Site icon Newsblaze.co.ke

KCSE Mokasa Kiswahili Papaer 3 Joint Exams and Marking Schemes Free Access

MWONGOZO WA MTIHANI WA II WA MOKASA

Hati ya Kuhitimu Kisomo cha Sekondari

102/3   –                       KISWAHILI                           –                       Karatasi ya 3

                                    FASIHI                                              

JULAI/AGOSTI  2023                      Muda: Saa 2½

  1. Shairi

Maswali

(3×1=3)

Kuonyesha maonevu/dhuluma wanazofanyiwa watu katika jamii na wenye nguvu/uwezo mkubwa (1×2=2)

(5×1=5)

  1. Inkisari – laoneya (linaoneya) –liso(lisilo)
  2. Mazida- lajigambaa (lajigamba)

(3×1=3)

Masikitiko/huzuni/kutamauka- kuwepo kwa fahali linalotesa, linaoneya na kujigamba kuhusu uwezo wake

(Kutaja alama 1, kueleza alama 1)

(3×1=3)

Nidaa/siyahi- imetumika kuhimiza/kusisitiza hatua ichukuliwe

(kubainisha alama 1, kueleza alama 1)

 

 

SWALI LA 2 RIWAYA

Sidhani kama moyo wa mja huyu uliwahi kutaka kujua lolote kuhusu ukuaji wangu. Sikumbuki hata siku moja akiniuliza kuhusu neema na mashaka yangu …

 

 

 

 

 

 

MWONGOZO

Msemewa: anajizungumzia/anasimulia kisa mawazoni

Mahali: Kituo cha Afya cha Mwanzo Mpya

Pete anasimulia mawazoni kuhusu namna mamake alivyotelekeza majukumu ya kumlea na kumwachia bibi yake (nyanyake Pete) kwa sababu ya ugomvi uliojitokeza awali kati ya mamake Pete na mumewe.

Msemaji ni Pete

 

 

 

SWALI LA 3

Kila alipokuja jijini Jumapili alikuwa kaandamana na wazazi wake kwa ibada.

(a) Eleza nafasi ya mrejelewa katika kuwajenga wahusika wengine riwayani. (alama 8)

  1. b) (i) Bainisha mbinu ya kimtindo katika dondoo. (alama 2)

(ii) Fafanua jinsi mbinu uliyotajwa katika b(i) ilivyotumika kuendeleza maudhui riwayani.                                                                                                           (alama 10)

Majibu

(a) Anayerejelewa ni Umu/Umulkheri  (uk. 85)

  1. Ametumika kuonyesha kuwa Bi. Dhahabu ni makini. Mwalimu Dhahabu anatambua kuwa Umulkheri alikuwa amezama katika mawazo hivyo anamwambia arejee darasani.
  2. Kuonyesha ubahili wa Naomi – Umulkheri anakumbuka wakati alipomwomba mamake Naomi noti ya shilingi kumsaidia ombaomba ila Naomi akakataa.
  3. Kuonyesha ukarimu wa Hazina – Hazina anamkaribisha Umulkheri katika hoteli ili wanywe chai.
  4. Kuonyesha mapuuza ya polisi – Umulkheri anaporipoti kisa cha kupotea kwa ndugu zake, Dick na Mwaliko, polisi hawakumsaidia kuwatafuta.
  5. Kuonyesha unafiki wa Sauna – Sauna anajifanya kuwa mchangamfu kwao na kuwaahidi kuwalea baada ya kifo cha baba yao. Hata hivyo, baadaye anawateka nyara; Dick na Mwaliko
  6. Kumsawiri Mwangeka kama mwenye mapenzi – Mwangeka anamlea Umu kwa kumwonyesha mapenzi hadi uchungu moyoni unaanza kumtoka.
  7. Kusawiri ukatili wa Naomi – Naomi anawaacha wanawe; Umulkheri, Mwaliko na Dick bila kujali kuhusu malezi yao katika umri huo mdogo.
  8. Kumsawiri Naomi kama mwenye mapuuza – Naomi anapuuza wajibu wake wa malezi anapotoka kwake na kuwaacha wanawe, Umulkheri, Dick na Mwaliko bila mlezi
  9. Kusawiri majuto ya Naomi – Naomi anajuta kuwatelekeza wanawe; Dick, Mwaliko na Umulkheri. Anaanza kuwatafuta wanawe karibu kwenye kila kituo cha polisi.
  10. Kumsawiri Hazina kama mwenye shukrani – anamshukuru Umulkheri baada ya kumpa shilingi mia mbili na kumwahidi kuwa, angemsaidia siku moja.
  11. Kubainisha huruma za Hazina – anatiririkwa na machozi wakati ambapo Umulkheri anamsimulia kisa chake.
  12. Ametumiwa kuonyesha uwajibikaji wa uongozi. Uongozi unawajengea makazi watoto ombaomba na kuwapa elimu.
  13. Kuonyesha kuwa Mwangeka ni mlezi mwema – anamlea Umulkheri kwa mapenzi na kumshauri kuhusu njia ambazo angetumia kukabiliana na mazingira mapya. Anamfundisha Umulkheri maadili mema.
  14. Kuonyesha kuwa Mwangeka ni mshauri mwema – anamshauri Umulkheri dhidi ya kusahau kilichompeleka uzunguni pindi afikapo huko.

