
    Anafahamu ka uzito wa kesi na ubishi unaotokana na ardhi.
    Isitoshe ana ufahamu mzuri wa namna ambavyo haki haipatikani
    kwa urahisi. Hivyo anaamua kumtafuta wakili aliye mwaminifu
    ambaye hatimaye anawaokoa kutokana na makucha ya matajiri
    wenye tamaa. Wanarudia kujenga vibanda vyao upya.
    a) JITU LENYE TUMBO
    Mhusika huyu hatujapewa jina lake halisi ila matendo yake ndiyo
    yanashangaza. Sifa zake ni kama zifuatazo:
    i) Ni katili
    Hana huruma anapobomoa makazi ya maskini. Anawafumania
    asubuhi na mapema na kuwafurusha. Anabomoa makazi ya watu
    ambao hawana pahala pengine pa kuita kwao, huku akiangua
    kicheko akiona namna wanavyohangaika.
    15.
    ii) Mwenye tamaa
    Anatamani ardhi za maskini wa Madongoporomoka na
    kuwapangia njama ya kuwafurusha kutoka makwao. Ingawa ana
    uwezo wa kutumia buldoza na polisi, anaishia kushindwa katika wizi
    wake na maskini hawa kurejelea makaazi yao.
    iii) Mwenye dharau/Kiburi
    Anawazungumzia Mzee Mago na wenzake pale kwenye mkahawa
    kwa dharau na mabezo.
    iv) Ni Mla
    Anafyeka vyakula vya aina mbali mbali bila kusaza chochote.
    Vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja pale kwenye
    mkahawa vinaliwa na yeye pekee. Mwishowe anatoa bweu kubwa
    linalochafua hewa yote pale.
    Mhusika huyu ametumiwa kama kielelezo cha watu wenye tamaa
    mbaya ya mali, waliojawa na ukatili na wanaoweza kutenda ukatili
    wowote ili kupata mali.
    Kabwe, Bi.Suruta na Bi. Fambo.
    Hawa ni wana-Madongoporomoka ambao wanaoshirikiana na
    Mzee Mago ili kujiandaa kwa wingu ambalo lingeanguka hapo
    baadaye. Ni wazi kwamba wahusika hawa ni wenye hekima na
    waliomakinika kwa mambo yajayo. Wahusika hawa wametumiwa
    kama kielelezo cha viongozi wenye mioyo ya ujasiri wa kupigania
    jamii zao.
    16.
    2.MAPENZI YA KIFARAUNGO
    Historia ya Mwandishi.
    Mwandishi wa hadithi hii anaitwa Kenna Wasike. Ni mwandishi
    ambaye yuko katika harakati zake za mwanzo katika ulimwengu
    wa uandishi. Yeye ni mwalimu aliyesomea chuo kikuu cha Nairobi.
    Dhamira
    Mwandishi amekusudia kutahadharish wasomaji wake dhidi ya
    kugawanywa kwa misingi ya utabaka. Analenga kukashifu
    migawanyiko ya watu kwa kuzingatia uwezo wao wa kiuchumi.
    Ufupisho wa Hadithi
    Mwandishi anatumia nafsi ya kwanza katika masimulizi yake.
    Anatupa hadithi yake mwenyewe akiwa chuo kikuu. Ingawa
    amefaulu kuka chuo kikuu, maisha sio mepesi kwa namna yeyote.
    Wazazi wake ni maskini hohe hahe wanaopigania mikono kuka
    kinywani tu. Bidii yake ndiyo ilimkisha katika chuo kikuu. Msimulizi
    anapoka katika chuo kikuu, anashangaa namna ambavyo
    wanafunzi wengi wanaandamana kwa mapenzi. Ingawa
    anatamani, haimpitii mawazoni mwake ya kwamba naye pia
    angeweza kuwa na mpenzi huko chuoni. Masomo chuoni ni magumu
    na ambayo hayaeleweki kwa wengi wa wanafunzi hao, ingawa
    wanajitahidi. Mwalimu anayewafunza ni Dkt. Maboga ambaye
    anatema dhana nzito nzito za fasihi. Wanafunzi wengi wanauliza
    maswali ilikuelewa Zaidi anavyomaanisha mwalimu huyu. Bila shaka
    hawaelewi mambo anayosema huyu mwalimu, lakini nani
    atadhubutu kumuzomea daktari mzima?
    17.
    Siku moja baada ya msimulizi kupika uji wake na kujiandaa kunywa,
    anasikia mtu akibisha mlangoni. Anapofungua, anamkuta binti
    mmoja mrembo ambaye baadaye anagundua kwamba ni
    mwanafunzi mwenzake nye darasa moja anayeitwa Penina. Penina
    anadai kwamba anampenda Dennis bila kujali umaskini wake.
    Ajabu ni kuwa Penina ni binti wa Waziri. Ni kinaya kwa msichana wa
    haiba yake kumpenda maskini kama Dennis. Baada ya masomo
    yao, Dennis na Penina wanaishi pamoja huku wazazi wa Penina
    wakilipa kodi ya nyumba na matumizi yao yote. Dennis anajaribu
    kutafuta kazi bila mafanikio. Anapata fursa katika shirika la
    uchapishaji wa magazeti. Anapopatikana katika chumba cha
    udodosi, anashindwa kufungua kinywa chake na kujitetea ni kwa
    nini anahitaji kazi ile. Dennis anafurushwa kutoka chumba cha
    udodosi kwa haya nyingi usoni na majuto mengi moyoni.
    Anaporejea nyumbani, anamkuta Penina ameketi akitazama
    televisheni. Anataka kupewa chakula ila anaariwa kuwa hakuna
    chakula chochote kile. Penina anamwarifu kuwa chakula hakipo
    kwani yeye Dennis hakuwacha chochote cha kuliwa. Kisha Penina
    anataka kujua ikiwa Dennis amefaulu kupata kazi. Dennis
    anapojibu kwamba hakufaulu, jibu la Penina linamshangaza.
    Penina anamwambia kwamba anajutia uamuzi wake kuolewa
    kwake. Anajuta kutowasikiliza wazazi wake kwani walimwonya
    kutokana na Dennis. Anadai kuwa anataka kuolewa na mtu mwenye
    kazi nzuri na pesa. Kisha Penina anishia kumfukuza Dennis kutoka
    kwake. Anamwamrisha afunge virago vyake na kuondoka. Dennis
    anapomdadisi kuhusu mapenzi yao, anamhakikishia kuwa yeye
    hataki kuolewa na maskini kama yeye. Ni ajabu kuwa mapenzi ya
    Penina yameyeyuka.
    18.
    Ni mapenzi ya kifaraungo. Dennis akiwa anaondoka na begi lake,
    anasikia sauti ikimwamuru nyumba ile aione paa na asiwahi kurejea.
    Hali hii inamletea majuto si haba. Kweli mapenzi ya Penina yalikuwa
    na kifaraungo. Yaguzwapo tu na wimbi ndogo yananyauka.
    MAUDHUI
    Baadhi ya maudhui yanajitokeza katika hadithi hii ni kama vile:
    a) Elimu
    Hii ni hali ya mhusika kupata maarifa yanayonuiwa kumpevusha
    kimawazo. Kuna aina mbili kuu za elimu:
    i) Elimu ya Vitabu.
    Hii ni elimu ambayo wahusika huipata kwa kuhudhuria madarasa
    shuleni na kuelimishwa katika masomo mbalimbali. Baadhi ya
    masomo haya ni kama vile kemia, hisabati, bayolojia, Kiswahili,
    kingereza, na masomo mengine mengi mno. Elimu hii hutumika
    kuwasaidia wanafunzi kuingia katika taaluma mbalimbali kama
    vile udaktari, ualimu, uhandisi na kadhalika. Penina na Dennis
    wanakutana pale kwenye chuo kikuu wakiwa wanafunzi wa fasihi.
    Wanatafuta elimu hii ili kuwahi kupata ajira bora baadaye. Ni
    elimu hii ambayo Dennis anaitumia kutafuta kazi katika shirika la
    uchapishaji wa magazeti. Watu wote wanaoendelea na
    kufanikiwa kwenye elimu hii huishia kufaulu sana maishani katika
    kupata taaluma wanazozipenda wao wenyewe. Wanafunzi wote
    katika chuo kikuu wanatia bidii masomoni ili waweze kupata kazi
    za aina mbali mbali.
    19.
    ii) Elimu ya Maisha.
    Elimu hii haihisiani na elimu ya vitabu. Haya ni maadaili
    anayokuzwa nayo mtu. Ni mkusanyiko wa tabia na itikadi njema
    ambazo mja hukabidhiwa katika aushi yake ili kuweza
    kutangamana vyema na umma. Dennis alikuzwa vyema na
    kufundishwa kuwaheshimu watu. Isitoshe, ni mvulana aliye na
    tabia nzuri. Anapoenda chuo kikuu, hajihusishi na tabia
    zinazoelekeza kupotoka kwake kwa maadili. Anawaheshimu
    wote. Kwa upande mwingine, Penina amelelewa kwa kuwabagua
    watu kwa misingi ya pesa uchumi wao. Ni wazi kuwa muda wote
    huu, alikuwa ameyacha makucha yake tu.
    a) Mapenzi
    Mapenzi ni hali ya kumkubali mtu wa jinsia tofauti na kumuenzi
    pamoja na kujihusisha naye katika mahaba. Mapenzi
    yanayoonekana katika muktadha huu ni ya aina mbili:
    i) Mapenzi ya kifaraungo.
    Penina ndiye anadhihirisha mapenzi haya. Anampenda
    Dennis ingawa kwa masharti. Licha ya wao kuishi pamoja,
    anamwambia Dennis ya kwamba hawezi kuolewa na mtu
    asiye na pesa. Ni wazi kuwa mapenzi yake hayaamuliwi na
    uzuri wa penzi bali kiwango cha pesa alichonacho mtu. Punde
    tu penzi lao linapoguzwa na upepo mdogo tu (ukosefu wa
    ajira) linanyauka na kupotelea mbali.
    20.
    ii) Mapenzi ya dhati.
    Dennis anampenda Penina kwa keweli. Anaishia kumpenda
    na hata kumtambulisha kwa wazazi wao. Ingawa alikuwa
    anashuku ukweli wa Penina kumpenda maskini kama yeye,
    anajitolea na kumpenda Penina kwa dhati. Anatazamia
    kumuoa haswaa pindi atakapopata kazi.
    b) Utabaka
    Hii ni hali ya jamii kugawika katika makundi tofauti kulingana
    na uwezo wa kifedha. Mahusiano yote kati ya wahusika
    yanaongozwa na fedha walizo nazo mfukoni. Penina
    anaonywa na wazazi wake kujihusisha na Dennis kwani yeye ni
    maskini. Ingawa anakataa mawaidha ya wazazi wake hapo
    awali, anaishia kumfurusha Dennis kwani anamwona kama
    maskini asiyefaa kumwoa.
    c) Umaskini
    Msimulizi wa hadithi hii (Dennis) ndiye kielelezo cha maskini
    wanavyoishi. Alisoma kwa shida kwani karo ilikuwa kero
    kubwa. Ni wazi kwamba jamii yake inamtazamia yeye
    kuikomboa kutokana na umaskini wao. Ingawa amefaulu kuka
    chuoni, chumba chake Dennis ni kitupu kisichokuwa na chochote
    cha kutamaniwa. Anapohisi njaa, anagutukuka kuwa hana
    chochote cha kupika. Anaamua kupika uji. Baadaye
    anagundua kwamba hata sukari ya kutia kwene uji wake
    mweupe hana. Anaishia kunywa uji hiyo bure kwa kujihurumia.
    21.
    Ingawa Dennis anafaulu kumpata mpenzi anayempenda,
    anajitegemeza kwake kwa kiasi kikubwa. Wanaishi pamoja
    lakini ni wazaziwe Penina wanaowakimu mahitaji yao yote sio
    Denniskwani yeye ni maskini. Baadaye, Penina anapochoshwa
    na Dennis anamfurusha. Ni ajabu kuwa Dennis anabeba kila
    kilicho chake kwenye begi moja tu! Anatembea akijutia masomo
    yaake ambayo hadi sasa hayajamsaidia kustawisha misuli yake
    ya kiuchumi. Anashangaa jinsi ataweza kuwaokoa wazazi wake
    na umaskini uliowagubika.
    a) Ukosefu wa Ajira
    Ajira ni adimu katika nchi anayoishi Dennis. Ametembea katika
    makampuni mengi na mashirika mengi akipeleka nyaraka za
    kuomba kazi. Amebisha huku na kule akiwacha tawasifu yake
    na ya Penina lakini tangu kumaliza masomo ya chuo kikuu,
    miaka mitatu baadaye hajafaulu kupata kazi. Dennis anaishia
    kufurushwa na mpenziwe kwani hana uwezo wa kukimu mahitaji
    yao ya kifedha.
    a) Majuto
    Dennis anachorwa kama mhusika anayejutia maisha yake.
    Anajutia umaskini wake kwani Penina anamfurusha kwa
    kisingizio kuwa yeye hawezi kutoa hela zozote za chakula na
    matumizi ya pale nyumbani. Anajutia kisomo chake kwani
    anatumaini kuwa kitampa ajira lakini ng’o! Anajuta
    akiwakumbuka wazazi wake na kukiri jinsi ambavyo anaweza
    kuwasaidia ili kuwaondoa katika umaskini. Anajutia bidii yao ya
    kumsomesha kwani sasa hivi hawafai wazazi inavyostahili.
    22.
    Anajutia fumbo ya maisha kuwa kinyume naye katika kila
    jambo analofanya. Anajutia kuonewa na maisha.
    MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI.
    a) Tashihisi
    i) Ninafuta chozi linalochungulia machoni. (Uk 13)
    ii) Njaa inanitafuna kama mbwa anvyoguguna mfupa. (Uk 17)
    iii) Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa
    hatimaye. (Uk 20)
    iv) Mapenzi yasiyujua kufa. (Uk 20)
    v) …bado bahati yangu haijasimama. (Uk 22)
    b) Tashbihi
    i) …kumuibia bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama
    kutajaria kuyapata maziwa kutoka kwa kuku. (Uk 13)
    ii) …sasa anaanza kututamkia maneno machungu kama
    shubiri. (Uk 14)
    iii) Mapenzi ni matamu kama uki…(Uk 26)
    iv) Njaa inanitafuna kama mbwa anvyoguguna mfupa. (Uk 17)
    v) Almuradi maskini na matajiri wametengana kama ardhi na
    mbingu. (Uk 17)
    vi) Mwili mzima unaanza kutetemeka kama ndama
    aliyenyeshewa…(Uk 17)
    vii) Waamatunaapendana kama ulimi na mate. (Uk 21)
    viii) Wanafanana kama riale kwa ya pili. (Uk 23)
    ix) Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa… (Uk 25)
    23.
    a) Kuchanganya ndimi
    i) Wanabeba vipakatalishi na Ipad zao mikononi, sa kabisa!
    ii) Hatimaye nimeka kwenye ghorofa ya tatu katika jumba
    la makazi ya Mastura Hall. (Uk 16)
    iii) Mimi na Penina tunaishi katika mtaa wa New Zealand. (Uk
    22)
    iv) …basi ni wazi kuwa your competence is doubtful. (Uk 25)
    v) Unajua tangu nianze tarmacking sijawa nikitazama
    runinga. (Uk 26
    b) Nidaa
    i) Wanabeba vipakatalishi na Ipad zao mikononi, sa
    kabisa! (Uk 13)
    ii) Laiti mama yangu angeliweza kunisomesha hadi shule ya
    kitaifa! (Uk 13)
    iii) La hasha! (Uk 14)
    iv) Looh! Kwani swali langu vipi? (Uk 15)
    v) Lo! Nitakula nini? (uk 17) Lo! Mlangoni yuko msichana
    mmoja mrembo. (Uk 18)
    vii) Ah! Pengo gani ilhali una mapenzi ya kweli…? (Uk 19)
    a) Misemo na nahau.
    i) Nikatupa macho huku na kule. (Uk 12)
    ii) Analaza damu usiku na mchana. (Uk 14)
    iii) Licha ya uchechefu wa pesa, nimejikaza kisabuni. (Uk 21)
    iv) Mama na baba wanakula mwata. (Uk 28)
    v) Lakini sitakata tamaa. (Uk 28)
    24.
    a) Uzungumzi nafsia.
    Mbinu hii imetawala kote kwenye hadithi kwani haya ni
    masimulizi katika nafsi ya kwanza. Mifano michache ya mbinu hii
    ni kama:
    i) “Kwa nini ninalia sasa?” (Uk 13)
    b) Kinaya
    i) Unajua watu waliosoma sana kama Daktari Mabonga hawajui
    lolote wala chochote. (Uk 14)
    ii) Utajifundishaje kula na chakula hukitafuti? (Uk 15)
    iii) Masomo ya chuo kikuu si masomo, ni madubwana
    yasiyojulikana yalikotoka.(Uk 15)
    iv) Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi.
    Sina majibu. (Uk 25)
    c) Maswali ya Balagha.
    i) Itakuwaje wewe ufundishwe kujinadhishia kesho yako? (Uk 15)
    ii) Utajifundishaje kula na chakula hukitafuti? (Uk 15)
    iii) Lo! Nitakula nini? (uk 17)
    iv) Nifunge mlango au nifungue? (Uk 17)
    v) Mbona asiketi kitini?…kwani ni lipi alilojia humu? (Uk 18)
    vi) Kabwela kama mimi nina faida gani? (Uk 23)
    a) Chuku.
    i) Darasa zima linangua kicheko. Msichana mmoja amecheka
    hadi ameanguka. (Uk 15)
    ii) Mtazamo wake unaweza kumwamsha mbwa aliyelala. (Uk 18)
    iii) Ukimtazama machoni, machozi ya furaha hayaachi
    kukutonatona. (Uk 18)
    iv) …kitambo kirefu kilichatawaliwa na kimya- kimya cha
    kuanguka pamba uusikie mlio wake. (Uk 18)
    v) Wasikilizaji wako watacheka mpaka midomo ianguke. (Uk 22)
    vi) Akanyagapo chini ardhi inatetemeka. (Uk 22)
    25.
    a) Methali.
    i) Mzungu wa kula haufunzwi mwana. (Uk 15)
    ii) Ujapokosa la mama, hata la mbwa huamwa. (Uk17)
    iii) Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezi. (Uk 20)
    iv) Mume ni mume hata akiwa gume gume. (Uk 21)m
    v) Mgomba changaraweni, haupandwi ukamea. (Uk 27)
    WAHUSIKA NA UHUSIKA.
    1. Dennis (Msimulizi)
    Huyu ni mvulana aliyesoma kwa bidii licha ya umaskini wake na
    kuka chuo kikuu, ni mpenziwe Penina. Ana sifa zifuatazo:
    a) Mwenye bidii.
    Licha ya umaskini uliopo pale nyumbani, anatia bidii
    masomoni. Anasoma na kufanya vyema kuanzia shule ya
    msingi, shule ya upili hadi chuo kikuu. Pia ana bidii ya
    kutafuta kazi ili aweze kuwasaidia wazazi wake na pia
    kumwoa mpenzi wake Penina.
    b) Mwenye mapenzi.
    Anampenda Penina kwa dhati. Anamuenzi na kutaraji kuwa
    siku moja atamwoa Penina. Anamwonyesha kwa wazazi
    wake ambao wanafurahia sana kumwona mwanao akiwa na
    mpenzi akama Penina.
    26.
    a) Mwenye matumaini.
    Ana matumaini ya kupata kazi ndiposa anatia bidii
    masomoni. Anaahidi kumwoa Penina endapo angepata kazi
    ambayo ingemwezesha kukimu mahitaji yao. Ana matumaini
    kwamba ingawa hana kazi sasa hivi siku moja bahati
    itamfungulia milango na mambo kumwendea vyema
    akapata kazi nzuri.
    b) Ni mwoga.
    Anapopewa fursa ya kuzungumza katika udodosi wa kazi
    katika shirika la uchapishaji wa magazeti, anaogopa
    kufungua kinywa chake. Kijacho chembamba kinamtiririka
    huku akitetema na kukosa maneno. Anafurushwa kutoka
    chumba kile bila kutamka chochote.
    a) Mwenye majuto.
    Licha ya yeye kutia bidii maishani na masomoni, anajuta
    kwamba bahati inakataa kumfungulia milango ya heri. Anajuta
    kutokuwa na kazi kwani anafurushwa kutoka chumbani na
    mpenziwe. Pia anajutia kutowasaidia wazazi wake baada ya
    wao kumsomesha kwa shida mno. Anajuta kumwamini Penina na
    kukubali mapenzi yake ya kifaraungo.
    27.
    1. Penina
    Huyu ni mpenzi wa msimulizi ambaye walikutana kule chuo kikuu
    wakisoma katika darasa moja. Anampenda msimulizi na kuahidi
    kuoana naye watakapokuwa matajiri.
    a) Ni mzembe.
    Anaketi chumbani mchana kutwa bila kufanya kazi yoyote
    ile.Kazi ni kutazama televisheni tu. Tawasifu zake zinapelekwa
    maosini na Dennis. Hana bidii ya kutafuta kazi. Anaamini
    kuwa Dennis ndiye anafaa kutafuta hela.
    b) Mwenye unaki.
    Licha ya yeye kudai kumpenda msimulizi, ni wazi kuwa penzi
    lake ni la kifaraungo. Upendo wake unaongozwa na tamaa ya
    pesa na utajiri. Anajifanya kumpenda Dennis lakini ukweli ni
    kwamba alitazamia ya kwamba Dennia angepata kazi ili
    waweze kuoana.
    a) Mwenye tamaa.
    Tamaa yake ya pesa inadhihirika wakati ambapo utulivu wake
    unakia kikomo. Anamfurusha Dennis kwa umaskini wake.
    Anadai kuwa hawezi kuolewa naye kwani Dennis hana pesa.
    Anaweza tu kuolewa na mtu mwenye pesa.
    28.
    b) Mwenye mawazo ganda.
    Penina anaamini kuwa ni mwanaume tu ambaye anapaswa
    kutafuta hela. In
    gawa wote wawili wameelimika, Penina hana bidii ya
    kutafuta kazi. Anamwac hia jukum u hilo Dennis
    anayezunguka katika maosi mengi bila mafanikio.
    1. Daktari Mabonga.
    Ni mwalimu wa fasihi katika chuo kikuu cha Mavuko. Ni wazi
    kuwa yeye ni mwalimu asiyependa kudadisiwa kwa
    vyovyote vile. Ni chanzo cha namna ambavyo mafunzo
    yanatendeka katika vyuo vikuu.
    a) Mwenye hekima
    Anatema maneno yaliyojawa na hekima na maarifa
    anapozungumza na wanafunzi wake. Anawapa maarifa
    kuhusu maisha ambayo yanawasubiri baada ya masomo
    yao. Anawanoa wanafunzi wake vilivyo.
    b) Mwenye kiburi/mabezo.
    Licha ya yeye kufundisha vizuri wanafunzi wake
    hawamwelewi. Anatumia lugha ngumu inayowashangaza
    wanafunzi. Wanafunzi wake wanapomtaka atumie lugha
    nyepesi ili waweze kuelewa, anawajibu kwa kiburi na
    mabezo.
    c) Mwenye mapuuza.
    Anapuuza maswali anayoulizwa na wanafunzi wake na
    kuyaona ya kitoto. Anatupilia mbali maswali yote
    yanayoibuliwa na wanafunzi wake wa fasihi.
    29.
    1. Shakila
    Huyu ni msichana ambaye walisoma pamoja na Dennis kwenye
    chuo kikuu. Mamake ni mkurugenzi mkuu katika shirika la
    uchapishaji wa magazeti. Ametumiwa na mwandishi kuendeleza
    maudhui ya ubaguzi.
    a) Mwenye dharau.
    Anapomkuta Dennis osini akisubiri kufanyiwa udodosi,
    anazungumza naye kidogo na kisha kutoa cheko kubwa
    lenye dharau linalomkera Dennis. Hii ni ishara tosha kwa
    Dennis kwamba hatapata kazi yoyote pale.
    b) Mwenye unaki.
    Anapomkuta Dennis osini, anamsalimu na kumzungumzia
    vyema. Ajabu ni kwamba anapoingia oni kwa mhazili,
    anatoa cheko kubwa pamoja na mamake. Anamcheka
    Dennis bila shaka.
    2. Mamake Shakila.
    Mhusika huyu ametumiwa na mwandishi kama kielelezo cha watu
    wenye mitazamo hasi kwa wenzao, wenye mabezo na
    kujishaua. Ingawa ni mkurugenzi hana utu wa ukurugenzi. Sifa
    zake ni panmoja na:
    30.
    3. SHOGAKE DADA ANA NDEVU
    Historia ya Mwandishi.
    Mwandishi ni mojawapo ya waandishi chipukizi wenye uwezo wa
    kipekee wa kubuni kazi za fasihi. Ni mwalimu aliyewahi kuandika
    Makala mbalimbali ya Kiswahili. Isitoshe ana tajriba ya muda
    mrefu wa kufundisha Kiswahili katika shule mbali mbali.
    Dhamira
    Mwandishi wa hadithi hii amedhamiria kuwaonya vijana dhidi ya
    kujihusisha na mapenzi ya kiholela. Anawatahadharisha vijana
    kuhusu hatari za kushiriki mapenzi ovyo ovyo. Hatari hizi ni mimba
    za mapema pamoja na kukumbana na mauti wakati wa kuavya
    mimba.
    Ufupisho wa Hadithi
    Hadithi hii inawasawiri wazazi wawili ambao wamejukumika
    kuwalea wanao vyema. Bwana Masudi na Bi. Hamida
    wamejukumika vilivyo na kumlea binti na mwana wao kwa
    uangalifu mkubwa. Wamemfunza dini na tabia njema.
    Wanamlinganisha binti yao na wasichana wengine pale kijijini na
    kuwona bora zaidi kuwaliko. Jina la msichana huyo ni Saa.
    Saa anawaomba wazazi wake ruhusa ya kumleta shogake
    anayeitwa Kimwana ili waweze kusoma kwa pamoja. Wazazi wake
    Saa hawana pingamizi kwa ombi hilo kwani wanamtakia binti yao
    fanaka katika masomo yake na ikiwa kuna shogake ambaye
    wanaweza kufaana katika kudurusu, basi hawaoni tatizo lolote.
    Kimwana anakuja siku baada ya nyingine na kudurusu pamoja na
    Saa kwenye chumba chake Saa. Kila anapokuja, mama mtu
    anawaruhusu kujifungia chumbani ili nduguye Saa asiwasumbue
    wakiwa katika shughuli za kudurusu.
    Ajabu inayokuwepo ni kuwa wazazi wa Saa hawajawahi kumsikia
    huyo shogake Saa akizungumza. Ni “Marahaba” tu ndiyo
    inamtoka kila anapokuja kusoma pamoja na Saa na kisha
    wanaandamana na kujifungia kwenye chumba cha Saa ili
    kuendeleza masomo yao. Hakuna anayewasumbua, iwe ni mama,
    baba au ndugu, kwani wanahitaji muda wao wa kutosha ili kusoma
    ipasavyo! Wazazi hawamwoni Kimwana kuwa na ila yoyote ile.
    31
    Baada ya miezi sita hivi, tatizo linaingia. Mama saa anaanza
    kuona mabadiliko katika mwili wa bintiye. Habaini ikiwa ni mawazo
    yake tu ama ni kweli kwamba mambo yalikuwa yakitendeka.
    Anapomdadisi bintiye, Saa anakana kuwepo kwa jambo lolote lile
    lenye utofauti katika mwili wake. Ila mamake anatambua ya
    kwamba kuna jambo. Lakini ushahidi atautoa wapi vile? Hajui.
    Anatulia tuli ila moyoni anasalia na done chungu la tuhuma kwa
    bintiye. Anapomuuliza babake Saa, mume anamzomea na
    kumhujumu kwa kumtuhumu bintiye.
    Siku ya siri kujulikana inapowadia, wanakuwa wameketi baba,
    mama na ndugu mdogo wa Saa. Ndugu anamweleza mamake jinsi
    ambavyo yeye na rakiye walikuwa wakicheza. Walicheza mchezo
    wa kujicha. Ila alipatikana kila mahala alipojaribu kujicha.
    Ndipo Lulua akaamua kujaribu kujicha katika chumba cha
    dadake. Akafungua mlango na kuona aliyoyaona. Aliwapata Saa
    na shogake wamelala kitandani. Walikuwa wamelala lakini huyo
    shogake ambaye muda wote huvalia buibui na kudhaniwa ni
    mwanamke, alikuwa na ndevu. Mama anagutuka na kudhihirisha
    tuhuma zake za siku nyingi.
    Kwa sadfa wakati huo, simu inalia. Baba Saa anapojibu, huyo
    anayempigia simu anampa habari zinazomkata maini. Saa
    amekuwa maiti. Saa anakuwa kaaga baada ya kujaribu kuavya
    mimba. Sasa inabainika wazi kwamba yule Kimwana
    anayeruhusiwa na wazazi wa Saa kuja kusomea hapo nyumbani
    pamoja na Saa hakuwa mwanamke, bali mwanamume
    anayejihusisha kimapenzi na Saa, mapenzi ya siri yanayoishia
    kumsha saa.
    32.
    MAUDHUI
    Maundhui mengi yameangaziwa katika hadithi yakiwemo:
    a) Unaki
    Saa ni msichana anayeaminika kwa wazazi wake. Wazazi
    wake wanajiamini wakijua kwamba binti yao ameshika
    maadili mema ya jamii. Isitoshe, anakuwa kajiweka na
    kuwekeka vyema. Anakuwa msichana mwenye tabia na
    heshima zake. Saa anapowaomba ruhusa ya kumleta raki
    yake pale nyumbani kwa madhumuni ya masomo, hakuna
    anayeshuku. Ajabu ni kwamba Saa anawadanganya
    wazazi wake. Yule anayedhaniwa kuwa msichana alikuwa
    mwanamume mwenye ndevu ambaye wanalala pamoja kule
    chumbani muda wote ule wanaodhaniwa wanasoma.
    Matokeo ya siri hiyo ni mimba ya mapema inayoishia
    kumkatizia saa masomo yake na pia kumletea mauti. Huu ni
    unaki wa hali ya juu.
    b) Majuto
    Wazazi wa Saa wanajuta kumruhusu binti yao kumleta
    mgeni nyumbani kwao kwa madhumuni ya kusoma, jambo
    ambalo halikutendeka hivyo. Badala ya kusoma, Saa
    anajihusisha kimapenzi na Kimwana na kwenda kinyume na
    maadili aliyofunzwa na wazazi wake.
    Ni wazi kwamba Saa pia anajutia vitendo vyake.
    Anapozungumza na mamake, anaonekana kuwa mwingi wa
    haya kwa kujutia vitendo vyake. Ni fedheha hiyo
    inayomwelekeza kutaka kuavya mimba, jambo ambalo
    linamwangamiza.
    33.
    c) Malezi
    Bwana Masudi na Bi. Hamida wamejukumika kumlea binti na
    mwana wao kwa uangalifu mkubwa. Wanamkuza Saa na
    kumpanda katika maadili. Wanamfundisha akujiwelka vizuri kama
    mtto wa kike. Wanampa ushauri mwema utakaomfaa maishani.
    Isitoshe elimu ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwao.
    Wanahakikisha kuwa wamemwelimisha binti yao. Ni furaha na
    shauku ya wazazi hawa kushuhudia saa akipaa na kuendelea
    masomoni. Wanapomwona akiwa na raki anayeweza kumsaidia
    kuimarika masomoni, wanampa nafasi yao kusoma kwa makini bila
    kusumbuliwa hata kidogo. Wanamruhusu Saa kujifungia
    chumbani na rakiye ili waweze kusoma kwa pamoja. Haya ni
    malezi mema kwa watoto hawa.
    a) Mapuuza
    Wazazi wake Saa wana mapuuza. Wanapoambiwa ya
    kwamba Saa na Kimwana wanasoma huko chumbani
    walikojifungia, wanaamini tu. Hakuna yeyote anayeshuku
    ikiwa ni uwongo. Hata hawashangai ni kwa nini shoga huyu
    Kimwana hapendi kuketi sebuleni au hata kuzungumza nao.
    Wazazi hawa wanafungia macho uwezekano wa Kimwana
    kuwa samba anayevamia zizi la kondoo.
    Kando na hapo, hakuna aliyewahi kujaribu kudhibitisha
    ukweli wa vijana hawa wawili kusomea chumbani. Wazazi
    h a wa wa n a p o a m b i wa n i m a s o m o ya n ayo k u wa
    yakiendelea, hawatilii shaka ukweli huo bali wanaamini
    moja kwa moja. Haya ni mapuuza ya hali ya juu. Mapuuza
    ya wazazi hawa yanaishia kumuangamiza Saa kwani
    anaaga baada ya kujaribu kuavya mimba.
    34.
    b) Mapenzi
    Kuna aina mbili za mapenzi yaliyoangaziwa karika hadithi hii:
    i) Mapenzi ya dhati.
    ii) Mapenzi ya uwongo.i)
    Mapenzi ya dhati.
    Haya ni mapenzi ya kweli kati ya wahusika. Mapenzi haya
    yanaweza kuwa kati ya ndugu wawili au kati ya mzazi na
    mwanawe au kati ya wahusika wawili wenye jinsia tofauti. Bwana
    Masudi na Bi. Hamida wanampenda binti yao. Upendo huu
    unadhihirika kwa namna ambavyo wanamlea kwa makini.
    Wanahakikisha kwamba binti huyu amekuzwa kwa maadili mema,
    amefundishwa kujiweka sawasawa. Akilinganishwa na wasichana
    wengine pale mataani, hakuna msichana wa kifuu chake. Huu ni
    upendo wa kweli. Isitoshe, wazazi hawa wanadhamini masomo ya
    binti huyu na kumpa msaada wotote kadri ya uwezo wao.
    Wanamtakia Saa mema maishani.
    Bwana Masudi na Bi. Hamida wanapendana kwa dhati. Hawa ni
    wazazi wawili wenye mapenzi ya dhati kati yao. Wanazungumza
    mambo mazito na ya ndani kila jioni wakisubiri usingizi uwachukue.
    Wao huzungumza mambo yote yaliyopo ndani ya nafsi zao. Haya
    ni mapenzi ya dhati.
    35.
    ii) Mapenzi ya uwongo.
    Mapenzi haya ni yale ambayo huibuka tu kwa mshawasho wa
    ujana na tamaa za mwili. Mapenzi haya yamejitokeza katika
    uhusiano uliopo kati ya Saa na Kimwana. Matokeo yake ni
    mimba haram u ambayo inamtia Saa mashakani.
    Wanapojaribu kuitoa wanamletea Saa mauti. Waama,
    mapenzi haya huwaletea wahusika majuto.
    a) Elimu.
    Elimu ya vitabu ni muhimu kwa maisha ya baadaye. Saa
    anahimizwa kutia bidii masomoni ili aweze kupata nafasi katika
    shule ya upili. Wazazi wake Saa, Bwana Masudi na Bi.Hamida
    wanamsaidia binti yao kwa lolote atakalo mradi tu apite
    mtihani huo wa shule ya upili. Katika kumsaidia Saa kupita
    mtihani, wanamruhusu kumwalika rakiye ambaye anamsaidia
    katika masomo yake. Wanasaidiana ili wote wawahi kupita
    mitihani yao na kuelekea katika shule za upili.
    MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI.
    a) Majazi
    i) Bwana Masudiii)
    Kimwana- Hili ni jina ambalo linapendekeza jinsia ya mtu
    huyu anayedhaniwa kuwa mwanamke. Yeye ni Mwana
    (MVULANA) bali sio msichana.
    iii) Saa- jina hili linapendekeza kuwa mhusika huyu ni sa wa
    tabia. Ni kweli kwamba yeye ni sa lakini mwisho tu ndio anatia
    doa hulka yake.
    iv) Lulua- hiki ni kitu cha thamani mno. Mwana huyu anapendwa
    mno na wazazi wake.
    36.
    b) Tashihisi
    i) …wanapokuwa kitandani wakingojea usingizi mtamu
    uwachukue.. (Uk 29)
    c) Maswali ya balagha
    i) Wangapi wanaozaa watoto wazuri kama au kuliko Saa
    wetu. Na watoto hao hutokezea kuwa na balaa tupu? (Uk 29)
    ii) Ya nini ushungi huo? (Uk 31)
    iii) Si hubaki humo mpaka wamalize kusoma na kujadiliana? (Uk
    32)
    iv) Itakuwaje waamini kila kitu anachesema Saa? (Uk 32)
    v) Kweli? Uongo? Kweli au uongo yale maneno ya binti yake?
    a) Nidaa
    i) …lakini matendo yake afadhali ya mbwa, tena mbwa koko!
    (Uk 29)
    ii) Saa mama, umo ndani mwenu ‘vyo! (Uk 31)
    b) Methali
    i) Lisemwali lipo, kama halipo linakuja. (Uk 30)
    ii) Siri ya kata iulize mtungi. (Uk 30)
    iii) Kidole kimoja hakivunji chawa. (Uk 31)
    c) Tanakuzi
    i) Saa halindwi, hujilinda yeye mwenyewe. (Uk 31)
    d) Taharuki
    i) Ni kwa nini Kimwana alijifunika buibui?
    ii) Ni kwa nini Kimwana hakuzungumza mambo yoyote?
    iii) Mbona Kimwana na Saa walijifungia mle ndani kwenye
    chumba? (Uk 32)
    37.
    e) Mdokezo
    i) Tena haishi kutapikatapika… (Uk 33)
    ii) Pamoja na kujilinda kwangu… (Uk 33)
    iii) Kumbe mlango haukufungwa… (Uk 34)
    iv) Ameshakufa…ameshakufa… (Uk 35)
    f) Kinaya
    g) Mfano mzuri mpaka leo ni kwamba wao wazazi hawajapata
    hata neno lake, ila “Shikamoo” inayotoka midomoni nyuma ya
    buibui kama kata ya maji mtungini. Ni ajabu kuwa wazazi wa
    Saa hawajui ni nani anahusiana na binti yao.
    a) Misemo na nahau
    i) Kwa hivyo watakuwa wanaongozana na kuzibana nyufa…(Uk
    31)
    b) Tashibihi.
    i) …ila “Shikamoo” inayotoka midomoni nyuma ya buibui kama
    kata ya maji mtungini.
    c) Takriri.
    i) Juzi…juzi… (Uk 34)
    ii) shogake…shogake…(Uk 35)
    iii) Ameshakufa…ameshakufa…(Uk 35)
    WAHUSIKA NA UHUSIKA.
    1. Saa
    Huyu ni msichana mdogo aliye katika shule ya msingi. Ni bintiye
    Bwana Masudi na Bi.Hamida. Anatarajia kujiunga na shule ya upili
    hivi karibuni ikiwa atapita mtihani wake wa shule ya msingi. Sifa
    zake ni pamoja na:
    38.
    a) Ni msiri
    Anafaulu kumcha raki yake wa kiume na kumvisha buibui
    ili kuwapumbaza wazazi wake kumdhania kimwana kuwa
    mwanamke. Wanaendelea na mchezo wao kwa siku nyingi
    hadi Saa anaishia kupata mimba. Isitoshe, anacha mimba
    yenye na kuikana mamake anapomdadisi ikiwa kuna jambo
    lolote mbaya limemtendekea. Anacha mimba yake na
    kujaribu kuiavya. Hapo tu ndipo wanazi wanabaini
    yaliyokuwa yakiendelea kwa muda wote huu.
    b) Mwenye Unaki
    Anawadanganya wazazi wake kwamba anasoma pamoja
    na rakiye wa kike ilhali Kimwana ni mvulana.
    Wanadanganya kwamba wanasoma ilhali ni mapenzi
    yanaendelea kule chumbani mwa Saa. Huu ni unaki wa
    hali ya juu.
    a) Msaliti
    Saa anasaliti uaminifu ambao wazazi wake walikuwa nao
    kwake. Wanamwamini wakijua yeye anasoma ilhali wakati
    huo, yuko kwenye mahaba ya Kimwana.
    b) Ni mwenye bidii.
    Anapokuwa nyumbani yeye hufagia, hupika, huosha
    vyombo, hufua, hupiga pasi na kutandika kila siku.
    c) Mwerevu.
    Katika kila mtihani, Saa aliibuka wa kwanza kabisa katika
    darasa. (Uk 30)
    39.
    1. Kimwana
    a) Mwongo
    Anajifunika buibui na kujifanya kama mtu wa jinsia ya kike.
    Kwa uwongo huu, anafaulu kuingia nyumbani kwa Saa na
    kuandamana naye hadi chumbani mwake wanakodhaniwa
    wanaendelea masomo.
    b) Mwenye unaki
    Katika mawazo ya wazazi wa Saa, Kimwana ni msichana
    ambaye ni raki ya Saa. Wanadhaniwa kusaidiana katika
    kudurusu kazi ya shuleni. Ajabu ni kwamba Kimwana ni simba
    anyemnyemelea kondoo na kumla mzima mzima akiwa zizini.
    2. Bwana Masudi
    a) Mwenye mapenzi.
    Anampenda mkewe na watoto wake. Ni baba mwenye
    upendo.
    b) Mwenye Bidii.
    Anajibidiisha kuhakikisha kuwa jamii yake inaishi vyema.
    Isitoshe anajibidiisha kumuelimisha Saa.
    a) Mwenye mapuuza.
    Anapoelezewa kuhusu mabadiliko yanayotokea kwa
    bintiye, anakana na kuyatupilia mbali.
    40.
    1. Bi. Hamida
    a) Mwenye mapenzi.
    Anampenda mumewe kiasi cha kumfungulia moyo wake
    wote. Isitoshe anawaenzi watoto wake na kuwapenda
    mno. Anamtakia Saa mema na hivyo kumfunza maadili
    mema.
    b) Mdadisi.
    Umakini wake unamfanya kugundua kuwa kuna jambo
    baya na bintiye. Anagundua kuwa bintiye ana tatizo na
    umbo lake limeanza kubadilika kwa kiwango fulani.
    Udadisi wake ndio unamuelekeza kugutukia hali mpya
    ya bintiye.
    1. Lulua
    a) Ni mkweli.
    Anapoulizwa maswali kuhusu dadake, anasema ukweli wote
    bila kucha chochote, jambo linalowapa mwangaza wazazi
    wake kuhusu tabia za dadake saa.
    4. SHIBE ITATUMALIZA
    Historia ya Mwandishi.
    Mwandishi ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Tanzania. Ni msomi na
    mwalimu wa Kiswahili. Amechangia pakubwa katika Isimu na
    lugha.
    Dhamira
    Mwandishi amedhamiria kuwaonya hasaa mataifa ya Afrika
    kuhusu tabia za ula na uroho.
    41.
    Ufupisho wa Hadithi
    Sasa na Mbura ni watoto wa mwanasiasa, Mzee Mambo. Mzee
    Mambo anawaandaa wanawe kuingia katika harakati za
    unyonyaji wa mali ya umma katika nchi husika. Anawataka wanawe
    pia waingie katika siasa na wizi wa mali ya umma.
    Baada ya uteuzi, sherehe zinaandaliwa za kufana ili kusherehekea
    ufanisi wa wanasiasa. Sherehe zinaandaliwa na matangazo yake
    kupeperushwa kwenye runinga. Watu wote nchini wanashuhudia
    jinsi ambapo wanasiasa wanasherehekea. Magari ya kifahari
    yanatumiwa na wanasiasa ili kujishaua na kuonyesha fahari ya
    wanasiasa.
    Kisadfa, wakati huo huo wa sherehe, wanasiasa wakiwa kwenye
    sherehe wakila, wananchi hawana chakula. Wananchi hawana
    dawa hospitalini. Pia kuna uhaba wa chakula. Wanasiasa
    wanafurahia shibe, ilhali wananchi wanateseka na kuumia kwa
    kukosa mahitaji ya kimsingi. Wanasiasa wanapeana makandarasi
    kwa kujuana
    .
    Katika sherehe, inadhihirika kuwa Dj alipewa kandarasi kuuza
    dawa ambazo zilistahili kuwasaidia wananchi. Dawa ambazo
    zilistahili kupewa wananchi zinafujwa na kupewa Dj ili aziuze.
    MAUDHUI
    a) Uongozi mbaya
    Uongozi mbaya unapelekea wananc hi kukosa huduma
    wanazostahili. Umma hauna dawa kwani viongozi wamejinyakulia
    madawa ambayo yanapaswa kuwa kwenye hospitali za umma na
    kisha kuwapa watu binafsi wanaojifaidi kama vile Dj (Uk 43).
    42.
    a) Ubinafsi na tamaa.
    Dj ananyakua dawa za wagonjwa na kuziweka kwenye duka lake
    mwenyewe, kuuza na kujifaidi huku mamia ya watu wengine
    wakiumia kwa kukosa dawa hizo.
    b) Usadi
    Sasa na Mbura ni watoto wa mwanasiasa, Mzee Mambo, na
    hawakustahili kupewa kazi yoyote kwenye serikali. Ajabu ni
    kwamba wanapewa nyadhifa ili kusimamia Mipango na
    Mipangilio. Nyadhifa hizi haziwafai hata kidogo kwani hakuna
    kazi yoyote wanayotekeleza. Isitoshe, Dj na wenzake wanavuna
    mabilioni ya pesa kwenye sherehe kwa njia za udanganyifu.