Zozote 8 x 1 = 8

  1. b) (i) Bainisha mbinu ya kimtindo katika dondoo. (alama 2)

Mbinu rejeshi/ mbinu ya kioo/ kisengere nyuma

Kupitia mbinu rejeshi tunatambua kuwa, Umu aliandamana na wazazi wake kila walipoenda jijini siku ya Jumapili.                                                                 2x 1 = 2

 

(ii) Fafanua jinsi mbinu uliyotajwa katika b(i) ilivyotumika kuendeleza maudhui riwayani.                                                                                                                           (alama 10)

  1. Ushirikina – Ridhaa anakumbuka matukio kama vile: kupepesa kwa jicho lake la kulia kwa muda wa wiki mbili mtawalia, kuanguka kwake bila kuona kilichomkwaa na jeshi la kunguru lililotua katika paa la maktaba yake. Aidha, anakumbuka milio ya kereng’ende na bundi usiku. Matukio hayo yote ni ishara ya mambo mabaya ambayo yangetokea.
  2. Ubabedume – Ridhaa anakumbuka maneno ya marehemu mama yake kuwa unyonge haukutunukiwa majimbibali makoo (uk. 3).
  3. Usaliti – Ridhaa alidhamini masomo ya wapwaze Kedi ilhali Kedi anateketeza familia ya Ridhaa.
  4. Udhalimu – sheria za kikoloni zilimpa Mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi. Hali hii iliwalazimu Waafrika kama Msubili kuwa maskwota au vibarua katika mashamba ya wakoloni.
  5. Utumwa – vijulanga vilinyakuliwa kutoka kwenye susu zao, hata vifua havijapanuka; na kupelekwa katika maeneo mbalimbali kufanya kazi.
  6. Upangaji uzazi – Mwimo Msubili alikuwa na watoto wa kiume ishirini. Hivyo, ardhi iligawanywa hadi haingewatosha tena. Aidha, Msubili anakabiliwa na changamoto ya kuwalisha wanawe wengi.
  7. Mgogoro katika familia – Wingi wa vinywa vya kulishwa katika familia ya Msubili ulizua mgogoro, uhasama na uhitaji mkubwa.
  8. Elimu – Mamake Ridhaa anatilia mkazo umuhimu wa elimu. Anadai kuwa, elimu inapaswa kuwa chombo cha kueneza amani na upendo.
  9. Uhasama wa kisiasa unasababisha kuvunjika kwa ujirani – Kedi ndiye aliyemtafutia Ridhaa shamba alilolijenga. Aidha, Ridhaa alidhamini masomo ya wapwa wake wawili. Hata hivyo, Kedi anashiriki katika mauaji ya jamaa za Ridhaa.
  10. Vitisho – vikaratasi vilisambazwa kuwatahadharisha akina Ridhaa kuwa, kuna gharika baada ya kutawazwa kwa Musumbi (kiongozi) mpya.
  11. Unyakuzi wa ardhi – baadhi ya mabwanyenye wanajenga majumba mahali ambapo pametengwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara. Mengine yalijengwa chini ya vigingi vya nyaya za stima.
  12. Ufisadi – kuna mabwanyenye ambao wanaonekana wakitoa milungula hadharani.
  13. Utamaduni – Mwangeka anakumbuka jinsi watu walivyoomboleza kifo cha nduguye, Dede.
  14. Ndoa – Kupitia mbinu rejeshi, mwandishi anasimulia jinsi Mwangeka na Apondi walikutana na hatimaye kufunga ndoa.
  15. Ubakaji – Sauna alibakwa na babake mlezi na kumpachika mimba.
  16. Nafasi ya mwanamke – Mamake Sauna alikuwa akiridhia yote yaliyosemwa na mumewe au angeishia kupigwa makonde, kutishwa au kutusiwa.
  17. Uavyaji mimba – Mamake Sauna anamsaidia kuavya mimba bila hiari yake.
  18. Umaskini – mamake Sauna anasema kuwa, Bwana Maya alimwokoa kutoka kwa umaskini aliopakazwa na babake Sauna baada ya kujizikia unywaji wa dengelua.
  19. Madhara ya ulevi – babake Sauna anapigwa kalamu kwa kujiingiza katika unywaji wa dengelua mitaani.
  20. Ulaghai – Sauna anashiriki biashara ya kuwauzia watu maji ya mito wakiambiwa kuwa ni ‘mineral water’.
  21. Utekaji nyara wa watoto – Bi Kangara anamwingiza Sauna katika biashara ya kuwateka nyara watoto.