    MBINU ZA LUGHA NA UANDISHI.
    a) Mdokezo
    i)…hata yeye mwenyewe hujikuta kimya kimya huku akisema
    nafsini mwake…(Uk 36)
    ii) Kwenye kioo cha taifa, fesibuku, gazeti la… (Uk 45)
    b) Methali
    i) Wajinga Ndio waliwao. (Uk 37)
    c) Utohozi – haya ni maneno yaliyoswahilishwa.
    i) Fesibuku (Uk 38)
    ii) Wasapu (Uk 38)
    iii) TV (Uk 38)
    iv) Monokotilidoni (Uk 43)
    v) Kwenye kioo cha taifa, fesibuku, gazeti la… (Uk
    45)
    vi) …mabomu, presha, obesity, sukari, …(Uk 44)
    d) Tashibihi
    i) …matumbo yao matupu yalishindana kunguruma kama
    radi. (Uk 39)
    43.
    e) Misemo na nahau
    I) Magari yanapina vikumbo kuingia na kutoka kwa Mzee
    mambo. (Uk 38)
    a) Tashihisi
    i) Jingine linamimina jamaa na mzee Mambo shereheni. (Uk
    39)
    ii) Njaa inawatafuna. (Uk 39)
    iii) Upepo unawapuliza na kuwabembeleza… (Uk 41)
    iv) Swali nalo linagoma kupuuzwa namna hii. (Uk 41)
    b) Tanakuzi
    i) Vyakula vyeupe. Vya rangi. Vitamu. Vikali. Vichachu.
    Baridi. Haya tu. (Uk 39)
    c) Matumizi ya mashairi
    i) Shairi 1- Uk 43- Shairi hili ni la kuwagutusha wanasiasa
    wanaolala. Ni shairi linalokusudia kuwazindua wanasiasa na
    kuwagutua wawe watu wa kujukumika.
    d) Matumizi ya nyimbo
    i) wimbo wa kwanza-Uk 37. Wimbo huu unatumika
    kuwaponza wahusika Sasa na Mbura ili kuwagutusha na
    kwamba Mola aliyewapa wao mali anaweza pia akawapa
    wengine.
    Wimbo wa pili- Uk 43. Wimbo huu ni jibu kwa ule wimbo wa
    kwanza. Viongozi dhalimu wanawajibu wananc hi
    wakiwaambia wananchi kwamba hawajali wala kubali
    lawama zozote zile wanazopewa.
    a) Takriri
    I) Kunywa na kunywa na kunywa tena.
    ii) Huiga kwa jamii. Huiga…huiga. (Uk 40)
    44.
    WAHUSIKA NA UHUSIKA.
    Wahusika wakuu katika hadithi hii ni wawili: Sasa na Mbura. Sifa
    zao zinafanana. Sifa hizi ni pamoja na:
    a) Ni wala.
    Wanapohudhuria sherehe, kazi yao ni kula na kula tu bila
    kujalli. Wanatunga foleni mara tatu tatu na kujaza vyakula
    kwenye masahani yao hadi pomoni. Wanakula na kumaliza
    vyakula vyote vilivyojaa kwenye masahani yao hadi pomoni
    .
    b) Ni sadi.
    Wamepokea kazi katika asi za serikali. Wanapewa
    nyadhifa za mipango na mipangilio kama wakuu lakini
    wanaishia kutofanya lolote. Kazi zenyewe hawakuzipata
    kwa njia halali. Ulikuwa ni usadi uliowaingiza katika osi
    hizo.
    c) Ni wazembe.
    Baada ya kula sahani tatu tatu za vyakula kwenye sherehe,
    wanalala usingizi mzito badala ya kwenda kazini.
    5. MAME BAKARI
    Mohammed Khelaf Ghassany ni mzaliwa wa Zanzibar ambaye ni
    mshauri na mwandishi wa hadithi fupi. Kwa sasa ni mwanahabari
    katika idhaa ya Kiswahili ya Redio Welle Ujerumani.Sena ni
    mwanafunzi,alibakwa akitoka masomo ya ziada.Kitendo hiki
    kinamsababishia uchungu moyoni,ukiwa na unyonge.Mara
    anaamua kubadilisha mtazamo wake kuhusu maisha .Anaamua
    kukabiliana na dunia,anaamua kutolia tena wala kujilaumu
    tena.Lazima maisha yaendelee .Anaamua kutoavya mimba
    ,kutojiua na hata kutokimbia pao.Ujasiri huu unamwelekeza
    kumfunulia moyo wake rakiye Sarina.Sarina anaahidi kumsaidia
    kubeba mzigo ule.Waliamua kuucha ujauzito chini ya
    Jilbabu(vazi pana linalifunika mwili ili kuweka heshima).Waliamua
    pia kuwa sehemu ya kujifungulia kuwa shamba kwa wazazi wake
    Sarina.
    45.
    Beluwa dadake Sarina alimhudumia Sara nyumbani ili kucha
    siri.Hatimaye anawaeleza wazazi wa Sara yaliyompata
    Sara.Wanapokutana pale hospitalini Sara anashtuka kwani
    hakutarajia kuwapata wazazi wake pale na zaidi ya
    hayo,alishtushwa na utu wa mapenzi waliyodhihirisha wazazi
    wake.Mimba ya Sara inaishia kuwa jambo la kawaida kwenye
    nyumba yao na mipango yote ya awali ikawa haina maana tena.
    Sara anajifungua mtoto wa kike ambaye alikuwa Mke wa babake
    mpya.Sara bado ana nia ya kulipiza kisasi kwa huyu mbakaji.Akiwa
    kwao anasikia ghasia na fujo huko nje.Ina sadfu kuwa fujo hiyo
    ilihusiana na Yule mbakaji.Alikuwa amelala huku anataka kutapia
    roho yake iliyokaribia kumtoka kutokana na kichapo alichokuwa
    amepata.Anapigwa kwa mvua ya matufali hadi anafariki.
    DHAMIRA
    a) Mwandishi anakusudia kukashifu tabia ya wazazi ya
    kuwadidimiza wanao na kutowaelewa.Inafanya watoto
    waogope sana wazazi wao na wanashindwa kuwaambia
    wanayopitia.
    b) Mwandishi alidhamiria kuonyesha umuhimu wa kuwajibika
    kazini.fano: Alivyowajibika Sakina na hatimaye anasaidia
    kupatanisha Sara na wazazi wake.
    c) Mwandishi alikusudia kukashifu tabia ya ubakaji kwa
    kuonyesha athari zinazotokana na tabia hii.
    d) Mwandishi pia alikusudia kukashifu taasubi ya kiume
    katika jamii
    WAHUSIKA:
    Baba Sara
    Katili
    Kulingana na Sara,babake angemchinja na kumlaumu kwa kubakwa.
    Hangemwamini Sara.Badala angemdidimiza zaidi pia
    angemfukuza toka nyumbani.
    a) Mkali
    Ni kutokana na kuwa mkali ndio sababu Sara anashindwa
    kumweleza kilichompata.
    46.
    Mama Sara
    Dhaifu/mnyonge
    Hawezi kujitetea mbele ya mumewe. Hawezi kutetea bintiye.Ni
    dhaifu kwa sababu ni mwanamke.
    Sara
    Mnyonge/dhaifu
    Baada ya kubakwa na kupata ujauzito aliishi kulia.Hakuwa na
    njia ya kujitetea .Aliamua kulia tu.
    Mwenye kisasi
    Hakuweza kumsamehe yule mbakaji,alitaka kulipiza kisasi.Hata
    baada ya kupata mtoto wake Sara bado alitamani kulipiza.
    Msiri
    Anaamua kutomwambia yeyote kuhusu kubakwa na hata kuhusu
    ujauzito wake.
    Mwenye Imani
    Alikuwa na imani na raki yake Sarina.Aliamini kuwa Sarina
    angemsaidia katika hali hii ngumu. Mtani
    Anamtania Sarina kuwa ni zamu yake kubakwa.
    Mcha mungu
    Tokea hapo awali alijulikana kama mcha mungu.Hata kuvalia
    jilbabu halikuwa jambo la kushangaza.
    BELUWA.
    Amewajibika ;
    Yeye ni mlezi wa Sakina .Pia anaahidi kumpa kila msaada
    uliohitajika kuhusu ujauzito.
    Mshauri mwema
    Alimshauri Sara aende hospitalini ujauzito ulipotimia miezi sita
    kwani vipimo vya sasa vingelishirikisha mambo mengine ambayo
    hayangeweza kufanyika nyumbani.
    Ni Mpatanishi
    Anawapatanisha Sara na wazazi wake.Baadaye wanakuwa na
    uhusiano mzuri .Ujauzito uliokuwa mzito Sara unakuwa mwepesi.
    Jasiri
    Anawaelezea wazazi wa Sara kuhusu ujauzito wa Sara na
    anapanga kuwakutanisha Sara na wazazi wake pale hospitalini.
    47.
    .MAJIRANI.
    i.Ni wadaku.
    Walikuwa wameanza kumsema Sara walipojua kuhusu ujauzito
    wake.
    MBINU ZA UANDISHI
    1. Mbinu Rejeshi(kisengere nyuma).
    Mwandishi hurudi nyuma na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa
    kimetendeka kabla ya alichokuwa(ashback).
    a)UK 47..Aliendelea kuliona lile janadume asilolijua likimvamia na
    kumbaka ghaa.Kisha likambamiza ardhini na ardhi ikashuhudia
    ukatili na udhalimu ule.
    b)UK 47…Anakumbuka vyema siku ile….ilikuwa ni jumatano moja
    ya bahali mbaya kwake majira ya saa tatu unusu usiku,akirudi
    darasani.
    2)Takriri
    Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili
    kusisitiza ujumbe fulani(Repetition). UK 47
    a).Anaona alivyokuwa akigeuzwa kushoto na kulia,kulia na
    kushoto.
    b).UK 46 Ndiyo mbo yake,mbo yamnyonge na mnyonge ni
    yeye sasa.
    c).UK 49-50 Nimekosa
    nini? Nini? Nini hasa?
    d).UK 49 Dunia we dunia,Dunia na mwenye nguvu.
    3Tashihisi/Uhuishaji(pensonication)
    Ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye
    uhai(sifa za kibinadamu). (UK 47)
    48.
    a).UK 47….Kisha likambamiza ardhini na ardhi
    ikashuhudia ukatili na udhalimu ule
    b).UK 48….Bwana Yule mwenye masikio makaidi
    c)UK 50……Kioo hakikumpa makini kamwe.
    d)UK 50…. Akili imehama chumbani mwake.
    Inaranda huku na huko kutafuta la kufanya.
    e)UK 50…. Kila wazo likatangaza suluhisho mwafaka.
    f)UK 53…. Kilio kikachukua nafasi.
    4.Taswira
    Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali/jambo
    fulani kwa msomaji.
    a). UK 47…Kisha likambamiza ardhi na ardhi ikashuhudia ukatili
    na udhalimu ule.
    b) UK 47…..Anaona alivyokuwa akigeuzwa kushoto na kulia,kulia
    na kushoto kama mdungo wa mshikaki juu ya tanuri la makaa.
    5. TASHBIHI
    a). UK 47…Anaona alivyokuwa akigeuzwa kushoto na kulia, Julia
    na kushoto kama mdungo wa mshikaki juu ya tanuri la
    makaa.
    b). UK 52…Waliubeba kishujaa hata wakauhisi mwepesi kama
    vunge la pamba.
    c). UK 49…Kutengwa kama mgonjwa wa ukoma.Waliubeba
    kishujaa hata wakauhisi mwepesi kama vunge la pamba.
    d). Sara anabadilika kutoka msichana na kuwa mama.
    e). Jina lake Sara linabadilika na kuwa mama Sara.
    f). Baba aliyekuwa mkali anabadilika.
    g). Uhusiano kati ya baba na mamake anabadilika na kuwa mzuri.
    49.
    6 MASWALI BALAGHA.
    Maswali yasiyotarajia kujibiwa.
    a).UK 49-50
    Udhaifu na unyonge si ndio maana ya uanauke? Si ndio
    unaotumiwa kutimiza unyama wao?Nimekosa nini? Nini?
    Nini
    hasa? Kipi kipya kilichotokea?
    7. Ritifaa.
    Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo)kana
    kwamba yuko pamoja nawe.
    UK 51…Sitakuua mwanangu kamwe,alikiahidi kijanacho.
    8. Jazanda.
    Matumizi ya maneno yenye maana che.
    a).UK 47….Muhuzi mpya(ule ujauzito)
    b)UK 47…Ukanda wa picha
    c)UK 48…Ukurasa(maisha mpya)
    9. UZUNGUMZI NAFSI.
    Mhusika hujizungumzia,ama kwa kuongea au kuwaza,bila
    kukusudia kusikika na yeyote.
    a). UK 47….Aaa,maskini Sara miye,maisha yangu ndiyo
    yameshakunjwa hivi! Alijiambia kimoyomoyo.
    b).UK 49…Lakini kwa nini?na kwa nini hasa? Sena
    aliendelea
    kujiuliza ilivyopasa.Je!Nimetendewa hayo kwa sababu
    ya
    udhalifu wangu.
    10.SADFA.
    Ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba
    vilikuwa vimepangwa,japo havikuwa vimepangwa. (coincidence)
    50.
    UK 51…Shauri la usiniuwe la Abdulaif Abdalla ambalo Sena
    alikuwa amelisoma siku mbili kabla ya mkasa huo kusudia
    kilichompata Sena;ule ubakaji na kushika ujauzito.
    UK 54….Wakati Sena alipokuwa akikiri atakavyo mwadhibu
    baba wa mtoto wake? Ilisadifu kuwa wakati huo kukawa na ghasia
    pale nje kwao.Ikawa aliyekuwa akipigwa na watu alikuwa ni Yule
    mbakaji.Hatimaye akafa.
    UK 52…Wakati Sena alipata ujauzito,kisadfa,babake akaanza
    kumwita mama Sena.
    Chuku:Kutilia chumvi.
    UK 47…Hadi sasa pua yake imejaa ile harufu kali ya kutuzi
    iliyompa kipalizi na kumkolizo.
    MAUDHUI.
    Mabadiliko.
    1. UK 46…kuna mabadiliko katika mwili wa Sara… Sara
    alishtuka wakati mkono wake uligusa tumbo lake, alihisi
    mabadiliko ya kitumbo chake kilichokwishaanza kufura.
    2. UK 50…Baada ya Sara kulia kwa muda mrefu, alitambua
    kuwa kilio chake hakikumsaidia .Anaamua kutulia tena ,
    kutojijutia na kutojilaumu tena.Anaamua kutafuta suluhisho la
    tatizo lake kwa kuikabili dunia moja kwa moja.
    3. Ujauzito uliokuwa mzigo mzito kwa Sara unabadilika na
    kuwa mwepesi baada ya Sara kumweleza Sarina.
    Ukatili
    Ukatili ni kule kukosa utu /ubinadamu.
    Lile janadume lililombaka Sara halina utu .Halikuwa na
    huruma lilimkabamiza ardhini kwa ukatili na udhalimu (uk
    47). Pia ni ukatili kwa jamii kumlaumu na kumtenda
    aliyebakwa badala ya kumhurumia.
    51.
    ELIMU
    Elimu imetiliwa maanani katika jamii hii na ndio sababu kuna
    mpango wa masomo ya ziada ..twisheni.
    NAFASI YA MWANAMKE.
    a) Mwanamke anaishi katika ndoa ambapo hajui kujitetea nafsi
    yake mbele ya mumewe kutokana na udhaifu wake.
    b) Kama aliyewakulaumiwa kila kulipokuwa na visa vya
    ubakaji.Yeye alionekana kuwa ndiye shetani.Kama chombo
    cha kutimiza uchu wa mwanaume,kama aliyetumiwa kutimiza
    unyama wa wanaume.Mwanamke ametengwa kutokana na
    kosa la mwanamume.Baada ya kubakwa na kupata
    ujauzito,mwanamke anatengwa shuleni,nyumbani na kila
    mtu.
    MAJUTO.
    Sara alipobakwa hakumweleza yeyote kilichomfanyikia.Alienda
    nyumbani na kukoga.Baadaye akawa anajuta kwa nini hakutoa
    taarifa kuhusu kubakwa na kwa nini akakoga.
    UNYONGE/UDHAIFU.
    Sara alipobakwa alijawa na unyonge na ukiwa.Ni mnyonge kwa
    sababu hata baada ya kubakwa hangepata haki,hangeweza
    kujijitea,hangeweza kuaminiwa.Kilichobaki ni kulia na kulipiza
    tu.Mamake pia ni dhalifu kwa kuwa hawezi kujitetea nafsi yake
    mbele ya mumewe.
    Sara anabakwa kwa sababu nimnyonge,unyonge unaotokana na
    yeye kuwa mwanamke.Anasema Udhalifu na unyonge ndio
    unaotumiwa na wenye nguvu zao.
    TAASUBI YA KIUME.
    Jamii hii inamuona kama mwanamume ni bora kuliko mwanamke.
    Katika jamii hii,mwanamke alilaumiwa ndiye shetani kila
    kulipotokea visa vya ubakaji.
    52.
    MASWALI.
    Nimekosa nini ?nini ? Nini hasa ?
    a) Eleza muktadha wa maneno haya.(AL4)
    b) Ni mbinu gani za uandishi zinazojitokeza katika dondoo hili ?
    (Al 2)
    a) Jadili maudhui ya udhalifu na unyonge kama
    yalivyojitokeza katika hadithi hii(AL 14)
    “Thibitisha ukweli wa methali.Hakuna siri ya watu wawili.
    Siri si siri inapotolewa kwa mtu mwingine”.
    Sara alipomwelezea Sarina kuhusu kubakwa na ujauzito
    wake.Waliamua kuwa wangeiweka kama siri.
    Wakapanga kuwa Sara avalie vazi ambalo litaweza
    kuucha ule ujauzito.
    Wakapanga pia kuwa sehemu ya kujifungulia itakuwa
    shamba kwa wazazi wake Sarina.
    Walimhadithia dadake Sarina,Beluwa ambaye alikuwa
    daktari wa uzazi.
    Beluwa naye alipaswa kuweka siri hii.Mwezi baada ya
    mwezi alichukua vifaa vya kupima mimba na kuvipeleka
    nyumbani kumhudumia Sara,maana walitaka iwe siri kubwa.
    Ujauzito ulipotimia miezi,Beluwa akamtaka Sena aende
    hospitalini kwani vipimo vya wakati huo vingelishirikisha
    mambo mengi ambayo hayangeweza kufanyika
    nyumbani.Sara alipoka katika chumba cha daktari,kumbe
    baba na mama yake Sara walikuwemo wanamsubiri ,kumbe
    Beluwa alikwisha waeleza wazazi wake kuhusu ujauzito
    wake. Siri ikawa si siri tena.
    6. MASHARTI YA KISASA.
    Na Alifa Chokocho
    Msuko
    Hadithi masharti ya kisasa ni hadithi fupi iliyoandikwa na Alifa
    Chokocho. kwa mapana na marefu amezungumzia suala la
    mapenzi. Anayalinganisha mapenzi na ugonjwa usiokua na dawa.
    Mwandishi anaelezea mapenzi kupitia kwa mhusika Dadi njia hasi,
    kuwa mapenzi ni mateso, utumwa, ukandamizaji, udunishaji na
    ushabiki usio na maana.
    53.
    Dadi ni mchuuza samaki, licha ya hayo amezaliwa na kukulia mjini.
    Dadi alikuwa amelemazwa na tamaa yake kwa Kidawa na alikuwa
    akimwinda mara kwa mara. Kidawa alimwekea ukuta ili kuyakata
    mawasiliano, mara kwa mara akajifanya kuwa hataki kuzungumza.
    Siku moja, Kidawa alimkujia Dadi na kwa wakati huu akawa
    mwingi wa maneno. Dadi alishangaa nakutoamini aliyokuwa
    akiyasikia. Mkururo wa maswali uliompikita Dadi kwa mshangao na
    wasiwasi mwingi kwa maana hakuamini.
    Jambo moja ambalo Kidawa alikariri mara si moja ni usasa. Hili
    halikumwia wazi dadi alilokuwa akimaanisha likawa ni fumbo
    ambalo hata Dadi mwenyewe hakuweza kulifumbua. Katika
    ukurasa 58, “nimekupimanisha Na kukuona mtu wa maana. Ila tu,
    Zaidi ya hayo, nataka ujue kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa
    na mwanamke wa kisasa hutafuta mwanamme wa kisasa, mwenye
    mapenzi ya kisasa. Huba ya Dadi kwa Kidawa ilimziba macho
    asipigikamae msasa maneno yenyewe. Alisikia neno kisasa kama
    mapigo yenye mahadhi mazuri.
    Mwandishi anasema kuwa hii ingekua ndoa ya ajabu kama Dadi
    angefahamu masharti ya ndoa. Lakushangaza ni kuwa alikubali
    basi kuelewa mzigo ulioambatana na masharti hayo.
    Bi Zuhura anamfanyia Dadi stihizai na kumtania sana.Baada ya
    kufanyiwa mzaha, anaamua kutomuuzia Bi Zuhura samaki.
    Tatizo la Dadi lilikua kumshuku mkewe kuwa ana uhusiano na
    mwalimu mkuu.Hali hii inampeleka kumpeleleza. Anafululiza hadi
    shulleni mahali ambapo mkewe alifanya kazi ya umatroni. Huko
    anagundua kuwa wasiwasi wake ulikua wa bure katika shuguli
    yake anatambua kuwa mkewe alikuwa radhi kuiacha kazi kwa hofu
    yakuwa mmewe hakuwa anamwamini. Dadi anapofumanishwa
    akichungulia anaanguka chini na kupoteza fahamu.
    MAUDHUI.
    1. MAPENZI
    Mwandishi anayaona mapenzi kama kitendawili,
    anayalinganisha na ugonjwa usiokua na dawa. Kupitia kwa
    mhusika Dadi anayaelezea kwa njia hasi anayafasili kuwa
    mateso, utumwa, ukandamizaji, udunishwaji na ushabiki.
    Hata hivyo, Dadi anajitumbukiza katika mapenzi haya bila
    kuyatalii. Kidawa anapendekeza mapenzi ya kisasa na
    kusema kuwa atakuwa mke wa kisasa. Dadi hakuwa na
    mtazamo huo. Mtazamo wake ulikuwa kupenda na
    kupendwa bila masharti yoyote. Jambo hili linamfanya
    kumshuku mke wake.
    54.
    1. USASA.
    Mwandishi kupitia kwa mhusika dadi anaonyesha jinsi usasa
    unavyoathiri maisha ya mwanadamu. Usasa ulikuwa na
    maana ya kuchukua majukumu kwa zamu. Kidawa
    alipendekeza wasaidiane katika majukumu ya kinyumba
    kwa mfano; iwapo ameenda kazini. Dadi apike na kupiga
    deki.Kidawa anasema kuwa yeye ni mwanamke wa kisasa.
    Dadi alikiri kuwa mizani kwa kuwa amezaliwa na kulelewa
    mjini anaelewa barabara. Hivyo basi, anayakubali yote
    aliyoambiwa na Kidawa bila kuyatia kwenye mizani.
    2. UTABAKA.
    Kuna matabaka mawili. Tabaka la juu ambalo linawakilisha
    mwalimu pamoja na Kidawa. Dadi ndiye anayejiweka katika
    tabaka la chini na kujidunisha. Utabaka huwa ni zao la watu
    wenyewe mfano utabaka unajitokeza pale ambapo tuna
    m a k u n d i m a w i l i k a t i ya wa l e wa l i o n a v yo n a
    wasiokuwanavyo. Dadi anaingiwa na kiwewe kutokana na
    hali hii ambayo inamlemaza na kuulemaza uhusiano wao.
    3. ELIMU.
    Dadi ndiye anatufahamisha kiwango cha elimu ya Kidawa.
    Yeye mwenyewe hatuambii alipokia anataja tu kazi yake.
    Hata hivyo tunaskia kuwa kiwango chake cha elimu kilikua
    chini kikilinganishwa na kile cha Kidawa.
    4. NDOA/KUTOAMINIANA.
    Ndoa inastahili kujengwa katika msingi unatokana na
    kuaminiana. Hata hivyo, ndoa baina ya Dadi na kidawa ina
    mushki kwa sababu Dadi ana wasiwasi . Wasiwasi huu
    unatokana na kujidunisha kwake. Kwa upande wa Kidawa,
    hana tatizo lolote. Kabla ya kuoana alikuwa ameyatoa
    mashrti ambayo yangekuwa mwongozo wa ndoa yao. Kila
    wakati ilipotokea hali ya swintofaham u Kidawa
    alimkumbusha masharti.Ndoa hii inapata msukosuko pindi
    Dadi anapoamu kumfuata mkewe akimshuku kuwa ana
    uhusiano na mwalimu mkuu.
    55.
    6.MASHARTI.
    Masharti yanayoambatana na tatizo linalotokana na
    makubaliyano mara nyingi huweza kusuluhisha migogoro fulani.
    Hata hivyo mojawapowa yale mawili anapokosa kuyatimiza, basi
    huwa kunatokea mvutano na mgongano. Dadi aliingia katika
    makubalioano kwa pupa bila kuyawazia hali hii inasababisha
    matatizo makubwa, pindi anapofanya kosa, anakumbushwa
    masharti.
    Dadi aliingia katika makubalioano kwa pupa bila kuyawazia hali
    hii inasababisha matatizo makubwa, pindi anapofanya kosa,
    anakumbushwa masharti.
    WAHUSIKA
    1. DADI
    Dadi ni mchuuza samaki kama tunavyofahamishwa katika
    utangulizi wa hadithi. Licha ya hayo Dadi mwenyewe anadhibitisha
    hayo anaposema kuwa mimi ni muuza samaki tu. UK. 58.
    Ingawa kidawa ameelimika dadi hataki kubaki nyuma, anasema
    kuwa amezaliwa mjini. Kulingana na Dadi kuwa usasa unaweza
    kulinganishwa na maisha ya mji.
    SIFA.
    a) Mwenye bidii.
    Dadi ni mtu mwenye bidii kazini. Kuzaliwa na kukulia mjini
    kumemfunza namna ya kuyakabili maisha. Dadi hakutegemea
    kazi ya kuajiriwa bali aliweza kujiajiri mwenyewe. Kazi ya
    kuuza samaki inahitaji mtu mwenye jitihada, kuwatafuta samaki,
    kuwatafutia soko kama tunavyoelezwa na mwandishi anapita
    akitembeza samaki wa mwishomwisho. Uk 59.
    b) Mwenye hamaki.
    Msanii amewasiri Dadi mwenye hamaki pindi anapolazimishwa
    kufanya hivyo. Hapendi kuingiliwa masuala yake ya ndani
    sana.Bi. Zuhura anapomwingilia kwa hamasa, Dadi alitamka “
    ukiwanunua utafanya heri” ukr 62. Bwana Dadi anachujia
    baiskeli yake anamweleza peupe “ wewe hutaki samaki,
    unataka umbeya na kujua mambo ya watu” Uk 63.
    56.
    c) Mwenye kujidunisha.
    Dadi anajiona duni mbele ya Kidawa. Ana mawazo nyu
    kuhusu hali yake na kazi yake. Anasema kuwa” mimi ni muuza
    samaki tu” uk 58.
    d) Mwenye kushuku
    Kutokana na hali yake ya kujidunisha, Dadi anakosa kujiamini
    kiasi kuwa hamwamini ata mkewe. Hali hii inafanya amfuate
    mkewe hadi mahali pa kazi akimshuku kuwa na uhusiano na
    mwalimu mkuu. Nusura hali hii inasababisha maafa makubwa.
    Wasiwasi wake haukuwa na mashiko.
    e) Mwenye pupa
    Kiini cha matatizo yake ni kutokana na pupa yake katika
    maamuzi. Kama angekua amemakinika asingeingilia ndoa
    bila kutafakari masharti aliyowekewa na kidawa. Kilichokuwa
    kimemzuga Dadi ni neno “kisasa”. Kiasi kuwa hangeweza
    kuona chochote wala kusikia lolote lile.
    UMUHIMU WAKE.
    Ni kiwakilishi cha watu ambao hufanya maamuzi bila kujali
    matokeo yake. Dadi ni mfano wa watu ambao hufanya
    maamuzi yanayoadhiri maisha yao kwa kiasi kikubwa.
    KIDAWA
    Hili ni jina la kimajazi amabalo linawakilisha dawa katika
    moyo wa kisasa ambaye anataka mambo yafanywe kwa
    usasa. Anafanya kazi katika shule kama matroni.
    SIFA
    a) Mwenye dharau
    Mwandishi anasema kuwa hawangeweza kupataan
    anatumia fumbo kwa kusema” wakati wa zile siku ngumu
    yeye alipotembea ardhini, kidawa aliruka hewani” ukr 56.
    kidawa anadhihirisha dharau kutokana na viwitabia vyake
    mfano
    a) Uk 56 a) kuiburia midomo kumbeza
    b) kidawa kumwambaa dadi
    c) kumpa dadi mgongo
    57.
    (ii) uk 57 a) nimefuatwa na wanaume wengi walionitaka
    uchumba.
    b) “wenye uwezo na wasio nao”
    (b) mwenye masharti
    Ndoa yao ilijengwa kwenye masharti magumu ambayo hatimaye
    yanaiadhiri kidawa alikuwa na mpango wake wa awali kuhusu
    maisha ambayo angetaka waishi lakini dadi hakuyaelewa
    masharti yale.
    Masharti yale yalikuwa mpango wa awali wa ndoa yao na kama
    dadi angeyaelewa ndoa yao ingekua ya kupigiwa mfano.
    a) Mwenye mapenzi ya dhati
    Kidawa alikua mwenye mapenzi ya dhati ni kutokana na
    hali hii ambayo anayaweka mashrti ili asivunjwe moyo.
    Alipomuuliza dadi kama mapenzi ni dhahiri kuwa
    hakutaka kuvunjwa moyo. Alipokua akitafutwa
    alionyesha kana kwamba hakutakauhusiano lakini ilikua
    njia ya kukadiria kiwango cha mapenzi ya dadi kwake.
    Kuandaa chakula ni ithibati kuwa alimpenda dadi. Hata
    hivyo alikua tayari kuacha kazi yake ili kuonyesha penzi
    yake kwa mmewe.
    (d) mwenye mapato
    Kidawa anasema kuwa alitafutwa na wanaume
    waliosoma nna wasiosoma wenye uwezo na wasio nao.
    Hii ilikua ni njia mojawapo ya kujigamba kuwa sio dadi
    pekee aliyemtaka.
    MWALIMU MKUU
    a) Mwenye bidii
    Mwandishi kupitia kwa mkewe mwalimu mkuu anaonyesha
    jitihada za mwalimu kazini hasa tukizingatia kuwa ilikua ni
    wakati wa jioni. Anazidi kusema kuwa huwa anfanya hivyo
    kila siku kazi inapozidi. Wakati kidawa alipoenda
    kwenye osi ya mwalimu mkuu alimpata akiwa kazini. Na
    hata sauti yake ilishauri uchovu. Hii inaonyesha kuwa
    mwalimu ni mchapa kazi.
    58.
    a) Mwenye hekima
    Kidawa alipoenda osini akiwa na wazo la kutaka kuacha
    kazi, mwalimu mkuu alimuuliza kama amekiria, anaonyesha
    kuwa mbali na kuwa na hekima ni mshauri bora kwa sababu
    anamwambia kuwa ni magumu. Anajali maisha yake na jamii
    yake kwani hangependa ataabike na maamuzi ya haraka.
    ZUHURA
    (a) Mwenye dharau
    Jinsi anavyomzungumzia dadi ni ithibati kuwa ana dharau.
    Anaingilia masuala yasiyomhusu hasa yanayoingilia jamii.
    Kumuuliza dadi kama wameshaoza ni kiwango cha juu cha
    madharau.
    (b) Mdaku
    Bi zuhura anajiingiza kwenye mambo ya watu wengine. Alitaka
    kujajua masual ya ndani ya kidawa na dadi
    © Mjeuri
    Anaposimamisha dadi anamuliza kama ana samaki wa kuuza au
    anao wa kumkaangia bi kidawa, lake lingekua la kununua
    samaki wala si mengine
    MBINU ZA KUGHA
    1. Maswali ya balagha.
    Maswali ya balagha au tashtiti ni maswali yanayoulizwa na
    msimulizi au mhusika ambayo yanahitaji jibu.
    (i) Uk 56……kwa nini misumari ya nyuki inamuuma sasa ila si
    wakati ule wa tamaa ya ushindi. Ilipokuwa mabli mbingu na
    ardhi.
    (ii) Uk 57……(a) bwana wewe unataka mapenzi utayaweza
    a) Tuseme kisasanini
    b) Ameshatuliza moyo wake
    c) Nani angeangamini?
    (iii) Uk 60…..(a) kwani dadi engewezaje kupuuza yale masharti
    ya ndoa ya kisasa?
    (b) yale masharti yanaendelea kumtamiriria
    (c) dhana au ukweli?
    (d) hata wepesi wa kufahamu kibinadamu hanao?
    59.
    (e) huyu mwanamke asiyechoka kujipodoa akiingiliana ndani?
    (iv) uk 62…….a- kwa nini limkere mtu
    b- watu inawahusu nini
    c- mbona nawaona laini namna hii?
    d- au wameshaoza?
    a) Unaona mashavu ya samaki yalivyo mekundu hivi?
    1. NIDAA
    Ni usemi unaoonyesha kushangazwa na jambo Fulani na
    huambatanishwa na alama hisi
    (i) Uk 56…ni ugonjwa usio na dawa
    (ii) Uk 57…..dawa ya ugonjwa wangu’
    (b)………sikiliza dadi
    (iii) Uk 58….ladha ya ajabu
    (iv) Uk 60……eti dhana
    (v) Uk 61…..masharti ya ndoa ya kisasa
    (vi) Uk 62……Jamani
    (vii) Uk63…….biashara haigombi hivyo
    2. KUCHANGANYA NDIMI
    Msanii anapoyaweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika
    sentensi ya Kiswahili, msanii anweza kufanya hivi kwa kusudia
    au bila kusudia. Anafanya hivyo kuonyesha ana ya mhusika
    anayehusishwa na uneni ule.
    Uk 65 (i) ‘stop your gaze’

    a) my dress, my choice’
    b) Celeb ama socialite
    1. UTOHOZI
    Hii ni mbiu ya kuswahilisha maneno ya kiingereza na kufanya
    yawe na mapigo ya silabi ya Kiswahili.
    a) Uk 60… fasheni
    b) Uk 61… umetroni
    c) Uk 66…friji
    d) Uk 67….paipu
    e) Uk 69…. Ambulensi
    60.
    1. TASHBIHI
    Huu ni mlinganisho wa kitu na kingine kwa kutumia kiunganishi
    kama :mfano wa, mithili ya , kama na ja
    1. uk 56….(i)akimwinda kama kunguru
    (ii)kuambaa kama ugonjwa wa tauni
    2. uk 57…..maskio kuwa wazi kama anga
    2. TAKRIRI
    Hii ni mbinu ya kurudiarudia neon moja au kifungu cha maneno
    ili kusisitiza ujumbe Fulani;
    (i) Uk 57…. Nani angeamini? Baada ya visa vyote vile dadi
    alivyofanyiwa nani angeamini?
    (ii) Uk 58…..(a) na mapenzi ya kisasa yana shuruti za kisasa
    (b) lazima ufanye wajibu wa kisasa kwa mimi
    nitakayekuwa mkeo wa kisasa
    (iv) ) uk 59…..kwa hatua, kipembe baada ya kipembe
    …….pom pom pom poom poom pom poom
    3. MDOKEZO
    Msanii hukatiza maneno au anaamua kuachia maneno bila
    kutaja kitu. Mdokezo huwa ni mbinu ya kumfanyia msomaji
    awze kujijazia kwa njia ya ubunifu
    (i) Uk 59… pom poom pom poom pom poom
    (ii) Uk 66,,,,,na tazama
    (iii) Uk 67……lakini leo ni leo
    (iv) Uk 68….labda anachungulia wasichana
    MIFANO MINGINE
    4. SADFA
    5. UZUNGUMZI NAFSIA
    6. MAJAZI
    7. MSEMO
    8. NAHAU
    61.
    7. NDOTO YA MASHAKA
    Ali Abdulla ndiye mwandishi wa hadithi Ndoto Ya Mashaka. Yeye ni
    mzawa wa Pemba. Ameondokea kuwa mwandishi stadi wa hadithi
    fupi. Amechangia pia mkusanyo wa Damu Nyeusi na hadithi
    Nyingine.
    Mashaka alikua kijana aliyeishi maisha yaliyojaa mashaka.
    Alizaliwa na baada ya muda akaitwa yatime. Mamake alifariki
    alipomzaa kishaa babake akafuata,akashindwa kuvumilia
    upweke. Biti Kidete akamchukua Mashaka na kumlea. Biti Kidete
    daima alilalamika kuhusu miguu yake ambayo haikusikia dawa.
    Ilimbidi Mashaka atafute vijibarua ili wapate riziki.
    Baada ya Mashaka kumuoa Waridi,maisha yao yalijawa na shida
    na umaskini. Jambo ambalo halikuwafurahisha wazazi wa Waridi
    hawakulipenda.
    Waliishi katika chumba kidogo ambacho hakikuwatosha. Walipata
    watoto saba, sita kati yao walizaliwa kwa pacha tatu na mmoja
    pekee. Waliishi katika mazingira yaliyokuwa duni na machafu. Siku
    moja Waridi alishindwa kuvulia na akarudi kwao na watoto wote.
    Mashaka aliyempenda Waridi sana alijawa na upweke na ukiiwe.
    Alijitahidi kuwasaka lakini hakuwapata.
    Kuna utabaka ambao unadhihirika wazi. Matajiri walio wachache
    wanazidi kuwa matajiri zaidi. Nao maskini walio wengi walizidi
    kuwa maskini zaidi . Ndotoni Mashaka anawaona maskini
    (wasakatenge) wakiandawana na hatimaye maisha ya
    wanabadilika na kuwa bora
    Anwani
    Anwani ‘Ndoto ya Maisha’ ni faafu kwa sababu hadithi nzima ni
    ndoto. Kuwapo kwa Waridi na maisha yao, ni ndoto. Mashaka
    anasema “Aaaa, kumbe ii yote ilikua ndoto, ndoto yangu Mashaka,
    ndoto ya mashaka yangu , ndoto ya Mashaka isiyo Waridi wala
    tamaa ya maisha kuboreka. Heri nisingeota.”
    Dhamira
    1.Mwandishi alikusudiwa kukashifu mfumo wa utabaka katika jamii.
    2.Mwandishi alidhamiria kuonyesha athari za umaskini katika jamii.
    3. Alitaka kuthihirisha ukweli wa methali, “Mapenzi ni majani,
    popote penye mbolea hujiotea.”
    62.
    MAUDHUI
    Umaskini
    Watu wengi katika jamii hii wameathirika na umaskini. Kutokana na
    umaskini wa Biti Kidete , Mashaka alilazimikakutafuta vijikazi ili
    apate riziki. Aliweza kwangulia watu nazi au kwenda pwani
    kurambaza au kuokota kombe na chanje.
    Mashaka alipomuoa Waridi maisha yao yalizidi kuwa na shida
    nyingi. Waliishi katika chumba kimoja kwa miaka mingi katika
    mazingira duni. Kuliponyesha, michinzi ya maji lilionekana kwani
    paa lilikua likifuja.
    Chumba chao kilik]ua hakiwatoshi. Usiku binti zao walibanana na
    mama yao kwenye kijichumba chao na wavulana wakalala jikoni
    kwa chakupewa, jirani yao. Chumbani mlikua na vitu vichache tu.
    Hawakua na sababu ya kuvinunua na pia hawakua na pesa za
    kuvinunua. Mkewe alilalia mayowe na watoto wa kike wakalala
    chini kwenye mbacha.
    Wasakatenge waliathirika mno na umaskini hadi wakatamani
    wafe.
    Uchafu
    Mazingira walimoishi wasakatenge yalikua machafu kupindukia.
    Kwa mfano, chuma cha Mashaka kilikumbatiana na choo cha jirani.
    Harufu yote kutoka chooni uliingia hadi chumbani mwa Mashaka.
    Upande mmoja wa kile chumba kukawa na mfereji wa maji
    machafu. Mvua uliponyesha , mfereji ule ulifurika na kwote kukawa
    na uvundo. Wakati mwingine hawa wasakatenge walitumia
    karatasi za plastiki kufanyia haja ndogo na kubwa kasha kutupa
    huko nje.
    Utabaka
    Kupitia kwa Mashaka , tunaelewa pengo ulilopo kati ya watu wa
    tabaka la juu na watu wa tabaka la chini ni pana sana (uk. 78)
    Mashaka anauliza , “Na je , hizo fedha hupatikana wapi ?Nini
    kinaleta tofauti hizi?kwa nini pengo hili kuzidi kukua na kupanuka
    kila uchao?…”Matajiri wanazidi kuwa matajiri na fukara wakizidi
    kufukarika na kudidimia
    63.
    Mapenzi ya dhati
    Waridi anampenda Mashaka kwa kweli bila ya kuangalia uduni
    na utupu wa Mashaka,alimpenda katika umaskini wake.
    Mashaka pia alimpenda Waridi ‘kufa’. Alimpenda kwa hamu na
    ghamu.Alipoachwa na Waridi hakua na dhamani ya maisha tena.
    Alijitahidi kuwasaka bila ya mafanikio.
    Ajira kwa watoto
    M a s h a k a a l i t a f u t a v i j i k a z i a l i v yo v i we z a . A l i c h u m a
    karafuu,akaangulia watu nazi. Alienda pwani kurambaza au
    kuokota kembe na change. Pia alisaidia mtu kijikazi chake mkono:
    kufyeka majani usoni pa nyumba yake ,kuyachanja kuni magogo
    yake na hata kufua na kupiga pasi nguo zake… yote kwa lengo la
    kutafuta riziki.
    Kifo/Mauti
    Kuna vifo vya watu tofauti. Mamake Mashaka alifariki alipomzaa.
    Babake naye aliposhindwa kuvumilia upweke baada ya kifo cha
    mkewe naye akafa. Hatimaye Biti Kidebe naye akaeafuata.
    Urembo
    Mashaka anaeleza kuhusu urembo wa Waridi. Anamlinganisha na
    ua lenye hauba iliyotukuka na aliye na harufu nzuri.
    WAHUSIKA
    Mashaka
    Ndiye muhusika mkuu
    Mwenye mapenzi
    1.Uk 74: Mashaka anasema alimpenda Waridi Kufa .
    Anapowakosa Waridi na wanawe pale nyumbani alijitahidi
    kuwasaka bila ya mafanikio.
    2.uk 77: Mashaka alipoachwa na Waridi hakuona thamani ya
    maisha tena.
    3.uk 79: Mashaka anasema “Nilimpenda mno bila shaka,
    nilimpenda kwa hamu na ghamu.”
    4.uk 80: Waridi aliporejea, Mashaka alifurahi sana na hata
    akasahau yote yaliyokuwa yamepita.
    64.
    Upweke na Ukuwe
    1.Uk 87:Alikua mwenye upweke na ukuwe Waridi alipomtoka
    katika maisha yake.
    2.Babake Mashaka aliposhindwa kuvumilia upweke baada ya kifo
    cha mkewe . Huo upweke ndio ulisababisha kifo chake.
    Mwenye Mashaka
    Maisha ya Mashaka ni mashaka matupu. Alipozaliwa, mamake
    akafa na baadae babake akamfuata kwa kushindwa kuvumilia
    upweke.Biti Kidebe aliyemchukua baada ya vifo vya wazazi wake
    akawa naye hajiwezi kiafya na kimali. Mashaka yakamzidia
    Mashaka. Huyo akawa anafanya vibarua ili apate riziki.
    Hatimaye naye Biti Kidebe akafa.Baada ya kumuoa Waridi
    matatizo yakawa chungu nzima. Yalipozidi Waridi akashindwa
    kuvumilia na akamuacha Mashaka pekee. Akabaki akiwa na
    umaskini.
    Kufa moyo
    Uk 79: Nikaona kira za nafsi yangu zinaendana na zile za moyo
    wanguuliokwisha tamauka.
    Uk 79: Mashaka anasema “Nimelioka hata naradua kufa kuliko
    kuishi.”
    Uk 80:Wanyonge wa tabaka la chini waliandamana huku
    wakipiga kelele , “Tunataka Tufe!Bora Tufe!”
    Waridi anashindwa kuvumilia maisha ya Mashaka na anaamua
    kurudi kwao.
    Maskini
    Uk 74:Waliishi katika chumba kile kile kibovu kwa miaka mingi na
    shida zikawa zinawatamirira kila upande. Kazi yao kubwa ikawa
    ya kijungu-meko,kazi ya kupigania tumbo.Walilala chini na hata
    kuomba nafasi kwa jirani. Hawakuwa na vitu chumbani kwani
    hawangeweza kununua.
    65.
    Waridi
    Mwenye mapenzi ya dhati
    Uk 74: Waridi alimpenda Mashaka kwa dhati. Hakuangalia hali
    duni ya Mashaka .Alimpenda katika umaskini wake.
    Mapenzi hayachagui fukara wala tajiri kwani mapenzi huota
    popote.
    Mvumilivu
    Aliweza kuvumilia maisha hayo ya umaskini kwa miaka mingi.
    Mrembo
    Uk 70: Mashaka anafananisha urembo wa Waridi na ua ambalo
    hupendeza macho na kumfurahisha mtima.
    Wasakatange
    Ni watu maskini wa tabaka la chini. Walitamani kutokana na hali
    yao duni.
    Mzee Rubeya
    Alikua babake Waridi.
    Alikua na asili ya Yemeni.
    Alikua tajiri ambaye alihuzunishwa na ndoa ya Mashaka na bintiye
    Waridi kwa sababu Mashaka alikua maskini.
    MBINU ZA UANDISHI
    Jazanda
    1.Ua la Waridi limetumika kijazanda kulinganisha Waridi mke wa
    Mashaka.(uk 70)
    2.Mashaka analinganisha mshahara wake na mkia wa mbuzi.( uk
    76)
    3.Nitaramba na kulmbatua asali yake tamu kama nyuki (uzuri
    wako).
    Maswali Balagha
    Ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo
    hayahitaji jibu (rhetorical question).
    66.
    Uk 70: Na harufu yake je?
    Leo harufu tu ina sifa hiyo, waridi lenyewe je?
    Ni Biti Kidebe mamangu, au waja tu na dharau zao?