 

Zozote 10 x 1 = 10

 

TAMTHILIA

  1. Si neno mama!…Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi. Mazuri hutoka mbali na wakati mwingine yana hadithi za kutisha. Maisha yetu ni mfano wa mbegu iliyopandwa. Mbegu hiyo haina budi kuoza kwanza ndipo ioteshe mche upendezao.
  2. a) Eleza muktadha wa dondoo hili(Alama 4)
  3. Msemaji ni Sara.
  4. Msemewa ni Neema.
  1. Sara anaeleza uvumilivu unamletea mja fanaka maishani.

 

 

  1. b) Tambua vipengele viwili vya fani. (Alama 2)
  2. Nidaa – Si neno mama!
  3. Tashbihi – Maisha yetu ni mfano wa mbegu iliyopandwa.

 

  1. c) Kwa hoja nne, fafanua wasifu wa msemewa. (Alama 4)
  2. Neema ni Karimu – Anawaeleimisha wanuna wake hadi kiwango cha juu cha elimu.
  3. Ni mwenye utu – Ana waajiria wazazi wake wafanya kazi wa nyumbani.
  1. Ni mwenye kujali – Anawasaidia wazazi wake kwa kumpeleka mamake hospitalini ana kumtumia masurufu babake.
  2. Ana mtazamo mpevu/ busara – Anamweleza dadake Asna jinsi ndoa si utumwa.
  3. Ni mvumilivu – Anavumilia tofauti baina yake na Bunju kwenye ndoa yao.
  1. Ni mlezi mwema – Anamlea mwanawe kwa mapenzi na uelewa mkubwa.
  2. Ni mpenda usasa – Anashikilia mtazamo wa kwenda kinyume na utamaduni; anasema haifai mke kuachiwa kazi zote.

 

  1. Ni vipi kauli iliyokolezwa wino inadhihirika katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. (Alama 10)
  2. Sara na Yona wanapata shida kwa kukosa watoto kwanza. Baadaye wanapata mabinti ambao wanawasaidia na kuwaheshimisha kijijini.
  3. Uhusiano wa Sara na Yona ulikuwa mbaya awali kwa kuwa Yona anamchapa Sara. Badaye, Yona anabadilika na kuwa mpole na mwenye mapenzi ya dhati kwa mkewe.
  1. Neema anapata ajali inayohatarisha maisha yake. Baada ya ajali anapata msamaria mwema ambaye ni Bunju; anamshughulikia hadi anapopona.
  2. Yona anazamia ulevi kutokana na shinikizo za maisha. Baadaye anaacha ulevi na kuwa mtu mwema na msaidizi wa mkewe.
  3. Sara anadhoofishwa na ugonjwa akiwa nyumbani. Neema anampeleka hospitali nzuri anakopokea matibabu mazuri.
  1. Sara anashindwa la kufanya mumewe Yona anapomhitaji kupika akiwa mgonjwa. Badaye jirani yake Dina anafika na kumwauni katika mapishi.
  2. Bunju anamkemea Neema kwa kumshinikiza kuchangia matibabu ya Sara. Baadaye anatulia na kuahidi kutafuta pesa na kumpiga jeki Neema.
  3. Wanawake awali wanasemekana kutegemea mifuko ya waume wao kwa mujibu wa Luka, lakini sasa wanajitegemea.

 

 

  1. (a) “ Japo nilipungukiwa na mengi niliyotamanai, nilitaka nyinyi muote mbawa mpae juu na kuitazama dunia kutoka kule juu kwa niaba yangu. Stahamala yangu haikuniletea hasara…”

(i) Tambua mandhari ya dondoo hili. (alama 1)

Nyumbani kwa Sara na Yona/ Nyumbani kwao Neema kule kijijini ambapo Sara anazungumza na bintiye Neema

(1×1=1)

(ii)  Bainisha toni inayojitokeza kwenye dondoo. (alama  1)

(1×1=1)

(iii) Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 8)

(b) Onyesha jinsi mhusika Sara alivyotumiwa na mwandishi kuendeleza msuko wa tamthilia hii. (alama 10)

MAANDALIZI YA MOKASA II 2023

102/3

MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE

 

Pupa: F.M. Kagwa

  1. a) “Pupa imenitumbukiza kwenye kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe …”
  2. Bainisha mbinu za kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Huku ukitolea mifano mwafaka, onyesha ukweli wa kauli hii. (alama 8)

 

  1. Jadili namna ukiukaji wa haki umeendelezwa katika hadithi zifuatazo: (alama 20)
  2. Sabina
  3. Kifo cha Suluhu
  4. Nipe Nafasi

Sabina

  1. Mimba za mapema – Nyaboke -kidato cha pili
  2. Kukataliwa baada ya kupachikwa mimba – Nyaboke
  1. Kutengwa – Sabina
  2. Elimu yam toto wa kike kupuuzwa – Sabina
  3. Kupigwa – Sabina
  1. Kuhusishwa katika biashara
  2. Kukosa natibabu – Nyaboke – anapelekwa kwa mganga maarufu kijijini
  3. Kukosa mavazi mazuri – Sabina kuvaa sare iliyoshiba viraka vya kila rangi

 

 

KIFO CHA SULUHU

  1. Mauaji – Bwana Suluhu – mamake Abigael
  2. Kunyanganywa mali – Bwana Suluhu kumnyanganya Mamake Abigael
  1. Kupachikwa mimba na kuachwa bila tumaini/msaada
  2. Kutumia njia za hila ili kuhitimu masomo kabla ya muda wa kuhitimu masomo kuwadia
  3. Kushiriki ukahaba – kuwanyonya wanaume
  1. Kufuja pesa za wananchi
  2. Uchafuzi wa mazingira – ukataji wa miti

 

 

 

 