    Uk 76:Wamekwenda wapi watu hawa?
    Uk 78: Na je ,hizo fedha hupatikana vipi? Mbona kuna pengo
    kubwa kati ya walionazo na wasiokuwa nazo? Nini kinaleta tofauti
    hizi?
    Nyimbo
    Uk 77: Wimbo uliopigwa na redio Tanzania Dar ulipendwa sana na
    Waridi. Wimbo huu unaonesha hisia za kutamauka. Mtu aliyekufa
    moyo
    Methali
    Uk 70: Baada ya dhiki faraja
    Jungu kuu halikosi ukoko
    Uk 75: siri ya mtungi iulize kata au kitanda usichokilalia hujui
    kunguniwe
    Uk 78: Subira ni ufunguo wa heri.
    Uk 79: Ngoja ngoja huumiza matumbo
    Chuku
    Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe Fulani
    au kusia kitu.
    Uk 71: Nikalienzi ua langu kuliko hata mboni za macho yangu
    Uk 74: Nampenda kufa
    Uk 76: Dhiki ndio ilikua nguo na harufu yetu.
    Uk 80: karne nzima imepita sasa pasi na kuliona ua langu. Ndio
    kwanza leo nilitie jichini baada ya miaka mia. (muda mrefu
    sana)
    Tabaini
    Matumizi ya kikanushi ‘si’
    Uk 72: Si maisha si wazimu
    Uk 71:Si ya sasa si ya baadae
    67.
    Tashihisi
    Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye
    uhai(binadamu)
    Uk 74: Harufu yote itapikwayo na domo la choohicho
    Uk 74:Nao hutema uchafu wao katika mto Msimbazi.
    Uk 76:Katika maisha hayo siku zilijisotora zikapita kama hazitaki.
    Uk 82:Rangi ya urujuani ulichungulia katika nyufa
    Uk 88: Mwili wangu niliuhisi mtamu. Ulinitafuna kama kidonda
    Uk 79: Haukutoka (msemo) na wala haukutaka kamwe kutoka
    Utohozi/Kuswahilisha
    Uk 74: Plastiki
    Takriri
    Ni mbinu ya kurudia rudia neon moja au kifungu cha maneno ili
    kusisitiza ujumbe fulani. (repetition}
    Uk 81: Ilikua radi iliyopiga kila mahali. Ilika kila mahali. Kila
    mahali uliingia.
    Uk 79: “Hadi lini lakini…hadi lini…”
    Tashbihi
    Hii ni mbinu ya lugha inayo linganisha vitu au hali mbili tofauti kwa
    kutumia maneno ya kulinganisha:kama, mithili ya,sawa na,je.
    Uk 72:Akaiga dunia bado mbichi kama jani la mgomba
    Uk 73:Rubaa ya watu wane ikajitema chumbani kama askari wa
    fanya fujo uone
    Uk 74:Choo chenyewe kimeinuka juu kama ghorofa
    Uk 75: Wavulana walilala jikoni kama nyau…
    Uk 76: Katika maisha hayo siku zilijisotora zikapita kama hazitaki
    Uk 77:Ilikua tamu kama ya ndege wa peponi.
    U k 7 7 : N i l i k u a k a m a n d e g e k a t i k a t u n d u
    uk 88: Ni maadamano yale walikua wamefwua na kufwuana kama
    unga
    68.
    Majazi
    Ni pale tabia za wahusika zinaambana na majina yao halisi
    Uk 73:Waridi: Mashaka anasema jina lake lilipige ndipo bila
    shaka. Linaelezea urembo wa Waridi
    Uk 74:Wasakatenge (maskini)
    Uk 75:Chakupewo ?(anawapa mahali pa kulala)
    Misemo
    Uk 72:Kusalimu amri
    Uk 72:Maji yalipozidi unga
    Uk 72:kupiga kite
    Uk 76:Ziligonga mwamba
    Uzungumzi nafsia
    Mhusika hujizungumzia, ama kuwa au kuongea bila kukusudia
    kusiko na yeyote.
    Uk 76:Nilijiuliza lakini jibu sikupata
    Uk 77:Niliwaza mengi zaidi. Nikawaza ya laity ningekua na
    maisha mazuri.
    Uk 78:Nafsi yangu uliniambia “subira ni ufunguo wa heri.”
    Uk 79:”Hadi lini lakini…hadi lini. Subira hiyo?” Moyo uliuliza
    Maswali
    1.Mashaka, Waridi na wasakatenge ni majina ya majazi. Thibitisha
    kutoka kwa hadithi
    2.Onesha jinsi mwandishi wa hadithi ya Ndoto ya Mashaka
    amefaulu katika matumizi haya
    a)Chuku
    b)Tashisi
    c)Tashbihi
    d)Nahau
    Chuku
    ni kutia chumvi katika jambo ili ufafanuke zaidi au lieleweke
    waziwazi.
    Uk 71:Nikalienzi ua langu kupita hata mboni za macho yangu.
    Uk 74:Nilimpenda kufa
    Uk 76: Sura zetu zilitosha kuwa sura za kusemea
    Uk 76: Dhiki ulikua ndio nguo na harufu zetu
    Uk 80:Karne nzima imepita sasa pasi na kuliona ua langu.Ndio
    kwanza leo nilitie jichoni baada ya miaka mia.
    69.
    8. KIDEGE
    ROBERT W EDUOR
    Msuko
    Hadithi hii imejikita katika mazingira ya bustani.Bustani ya ilala ni
    mahali ambapo wapenzi walikuwa wakikutana.
    Taswira inayojitokeza ni ya watu wanaopendana.Ili kusisitiza
    jambo hili,mwandishi anazungumzia rangi.Rangi inapotumika
    kisanaa huweza kuwasilisha wazo Fulani.Msanii anasema kuwa
    ,’Nyasi zilikuwa zimepiga umanjano na kukaribisha binadamukwa
    hali za kila aina’uk83.
    Msimulizi anasema kuwa mahali hapa ni mandhari ya
    wapendanao.Ni mahali ambapo waja huzungumzia mambo mengi
    na wengine wakiwa na mambo mengi.Tunaelezewa kuwa mahali
    pale ni mahal I pa kuanzisha uhusiano.
    Msimulizi anasema kuwa,kati ya waliokuwa wakizuru Bustani ile ni
    Joy na Achesa,Siku hiyo walikuwa na mchezo wa kitoto.Wakiwa
    katika mchezo,mawazo ya Achesa yanatekwa na ndenge
    mmoja.Ndenge Yule alimfanyia mambo ya ajabu,akawa ni
    mhusika muhimu katika masimuluzi haya.Pamoja na ndenge Yule
    inasadifa kuwa Mose alikuwa amejibanza………
    Jina halisi la mose ni Musa.Mose alikuwa mapenzi makuu kwa
    samaki waliokuwa kwenye kidimbwi.Kutokana na mapenzi yale
    akawa na mazoea ya kuwasilisha na kuwatunza.Mose alikuwa na
    raki yake kwa jina Shirandula.Shirandula alikuwa mtani mkubwa
    wa mose,alimtegea mose kitendawili ambacho kilimlemea.
    Mose aliota ndoto usiku wa kuamkia jumamosi,ndoto ilikuwa juu
    yan midege ya ajabu.Katika uhalisia anaamua kuelekea kwenye
    bustani.
    MAUDHUI
    a) Uhusiano mwema.
    Uhusiano mwema hudhihirika kutokana na mahusiano na
    mwingiliano barua ya watu.Katika hadithi kidege
    unadhihirika kati ya Joy na Achesa.Wanaonyesha hali hii
    kwsa kucheza pamoja mchezo wa kitoto.
    Mose anataniana na maraki hawa bila kuwaudhi UK85
    wakabaki wanachekeana,ama wanachekacheka ovyo.
    70.
    a) Mapenzi
    Mapenzi yanadhihirishwa na wanadamu wanapojituliza
    chini kwenye vipimbe vilivyowacha wakiendeleza
    mining’ono ya mapenzi.Mapenzi yanayolengwa ni ya
    mwanamke.Mwandishi anasema kuwa mahaba
    yamewafura.Anamaanisha kuwa mapenzi yamekita mizizi
    katika jamii hii,mwandishi anatutilea taswira ya ndege
    wanaotazama wanadamuwakiwa katika haba.
    b) Utunzaji wa mazingira na viumbe.
    Mose alijipatia wajibu wa kuwatunza samaki na
    ndege.Aliwatupia samaki kipande cha sima bila kuwasahau
    ndege.
    B u s t a n i ya i l a l a i l i k u wa i m e h i f a d h i wa v i z u r i .
    Mwandishianasema kuwa uzuri………………???????????
    h a wa k u wa wa n aya h a r i b u m a z i n g i ra ya l e. H a t a
    samakiwaliokuwa kwenye kidimbwi hawakudhuriwa na
    wanadamu.
    c) Uraki
    Uraki unajitokeza kwenye hadithi Joy na Achesa ni
    miongoni mwa maraki waliokuwa wakijituliza kwenye
    bustani.Ni maraki tu ambao wanaweza kuwa na mchezo
    uliokuwa ukichezwa.Licha ya hao wawili,kulikuwa na Jozi
    nyingine ya maraki nao ni Mose na Shirandula.
    d) Starehe
    Katika hadithi hii,mwandishi anatupeleka kwenye mazingira
    ya bustani.Bustani ya ilala ilikuwa na uzuri wake ndio maana
    watu walikuywa wakienda mahali pale ili kustarehe.
    WAHUSIKA
    Hawa ni watu,vitu au viumbe wanaoishi katika kazi ya
    kisanaa kwa lengo nla kubeba dhamira mbalimbali na
    kuiwasilisha kwa wanajamii.Mwandishi wa hadithi kidege
    amewatuma wahusika wa aina mbalimbali.Amewatuma
    wahusika wanadamu,ndege na samaki wote kwa lengo la
    kuwasilisha madhumuni yake.Kuna wale aliowadokeza na
    hawa kuendelea zaidi wakawapokeza wengine majukumu
    ya kuendeleza maudhui.
    71.
    1) MUSA
    Jina la utani ni Mose,jina hili linaendelezwa hadi mwisho wa
    hadithi.
    SIFA
    a) Mwenye bidii
    Licha ya kuwa na shughuli zake aligeuza uhusiano wake
    na samaki kuwa wajibu.Vipande vya sima alivyokuwa
    akivibeba havikuwa vyake bali vilikuwa vya kuwalisha
    samaki na ndege.Hata katika ndoto yake anapovamiwa
    na midege,kra zake zinampeleka mfukoni kwani
    yalikuwa ni mazoea yake kuwalisha.
    b) Mwenye mapenzi makubwa kwa samaki.
    Mose aliwapenda samaki na kuwafanya uraki
    nao.Aliwatunza samaki hata kama haikuwa kazi
    yake,alichukua wajibu wa kutenda hayo (uk86).Samaki
    walimjua na kumzoea, hii inatokana na hali ya kuwatupia
    vipande vya sima.
    c) Mtani
    Mose alitaniana na shirandula ndio shirandula alimtegea
    mose kitendawili.Kitendawili ambacho aliomba siku mbili
    ili akitegue.
    d) Mkarimu
    Aliweza kuwatunza na kuwalisha wale viumbe.Iwapo
    angekosa siku mbili au tatu,siku ya nne angefanya juhudi
    kuwatembelea.Hali hii inaonyesha ukarimu wa muda
    wake na kidogo alichokuwa nacho…..ni yeye tu ambaye
    angeweza kuwatembelea kwa madhumuni ya namna
    hii.(UK 89)
    e) Mtabiri
    Ndoto yake inakuwa ni utabiri wa mambo ambayo
    yangetokea.Ndoto ni kioo cha yaliyojiri baadaye.
    f) Anamlahaka mwema
    Mhusika huyu anaonyesha jinsi wanavyoingiliana na
    maraki zake.Hii ndiyo sababu iliyomfanya ajibanze
    mahali akiwatazama Joy n AchesA.Yeye na shirandula
    hawakuwa na utofauti.
    72.
    1) Shirandula:
    a) Mtani
    Mwandishi anatuelezea kuwa Shirandula alizoea
    kumtania mose kila wakati kutokana na utani wake
    hakosi la kusema anavyoeleza kuwa c hoo
    kinachimbwa kasha kinajengwa..(UK87)
    b) Mbunifu
    Mtu mbunifu hakosi la kusema pindi tu anapojipata
    katika hali ya kujitolea.Shirandula hakukosa la
    kusema katika kitendawili.Mfano wanapozungumzia
    kuhusu choo na kuelezwa kuwa choo hakijengwi
    kinachimbwa…(UK86)
    Anatoa jibu mara moja…(UK87)
    c) Mcheshi
    A n a p o p a t a j i b u l a m o j a k wa m o j a . Awa l i
    anazungumzia kuhusu vijisamaki ambavyo anasema
    huwezi kuvila na anauliza ni vya faida gani.
    d) Mshamba
    Watuwa mji wanamwita mshamba kwa kuwa yeye
    alizaliwa kijijini.Mbali na kuzaliwa kijijini,tabia zake
    zinadhihirisha hali hii kutokana na mawazo yake
    kuhusu samaki.
    2) JOY NA ACHESA.
    Hawa ni baadhi ya wale waliokuwa wakizuru bustani ili
    kujituliza.
    SIFA
    a ) Wenye mapenzi ya dhati.
    Hawa wawili wanaonekana kuwa na mapenzi ya muda
    ,kama tunavyoelezwa na mwandishi kuwa walikuwa na
    mazoea ya kuzuru mahali pale.
    73.
    b) Watani
    Kutokana na mchezo wanaocheza wa kitoto ni bayana
    kuwa lazima wawe wametaniana.Joy kumrukia Achesa
    na wote kujikuta wakiwa chini.
    c). Wacheshi
    Kila mmoja anaangua kicheko kutokana nay ale
    wanayoyashuhudia.
    MBINU ZA LUGHA.
    1. Uhuishi/Tashihisi.
    Hii ni tamathali ya usemi ambayo msanii huvipatia
    vitu sifa walizonazo binadamu kutenda na kufanya
    kama wanadamu..
    a)Ndege walijibizana,mmoja huku na mwengine kule
    wakizungumza(UK83).Ingawa ndege wana uhai
    huwa hawazungumzi,msanii amewapatia sifa ya
    kuzungumza.
    b) Ndege naye pale mtini akaona na kushangilia..(UK
    85)
    C) Ndege akaamua kuwafunganisha ndoa…(UK85)
    d) Fikra zikamtuma mfukoni (UK89)
    2. Tabaini
    Ni tamathali ya usemi ambayo msanii hutuma usemi
    unaosisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani
    a) Jua si jua,baridi si baridi(UK 83)
    b) Si wakubwa ,wala si wadogo(UK89)
    c) Mwewe si mwewe,tai si tai(UK89
    3) Takriri
    Ni mbinu inayotumiwa na msanii ya kurudiarudia neno moja au
    kifungu cha maneno kwa lengo la kusisitiza : Mfano ;
    i. Wakabingiria,Wakabingiria ….UK 84
    ii. Samaki kumvutia mose,mose kumvutia ndege,Ndege
    n a y e k u m v u t  a n a n i ? M o s e n a
    Ndege,………………UK88
    iii. Vuta,Vuta ………….….UK92
    Shika, shika……………….UK86
    74.
    1) Nidaa
    Huu ni msemo unaotumiwa na msanii kuonyesha kushangazwa na
    jambo Fulani na huambatana na alama ya hisi au mshangao.
    a) Poa! UK 83
    b) Usivue! UK 86
    c) Lakini wapi! UK 89
    d) Lo! UK 94
    e) Hawa watu na matamshi yao! UK 87
    1) Tashbihi
    Tamathali ya usemi ambayo msanii anavilinganisha vitu viwili
    au zaidi, kwa kutumia maneno kama vile
    Mfano wa mithili ya,kama na ja.
    i. Alifuata desturi kama ibada…UK 89
    ii. Midomo kama panga….UK 91
    2) Tanakali za sauti
    Hii ni mbinu ambayo msanii hutumia kuiga sauti za milio
    mbalimbali. Milio inaweza kuwa ya vitu,wanyama n.k
    i. Ndege alitoa sauti chwi!UK 84
    ii. ………alikuwa keshamrukia pu !UK 84
    iii. Kikalenga kwenye pua, chwa !UK 85
    iv. ………Sauti yake ya kawaida chwi!UK 90
    Chwi!……Chwi!……Chwi! UK 92
    MTINDO WA UANDISHI
    Msanii ametumia mtindo wa fasihi simulizi.Ameweza
    kuingiza tanzu za fasihi simulizi katika masimulizi
    yake.Lengo la kufanya hivi ni kuendeleza dhamira yake
    na kuyakuza maudhui:
    a) Utanzu wa maigizo
    Mwandishi ametumia kipera cha kitendawili UK
    90Kitendawili!Tega! Anayejenga choo na
    anayejenga?
    75.
    8. NIZIKENI PAPA HAPA
    Ken walibora ni mkaazi wa Kenya, na mwandishi maarufu wa
    Kiswahili. Ni mwandishi mtajika wa kazi ya fasihi ya Kiswahili.
    MUHTASARI
    Nizikeni papa hapa .Haya yalikuwa maneno ya otii mwenyewe.
    Otii alikuwa akisakatia kandanda timu ya Bandari FC Kwenye
    uwanja wa manispaa na kote inchini.Wakati huo alikuwa na siha
    yake na aliishi Mombasa.
    Anakutana na Rehema Wanjiru msichana aliyekuwa mrembo Zaidi.
    Rehema alimwambukiza Otii ugonjwa.Akawa anaendesha
    akakonda sana na akawa na kikohozi kisichokoma .Ugonjwa huu
    unampeleka hadi kaburini .
    Kabla ya kifo chake ,wanachama wa chama cha nyumbani
    wananza kukutana kwake kupanga mipango ya mazishi .Walihitaji
    kuchangisha fedha za kukondisha magari yakuchukua maiti na
    waombolezi kutoka Mombasa hadi sidindi karibu na Kisumu.Otii
    hakuona umuhimu wa safari hii ya kutoka Mombasa hadi sidindi
    .Anapendekeza azikwe hapo Mombasa.
    Hakuna anayesikiza ombi la Otii .Wanasisitiza lazima
    {azikwe]maiti ya Otii angepelekwa Kisumu kulingana na mila na
    desturi zao. Jamaa na maraki na watu wa nyumbani lazima
    waandamane kupeleka maiti Kisumu. Walipoka mtito Andei
    wanakabiliana na Lori refu ambalo lilikuwa likija kasi huku
    linayumbayumba barabarani. Dereva wa matatu iliyokuwa
    imebeba maiti alijaribu kukikwepa kichwa cha lori lakini
    hakufanikiwa. Watu arubaini walifariki hapo papo . Wengine kumi
    na watatu walijeruhiwa ,baadhi yao vibaya sana.
    Yote haya yalisababishwa na kupuuza . wangemsikiliza otii mambo
    hayangeishia vile;
    ANWANI
    Anwani ya hadithi hii nizikeni papa hapa inaoana na yale
    yaliyomo. Hili lilikuwa ni pendekezo la Otii kuwa akifa maiti
    yake isisarishwe hadi Kisumu lakini azikwe papo hapo
    Mombasa.
    76.
    DHAMIRA (LENGO)
    1. Mwandishi anakusudia kuonyesha umuhimu wa uhusiano
    katika kufanya mambo
    2. Anadhamiria kukashifu mapenzi ya kiholela na kutuonyesha
    athari zake. Mf uhusiano kati ya Otii na Rehema Wanjiru.
    3. Mwandishi alidhamiria kuonyesha ukweli wa methali
    asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    MAUDHUI MILA NA DESTURI
    Wananchama cha watu cha nyumbani wanasisitiza kuwa lazima
    otii(maiti) ipelekwe Kisumu kulingana na mila na desturi.
    Wanasema katika mila na desturi zetu kauli ya marehemu si
    chochote, si lolote, muhimu ni kwmba sharti mtu wa kwetu azikwe
    nyumbani.
    USHIRIKIANO/ UMOJA
    Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani wanatangamana
    na kupinga mipango ya mazishi ya oti. Baada ya kifo cha otii,
    jamaa na maraki wa watu wa nyumbani ya mazishi walikjumuika
    kwa wingi, katika kitongoji duni cha Kisumu ndogo kupanga
    mazishi. Kwa pamoja wanachangisha fedha za kununua jeneza,
    mavazi ya kumvalisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari
    ya kuchukua maiti nyumbani, siku ya kupeleka maiti nyumbani
    wanajitokeza kwa wingi.
    UJEURI NA ATHARI ZAKE
    Wanachama wa chama cha watu wa nyumabani walipoanza
    mipango ya mazishi na hata kufanya michango ili kugharamia
    mipango ya kupeleka maiti nyumbani.Otii aliwaambia mara
    kadhaa wamzike papo hapo Mombasa laikini hawakumsikiza.
    Walipokuwa safarini kuelekea Kisumu, kunatokea ajali mbaya
    ambayo inawaangamiza wengi na wengine wanapata majeraha
    mbaya.
    (uk100) rakiye Otii anamtahadhirisha Otii dhidi ya kuwa na
    uhusiano na wasichana wazuri Zaidi kama Rehema Wanjiru. Otii
    hakutilia makini hayo. Alisema “pana hasara gani nzi kua
    kidondandani?”Aliendelea na uhusiano huu. Akapata ugonjwa
    uliompleka kaburini.
    77.
    SIFA ZA WAHUSIKA
    OTII
    Otii ndiye mhusika mkuu
    Mchezaji hodari.
    Aliyechezea timu ya Bandari FC kwenye uwanja wa manispaa na
    kote nchini. Alichezea timu ya taifa Harambee stars wakati
    alipotambaa jijini Mombasa .UK98 anakumbuka mataifa mengi ya
    kigeni alikosari kwenda kusakata Kabamba kwa niaba ya taifa
    lake na jukumu la kupeperusha bendera ya nchi yake.Alipokuja
    tamko la michezo lililonukuliwa gazeti lilikisi kira za wengi. Pengo
    la Otii haliwezi kuzibwa.
    MBADHIIFU
    Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani walipokutana
    kupanga mipango ya mazishi, walikusudia kuchangisha fedha za
    kununua jeneza, mavazi ya kumvalisha maiti pamoja na fedha za
    kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombolezaji hadi sindindi
    yeye hakutaka hayo alisema, ‘ gharama zote hizo za kunipelka
    sidindi za nini? Lakini wenzake wakasisitiza kuwa gharama hizo ni
    zao si zake{UK97]
    UJEURI/MWENYE MAPUUZA
    Alipotahadharisashwa dhidi yakuwa na uhusiano na huyo msichana
    mrembo Rehema Wanjiru alipuuza.Hatimaye akaambukizwa
    ugonjwa uliompeleka kaburini.
    CHAMA CHA WATU WA NYUMBANI
    1.Umoja/ushirikiano
    Wanashirikiana kuanzia mwanzo hadi mwisho katika kupanga
    mazishi ya Otii wanachanga pesa, wanakutana kwa Otii na
    wanafuatana kuelekea sidindi kuhudhuria mazishi ya Otii.
    2.Wanamapuuza
    Otii alisisitiza kuwa yeye angetaka azikwe palepale Mombasa
    lakini wakapuuza. Hatimaye wakapata ajali mbaya sana wakiwa
    safarini kwenda sidindi kuhudhuria mazishi.
    78.
    3.WATAMADUNI
    Wanasisitiza lazima wamzike otii nyumbani kulingana na mila zao.
    Ni kinyume cha mila na ada zao kumwadia mwenzao kutupiliwa
    mbali kana kwamba hana kwao.
    WAKARIMU
    Wanahakikisha wamechanga pesa za kutosha kugharamia mazishi
    ya otii.
    REHEMA WANJIRU
    Ni msichana wa aina yake, mwenye urembo wa kutikisa jiji zima,
    urembo wa kulikausha bahari, urembo uliompa wasichana wenziwe
    husuda na wanaume mshawasha Fulani.
    MZINIFU
    Kuna uwezekano kuwa ugonjwa huu aliupata kupitia tabia ya
    uzinifu.
    MBINU ZA UANDISHI
    Chuku(hyperbole)
    Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbefulani au
    kusifu.
    Uk 96…. kituamepotelea kwenye kitanda chake( mdogo Zaidi)
    Uk 97…..Alipokua anakanyaga ardi mpaka inatetemeka( kwa
    nguvu kutokana na afya nzuri)
    Uk 100.. urembo wa kulitikisa jiji zima( mrembo sana)
    Uk 101.. pengo aliloacha otii haliwezi kuzibwa( mchezaji stadi)
    Uk 102.. wanahabari waliotiwa mbinu ya kupiga picha
    hawakuweza kula nyama tena mazishini mwao.
    Istiara
    Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja.
    Uk 96….. kabakia sindano (ameendelea sana)
    Uk 96 wanamwita mbu ( mdogo Zaidi)
    79.
    Tashbihi (simile)
    Ni mbinu ya lugha unayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa
    kutumia maneno ya kulinganisha, kama mithili ya, sawa na ja;
    Uk 98. Hakuweza kunyanyuka pale chini alikoabwagikie kama
    gunia la chumvi.
    Uk 99…. Alikuwa ametupwa kama masimbi yabuzaa
    Uk 102…. Akajaribu kukwepa kichw acha hari kilichokua
    kimemkodolea macho kama simba wa Hifadhi ya Wanyama ya
    Tsavo.
    Jazanda:
    Kutumia maneno yaliyo na maana che.
    Uk 96…jamaa zake si watu wa kusubiri mvua kunyesha ndipo
    waanze kutafuta pahali pa kununua mwavuli..(jeneza)
    Uk 98…. Alikua mwibe.
    Uk 97,,, mbwa( kitu kisicho na thamani)
    Uk 100… pana hasara gani nzi kua kidondani.
    Utohozi
    Ni mbinu ya kuwahilisha maneno ya lugha yatamkike kama ya
    Kiswahili.
    Uk 98…. Manispaa(Municipal)
    Uk 98…..mechi(march)
    Uk 99 eksirei(xray)
    Uk 99… klabu (club)
    Uk 96 fremu
    MSEMO
    UK 97… Anapiga chafya.
    Uk 99…. Akichungulia kaburi.
    Uk 99…..Hawakujali hawakubali.
    Uk 99….kufumba na kufumbua.
    Uk 100..akapigwa na butwaa.
    80.
    Tashhisi/ Uhuishaji.
    Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye
    UK100 urembo wa kulikaulisha bahari.
    Uk.101.sifa za kibroda waombolezaji na kutapika wengine.
    102 akajaribu kukikwepa kic hwa c ha lori kilic hokuwa
    kimemkondolea macho.
    METHALI
    Uk.99. Mwacha kile hanacho na chema kimpotele.
    Uk.99.aliyeumwa na nyoka akiona ungongo hushtuka.
    Tabaini
    Ni tamathali ya semi ambayo kwayo maneno/mawazo
    yanayokinzana hutumiwa katika sentensi ili kuleta msisitizo wa
    wazo.
    UK99.si barabara ya mlango wa papa ,si barabara ya Nkrumah, si
    barabara ya jomo Kenyatta, si ya Digo
    UK100..Si kuendesha, si kukonda, si vipele si si kukichwa
    kukikokome….
    Mbinu rejeshi
    UK96….Ukutani kumetundikiwa fremu yenye picha yake alipokuwa
    bado na siha yake alipokuwa akisakatia kandanda timu ya
    bandari FC.
    Uk95…anakumbuka jinsi alivyokuwa akiwala chenga wachezaji
    wa timu pinzani.
    MASWALI
    1. Anwani Nizikeni papa hapa ni mwafaka kwa hii
    hadithi.Fafanua.[al 20]
    2. Anzeni mapema kuchangisha fedha za kusarisha
    maiti.
    a] Eleza muktadha wa dondoo hili. [al 4]
    Haya ni maneno ya mwenyekiti wa chama watu wa nyumbani
    walikuwa kwa Otii kando ya kitanda cha Otii ili kupanga mikakati
    ya mazishi. Hii ilitokea baada ya daktari kuwaeleza wamrejeshe
    Otii nyumbani kwa kuwa hakukuwa na matumaini ya kupata afueni.
    81.
    b] Walihitaji pesa za nini? [al 4]Walipaswa kununua jeneza,mavazi
    ya kumvisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya
    kuchukua maiti na waombolezaji kutoka hapa
    Mombasa hadi Kisumuasilia.
    c)Kwa kurejelea hadithi ya nizikeni papa hapa , eleza maafa
    yanayotokana na ujeuri na mapuuza.
    Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani walipoaanza
    mipango ya mazishi na kufanya michango ili kugharamia mipango
    ya kupeleka maiti ya Otii nyumbani.Otii alipendekeza azikwe pale
    Mombasa lakini hawakumsikiza kabla ya Otii kukata roho. Pia
    aliwakumbusha pendekezo lake la kuzikwa pale Mombasa,lakini
    bado hawakutilia pendekezo lake maanani. Walipokuwa safarini
    kuelekea Kisumu walipata ajali mbaya ambayo iliangamiza wengi
    na wengine wakapata majeraha mabaya.Wangemsikiliza Otii
    hawangepanga safari ya kwenda Kisumu na basi hakungekuwa na
    ajali hii ambayo ilileta maafa Zaidi.
    UK100….Rakiye Otii anamtahadharisha Otii dhidi ya kuwa na
    uhusiano na wasichana warembo kama Rehema Wanjiru lakini Otii
    alipuuza .
    Aliendelea na ule uhusiano akaambukizwa ugonjwa uliompeleka
    kaburini.
    MASWALI
    Methali ni nini? taja na ufafanue
    Methali zilizotumwa katika hadithi ya mama bakari.
    10.TULIPOKUTANA TENA
    ALIFA CHOKOCHO
    Hadithi hii inasimuliwa na Sebu,Msimulizi akiwa mkewe pamoja na
    rakiye Kazu aliyekuwa na mkewe pia,walikuwa kwenye Hoteli
    Rombeko. Maraki hawa walikuwa na mazoea ya kukutana kila
    mara walipopata wakati,kwa lengo la kubadilisha mazingira
    Kutokana na mazungumzo yao,ni bayana kuwa maraki hawa ni
    watani.Utani wao unawajumuisha wote wanne bila kuudhika huku
    wakijihusisha jamii zao.
    82.
    Siku hiyo walizungumzia kuhusu uchawi.Vicheko vyao vilidhihirisha
    uhusiano mwema,hali hii inaonyesha mlahaka uliokuwepo baina
    wane hao.
    Mazungumzo yalibadilika pale msimulizi alirejelea maisha yake ya
    awali ambapo alikuwa na kumbukizi ya raki yake wa utotoni kwa
    jina Bogoa.Msimulizi anasema kuwa yeye Bogoa waliyafanya
    mengi ya utotoni lakini walitengana baada ya kuhitimu miaka 19
    mwaka wa1966.
    Kazu anazungumzia kuhusu Bogoa aliyetoka sehemu za
    mate.Anaelezea kuwa Bogoa alijifuza usonari na alikuwa
    akikifahamu kitinya kama lugha Yake mwenyewe.Inasadifu kuwa
    Bogoa wanaye mzungumzia ni yuyo huyo mmoja.
    Hofu ya Sebu ilikuwa uwezekano wa Bogoa kukubali mwaliko kwa
    sababu anavyotueleza msimulizi ni kuwa aliipuuza nchi yake na
    hata kuwasahau wazazi wake.
    Miradi yao ilikuwa wakutane club Pogopogo,kwa watu wa kupata
    cha chini.Bogoa alimtambulisha mkewe Sakina kwa raki yake
    Sebu naye akamtambulisha Bogoa kwa mkewe Tunu.
    Bogoa anaturejesha katika maisha yake kwa uc hungu
    mwingi.Ilikuwa ni hadithi ambayo hakuwa amemsimulia yeyote
    hata mkewe.Anayakumbuka maisha aliyoyapitia kwa mlezi
    wake.Alinyimwa hata uhuru wa kucheza na badala yake akafanya
    ngumu.
    Wazazi wa Bogoa wanaonyesha hali ya kutoajibika majukumu yao
    kama wazazi.Hawakuwa na wakati na mtoto wao hata baada ya
    kumuachia mle hawakufaidia maisha yake .Bogoa anabaki kuwa
    na kisasi kuwa na kisasi na wakazi wake.
    DHAMIRA
    Mwandishi anawakashifu wazazi ambao hawayatekelezi
    majukumu yao ya uzazi.Wengi wa wazazi wanawaachia walezi
    majukumu yote bila kujali hisia za watoto wao.
    83.
    Bogoa utotoni anayapitia maisha magumu na hakuwa na
    wakumwelezea madhila aliyoyapitiaila ila tu aliangalia ndani kwa
    ndani.Hali hii inapalilia kisasi dhidi ya wazazi wake.
    MAUDHUI.
    1. Ulezi
    Jukumu la kila mzazi ni kumlea mtoto kwa njia ifaayo na
    kuyatekeleza mahitaji ya huyo mtoto.Jambo la msingi ni
    kumwelimisha na kumpatia mashauri.
    Wazazi wa Bogoa waliyakwepa majukumu yao na kumtwika
    mlezi ambaye alimdhulumu mwanao.Malezi hayo yanamfanya
    Bogoa kulipiza kisasi dhidi ya wazazi wake hata wanapoaga
    dunia hakuhudhuria mazishi yao..
    2. Ukatili
    Sinai alimtendea ukatili Bogoa kwa kumnyima fursa ya kucheza na
    wenzake.Fauka ya hayo alimpiga pindi tu alipochelewa
    kurudi.Babake Bogoa aliutenda unyama kwa kumpeleka
    mwanawe kwa mlezi bila kufuatilia maisha yake yalivyokuwa
    kwa mfadhili wake.
    3. Elimu
    Elimu ni mwanga kwa kila mja.Njia moja ya kuelimika ni kwa
    kupelekwa shule.Hata hivyo kuna elimu inayopitishwa na
    wanamrika(peer);mfano:Sebu alimfunza Bogoa kusoma mpaka
    akaweza kusoma hadithi nzima.Kulikuwa na mtazamo hasi
    kuhusu watoto wa kimaskini ambao ilisemekana kuwa hawastahili
    kusoma shuleni.Mtoto ambaye hakwenda shule alidhaniwa kuwa
    mtoro.
    4. Umaskini
    Sababu kuu ya umaskini kulingana na mwandishi ni idadi kubwa ya
    watoto.Wazazi wa Bogoa walikuwa na watoto takribani kumi na
    sababu ya kumpeleka Bogoa kwa mlezi ilikuwa ni kutowamudu.
    Ishara ya umaskini inadhihirishwa na vazi alilovalia msimulizi
    a n a s e m a . ” K i l i k u wa n i k i v a z i p e k e e c h a m t u n g i n i
    kwangu”.Hawakuwa na fedha hata za kununulia viatu.Vile vile
    hakuwa na pesa za kulipia nauli ndiyo maana walitembea kutwa
    hadi jijini.
    84.
    1. Uraki
    Uraki wa maraki haya ni wa dhati.Maraki hawa walikuwa
    wanakutana si mara moja kwani anasema kuwa …….`tulipenda
    kuja seka kubadilisha mazingira na kuonana na maraki
    z e t u . ” … ( U K 1 0 4 ) . K w a k u w a w a l i k u w a m a r a  k i
    wakubwa,waliwahusisha wake zao.Ni kutokana na mojawapo wa
    mikutano yao. Kazu anapomtaja Bogoa. Kutajiwa Bogoa kunaleta
    kumbukumbu katika mawazo ya Sebu.Anamkumbuka raki yake
    wa utotoni.Kutokana na mjadala ule ndipo wanapokutana tena.
    Maudhui mengine:
    1. Ukandamizaji wa watoto
    2. Uchawi
    3. Bidii
    4. Uwajibikaji
    5. Uhuru wa watoto
    6. Nafasi ya wazazi katika malezi.
    WAHUSIKA.
    a) SEBU
    Huyu ndiye msimulizi, jina lake halisi tunalitambua kutoka kwa
    wahusika wengi kama Kazu na Mkewe.
    a) Mtani
    Sebu pamoja na rakiye wanataniana kwa kiwango kikubwa bila
    kuudhika .Ni watani wa muda mrefu kwa sababu wanataniana
    kuhusu jamii zao.
    b) Ana mlahaka mzuri
    Kutokana na mazungumzo yao tunaelewa kuwa uhusiano wao ni
    mzuri.Anatueleza kuwa huwa wanakutana pindi wanapopata
    upenyo .Hali hii ndiyo iliyomfanya kuwa na uhusiano mwema.
    c) Mwaminifu
    Bogoa alimwaamini tangu wakiwa watoto.
    85.
    a) BOGOA.
    Raki wa utotoni wa msimulizi.
    Sifa:
    Msiri;
    Hakumwelezea Sebu shida alizokuwa akizipitia kwa mlezi
    wake.Hakuwaelezea wazazi wake madhila aliyokuwa
    akiyapitia.Wanafunzi wenzake hawakujua asili yake kwa maana
    hakuwaelezea walibaki tu kukisia.(UK 116)
    Mvumilivu;
    Aliyavumilia mateso kutoka kwa mlezi wake.Katika umri wake
    mdogo alifanyishwa kazi nyingi zilizopita umri huo.Kama
    anavyoeleza ni kuwa angechelewa,alitafutwa na kupigwa vibaya
    sana..(UK 116).
    Mwenye Bidii;
    Licha ya kupitia madhila hayo,Bogoa alikuwa mwenye
    bidii.Alijifunza kazi ya usonara na kuajiriwa.
    Ameajibika;
    Aliwajibikia jamii yake na ndoa yake ilikuwa imesimama imara,
    zaidi ya hayo ni kuwa watoto wake walikuwa wamekomaa.
    Mwenye Kisasi;
    Alikasirika kiasi cha kutorudi kwao tena,Hata mazishi ya wazazi
    wake hakuhudhuria.Alikuwa na kisasi na wazazi wake.
    MATUMIZI YA LUGHA
    a) Tashbihi
    Tamathali ya usemi ambayo msanii huvilinganisha vitu viwili au
    zaidi kwa kutumia maneno ya kulinganisha kama vile:Mithili
    ya,sawa na,ja,na mfano wa:
    · Kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga(UK
    109)
    · Kumtoka kama maji yanavyotiririka bombani.
    86.
    a) Uhuishi
    Uhuishi/Tashihisi/Uhaishaji ni tamathali ya usemi ambayo msanii
    huvipatia vitu visivyokuwa na uhai sifa walizonazo binadamu na
    kutenda kana kwamba vina uhai.
    a) Vicheko vilivyovuma na kuparamia kuta.(UK 107).Vicheko
    vinapatiwa sifa ya binadamu ya kuparamia kuta.
    b) Kuikimbiza furaha na kuileta huzuni(UK 109)
    c) Ukweli wenye makali yanayochinja bila huruma (UK 117)
    b) Nidaa
    Ni msemo unaoonyesha kushangazwa na jambo Fulani na
    huambatana na alama ya mshangao.
    a) …….na kuwatema watu hao huko magharibi!(UK 105)
    b) ……mimi ni binadamu mwenzako!(UK 105)
    c) …..hatukupata hata fununu ya kuwepo kwake(UK 110)
    c) Maswali ya balagha
    Haya ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika na
    hayahitaji majibu ya moja kwa moja.
    a) …..huoni kwamba unaniumiza?(UK 105)
    b) …..uchawi si sayansi?(UK 106)
    c) ……kabadilika vipi? (UK 111)
    d) Semi
    Haya ni mafungu ya maneno ambayo yanapotumika,hutoa maana
    nyingine badala ya ile ya maneno yaliyotumika.Hutumika ili
    kuipamba lugha .Kuna:
    NAHAU
    Huu ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la
    k u l e t a m a a n a i l i y o t o f a u t i n a m a n e n o h a y o
    yaliyotumiwa.Tofauti na msemo huwa na vitenzi.
    a) Napiga funda (UK 106)
    b) Kupiga funda (UK 114)
    87.
    MISEMO
    Hizi ni semi fupi fupi zinazotumiwa mara kwa mara kwa
    lengo la kuleta maana maalum.Mfano;
    Pua na mdomo(UK 108)
    11.MWALIMU MSTAAFU
    Dumu Kayanda ni mwandishi chipukizi mwenye uwezo wa kubuni
    hadithi ilio na upeo usiokadirika. Amekuwa mwalimu wa somo la
    Fasihi kwa muda katika shule mbalimbali.
    Mwalimu Mesi ndiye mhusika mkuu katika hadithi hili. Anwani hii
    inafaa kwa sababu hadithi inaelezea kuhusu maisha ya Mwalimu
    Mesi Kabla na baada ya kustaafu.
    Kutokana na kuwajibika kama mwalimu,Mwalimu Mesi alipewa sifa
    chungu nzima. Aliweza ‘kuwanyanga’ wanafunzi wake mpaka
    hatimaye wakawa watu wa kutajika. Wengine wakawa
    mawaziri,wabunge,marubani,wahandisi,madaktari na wengine
    wahasibu.
    Siku ya sherehe ya kumuaga shuleni,wazazi wa wanafunzi wa
    zamani na wampya walihudhuria na kumletea zawadi za aina
    tofauti tofauti. Hotuba zilizotolewa zilisheheni sifa isipokuwa
    hotuba ya Jairo iliyokuwa ya kumlaumu tu Mwalimu Mesi.Jairo
    alikuwa zuzu hata darasani , anamlaumu mwalimua eti
    alimpotezea muda wake na ndio kwa sababu yeye ni maskini.
    Mwalimu anampa Jairo zawadi zote lakini Jairo hana shukrani.
    Anakiona hicho kitendo cha kupewa zawadi kama kuaibishwa na
    Mwalimu. Jairo anawaleta mke na watoto wake kwa mwalimu
    kama zawadi. Mke wa Jairo alipewa nyumba kwenye kichumba
    cha mwalimu na akakaa na watoto wake.
    Jairo hakuwapitia kwa Mwalimu Mesi kuwaona jamaa yake hadi
    siku alipokiwa na tetesi kuwa mwalimu amemwoa bintiye. Kumbe
    ilisadifu kuwa mwalimu na kile kisichana walipoandamana kwenda
    kununua kitabu mjini, mwalimu akawa mgonjwa na Yule msichana
    akapelekwa shule ya bweni. Ilikua ni sababu tosha ya wenye
    umbeya kueneza uvumi kwa mwalimu na bintiye Jairo.
    Hawakuonekana na ni kwa sababu wameanza kuandika kurasa
    mpya za maisha yao pamoja.
    88.
    Anwani.
    Anwani hii MWALIMU MKUU inafaa kwa sababu hadithi mzima
    inazungumza kuhusu maisha ya Mwalimu mstaafu Mesi .
    Dhamira
    1.Mwandishi alikusudia kuonyesha umuhimu wa kuwajibika kazini
    kama alivyowajibika Mwalimu na mazao ya kazi yake
    yanaonekana.
    2.Mwandishi pia anadhamiria kuonyesha tofauti ya watu wa elimu
    maishani. Kuna tofauti ya watu waliosoma na wale ambao ni zuzu
    kama Jairo.
    WAHUSIKA
    Mwalimu Mesi
    1.Amewajibika
    Kutokana na kule kuwajibika, anapewa sifa chungu nzima .
    Wanafunzi wanaishia kuwa madaktari,, mawaziri, marubani n.k.
    Wengi wanahudhuria sherehe yake ya kumuaga na kumletea
    zawadi nyingi kama ishara ya shukrani.
    2.Karimu
    Anampa Jairo zawadi Zote alizoletewa katika sherehe ya
    kumuaga.
    Anakubali mke na watoto wa Jairo waishi kwake.
    Kisichana cha Jairo kilipofukuzwa shuleni kwa kukosa kitabu,
    waliandamana hadi mjini kukinunulia kitabu.
    3. Mwenye utu/ubinadamu
    Anaamini watu wote ni sawa, hakuna mtu nusu mtu. Anasisitiza watu
    ambao hawakuja kwa magari mazito pia wapewe nafasi ya kutoa
    hotuba walivyopewa wengine wa tabaka la juu. Jairo anapotoa
    hotuba yake, alimlaumu tu Mwalimu lakini hilo halikumkera
    Mwalimu.Anampa Jairo zawadi zote , anaamini jairo alizihitaji
    zaidi.
    89.
    4.Mwenye sifa tele
    Uk 120…Wanafunzi wake wote hao hawamsahau kwa nasaha
    zake, kwa insafu yake, kwa huruma yake, kwa hekima yake,kwa
    ustaarabu wake,kwa uadilifu wake ,kwa uwajibikaji wake, kwa
    nemsi yake,kwa ucheshi wake.
    Hotuba zao zilijaa sifa tele.
    JAIRO
    Alikua mwanafunzi wa Mwalimu msaafu ambaye mambo
    hayakumwendea vizuri.
    1.Mwenye Kulaumu
    Jairo alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Mwalimu Mstaafu. Yeye ni
    tofauti na wengine wengi, aliishia kuwa mtu ovyo . Hali yake ya
    umaskini inamfanya amlaumu Mwalimu eti alipotezea wakati kwa
    kumueka darasani na kumpa tumaini za uongo.
    2.Zuzu
    Hata baada ya kuwa shuleni kwa miaka yote ile hakuweza kuunga
    moja na moja. Pia alipata sufuri masomoni.
    3.Mcheshi
    i)Haelewi kwa nini Mwalimu alimshauri asilewe ilhali anaamini
    tembo inampa raha ya kuishii. Alisema kuwa alipolewa hata
    akitembea bila viatu na kujikwaa au kudungwa na miiba, hakuhisi
    kitu.
    ii)Hakuelewa pia kwa nini kuepukana na ulevi, kusubiri hadi ndoa
    ndipo ‘kuchana ngazi.’
    iii)Anapeleka mkewe na wanawe kwa Mwalimu na kumpa kama
    zawadi.