NIPE NAFASI

  1. Kukosa vyakula
  2. Kutelekeza majukumu – msimulizi anasema baba yao Moshi hakuwa akimtumia mama yake pesa za matumizi mwaka mzima.
  1. Mamake Kazili kukosa kupewa pesa ambazo mumewe Moshi anatetemeka
  2. Kukosa mavza mazuri yanayositiri baridi. Msimulizi amasmea …tulikuwa tumevaa marumaru
  3. Kifo

7.b) “Pupa imenitumbukiza kwenye kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe…”

  1. Mbinu za kimtindo
  2. Jazanda -kisima nilichochimba sasa naingia mwenyewe (mahali penye matatizo)
  3. Mdokezo …kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe
  1. Tashihisi- pupa kuwa na uwezo wa kutumbukiza

b)

  1. Kusafirishwa asikojua – Mkwakuona
  2. Kuvalishw anguo zinazoomyesha mwili wake bila hiari
  1. Kuingizwa kwenye chumba amnacho anasubiriwa na mwanamume mkota-dume
  2. Kufungiwa mlango kutoka nje na mwanamapokezi
  3. Kuuzwa kwa mtu mwenye umri mkubwa kuliko babake mzazi siku yake ya kwanza katika jengo la Chenga- Ways
  1. Anakatiziwa masomo
  2. Kutawishwa katika jengo la Chenga Ways – haruhusiwi kutoka nje
  3. Kulindwa anapoenda msalani

 

 

 

 

Kila Mchezea Wembe: Pauline Kea Kyovi

  1. “Dunia hii nayo kubwa, anasa zake nyingi huwezi kuzimaliza”
  2. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  3. Fafanua toni katika dondoo hili. (alama 2)

Muktadha

  1. Ni kauli ya Emmi
  2. Anamwambia Tembo
  1. Ni baada ya Bwana Tembo kujutia matendo yake ya uraibu wa pombe ambayo yanamsababishia madhara ya kiafya.
  2. Toni

Toni ya kushauri – Emmi alikuwa anamshauri mumewe, Bwana Tembo kuacha tabia zake za kupapia anasa za dunia

  1. Anasa
  2. Kuwa mraibu wa ulevi/pombe
  3. Kusakata rhumba- Bwana Tembo na wenzake (walevi)
  1. Kulala kwa mwanamke asiyemjua
  2. Kuendeleza ukahaba – Angelica
  3. Kufuja pesa

 

FASIHI SIMULIZI

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata

Tumbo:           Leo nitakuwa baba na wewe mama. Mimi sipendi mwajificho.

Chausiku:        Sawa basi. (Anaimba huku akishika masikio yake) Maskini punda, alinyimwa                               pembe, akapewa masikio hiyo ndiyo pembe. Pembee pembe, akapewa masikio                                hiyo ndiyo pembe.

Tumbo:           Mamake Chausiku, nahisi njaa. Napeza kula samaki.

Chausiku:        Ala! Umejuaje kuwa ninapika samaki? Baba Chausiku, samaki kutoka Soko                                     Mjinga ni tamu kama asali. Chakula ki tayari. (Anampa kitawi chenye vipande                                   vya vijiti). Ndio hii samaki.

Tumbo:           (Akiimba) Nimeshiba sana. Asante. Nataka kwenda katika shamba la mahindi                                   kukaza seng’enge. (Anachukua kipande cha mti) Nimechukua nyundo yangu                                     kwenda kujenga ua. (Anatumia kijiti hicho kupigia vijiti vingine ardhini huku                             akisema kuwa anajenga ua).

Chausiku:        Nimechoka sasa. Tuimbe kidogo.