    MKE WA MWALIMU
    1.Mwenye utu
    Anakubali mke wa Jairo na wanawe waishi kwao. Anamtunza kama
    bintiye. Anamwambia , “Hapa paite nyumbani. Upaone hapa
    kwenu kama si nyumbani pako. Ukae upumzike. Ukae uone raha ya
    kuishi.”
    90.
    2.Mwenye bidii/Anauhusiano mzuri na watu
    Wanaandamana na mke Wa Jairo kwenda kondeni kupanda
    mbegu, kupalilia, kumwagia mazao kondeni mbolea. Pia walienda
    k u t e k a m a j i n a k u t a f t a k u n i . Wa l i c h u m a k u n d e n a
    mchacha,mabenda kondeni wakiziambua na kuzikata mboga hizo
    pamoja pale uani.
    MKE WA JAIRO
    1.Mvumilivu
    Mwandishi anaeleza maisha ambayo mkewe Jairo ameyapitia.
    “Katika maisha yake na Jairo, ameonja ladha zote za dhiki, thakili,
    bughudha na kero. Hakuna mwanamke anayejua kumezamate
    machungu kama Mke wa Jairo.”
    2.Mtiifu
    Anapopelekwa kwa Mwalimu kama zawadi, Mwalimua
    anamshauri arudi kwake lakini anakataa. Anasema “sharti ni mtii
    mume wangu. Mume ni mume hata akiwa gumegume.” Mwalimu
    aliposisitiza, mke wa Jairo alimweleza kuwa hawezi kwenda
    kinyume na amri ya Jairo mume wake.
    3.Mwenye bidii
    Waliandamana na mke wa Mwalimu kondeni kupanda, kupalilia,
    kuteka maji vijitoni na kutafta kunikuni.
    WANAFUNZI NA WAZAZI
    1.Ni wenye shukrani
    Wanaka katika sherehe ya kumuaga Mwalimu kwa wingi wakiwa
    na zawadi chungu nzima.
    2.Karimu
    Wanamletea Mwalimu zawadi chungu nzima.Wanaendesha
    magari makubwa na ni waadilifu kwa sababu walifuata ushauri wa
    walimu wao. Wale ambao hawakupata elimu wameishia kuwa
    maskini , walevi ambao hawana mbele wala nyuma. Pia hawana
    maadili mema.
    91.
    3.Uzuzu/Ujinga
    Hata baada ya kuhudhuria shule ya msingi, Jairo hawezi kuunga
    moja na moja. Haoni umuhimu wa elimu. Anamlaumu Mwalimu Mesi
    eti alimpotezea muda wake bure shuleni kwa kumwambia kila
    uchao kwamba ataimarika na hakuwahi imarika. Anamlaumu
    Mwalimu kwa kumshauri asinywe tembo ilhali anaamini hiyo tembo
    ndio humpa raha ya kuishi. Anaamini kinyume cha nasaha za
    Mwalimu ndio utamu na uhondo wa maisha. Uzuzu unamfanya
    awapeleke mke na watoto wake kwa Mwalimu kama zawadi.
    Anaona soni kupokea zawadi kutoka kwa Mwalimu. Haelewi
    mbona akapewa zile zawadi ilhali alizihitaji zaidi.
    MAUDHUI
    Kuwajibika
    Hii inadhihirika zaidi siku ya sherehe za kumuaga Mwalimu Mesi
    pale shuleni.
    Waliohudhuria sherehe hii walikua wengi mno. Mwandishi asema
    “walika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki wa mchuano
    wa soka wa kuwania kombe la dunia kutokana na kazi nzuri ya
    Mwalimu, wanafunzi wake waliishia kuwa madaktari, wabunge n.k.
    Hotuba zilizotolewa zilisheheni sifa kwa Mwalimi Mesi.
    Elimu
    Mwandishi anatuonyesha umuhimu wa Elimu.watu waliomakinika
    k a t i k a e l i m u h a t i m a y e w a l i k u w a ‘ w a t u ‘ , w a k a w a
    mawaziri,wabunge, marubunu n.k. Wakawa pia wanaendesha
    magari ya nguvu. Elimu unawafanya watu kuwa watu wa maana
    ,watu bora kwa hadafu. Lakini wale ambao hawakumakinika,
    hutumia yao duni, maisha ya umaskini. Pia wana mitazamo hasi
    kuhusu maisha.
    Utabaka
    Utabaka unasababishwa na kupata au kukosa elimu. Waliosoma
    na kufaulu katika elimu, wanaishi kama ‘watu’. Wanapata kazi
    nzuri, zinzwapa mshahara.
    92.
    Ukarimu
    ukarimu unajitokeza wakati Mwalimu Mesi anampa Jairo zawadi
    zake zote, anasema “mimi nimeamua kwa hiari yangu kukupa
    wewe zawadi hizi.”
    Mwalimu na mkewe (Bi Sera) ni karimu,wanawakaribisha mke na
    watoto wa Jairo kwao.
    MBINU ZA LUGHA
    Kuorodhesha
    Mwandishi anatumia mbinu ya kuorodhesha mfano;
    Uk 120: Wanafunzi waje wote hao wanafunzi wake hawamsahau
    kwa nasaha zake,kwa insafu yake, kwa huruma zake ,kwa hekima
    zake, kwa ustaarabu wake, kwa uadilifu wake…
    Uk 121:Wanafunzi wake waliokuwa bado wanasoma kwenye shule
    hiyo waliimba tele, nyimmbo za jamii mvbalimbali, wakacheza
    zeze,mariamba, lelemama, mdundiko, violoni.
    Uk 122:…sikwambii haya madude makubwa waliokuja kututisha
    nayo akina Bariki,Festo, Mshamba ,Nangeto na hali kadhalika.
    Tabaini
    Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzola mchanga,si
    makubadhi ,si meza na samani aina aina, si fedha
    Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzolea mchanga,si
    makubadhi,si meza na samani aina aina,si fedha.
    Takriri/Uradidi
    Uk 126:Wanafunzi wako wote hao wanafunzi wake.
    Uk 128:Jairo aliambiwa , akaambiwa na kuambiwa na wajuao.
    Tashbihi
    Uk 120:…mvi zimemkaa kwa haiba kama theluji kwenye mlima
    Kilimanjaro.
    Uk 121:…walifurika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki
    wa mchuano.
    93.
    Uk 122:Kichwa chake chenye upana killing’aa utosini kama sufuria
    kwenye duka la Buniani.
    Uk 125:…wakapokeza hotuba hio kama huizi kutoka kizazi kimoja
    hadi kingine.
    Uk 129:…kimenawiri kama ua linalotimbuka kudamu.
    Uk 129:Aliona madodo yamesimama kifuani kama kanzi mbili za
    mwanamasumbwi.
    Uk 129:…kiuno kimechukua umbo mduara kama cha nyigu.
    Tashhisi
    Uk 120:Alijaaliwa mvi nyeupe zilizojianika kwenye kichwa chake
    kidogo.
    Methali
    Uk 121: Anayo maneno ya kuweza kumtoa nyoka pangoni.
    Uk 123: : Kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.
    Uk 128:Alikuwa ametuma jongoo na mti wake.
    Jazanda
    Matumizi ya maneno yenye maana che.
    Uk 121:…wenzao hao waliokuwa wamekua watu.
    Uk 121:…lakini nadhani ni jambo la busara kutotia mchanga
    kitumbua.
    Uk 129:Walitafuta kitabu cha maisha na kuanza kuandika kurasa
    mpya za maisha yao pamoja.
    Uk 124:…kusubiri hadi ndio ndipo kuchuna ngozi.
    Kinaya
    Kinyume cha matarajio
    Uk 123: Ni kinaya kwa Jairo hakuona sifa nzuri ya Mwalimu Mesi.
    Yeye anamuona kama kikwazo kikubwa kwake. Kama yeye Jairo
    anaishi maisha duni kwa sababu ya Mwalimu Mesi.
    Uk 126:Ni kinaya Mwalimu Mesi kumpongeza Jairo kwa hotuba
    yake kumhusu ambayo ilijaa kumlaumu Mwalimu kisha Mwalimu
    Mesi anamueleza akifa mwanzo azungumze siku ya mazishi yake.
    Uk 126:Ni kinaya Jairo anapopeleka mke wake na watoto kwa
    Mwalimu Mesi kama zawadi.
    Uk 127:Ni kinaya kwa mkewe Mwalimu Mesi (Bi Sera)kumkaribisha
    mke na watoto wa Jairo kwao “Mwachie akae huyu binti na watoto
    wake, tutawatunza.”
    94.
    Msemo
    Uk 121:Wanafunzi wake wa zamani waliopewa kisogo na dunia
    Uk 126:Hakuna mwanamke anayejua kumeza mate machungu.
    Mdokezo/Kauli isiyokamilika
    uk 120:kisa na maana ni huyo Mwalimu Mesi.
    uk 123:kwamba kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.
    UK 125:…umefanya makosa makubwa sana.
    Uk 125:…hamna mwendawazimu wala mahaka kati yetu.
    Uk 126: “Badala ya ngojera nyingi za huyo anayemwita si siri au
    siri sijui.
    Sadfa(matukio mawili yanayotokea kwa pamoja).
    Inasadifu kuwa baada ya Mwalimu kuondoka na kile kisichana
    kununua kitabu hakuonekana tena. Watu wakakiri eti Mwalimu
    alikua amekioa kile kisichana. Kumbe wakati huu Mwalimu alikua
    akiugua na alikua ndani(nyumbani) wakati wote huo na ndio
    sababu hakuonekana.
    Maswali
    1.Onyesha umihimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya
    Mwalimu Mtaafu.
    i)Mwalimu Mesi
    ii)Jairo
    iii)Mkewe Jairo
    iv)Wanakijiji
    (al 20)
    2.Fafanua maudhui yoyote manne katika hadithi hii. (al 20)
    Ukarimu
    Mwalimu Mstaafu ni mkarimu. Hii inadhihirika anapopokea zawadi
    kutoka kwa wazazi na wanafunzi na kumpa Jairo zote.
    Pia Mwalimu na mke wake ni wakarimu kwa mke wa Jairo na watoto
    wake. Waliwapa nyumba akae na watoto wake. Waliwachukua
    kama binti yao. Bintiye Jairo alipofukuzwa shuleni kwa kukosa
    kitabu, Mwalimu Mstaafu alimnunulia.
    95.
    Utabaka
    Utabaka umesababishwa na kupata au kukosa elimu. Waliopata
    elimu walipata kazi nzuri kama za uwaziri ,ubunge, udaktari, urubani
    n.k. kazi zilizo na mshahara mzuri. Wakawa wanaishi maisha mazuri
    na kuendesha magari ya nguvu. Wale nao ambao walikosa elimu,
    waliishi kuwa maskini na walevi.
    Kuwajibika
    Hii inadhihirika zaidi siku ya sherehe za kumuaga Mwalimu Mesi.
    Kutokana na kuwajibika kwake kama Mwalimu,wanafunzi wake
    wa n a f a u l u m a i s h a n i . Wa n a p a t a k a z i n z u r i k a m a z a
    udaktari,ubunge,uwaziri n.k. Hii ndio sababu walikuja kwa wingi
    kumshukuru Mwalimu Mesi. Hotuba zao pia zilijaa sifa tele.
    Bidii
    1.Mwalimu anajibidiisha katika kuwafunza na kuwashauri wanafunzi
    wake.
    2.Wanafunzi walifanya bidii na kufaulu mitihani yao.
    3.Mkewe Mwalimu na mkewe Jairo wana bidii pale kondeni wanapo
    panda mbegu,wanapalilia,wanateka maji.
    12.MTIHANI WA MAISHA
    Eunice Kumaliro ni mzaliwa wa Kenya. Mshauri na mtaalam wa elimu
    aliyeandika vitabu kadhaa.
    Muhtasari
    Je,Samueli alikuwa amepita mtihani wake wa Elimu? Kuanguka
    mtihani wa elimu ni kuanguka pia mtihani wa maisha?
    Samueli ambaye ni mhusika mkuu katika hadithi anaenda shuleni
    kuchukua matokeo yake ya mtihani. Akiwa pale foleni nafanya moyo
    wake kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa alikuwa amepita mtihani
    wake vizuri.
    Kule ndani ya osi , Mwalimu Mkuu ameketi pale na anapuuza
    kuwepo kwake osini humo. Hatimaye anamtupia Samueli stakabadhi
    ya matokeo yake.
    Samueli anapotambua alivyokuwa amefeli mtihani wake,
    anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo yake kwa dai ya
    kutokamilisha kulipa karo ya shule.
    Samueli haoni haja ya kuishi tena. Anakata kauli kujitosa majini afe.
    Hakuwa tayari kupata aibu kutokana na matokeo yake mabaya.
    96.
    Mamake Samueli ana matumaini kuwa kuanguka mtihani wa elimu
    si kuanguka mtihani wa maisha. Anamshika Samueli mkono na
    wanaelekea nyumbani.
    Anwani
    Anwani ya hadithi hii, MTIHANI WA MAISHA inaoana na yale
    yaliyomo. Kupitia kwa mamake Samueli, mwandishi anaonyesha
    kuwa kuna maisha hata baada kuanguka mtihani wa elimu.
    Kuanguka mtihani wa elimu sio kuanguka mtihani wa maisha.
    Dhamira
    Mwandishi alikusudia kuonyesha;
    1.Kuanguka mtihani wa elimu sio mwisho wa maisha. Bado kuna
    matumaini.
    2.Umuhimu wa kumakinika katika masomo kwani athari za
    kuanguka mtihani ni hasi.
    MAUDHUI
    Ukatili
    Samueli analinganisha babake na hayawani ambaye anaweza
    kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Samueli alipofeli mtihani
    wake, anavunjika moyo na kuona maana ya kuishi. Anakata kauli
    ya kujiangamiza kwa kujitosa majini. Babake hata baada ya
    kumuona mwanawe katika hali ya kuvunjika moyo, hakumhurumia,
    badala yake anaamrisha watu wamuache ajitose majini afe. Pia
    anampa kamba atumie kujitia kitanzi.
    Ucheshi
    Samueli ni mcheshi. Anachekesha anaposema udongo uliowaumba
    babake na mamake ni tofauti na ndio sababu mama angeweza
    kuelewa kidogo atakapojua amefeli mtihani lakini baba hawezi.
    Anapomwangalia Mwalimu Mkuu, anamwona ni kama aliyezidiwa
    na maumivu au anayepaswa kufanyiwa oparesheni ya ubongo na
    anayehitaji maombi.
    Anapoamka kuchukua hatua ya kujiangamiza ,anatazama juu
    kumpasha Muumba wake ujumbe kuwa alikuwa njiani akielekea
    mbinguni. “Naja huko juu mbinguni mapena kidogo Baba.
    Nitengee nafasi. Nimeruka foleni…”
    97.
    Nafasi ya Mwanamke
    Mwanamke anapuuzwa katika jamii hii. Inathibitishwa na mtazamo
    wa baba kupitia elimu. Ingawa baba aliyaonea fahari mafanikio
    ya binti zake, aliwaona kama wanawake tu. Fahari yake ya dhati
    ilikuwa katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Samueli
    haamini vipi angeweza kushindwa katika mtihani na dada zake
    ilhali ni wanawake.
    Mwanamke kupitia kwa mhusika mama amechorwa kama aliye na
    utu na matumaini. Anamshika Samueli mkono na kumwambia
    waende nyumbani na kumweleza maneno ya kumpa tumaini. Pia
    anapenda amani na ni mshauri mwema. Anamshauri mumewe
    aende shuleni wasuluhishe sintofahamu kuhusu karo.
    Kufa moyo/kuvunjika moyo
    Samueli alipoanguka mtihani hakuona haja ya kuendelea kuishi na
    anaamua kujitosa majini afe. Anasema, “Acha nijiondokee duniani
    niwaachie wafanisi wafanikiwe.” Katika ujumbe wake na Muumba
    anasema itabidi aende mbinguni kwa sababu stahamala
    zimekwisha.
    Elimu
    Elimu ni muhimu maishani. Wasichana katika jamii hii wanafanya
    vizuri kuliko wavulana. Wavulana wanamchezo shuleni (Mahoka)
    unaochangia kuanguka kwao. Hakuna anayepewa matokeo yake
    ya mtihani kabla ya kumaliza kulipa karo. Athari za kuanguka
    mtihani ni kama vile aibu na hata kujiangamiza.
    WAHUSIKA
    SAMUELI
    Ndiye mhusika mkuu
    Mcheshi
    1.Anaposema, “labda Mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu. Labda
    anapaswa kufanyiwa operesheni ya ubongo ama anahitaji
    maombi hasa atakuwa na akili razini tena.”
    2.Samueli anasema kuwa mamake na babake wameumbwa kwa
    aina tofauti kabisa ya udongo.
    3.Anamuarifu Muumba kuwa yumo njiani akienda mbinguni basi
    atengewe nafasi kwani ameamua kuruka foleni.
    98.
    Mwenye Matapo
    Anaposema yeye hana moyo wa bua. Kile asomacho ndicho kijacho
    kwenye mtihani. Anaelewa kuwa yeye si mwerevu sana laikini
    anajua kupanga mikakati na pia anaamini ana bahati ya mtende
    anaamini kuwa amepita mtihani wake vyema na kuwa motokeo
    yake yangemshtua Mwalimu mkuu ambaye hakuwa na imani naye.
    Mwongo
    (uk 137) Samueli anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo
    yake kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.
    Mwoga
    Uk 133: Anaogopa anapoingia katika osi ya Mwalimu mkuu.
    Woga unajitokeza kutokana na anavyozungumza/anasitasita.
    “Mwa…limu nimekuja kuchu…chukua matokeo…” “samaha…ni.
    Waa…zazi wangu.” Samuel anatetemeka anapomwona babake
    pale kwenye bwawa(uk 132)
    Mwenye machoka
    (uk 134)ni kutokana na tabia hiyo pale shuleni ndipo akapewa jina
    ‘Rasta’
    Kufa moyo/kuvunjika moyo
    Kuanguka mtihani kwa Samwueli si jambo alilokuwa akitarajia.
    Alikuwa ana uhakika kuwa amepita mtihani wake.Jambo hili
    ameliona kama la kumletea aibu mbele ya wazazi wake,
    alivyopendekeza Samueli.
    Anakata kauli kujitosa majini afe. Hakuna maana ya kuuendelea
    kuishi. Anasema “Acha nijiondokee duniani niwaachie wafanisi
    wafanikiwe anamwambia Mungu kuwa amekosa stahamala.”
    MAMAKE SAMUELI
    Mwenye utu
    Mamake Samuel anaka kwenye bwawa la maji alipokuwa
    amejitosa Samuel, anamshika Samuel mkono na kumwomba
    waende nyumbani. Anamwambia Samuel maneno ya kumpa moyo,
    “huwezi kushindwa na mtihani wa shule na vilevile kushindwa na
    mtihani mwisho.
    99.
    Mwenye Matumaini
    Hata kana kwamba Samuel ameanguka mtihani wa shule, mamake
    Samuel anaamini kuwa kuna matumaini hata baada ya kuanguka
    mtihani huo. Anaamini Samuel hajaanguka mtihani wa mwisho.
    Anaamini pia kuwa Mungu hamkoseshi mja wake yote. (UK 139)
    Mwenye Kuelewa Mambo
    Samuel anasema kuwa kweli amemusaliti mamake kwa kuanguka
    mtihani lakini mamake tofauti na babake, ataelewa.
    Mpenda Amani
    Samuel anapomdanganya babake kuwa hakupata matokeo ya
    mtihani wake ati kwasababu hajamaliza kulipa karo, anakereka.
    Mamake Samuel anaingilia kwa upole na kumshauri mume wake
    amuone Mwalimu mkuu ili wasuluishe suitofahamu hiyo.
    BABA SAMUEL
    Katili
    Samueli anamlinganisha babake na hayawani ambaye anaweza
    kumrarua mtu na kumla mzimamzima.
    Baada ya Samueli kuanguka mtihani alikuwa na kipindi kigumu na
    anaamua kujiangamiza. Babake hakuwa na huruma naye hajali
    kama atajitosa maji afe. Anasema “mnamzuia kwa nini? Mwachie
    ajitose majini kama anataka. Ana faida gani huyo? Sikuzaa
    mwana nilitoa tu maradhi tumboni.” Uk 139 Anampa Samueli
    kamba aitumie kujiangamiza.
    Mwenye moyo mgumu
    Babake Samueli ana moyo usiojua kusamehe. Anaamrisha watu
    wamuache ajitose majini afe. Anampa Samueli kamba ajitie
    kitanzi ikiwa anaogopa kujitosa majini. Samueli anasema kuwa
    mamake ataelewa atakapojua kuwa Samueli amefeli mtihani.
    Lakini babake aliyeumbwa na udongo tofauti hawezi.
    Amewajibika
    Aliweza kulipa karo yote ya shule.
    100.
    MWALIMU MKUU
    Mwenye madharau
    Samueli alipoingia katika osi yake,anachukuwa muda mrefu sana
    kuinua uso wake kumuangalia Samueli. Baada ya kuzichambua zile
    stakabadhi za matokeo, anatoa moja na kumtupia Samueli.
    Anamtupia kwa mtu anavyomtupia mbwa mfupa.
    Amemakinika kazini
    Hakuamini Samueli alipomwelezea kuwa amekamilisha kulipa
    karo, alitumia “daftari la karo” kuhakikisha. Anasema mali bila ya
    daftari hupotea bila ya habari. Ndio maana ameweka daftari la
    kuweka kumbukumbu ya wanaodaiwa karo na waliolipa karo.
    MBINU ZA UANDISHI
    Tashbihi
    Uk 131:waliokuwepo waliotoka wamenywea kama kuku walionoa
    maji ya mvua.
    Uk 132:akitoka ndani atakuwa akitembea kama fahali.
    Uk 131:amamtupia kama mbwa anavyomtupia mbwa mfupa.
    Uk 137:anamuona baba akilini kama hayawani.
    Uk 135:imekwenda kama chendacho kwa mganga kisichokuwa na
    marejeo.
    Tashhisi/uhaishaji/uhuishi(personication)
    Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye
    uhai(sifa za kibinadamu).
    Uk 134:Nzi wa kijani ya samawati waliokula wakashiba.
    Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unampokea kwa
    vigemo.
    Uk 135: Safu sa ya D na E ilimkodolea macho bila kupesapesa.
    Uk 137:Ilimuradi mawazo yana mwadhibu sasa.
    Uk 138:Alitupia jicho safu ya maji akaona yanasumbuka na
    kuhangaika.
    101.
    Msemo
    Uk 132:Uso wake wenye makunyanzi ulipiga mapeto.
    Uk 133:Anakitazama kidole cha Mwalimu mkuu kupiga masafa.
    Uk 135:Juhudi zake zimegonga ukuta.
    Uk 137:Nina kuambulia patupu.
    Uk 139:…huhu kila mtu akipigwa na kibuhuti.
    Kichanganya ndimi
    Kutumia zaidi ya lugha moja tofauti.
    Uk 132:come on
    :yes
    Utohozi
    Kuswahilisha maneno/kutamka maneno yasiyo ya Kiswahili kama
    ya Kiswahili.