Wote:              (Wanaimba huku wakirukaruka)

Watoto wangu ee

Ee

Mimi mama yenu

Ee

Sina nguvu tena

Ee…

 

Maswali

(a) Bainisha utanzu ambapo utungo wa aina hii unapatikana.                                  (alama 1)

(b) Wewe ni mmoja wa wawasilishaji wa utanzu huu wa fasihi simulizi. Eleza sifa unazofaa kuwa nazo.                                                                                                                  (alama 5)

(c) Eleza sifa zozote nne za kipera hiki.                                                                    (alama 4)

(d) Eleza shughuli mbili za kiuchumi zinazodhihirika katika utungo huu.               (alama 2)

(e) Unanuia kufanya utafiti kuhusu kipera hiki. Eleza changamoto zinazoweza kukukabili unapotekeleza shughuli hiyo.                                                                                                 (alama 6)

(f) Eleza udhaifu wa maandishi kama kifaa cha kuhifadhi data.                              (alama 2)

 

 

 

 

 

MWONGOZO

(a) Bainisha utanzu ambapo utungo wa aina hii unapatikana.                                  (alama 1)

Maigizo al. 1

(b) Wewe ni mmoja wa wawasilishaji wa utanzu huu wa fasihi simulizi. Eleza sifa unazofaa kuwa nazo.                                                                                                                  (alama 5)

  1. Awe jasiri ili aweze kuigiza mbele ya watu/hadharani.
  2. Awe na ubunifu ili aweze kufanya uigizaji kuvutia na kuondoa ukinaifu.
  1. Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
  2. Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza kama vile huzuni.
  3. Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa maswali ya balagha ili kuondoa uchovu.

                                                                              zozote 5 x 1 = 5

 

(c) Eleza sifa zozote nne za kipera hiki.                                                                    (alama 4)

  1. Waigizaji ni watoto.
  2. Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni kama vile arusi, siasa, ukulima.
  1. Huwa na miondoko mingi kama vile kujificha, kuruka.
  2. Huwa na matumizi mengi ya takriri.
  3. Huchezwa popote.

Zozote 4 x 1 = 4

(d) Eleza shughuli mbili za kiuchumi zinazodhihirika katika utungo huu.               (alama 2)

  1. Uvuvi – samaki kutoka Soko Mjinga
  2. Biashara – samaki kutoka Soko Mjinga

(e) Unanuia kufanya utafiti kuhusu kipera hiki. Eleza changamoto zinazoweza kukukabili unapotekeleza shughuli hiyo.                                                                                                 (alama 6)

  1. Gharama ya utafiti kuwa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu kama vile gharama ya kusafiria na kununulia vifaa.
  2. Kutojaziwa hojaji kutokana na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya ujazaji wake.
  1. Wanajamii wengine kudai walipwe kabla ya kutoa habari na hivyo kukwamiza utafiti.
  2. Mbinu nyingine kama vile hojaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika na ikiwa mhojiwa hajui utafiti utakwamizwa.
  3. Uchache wa wazee na wataalamu wa fasihi simulizi kusababisha kukosekana au kupatikana kwa data isiyo ya kutegemewa.
  1. Muda wa utafiti kutotosha na hivyo kutopata habari za kutosha kuhusiana na mada yake.
  2. Kikwazo cha mawasiliano ikiwa mtafiti na mhojiwa hawatumii lugha moja na mhojiwa hajui lugha nyingine na kumbidi mtafiti kukodi mkalimani na gharama kuongezeka.
  3. Ukosefu wa vyombo vya usafiri kunakochelewesha utafiti na kutomalizika katika muda uliopangwa.

Zozote 6 x 1 = 6

 

(f) Eleza udhaifu wa maandishi kama kifaa cha kuhifadhi data.                              (alama 2)

  1. Kuna baadhi ya mambo kama vile kiimbo, toni na ishara ambayo hayawezi kuandikwa kama yalivyowasilishwa na fanani, kwa hivyo hupotea.
  2. Uhai asilia wa fasihi simulizi hufifishwa na kupotezwa na maandishi.
  1. Kuandika fasihi simulizi huifanya kukosa ile taathira asilia kwani kunaipokonya hadhira yake ile fursa ya kushirikiana ana kwa ana na fanani.
  2. Kuiandika fasihi simulizi huidhibiti na kupunguza hadhira yake na kuathiri vibaya usambazaji wake.

                                                                                                            Zozote 2 x 1 = 2

 

 

 

Exit mobile version