    Uk 133: Bodi,operesheni.
    Maswali balagha
    Maswali yaliyoulizwa bila ya kutarajia majibu.
    Uk 131: Mtu angesemaje ati? Wanafunzi na wakati huo huo
    wanasononeka?
    Uk 133: Nazo fedha ulitoa wapi mtoto pale ulipo.
    Uk 135: Karo yote niliolipa iwe bure? Pesa aliyolipa baba tusome
    imekwenda bure?
    Uk 136: Ali umefeli mtihani ? sasa nitafanya nini?
    Methali
    uk 132:Mdharau biu hubiuka.
    uk 132:Usione wembamba wa reli kwani gari moshi hupita juu
    yake.
    uk 135:Imekwenda kama kiendacho kwa mganga kisichokua na
    marejeo.
    uk 139: Mambo ni kuganga huenda yakaja.
    102.
    Uzungumzi nafsia
    Mhusika hujizungumzia ama kwa kuongea au kuwaza bila
    kukusudia kusikika na yeyote.
    Uk 132:mimi tangu hapo najijua bwana. Sina moyo wa bua. Mtihani
    haunibabaishi sana.
    Uk 132:hajawai kuniamini huyo hambe. Lakini mimi mwenyewe
    najiamini. Lazima mtu ajiamini… au sio?
    Uk 135: Hivyo ndivyo kusema lolote wala chochote . kwamba mimi
    si lolote wala chochote. Kwamba mimi si chochote wala lolote
    katika medani ya masomo?
    Mdokezo/usemi usiokamilika
    Uk 132:tena angaa sikukutana na paka mweusi njiani siku zote za
    mtihani…
    Uk 133:…chukua matokeo…
    Uk 135:si mjinga mimi. Najua vitu vingi tu…
    Uk 136: Mama ataelewa lakini baba…
    Sadfa
    Matukio mawili au zaidi yanayotokea kwa pamoja bila ya
    kupangwa.
    Uk 135:Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitaka
    kujitosa majini ili afe, siku hiyo ilikua tofauti kwani wachunga
    wapitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni hawakuwepo. Ikawa
    rahisi kuweko kujitosa majini.
    Uk 138: Inasadifu pia kuwa baada ya Samueli kujitosa majini na
    kupiga mikupuo kadhaa ya maji, mwanamume mmoja akawa
    ameachwa na basin na akaamua kutumia njia karibu ya kamwokoa
    Samueli.
    Taharuki
    1.Kuna wanafunzi waliotoka osini mwa Mwalimu mkuu wakiwa na
    furaha na huku machozi yanawatoka. Msomaji anabaki hata hamu
    ya kujua ikiwa walikuwa wamepita mtihani au la.
    2.Msomaji pia angetaka kujua ikiwa Nina alimuacha Samueli
    kutokana na vituko vyake au la.
    3.Msomaji anabaki na hamu ya kutaka kujua maisha ya Samueli
    yaliendelea vipi. Je alifaulu maishani. Baba alibadilika na
    kumsamehe .
    4.Kuanguka mtihani wa elimu na kuanguka mtihani wa maisha?
    103.
    Maswali
    1.Andika sifa za wahusika hawa kama zinavyojitokeza katika
    hadithi ya mtihani wa maisha.
    i)Samueli
    ii)Babake Samueli
    iii)Mamake Samueli
    iv)Mwalimu Mkuu
    Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Mtihani wa Maisha.
    Mwanamke amepuuzwa katika jamii. Hii inadhibitishwa na
    mtazamo wa baba kupitia elimu. Ingawa baba aliyaonea fahari
    mafanikio ya binti zake,aliwaona kama wanawake tu. Fahari yake
    ya dhati ilikua katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu.
    Samueli hakuamini vipi angeweza kushindwa katika mtihani na
    dada zake ilhali ni wanawake.
    Mwanamke ni mpenda amani na mshauri mwema. Anamshauri
    mumewe aende shuleni wasuluhishe sintofahamu kuhusu karo
    Pia ni mwenye utu.Anamshika Samueli mkono na kumwambia
    waende nyumbani. Anamwambia maneno ya kumpa tumaini.
    13. MKUBWA
    Na Ali Mwalimu Rashid
    UFAAFU WA ANWANI MKUBWA
    Neno mkubwa linatokana na kivumishi ‘–kubwa’ ambalo lina maana
    ya kuzidi kwa umbo au kimo; -siyo ndogo. Pia neno hili lina maana ‘-
    enye kwisha kukua’ au ‘kuwa juu’.
    Anwani ‘Mkubwa’ inaaki kazi hii kwani yafuatayo ni mambo yaliyo
    wazi zaidi;
    F Msimulizi anatueleza kuhusu mhusika mkuu kazini aliyeitwa
    Mkubwa. Alikuwa anajihusisha na biashara ya kuuza pweza wa
    kukaanga. Hii ndiyo biashara iliyompa kipato na faraja.
    F Mkubwa alipoingia uongozini alikuwa na madaraka makubwa.
    Alikuwa na uwezo uliozidi. Viongozi walipapata pasipoti za
    kidiplomasia ziliwawezesha kutosachiwa bandarini wala
    kwenye uwanja wa ndege.
    104.
    F Uovu wa Mkubwa ulikuwa umezidi. Aliweza kumwingiza raki
    yake Mkumbukwa kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya.
    Mkumbukwa aliponaswa na kutiwa ndani kwa kupatikana na
    mkoba uliojaa dawa hizo alijuta mno. Majuto yake yalikuwa
    makubwa.
    F Ushawishi wa Mkubwa ulikuwa umezidi. Aliweza kumtoa
    Mkumbukwa ndani baada ya siku tatu. Pia alipewa mzigo wake
    ukiwa katika hali ile ile.
    F Baada ya Mkumbukwa kutolewa ndani , aliichukia sana
    biashara ya kuuza dawa. Aliapa na Mola kuwa hatofanya tena
    biashara hiyo tena.
    F Mkubwa alipojilaza kwenye kochi na usingizi kumchukua anaota
    kuwa vijana wameongezeka mjini wanaosinzia ,wengine hali
    yao imedhooka sana na wizi umewazidi mitaani.
    F Mshituko wa Mkubwa ulizidi alipoona kuwa watoto wake wa
    kiume walikuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wameandikwa
    kwenye nyuso zao ‘mla unga’ jambo liliomfanya chizi.
    DHAMIRA YA MWANDISHI
    Mwandishi amelenga kupiga vita biashara haramu ya uuzaji wa
    dawa za kulevya au “kuuza unga”. Kupitia kwa Mhusika Mkubwa
    tunagundua kuwa viongozi ndio walanguzi wakuu wa dawa hizi.
    Viongozi wawa hawa huwatafuta vijana ambao huzipeleka dawa
    hizo kwa wateja. Wanaoumia zaidi ni vijana ambao wanaponaswa
    hutiwa ndani huku walanguzi halisi wakiufurahia uhuru wao nje.
    WAHUSIKA
    1. Mkubwa – alikuwa muuzaji wa pweza wa kukaanga kabla
    ya kuingia kwenye uongozi alikoingilia biashara haramu ya
    kuuza dawa za kulevya. Ana sifa zifuatazo:
    a) Mwenye bidii- alikuwa akishughulisha na kazi ya kuuza
    pweza wa kukaanga na baadaye akauza kipande cha ardhi
    ili kuingia uongozini.
    b) Mwenye utani- anamtania utingo kuwa huwa haogi jambo
    lililomfanya utingo kukimia kwa kuchekwa na abiria.
    c) Ni mtambuzi- aliweza kuelewa maana ya unga japo
    hakuwahi tu kuona vituko vyake.
    105.
    a) Mwenye utu- alimpigapiga kijana mbwia unga aliyekuwa
    ameinama kama kwamba anarukuu na kumuuliza iwapo
    anaumwa.
    b) Mwenye tamaa ya mali- alipotanabahi namna viongozi
    wanavyotajirika kwa kuuza unga , maneno ‘unga na utajiri’
    yalimkaa moyoni kiasi chake kukosa usingizi usiku huo.
    c) Ni maskini- alikuwa akifanya biashara ya kuuza pweza
    iliyokuwa na kipato kidogo . vilevile kabla ya kupata uongozi,
    alikuwa na suruali na shati kipande papa
    d) Ni sadi- baada ya kutia na kutoa, aliamua kufanya
    biashara haramu ya kuuza dawa za kulevya biashara
    ambayo huonekana kama ya kishetani. Vile vile alitoa kiasi
    kikubwa cha pesa ili kuwashawishi wapiga kura kumpendelea
    na ndipo akaupta ushindi.
    e) Mwenye msimamo dhabiti- baada ya kuyatia moyoni
    maneno aliyopewa na kijana yule kuhusu utajiri na unga
    aliamua kutafuta kwa udi na uvumba na ndipo akamwendea
    rakiye kwa jina Mkumbukwa.
    f) Ni msiri- mwanzoni hakumweleza Mkumbukwa sababu yake
    kuutafuta uongozi.
    g) Mwenye wasiwasi- aliogopa kuwa huenda kisomo chake
    kingemzuia kupata uongozi.
    2. MKUMBUKWA – ni rakiye Mkubwa aliyejitwika jukumu la
    kuwarai watu ili wampigie Mkubwa kura.
    a) Raki wa dhati- Mkumbwa alimwendea kwa mawaidha
    baada ya kuamua kuugombea uongozi na ndipo
    Mkumbukwa akamshauri Mkubwa augombee.
    b) Mkakamavu – alimweleza Mkubwa bila kupepesa macho
    wala kugugumizi kuwa pesa na ukaragosi wa chama ndiyo
    mambo muhimu pale Mchafukoge yatayomwezesha
    kuupata uongozi.
    106.
    c) Mwenye kutimiza ahadi- alimwambia Mkubwa kuwa
    akitafuta milioni kumi kisha ampe yeye ataupata uongozi na
    kuapa kuwa iwapo ataukosa amuue.
    d) Ni mwenye bidii- baada ya Mkubwa kujaza fomu; alianza
    kazi ya kuingia /kupita nyumba baada ya nyumba kumtafutia
    kura mkubwa.
    e) Mwenye busara- alifahamu ka kuwa ili kufanya kazi vyema
    ni lazima angemtafuta Bi Kibwebwe (Sada) na kumhusisha
    katika harakati za kumtafutia Mkubwa kura.
    a) Mwenye majuto- aliponaswa na askari wa kitengo cha
    kupambana na dawa za kulevya alijuta kimoyomoyo.
    b) Mwenye kulalamika- alipotiwa ndani alikuwa
    akilalamika kupuuzwa kwa haki za mahabusu.
    Zoezi
    1. Fafanua sifa za wahusika hawa.
    a) Sada
    b) Vijana wabwia unga
    c) Askari
    1) ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA
    F Vijana wanaolangua dawa za kulevya(unga) huishi kwa
    woga huishi kwa mfano yule kijana baada ya kumrushia
    Mkubwa maneno aliogopa wenyewe wasije wakamwona.
    F Vijana wabwia unga(wanaotumia dawa hizi) hugeuka
    karakana za matusi. Km yule kijana mbwia unga alimuuliza
    Mkubwa kijeuri “kwani tunakula kwa babako? Vile vile kijana
    aliyekuwa kichochoroni alimwita Mkubwa juha.
    MAUDHUI
    Maudhui ni mengi yaliyomo katika kazi. Haya ni masuala
    yanayoangaziwa na mwandishi wa kazi husika.
    Mwandishi ameangazia maudhui yafuatayo;
    107.
    F Vijana wanaozitumia dawa hizi hugeuka na kuwa mazuzukm
    kijana mwingine aliyekuwa kichochoroni alikuwa
    akitokwa na denda mdomoni huku amefumba macho.
    F Vijana wabwia unga huota ndoto za kiajabu – kwa mfano
    kijana aliyekuwa kichochoroni alimkasirikia Mkubwa kwa
    kuwa aliikatiza ndoto yake na kumkatizia stimu. Analalamika
    kuwa Mkubwa aliiangusha ndege yake (katika ndoto)
    alipomshtua.
    F Viongozi wanaojihusisha katika biashara hii haramu hugeuka
    matajiri na hatimaye kuliumiza taifa kama anavyorai kijana
    aliyeandamana na Mkubwa.
    F Wabwia unga husinzia mchana. Hukauka midomo. Hujidunga
    mili yao ikawa kama jahazi la mtefu. Zaidi ya mno vijana
    hawa hujitoboa mishipa ya damu ikashabihiana na chungio.
    F Vijana wanaojihusisha na biashara hii haramu huishia kwenye
    seli. Wanafungwa miaka mingi huku wakuu wao
    wakiyafurahia maisha yao nje.
    1) UFISADI
    Usadi ni uovu ambao umejitokeza katika hadithi kama
    ifuatavyo;
    F Pindi tu viongozi wanapopata pasipoti ya kidiplomasia wao
    hujiingiza katika biashara haramu za kuuza dawa za
    kulevya. Mkubwa aliweza kupita vizuizi vyote akiwa
    ameubeba mkoba wenye dawa hizo na hakusachiwa.
    F Mkubwa alipungiana mkono na wale askari ndani ya gari ;
    pungiano hili lilikuwa na maana yake. Baadaye Mkubwa
    alifanya mikakati na kumtoa Mkumbukwa ndani alikokuwa
    amefungiwa. Bila shaka aliwahonga askari wamweke
    Mkumbukwa huru.
    F Vijana wanaopewa kazi ya kuviuza vidonge vile
    wanapokamatwa hutiwa magerezani na kuwaacha viongozi
    walanguzi wakiendeleza shughuli zao.
    (mwanafunzi aongezee hoja ili kuonyesha namna usadi
    unavyojitokeza)
    108.
    1) UONGOZI MBAYA
    Uongozi wa Mkubwa ulikuwa uingozi mbaya kwani;
    FAlishiriki usadi- alitumia ushawishi wake kisiasa kumtoa
    Mkumbukwa ndani na kuuokoa mzigo wake(dawa za
    kulevya)
    FAlikuwa akiuza dawa za kulevya- sababu kuu ya Mkubwa
    kujiingiza mamlakani ilikuwa ni utajiri na unga(dawa za
    kulevya). Alimwingiza Mkumbukwa kinaki kwenye
    biashara hii.
    FViongozi hawasachiwi kwenye viwanja vya ndege na hivyo
    basi kuwarahishia mipango ya kubeba dawa za kulevya.
    Idara yauchunguzi imefeli.
    FIdara ya magereza haijukumiki kuwaweka ndani vigogo
    wanaolangua dawa hizi. Wao huwaweka ndani vidagaa.
    (mwanafunzi aongezee hoja)
    2) DHULUMA
    Vijana mahabusu walio magerezani wanadhulumiwa kama
    ifuatavyo:
    F Wanalazwa chini kama magunia ya viazi mbatata.
    F Wakiwa mle ndani kwenye vyumba vya mahabusu
    wananyimwa chakula,hawakogi,hawafui nguo zao,
    F Vijana hawa huhukumiwa kabla na kufungwa pasi
    kupewa nafasi ya kujitetea
    F Vijana hawa huteswa sana kwani hata chakula
    wanachokileta jamaa zao huliwa na walinzi wa
    magereza.
    F Viongozi huwauzia dawa vijana ambao huathirika si
    haba. (tazama athari za dawa za kulevya)
    ZOEZI
    · Jadili maudhui yafuatayo kama yanavyojitokeza katika
    hadithi ya Mkubwa.
    a) Ajira na kazi
    b) Tamaa
    109.
    FANI
    Katika Fani tutashughulikia mbinu za uandishi pamoja na tamathali
    za usemi.
    1. Ndoto:
    Mkubwa aliota alipojilaza kwenye kochi lake. Katika ndoto hii
    mambo yafuatayo yalijitokeza;
    F Vijana wanaotumia dawa wameathirika mno kwani
    walikuwa wakisinzia tu.
    F Baadhi ya vijana(wake kwa waume) wamekondeana
    kana kwamba wanaugua ukimwi au kifua kikuu.
    F Vijana hao walikuwa wac hafu na walikuwa
    wakivitenda vitendo vichafu vya kihayawani.
    F Watu wengi aliowaona hawakuwa na raha kwani wizi
    ulikuwa umewazidi.
    F Nyumba zote zilikuwa zimechanwa nyavu.
    F Vijana aliowaona wote walikuwa wameandikwa
    kwenye vipande vya nyuso zao “mla unga”
    F Mkubwa aliwaona watoto wake wa kiume miongoni
    mwa vijana hao.
    2. Tashbihi
    Tashbihi zimetumiwa kwa mapana na mwandishi wa hadithi hii.
    Mifano michache ya tashbihi ni kama
    F Yule kijana alipita kama umweso…
    F Majumba makubwa yamefumuka kamau yoga…
    F … akipeleka pumzi juu kama mtu aliyepanda…
    F …yalimkaa kama ngoma ya kimanga…
    F Yalitembea kichwani kama damu itembeavyo mwilini…
    F …alilidaka begi la Mkumbukwa kama mwewe anavyodaka
    kuku…
    F Alipita kama umeme…
    F Mkubwa alikuwa amesimama kama mlingoti wa bendera…
    F Lilikwama kooni kama mtu aliyekuwa anakula vigae…
    110.
    3. Mbalagha
    Maswali ambayo hayahitaji majibu moja kwa moja yametumiwa
    mara moja moja na mwandishi kama ifuatavyo;
    F Kwani ulikuwa mwavuli?
    F Wapi?
    . Onomatopea /tanakali
    Mbinu hii imetumika kazini kama ifuatavyo.
    FPopooooooo! Popooooooo! – kuashiria jinsi gari lilivyopiga
    honi.
    5. Utohozi
    Mbinu ya kuyaswahilisha maneno ya lugha ya kigeni ili yatamkike
    na kuandikika kama yale ya Kiswahili.
    FPasipoti – kutokana na ‘passport’
    FKidiplomasia- kutokana na ‘diplomacy’
    FHusachiwi- kutokana na ‘search’
    FProfesa- kutokana na ‘professor’
    FBegi- kutokana na ‘bag’
    FKiboksi- kutokana na ‘box’
    FPresha- kutokana na ‘pressure’
    6. Kuchanganya ndimi
    Kuna mara kadha ambapo mwandishi amevichopeka vifungu vya
    lugha ya Kiingereza katika muktadha wa mazungumzo. Kwa
    mfano;
    F Form four
    F Birthday
    F Brother
    F Sober house
    7. Kinaya
    Kinaya ni kinyume na matarajio. Mbinu hii imejitokeza kama
    ifuatavyo;
    F Ni kinaya kuwa , ili kuwa kiongozi katika eneo la
    Mchafukoge huhitaji kuwa umesoma kwani cha muhimu ni
    pesa na kuwa mzalendo kwa chama chako(ukikatwa, damu
    yako inakuwa rangi ya chama)
    111.
    F Ni kinaya kuwawanafunzi wa Profesa walimpa kura
    Mkubwa ambaye hakuwa na masomo.
    F Ni kinaya kuwa walanguzi halisi wa dawa za kulevya
    huachwa huru( kama vile Mkubwa)na wanaofungwa ni vijana
    wanaowafanyia walanguzi hao kazi.
    (mwanafunzi aongeze hoja)
    8. Takriri
    Pia hujulikana ka uradidi. Lengo la kutumia mbinu hii huwa ni
    kusisitiza ujumbe.
    Mifano ya takriri ni kama ifuatayo;
    F Halimezeki, halimezeki…uk 151
    F Hapo hapo!…154
    F Kifo,kifo,kifo…uk 150
    F Unga!unga!…uk 142
    9. Istiara
    Tofauti na tashbihi, istiara huwa haitumii maneno ya ulinganisho
    kama ‘kama’. Mbinu hii imetumika kama ifuatavyo.
    F Magereza kuna vitawi vitupu- vijana wanofungwa
    wameitwa vitawi
    F …wao ni matela tu- vijana wanaowafanyia kazi vigogo
    kama akina Mkumbukwa wanaitwa matela.
    F …vichwa vya treni huachiwa…- viongozi (vichwa vya treni)
    huachwa nje wakiendelea na biashara zao haramu.
    (mwanafunzi aongezee hoja)
    Zoezi
    F Onyesha namna mbinu hizi zimejitokeza.
    a) Nidaa
    b) Chuku
    112.
    Maswali ya kudurusu.
    1. “ Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi,rudi
    kwa Mola wako.”
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Fafanua sifa za msemewa.
    c) Tambua tamathali ya usemi iliyotumika hapo juu.
    d) Ni kwa nini msemewa anatakikana kurudi kwa Mola wake?
    Majibu
    a) Msemaji wa maneno hay ni Mkumbukwa. Anamweleza Mkubwa.
    Walikuwa kwake Mkubwa.
    b) Msemewa ni Mkubwa. Ana sifa hizi.
    I. Mwenye bidii- alikuwa akishughulisha na kazi ya kuuza pweza
    wa kukaanga na baadaye akauza kipande cha ardhi ili kuingia
    uongozini.
    ii. Mwenye utani- anamtania utingo kuwa huwa haogi jambo
    lililomfanya utingo kukimia kwa kuchekwa na abiria.
    iii. Ni mtambuzi- aliweza kuelewa maana ya unga japo hakuwahi
    tu kuona vituko vyake.
    iv. Mwenye utu- alimpigapiga kijana mbwia unga aliyekuwa
    ameinama kama kwamba anarukuu na kumuuliza iwapo
    anaumwa.
    v. Mwenye tama ya mali- alipotanabahi namna viongozi
    wanavyotajirika kwa kuuza unga , maneno ‘unga na utajiri’
    yalimkaa moyoni kiasi chake kukosa usingizi usiku huo.
    I. Ni maskini- alikuwa akifanya biashara ya kuuza pweza
    iliyokuwa na kipato kidogo . vilevile kabla ya kupata uongozi,
    alikuwa na suruali na shati kipande papa
    113.
    ii. Ni sadi- baada ya kutia na kutoa, aliamua kufanya biashara
    haramu ya kuuza dawa za kulevya biashara ambayo
    huonekana kama ya kishetani. Vile vile alitoa kiasi kikubwa cha
    pesa ili kuwashawishi wapiga kura kumpendelea na ndipo
    akaupata ushindi.
    iii. Mwenye msimamo dhabiti- baada ya kuyatia moyoni maneno
    aliyopewa na kijana Yule kuhusu utajiri na unga aliamua
    kutafuta kwa udi na uvumba na ndipo akamwendea rakiye
    kwa jina Mkumbukwa.
    iv. Ni msiri- mwanzoni hakumweleza Mkumbukwa sababu yake
    kuutafuta uongozi.
    v. Mwenye wasiwasi- aliogopa kuwa huenda kisomo chake
    kingemzuia kupata uongozi
    c) Tashbihi- Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto.
    d) Amevitenda vitendo vingi viovu kama vile ;
    F kuuza dawa za kulevya.
    F Kutoa hongo ili apate uongozi.
    F Kumtapeli raki yake Mkumbukwa na kumuingiza katika
    uuzaji wa dawa za kulevya. Kutumia pasipoti ya
    kidiplomasia vibaya. nk
    114.